Simba yaanzisha mashindano mapya

Simba yaanzisha mashindano mapya

Headcorner

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2020
Posts
205
Reaction score
292
Klabu ya Simba ya Tanzania imeanzisha mashindano mapya ambayo yatajulikana kama Simba Super Cup, Akizungumza na vyombo vya habari CEO wa timu hiyo Barbara Gonzalez amesema mashindano hayo yatazishirikisha timu za TP Mazembe ya Congo na Al Hilal ya Sudan na yanatarajiwa kuanza tarehe 27 mpaka 31 mwezi huu.
 
Hapo wamejiongeza maana kuna TP Mazembe ambae anatoka nchi moja na mpinzani wake kwenye klabu bingwa na Al Hilal pia anatoka na mpinzani wq Simba klabu bingwa
Wanaa lengo zuri sana lakini namna walivyoipanga ratiba ndio tatizo. Mechezo imepangwa karibu karibu sana, na pia zimebaki siku chache timu kucheza mechi za hatua za makundi. hapa kuna uwezekano wa timu kama TP Mazembe kuweka kikosi dhaifu kukwepa majeruhi sio rahisi kupata kipimo sahihi labda kama lengo ni kuwa na ushirikiano na kupata mapato
 
Hii kama maandalizi kujipima. Mazembe ni league moja na mpinzani wao Vita na Al Hilal wakona Merrekh itakuwa kujipima kuona nini cha kutegemea wakija kukutana.
 
Ni wazo jema kwa kuwa simba itacheza na wakubwa wenzake.

Lengo ni kuwatest wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba, pia kumpa nafasi kocha mpya wa Simba kuwajua wachezaji kabla michezo ya CAF
 
Back
Top Bottom