Simba Wameongeza Squad Depth, Ila Hawajaboresha Squad Quality

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Kutoka katika jicho la kiufundi, nimejaribu kutafakari kwanini mpira wa Simba SC dhidi ya Power Dynamo haukuwa na na ubora wa kiufundi uwanjani?

Nimejaribu kuwaza labda wageni Power Dynamo ndio walikosa ubora kwenye kikosi chao? Lakini hapana, hawawezi kuwa na ubora kwasababu wanatokea katika ligi ambayo ni namba 10 kwa ubora africa.

Ila wengi tulitarajia ubora kutoka kwa mwenyeji wa mchezo.

Huo ubora haukuweza kuonekana hata kusababisha kukosesha raha mashabiki wa klabu. Wasiwasi imetanda juu ya kwamba ni namna gani kwa ubora wa kukosi chao wataweza kusimika mataji msimbazi.

Kimsingi Simba SC amefanikiwa kuongeza squad depth.

Sasa angalau kila nafasi ina wachezaji wawili wenye kufanana uwezo kwa ukaribu na sio kwa usawa.

Hili ni jambo ambalo litawatesa sana msimu ujao kwasababu walio mashabiki wengi walitarajia usajili wa wachezaji ambao wangeweza kuingia moja kwa moja kwenye first 11 ya timu.

Kati ya wachezaji wote wapya walio sajiliwa ni mchezaji mmoja tu ambaye mpaka sasa ana uhakika wa kuanza kukosi cha kwanza mara kwa mara. Huyo ni Che Malone.

Hao wengine wote waliosajiliwa sioni wakitoboa kikosi cha kwanza.

1. Miqquesone sioni akimtoa Kibu Denis kwenye nafasi ya winga wa kulia. Komde boy karudi bongo akiwa Konde Bonge. Sioni akipungua uzito ukifiria zaidi namna jiji la Dar lilivyo jawa na starehe pia.

2. Ngoma ambaye ni CM sioni akimuweka bench Chama. Kimsingi hajaja kuongeza quality bali kaongeza idadi ya wachezaji wa wastani wa bench.

3. Aubin Kramo ni wa kawaida mno. Yaani ametokea Asec lakini naona anakosa namba mbele Onana ambaye hamfikii Godfaza wa Bujumbura.

Simba wanahitaji quality signings ambazo za kuingia moja kwa moja kwenye kikosi na sio back up players ambao wanaongeza squad depth tu.
 
Chama ni AM
Attacking midfielder sawa?

Team inacheza hivi
Kanoute as a DM
Ngoma as a CM
Chama as AM
Miqquisone as AM
Saido as AM na CF mmoja

Mimi sio mchambuzi ila leo wale watatu wa pale juu walikua wanafree roam hasa hasa Chama na saido atleast onana ndo alikaa upande mmoja

Mwanaume bora usiangalie mpira ijulikane kuliko uangalie mpira afu utoe mashudu kama haya
Cheza basi hata fifa

Kwahyo che malone unaona sio improvement
F ngoma je?
Onana je?
Basi kijana lala mpira hukufai
 

Nikusalimu kwa Jina la football,wew kaka sio mtu wa mpira kabisaa,Yan huoni ubora wa Ngoma,Onana? Alafu huwezi wapima wachezaji wa kucheza dk 10 Au 20 .kachamue rede mzee huku sio kwake.
 
Usijiaibishe! Jicho la ufundi ulilipata wapi? Una leseni yoyote ya ngazi ya juu ya ukocha!! Sema kutoka katika jicho la utopolo halafu endelea ..................
 
Huyo hajui kitu halafu ana roho mbaya.
 
Ngoma hukuona jipya lolote na ulichokisema depth sijui na quality unamaanisha nini haiwwzekani ukawa na wachezaji umekiri halafu ukatae u bora wao
 
usingemjibu tu maana hata mpira halijui
 
Nikusalimu kwa Jina la football,wew kaka sio mtu wa mpira kabisaa,Yan huoni ubora wa Ngoma,Onana? Alafu huwezi wapima wachezaji wa kucheza dk 10 Au 20 .kachamue rede mzee huku sio kwake.
Messi akicheza mpira dakika 5 zinatosha kuutambua ubora wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…