Wambugani
JF-Expert Member
- Dec 8, 2007
- 1,757
- 277
View attachment 215088Simba wanane waliotoka nje ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na kuingia eneo la Kijiji cha Kibaoni wilayani Babati mkoani Manyara, wameuawa kwa kuchomwa mikuki na wananchi.
Kijiji cha Kibaoni kipo hatua chache kutoka Hifadhi ya Tarangire ambayo ni mojawapo ya vivutio vya kitalii na mara nyingi wanyamapori huzagaa kijijini hapo, hasa nyakati za masika kuepuka majani marefu hifadhini.
Tukio hilo linaloelezewa kuwa ni janga kubwa kwa sekta ya uhifadhi na utalii nchini, lilitokea jana alfajiri na hadi Saa 6.00 mchana na mizoga saba ya Simba ilipatikana, huku mmoja akiaminika kufia kwenye vichaka baada ya kukimbia alipojeruhiwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ameziagiza mamlaka zinazohusika kuwasaka na kuwatia mbaroni wote waliowahamasisha na kuwaongoza wakazi wa kijiji hicho kuwaua Simba hao.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha jana, Nyalandu alitoa maagizo kwa polisi kuchunguza uhalali wa bunduki inayomilikiwa na mmoja wa wakazi wa kijiji hicho iliyotumika kuwaua Simba wawili kati ya saba.
"Kuua idadi kubwa ya Simba kwa wakati mmoja, tena katika siku ya kwanza ya Mwaka Mpya ni jambo la kusikitisha na linastahili kulaaniwa na wote wenye mapenzi mema na uhifadhi ndani na nje ya nchi," alisema Nyalandu na kuongeza:
"Hatuwakamati wakazi wote 100 walioshiriki kuwaua simba hawa, bali tutashughulika na wale waliochochea mauaji ili kutoa fundisho kwa wale wanaochukua sheria mkononi kwa kuwaua wanyamapori," alisema Nyalandu.
Chanzo: Gazeti la MWANANCHI