Simba yaifunga Yanga 2 - 1 huko Marekani.
Mabingwa wa Tanzania North America Simba Sports Club ya Ughaibuni, leo walitetea taji lao baada ya kuifunga Yanga Sports Club ya Ughaibuni bao 2-1 katika mchezo mkali kabisa na wa kusisimua uliowanyika uwanja wa Columbus Global Academy jijini Columbus.
Mpira ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu na Simba kumiliki zaidi sehemu ya kiungo iliyowafanya kupata mabao mawili ya kuongoza. Baadaye Yanga walikaa sawa na kuweza kubalance sehemu ya kiungo na kuweza kujipatia goli 1 ambalo ndilo lilikuwa goli la kufuta machozi. Mpaka kipindi cha Kwanza Simba Ughaibuni ilikuwa inaongoza 2 na Yanga 1
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko lakini walikuwa ni Yanga walionufaika na mabadiliko kwa kuweka kutawala sehemu ya kiungo na kuichosha defence ya Simba. Lakini umakini wa mabeki wa Simba na uimara wa kipa wao uliwafanya Simba kuweza kulinda goli lao la kuongoza mpaka kipenga cha mwisho Simba ilikuwa 2 na Yanga 1
Baada ya mchezo huo Simba walikabidhiwa kombe lao na kuzidi kuwa miamba ya soka North America. Unaweza kufuatilia huo mpira kupitia stream za Vijimambo iliyorusha mpira live.
Tutawapiga ndani na nje