Simba wamuongeze dirisha dogo Gerald Gwalala, Mtenje Albano na Kelvin Nashon ili wamsaidie Yussuf Kagoma

Simba wamuongeze dirisha dogo Gerald Gwalala, Mtenje Albano na Kelvin Nashon ili wamsaidie Yussuf Kagoma

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Uchezaji wa Yussuf Kagoma ambaye alionekana kumudu kiungo cha chini unafanana sana na viungo hawa akina Gerald Gwalala wa Coastal Union, Kevin Nashon wa Singida Black Stars na Mtenje Albano wa Dodoma Jiji.

Jana kipindi cha pili tumeelewa sana alipoingia Okajepha, alikuwa akicheza sana nyuma Okajepha, ni mchezaji mkubwa lakini aliingiwa na ubaridi, Mtenje Albano au Kevin wanaingia sana uvunguni, ni kama anavyofanya Kagoma vile.

Wengi tuliokuwepo uwanjani Jana watakubaliana na Mimi kuwa kipindi cha pili alipoingia Okajepha naona Yanga walitakata sana, mzigo mkubwa ulimwelemea Fernandes, Ahoua hakuwa na uwezo wa kuwawin viungo wa Yanga, Kevin Nashon ni mkata shombo mzuri sana, hata Aziz Ki anamjua vizuri, Aziz Ki angebaki kumlalamikia mwamuzi TU hiyo Jana, viongozi wa Simba wasipuuze, wafuatilieni wachezaji hawa mtakuwa kunambia, mwingine ni yule msomali aliekuwepo pale KMC.Wanajua sana boli, sio Kila kiungo mzuri lazima atoke nje ya nchi, hapana.

Kuhusu Ramadan Kayoko, amefanya makosa ya kibinadamu lakini naona kama tunajificha sana kwenye makosa yake wakati sisi wenyewe hatuna cha maana tulichokifanya kipindi cha pili zaidi ya dakika za mwanzo mwanzo ambazo faulo na Kona nyingi Bila mafanikio, Yale mambo ya zamani kuwa mchezaji Fulani katuhujumu tuachaneni nayo, mbona Yanga alipotufunga 5, akatunga 2, akatunga 1, zote mlikuwa kimya, Ina maana mlikuwa mnajua matokeo c ndio, Leo mko pamoja mnatuaminisha kuwa Kayoko ndio msababishi, hapana, hapana.
 
Back
Top Bottom