Simba yamuuza Clatous Chama nchini Morocco

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Kutoka kwenye ukurasa wa Maulid Kitenge huko Twitter ameripoti kuwa kuna tetesi kuwa nyota mahiri wa Simba Sc kutoka Zambia, Clatous Chota Chama ameuzwa kwa klabu moja nchini Morocco.

Hiyo ni baada ya Mtenda Mkuu wa Simba, kuwa nchini huko kwa muda wa siku kadhaa sasa.

Kitenge ametumbia atatuambia timu anayoenda Chama na kiasi alichouzwa!

Kama ni kweli, Simba Sc inaweza ikapoteza key players wake wawili ndani ya dirisha hili ambao ni Chama na Miquissone, unawaona Simba wakiwa katika nafasi gani msimu ujao?

 
Katika watu wenye matatizo na kutunga taarifa za kuzusha mitandaoni ndio huyu namba moja naona sijui tcra wanashindwa nini kuanza nae ili liwe fundisho kwa washirika wenzie wenye mtindio wa ubongo

Binafsi naona kitenge sidhan km alisoma na anacheti naafiki ile kila mwandishi awe na diploma kwenda juu

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo sio kupoteza key players. Tatizo ni kuweza ku identify suitable replacements. Hata kama wakiwa hawajafikia kiwango cha Luis na Chama lakini angalau wawe na potential.

Hivyo ndivyo clubs zinavyojiendesha. So kama ni biashara ifanyike lakini kusajili kwa mihemko hakutakiwi.

A lot of scouting is needed for proper replacements.
 

Kwahyo tunahujumiwa?
 
Mbona huyu huyu Maulid Kitenge ( Mtangazaji Mnafiki, Mswahili, Mpenda Majungu na anayeichukia Simba SC ) hakutupa 'Tetesi' za Yeye kuhama kutokea Wasafi Media na Kurejea EFM na TvE?

Na kuhusu Mchezaji Clatous Chota Chama kutakiwa huko nchini Morocco na Klabu ya FAR Rabat anayofundisha aliyekuwa Kocha wa Simba SC Sven Vandebroek hizo Tetesi hazijaanza leo na nashangaa Mtu kama Maulid Kitenge amechelewa Kuzipata.

Sidhani kama 'Simba SC' itamuuza CCC.
 
Hii ndo tofauti ya Simba na timu zingine,Simba inatengeneza mambo kwa faida sio kelele kama za mashabiki wa Manara f.c.
 
Reactions: mmh
Tetesi ni Jambo la kawaida katika soka na wachezaji kuuzwa ni Jambo la kawaida, wachezaji wanacho angalia ni maslahi Bora kwaajili ya maisha yao.
 
Tetesi ni Jambo la kawaida katika soka na wachezaji kuuzwa ni Jambo la kawaida, wachezaji wanacho angalia ni maslahi Bora kwaajili ya maisha yao.
Ngoja uje kutukanwa na mikia,wamevurugwa kila anaepita karibu nao anaambulia matusi hadi huku mitaani Shadeeya au sio πŸ˜€
 
Walinunuliwa sharti wauzwe ndo mchakato wa soka duniani unadhani walisajiliwa kuzeekea team kama Messi leo anahama huku analia kama ni mzalendo kweli kwa nini aondoke jibu ni pesa kwa maslahi ya wote yaani club na mchezaji mwenyewe
 
Ni kweli,timu iliyompokea barbara huko morocco ndio iliyomnunua chama

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…