Simba walikoroga usajili wa Mavugo

Simba walikoroga usajili wa Mavugo

MUSONI

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
904
Reaction score
687
LAUDIT MAVUGO KUIPONZA SIMBA SC FIFA? VITALO ' O WANG'AKA

Na Samuel Samuel

Wakati Simba SC wakiiweka rehani leseni ya beki wa kulia wa Young Africans Hassani Kessy kuichezea timu hiyo kwa kile kinachodaiwa mchezaji huyo na klabu ya Young Africans kukiuka mkataba wa awali wa klabu hiyo na mchezaji huyo , Simba imeuvagaa mkenge kwa mchezaji wao wakimataifa Laudit Mavugo waliyemsajili siku nne zilizopita kwa kandarasi ya miaka miwili.

...
Klabu ya Vitalo 'O inayoshiriki ligi kuu nchini Burundi imetanabaisha bado ina mkataba wa mwaka mmoja na mshambuliaji huyo tegemeo kwenye timu hiyo na imeshitushwa sana kusikia na kuona Mavugo katia Tanzania kwenye klabu ya Simba bila ya wao kuwa na taarifa.

Vitalo 'O wamesisitiza jina la mshambuliaji huyo lipo kwenye orodha yao iliyoenda CAF na ndani ya shirikisho la soka nchini Burundi kwa msimu ujao wa ligi.

Tayari klabu hiyo imeamua kuishitaki Simba SC FIFA kuingia mkataba na mchezaji wao aliye ndani ya kandarasi ya mwaka mmoja muda ambao unamzuia mchezaji kufanya mazungumzo na klabu yoyote kiusajili bila klabu husika kupitia kwa timu stahiki yenye kandarasi na mchezaji juu ya miezi sita.

Vitalo ' O wanasisitiza kufanyiwa hujuma na wakala wa mchezaji wao na viongozi wa Simba SC baada ya mchezaji huyo kuomba kibali cha kwenda ufaransa kwenye majaribio ya kuichezea timu moja ya second division lakini ghafla wanashangaa mchezaji huyo kutua Tanzania kwa klabu ambayo wamekuwa wanashindwana kufikia muafaka kwa muda mrefu kuhusu manunuzi ya mshambuliaji huyo.

Simba SC bado wapo kimya kujibu tuhuma hizo lakini kama ni kweli mchezaji huyo ana kandarasi ya mwaka mmoja na Vitalo 'O na tayari wamemvisha jezi za timu hiyo na kuichezea klabu hiyo mechi ya kimataifa dhidi ya AFC Leopards toka Kenya, basi Simba SC wanakila dalili kukumbana na rungu la FIFA.

Nini kinaendelea Tanzania ?! Kila kukicha ni vituko ndani ya soka la nchi hii kuanzia ngazi ya shirikisho jadi kwenye vilabu.

Nachelea kuamini klabu kongwe kama Simba SC kufanya uhuni huu ilihali taratibu wanazijua . Tusubiri tamko la klabu hiyo maana haingii akilini Simba SC kumsajili mchezaji wakimataifa bila kujua kandarasi yake na timu ya awali .ITC yake wataipata vipi, ?

Huenda Vitalo 'O wanakurupuka kuibania Simba SC ? Muda utaongea
 
Katika orodha ya wachezaji wa Vitalo O' mbona Mavugo hayumo.. Mkodisho FC bhana
 
Club ya vitalo Burundi imrandika barua kuishtaki simba kuhusu mchezaji wao l.mavugo ambae bado anamkataba

Wamesema mavugo aliaga aanaendamajaribio..France NA barua tumempaa ya timuya ufaransa NA sio Simba

Loh KESSY PART-II
 
Club ya vitalo Burundi imrandika barua kuishtaki simba kuhusu mchezaji wao l.mavugo ambae bado anamkataba

Wamesema mavugo aliaga aanaendamajaribio..France NA barua tumempaa ya timuya ufaransa NA sio Simba

Loh KESSY PART-II
figisu figisu zimesha anza hawana lolote wanataka pesa tu hao
 
Hitimisho lako limekaa vibaya japo mi sio shabiki wa simba wewe mwenyewe huna uhakika kama hao vitalo wanachoongea ni cha kweli umeona mikataba ya pande mbili kati ya mchezaji na timu yake ya zamani?
 
Wakati Simba ina mchezaji mmoja mwenye utata katika usajili wake, Yanga haijapeleka kabisa majina yote. Wakati Simba inavutana na Vital'o, Yanga inavutana na FIFA. Wakati Simba inaweza kuachana na Mavugo na kuendelea kushiriki ligi, Yanga inaweza kushushwa daraja hadi lisilokuwemo kwenye mfumo wa TMS, yaani daraja la tatu.
 
Wakati Simba ina mchezaji mmoja mwenye utata katika usajili wake, Yanga haijapeleka kabisa majina yote. Wakati Simba inavutana na Vital'o, Yanga inavutana na FIFA. Wakati Simba inaweza kuachana na Mavugo na kuendelea kushiriki ligi, Yanga inaweza kushushwa daraja hadi lisilokuwemo kwenye mfumo wa TMS, yaani daraja la tatu.
Ha ha ha,
Wakukodishwa FC wana kazi sana mwaka huu.
 
Wawalipe tu, kesi iishe.Hii figisu si nzito kihivyo.Mavugo kaja mwenyewe simba,wamshitaki Mavugo kwa kuvunja mkataba kimyakimya.
 
Back
Top Bottom