SIMBA SC imeachana na kocha wake, Mkuu wa Simba SC, Muingereza Dylan Kerr pamoja na kocha wa makipa, Iddi Salim na sasa timu itakuwa chini ya Mganda, Jackson Mayanja.
Maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika kutwa ya leo makao makuu ya klabu, Msimbazi, Dar es Salaam.
Msemaji wa Simba SC, Hajji Sunday Manara ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba, klabu imevunja mikataba yake na makocha wote, Kerr na Mkenya Iddi Salim.
Manara amesema kwa sasa Mayanja atakuwa na timu, huku mchakato wa kumpata kocha mkuu ukiendelea.
Kerr anaondoka Simba SC baada ya kuiongoza timu katika mechi 30 za mashindano yote tangu atue Julai kuchukua nafasi ya Mserbia, Goran Kopunovic akishinda 19, kufungwa tano na sare sita.
Na Kerr anafukuzwa baada ya Simba SC kutolewa katika Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar Jumapili, jambo ambalo limemfanya apoteze imani mbele ya uongozi.
Kerr anatuhumiwa kwa kushindwa kuifanya Simba SC icheze vizuri na uongozi unaamini kiwango cha timu kimeporomoka kwa kiasi kikubwa kutoka alivyoikuta Julai mwaka jana ilipoachwa na Mserbia, Goran Kopunovic.
Aidha, anashutumiwa kwa ushauri wake mbaya kwa uongozi uliosababisha wachezaji kadhaa wazuri akiwemo Elias Maguri wakaachwa na wakasajiliwa wachezaji wa kiwango cha chini kama Msenegali, Abdoulaye Pape N’daw aliyeachwa Desemba