Hans Poppe, amesema tangu kumalizika kwa michuano hiyo walikuwa wakijipanga kwa ajili ya kumalizana na wachezaji wengine ambao tayari walishaanza mazungumzo na baada ya kumalizana nao sasa wameona ni muda muafaka kumfukuzia mshambuliaji huyo.
“Ni mchezaji mzuri tumemuona hapa alipokuwa na timu yake ya AFC Leopards, ni mchezaji mwenye uwezo wa kucheza hata eneo la kiungo hata kocha Joseph Omog, alivutiwa naye na ndiyo ametushauri kumsajili,”amesema Hans Poppe.
Kiongozi huyo alisema Kateregga ndiyo atakuwa mchezaji wa mwisho kumsajili msimu huu, na kazi itakayobaki ni kujazia nafasi zenye mapungufu kwa kusajili wachezaji wazawa ambao wataona wanastaili kuichezea timu yao.
Amesema wapo wachezaji ambao tayari walishawaanda kwa kufanya mazungumzo nao ya awali na hivi karibuni wataanza harakati za kukamilisha usajili wao ili kufunga rasmi zoezi la usajili kwa ajili ya msimu ujao.
Simba ilikuwa ikimfukuzi Donald Ngoma wa Yanga, lakini mshambuliaji huyo tayari amewaponyoka na baada kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Chanzo: Shaffih Dauda