Simba wasipochukua ubingwa wa ligi kuu msimu huu patachimbika

Simba wasipochukua ubingwa wa ligi kuu msimu huu patachimbika

King Jody

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2022
Posts
1,834
Reaction score
3,456
Linapokuja swala la ushabiki hapa Bongo, ni wazi kuna timu mbili zenye ushawishi na mashabiki wengi.

Hapa nazungumzia Simba na Yanga.

Kuhusu mashabiki wa timu hizi mbili kuna utofauti kama ifuatavyo,
-Yanga ina mashabiki waelewa hata kama timu yao ikifanya vibaya bado wataendelea kui-support timu yao.

Mfano mzuri ni Yanga ilipokosa ubingwa kwa misimu minne mfululizo, bado walijipa moyo na kujipanga upya na mashabiki waliendelea kujivunia timu yao.

Ukija kwa upande wa Simba hali ni tofauti, mashabiki hawana uvumilivu, pasipokujua asiyekubali kushindwa si mshindani.

Angalizo: endapo Simba wakikosa ubingwa msimu huu yaani kwa mara ya 3 mfululizo patachimbika, nipo nimekaa pale.
 
Mimi si mchambuzi wa soka lakini naupenda mpira kweli. Wana Simba wajiandae kisaikolojia
 
Back
Top Bottom