Simba yachapwa 6-0 huko Uturuki

kiben10

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2018
Posts
613
Reaction score
791
Habari ambazo zimetrend leo huko mjengoni Clouds zinasema kuwa Club ya Simba inayoendelea na kambi yake Mtoni Uturuki zinaeleza kuwa baada ya kufanya mazoezi ya siku 5 jana wakaomba mechi ya kirafiki na KUCHARANGWA BAO 6-0 kwani hii ni dhoruba ambayo hawajahi kupitia toka enzi zile za Sunderland.

Ila kutoka kwa msemaji wa Club wa Simba Haji Sunday Manara anasema sio kweli hata kidogo, ingawa msemaji huyo yupo hapa hapa Bongo. Awapa Onyo kali na kuwaomba Clouds wazikanushe habari hizi kwani zimechafua taswira za Club ya Simba kabisaaa.

Sasa je kwa ambao wafuatialiji wa Club yetu pendwa hii ya Simba hii taarifa ambayo Clouds wameitoa kwa hewa ni kweli???

Taarifa hii haina uthibitisho wa picha kwa hiyo mwenye picha anaweza kuitoa hapo hadharani.
 
Hii taarifa karibia off-seasons 3 nimeisikia, kuna moja tuliambiwa South Africa pia ila mpaka leo haikuthibitishwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…