Simba wapo sahihi kukataa nembo ya GSM

Simba wapo sahihi kukataa nembo ya GSM

Dabil

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2021
Posts
6,823
Reaction score
15,293
Vunja Bei ni kit supplier wa jezi za Simba, GSM ni kit supplier wa Yanga. Halafu halafu nembo ya supplier wa Yanga ibandikwe kwenye Simba .

Yaani NIKE wabandikwe nembo ya Adidas na nembo zote mbili ziwe kwenye jezi moja ,kama siyo akili ya matope ni nini?

Msimu uliopita KCB walikuwa mdhamini mwenza wa Voda ,hatujawahi kuona nembo ya KCB kwenye jezi maana kanuni zinamruhusu tu mdhamini mkuu.

GSM wakae kwa kutulia awe mdhamini mwenza na nembo yake hatuvai ,wavunje kanuni wao hata twiga alibadilishwa rangi ingawa kanuni haziruhusu halafu wao leo wanavunja kanuni? TFF ijibu barua ya Simba kwamba nembo ya mdhamini mwenza inavaliwa kwa misingi ili ya Sheria ? Jibu simple tu.

TFF inasaini mkataba na GSM halafu wanatoa tamko mtu yeyote au club isihoji mkataba ,sawa mkataba hamjashirikisha wadau basi na mambo ya nembo yanatuhusu nini?
 
Vunja Bei ni kit supplier wa jezi za Simba ,GSM ni kit supplier wa Yanga . Halafu halafu nembo ya supplier wa Yanga ibandikwe kwenye Simba .

Mkuu mbona nembo ya "Sport Pesa" ipo kwenye jezi zote mbili za Yanga na Simba

Au nembo ya "Fly Emirate" au "Etihad" ipo kwenye jezi nyingi za timu za ulaya

Acheni ramli chonganishi, cha muhimu klabu zipige pesa ili zijiendeshe vizuri. ova.
images (6).jpeg
 
Umeandika bila kuelewa au kishabiki,mfano wako apo ulitakiwa uje kwa timu ambazo zina mdhamin mmoja na mtengenezaji jez mmoja mfano ,puma wakat huo huo kukawe na adidas.

Fly Emirate au Etihad ,au sportpesa sio watengenezaji jez ni wadhamin wakuu wa club nyng dunian ,swali je inawezekana vip vunja bei anaitengenezea jez simba na ni mdhamin wa vifaa vya simba, halaf kuna gsm ni mdhamin ambae pia ni mtengenezaji jez wa yanga inakuaje mmoja akaweke tangazo lake kwa mwenzake wakat si mdhamin mkuu wa ligi.
 
Mkuu mbona nembo ya "Sport Pesa" ipo kwenye jezi zote mbili za Yanga na Simba

Au nembo ya "Fly Emirate" au "Etihad" ipo kwenye jezi nyingi za timu za ulaya

Acheni ramli chonganishi, cha muhimu klabu zipige pesa ili zijiendeshe vizuri. ova.
Sportpesa hajishugulishi chochote na mambo ya uongozi wa hizi timu mbili ila gsm huwezi kumwondoa na uongozi wa yanga.
 
Umeandika bila kuelewa au kishabiki,mfano wako apo ulitakiwa uje kwa timu ambazo zina mdhamin mmoja na mtengenezaji jez mmoja mfano ,puma wakat huo huo kukawe na adidas...
Kwahiyo unashauri nini?
 
Vunja bei ametoa bilioni 2.1 kutengeneza jezi ya Simba. Huoni kuwa wanambaribia Biashara yake ya jezi?
Kwani GSM anataka kuuza jezi za Simba?

Kwani mbona Vunjabei anauza jezi za Polisi Tanzania na hamsemi?
 
Simba walitoa tender ya kutengeneza jezi Vunja bei alishinda. Akatia bilioni 2.1 kutengeneza jezi na timu Ili auze kama Biashara.Huoni kuwa ni kumuhalibia Vunja bei Biashara yake. Hii kisheria imekaaje Wakuu Vunja bei atarudishaje hela yake?
 
Umeandika bila kuelewa au kishabiki,mfano wako apo ulitakiwa uje kwa timu ambazo zina mdhamin mmoja na mtengenezaji jez mmoja mfano ,puma wakat huo huo kukawe na adidas...
Mkuu katika watu wanashindwa ku-reason ni hao Utopolo. Ona mfano yao!! Haelewi anachokisema, yupo kwenye uyanga bila kuzingatia. Hajui maana au tofauti ya mdhamini na mtengeneza majezi!!
 
Back
Top Bottom