Simba wakubali yaishe kwa Lameck Lawi, aanza kwenye kikosi cha Coastal Union dhidi ya Mashujaa FC

Simba wakubali yaishe kwa Lameck Lawi, aanza kwenye kikosi cha Coastal Union dhidi ya Mashujaa FC

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Beki wa kati, Lameck Elias Lawi, ameanza rasmi leo katika kikosi cha Coastal Union kinachocheza dhidi ya Mashujaa FC, mechi ya ligi kwenye uwanja wa KMC Complex.
1726233033251.png
Lawi amejiunga na Coastal Union baada ya majadiliano ya muda mrefu kati ya Simba Sports Club na Coastal Union, ambapo Simba ilikubali kumuachia kwa manufaa ya taifa.

Soma pia: Lameck lawi alisainiwa na simba akatambulishwa ila yupo kambini na coastal union

Simba iliridhia kuachia mchezaji huyo baada ya kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kuwataka klabu hizo mbili kukaa meza moja na kufikia makubaliano.
Line up.jpg
Lawi alialikwa kwenye majaribio ndani ya klabu ya AIK ya Ligi Kuu nchini Sweden baada ya kufeli majaribio yake kwenye klabu ya KAA Gent ya Ubelgiji, nyota huyo wa Coastal Union mwenye umri wa miaka 18 alifanya mazoezi na timu ya vijana ya AIK ya Umri chini ya miaka 19 na timu ya Wakubwa ikiwa ni sehemu ya majaribio yake.

Soma:
=> Maswali kuhusu usajili wa Lameck Lawi
 
Simba sc baada ya maringo yake Lameck, kujiona staa mkubwa wa kuuzwa nje 😀 na kwa kudanganywa na yanga,Simba sc iliamua kumuonyesha Simba sc ni club kubwa ..sasa hivi yeye ndio anahaha huku Simba haina mpango naye tena..namshauri aende yanga
 
We kunguru maji yanga inahusika vipi?
 
Sasa yule msemaji wao alikuwa ana kiherehere cha wapi kwa kumtangaza mchezaji ambaye hajakamilisha usajili!
 
Wenyewe wanakwambia wana wanasheria makini, kwa Lawi wamechemka Coast wakakataa kukaa kwenye vibenchi vya busara, haya kwa Awesu wakachemka, wakaamua waanze upya mchakato wa usajili na KMC ndipo wakampata Awesu.

Yani wanasheria wao ndani ya mwezi mmoja washabwagwa kwenye mashauri mawili ya Lawi na Awesu.
 
Back
Top Bottom