Lisungu David Kambona
Member
- Jun 22, 2023
- 5
- 3
Vilabu Vya Simba na Yanga ni Vilabu Vikongwe zaidi Hapa Nchini Kwetu lakini Sio Vilabu Vinavyoleta Maendeleo Kwasasa Bali vimekuwa Vilabu vinavyochochea Umaskini Kwa Watanzania na Nadhani Unajiuliza Vinachocheaje Umaskini Kwa Watanzania ?
Timu Hizi Kubwa Mbili zimekuwa na Mashabiki wengi Sana Hapa Nchini Hata Nje ya Nchi Kiujumla lakini Hapa Kwetu ni Vilabu Vya Asili Vilabu Hivi Vimekuwa Vikieneza Propaganda Kwa Watanzania Katika Swala La Uhamasishaji Hadi Kufikia Hatua Watanzania Kusahau Kufanya Kazi za Kujiiingiza Kipato cha Kila Siku na Kila Jua Linapochomoza na Jamii yetu ya Kitanzania ni Jamii inayopoenda na Kufuatilia Habari za Mihemko sana nakutumia Muda Mwingi Kufuatilia Umbea .
Ukipita Katika Vijiwe Asubuhi na Mchana ambako Ndiko Vijana Wengi hukaa Wamekuwa Wakitumia Muda Mwingi Kujadili Mipira ya Simba na Yanga Kwa Muda Mrefu na Kuacha Kufanya Shughuli za Kujiiingiza Kipato Cha Kila Siku na Zaidi Baada ya mitandao Mikubwa ya Kampuni za Kubashiri Kuziingiza Timu Hizi Katika Mitandao Yao ndio Imezidisha Hali ya Kuwafanya Mashabiki wa Timu Hizi na wanapenda Michezo Kiujumla Kujikita Katika Michezo ya Kamali ambayo kumefungliwa Maduka Makubwa ya Kubashiri
yajulikanayo kama Casino na Kuzidi Kupoteza Pesa Nyingi zaidi, Na Kama Ujuavyo Moja Kati ya Kanuni Kubwa ya Mchezo wa Kamali Ni " The House Always Win " yaani Kampuni ndio inayoshinda Zaidi Kuliko Mcheza Kamali Kwa Tafsiri ya Haraka .
Timu hizi sio Tu Kwa Wanachi wa Kawaida Bali Hata Katika Maeneo Nyeti ya Taifa letu Mfano Bungeni kunakojadiliwa Miswada Mbalimbali ya Kiuchumi na Kisheria Ikitokea Timu Moja wapo imeifunga Timu yoyote Kubwa Kutoka Nje ya Nchi Vilabu Hivi Vya Simba na Yanga Vinaweza Kujadiliwa Muda Mwingi zaidi na Hapo Ndipo Huibuka Kejeli za Hapa na Pale na watu Hufwatilia Bunge sio Kwasababu Kuna Jambo zito la Hasha Bali Simba na Yanga Zimeshika Hatamu Klabu Hizi Zinaweza Kusababisha watu wakasahu Majukumu Yao ya Kila Siku na Kuanza Kuzishabikia .
Mfano Kuna wakati Klabu ya Yanga Ilicheza Michuano ya Kimataifa na Moja Kati ya Wadhamini wa Timu Yusuph Manji Alinunua ticket zote na Kuamuru Mageti yafunguliwe Saaa Tano Asubuhi! Kufika Saba Mchana Uwanja wa Benjamin Mkapa Ulijaa Kufika Saaa Saba Mchana na Kiwanja Kile Kinachochukua watu Elfu Sitini Kwa Siku Hiyo watu Elfu Sitini walikuwa Hawako Kazini na Ilikuwa Siku ya Kazi .
Nadhani Umeanza Kunielewa Kuwa Ni Kwa Namna Gani Vilabu Hivi Vimekuwa Kikwazo Cha Uchumi Japo Kosa Sio la Kwao Kiutendaji ni wakati Umefika Kwa Timu hizi kutazama Pia Maisha ya Mtanzania Kwa Kubuni Njia ya Mpya ya Kuhamasisha Jamii pia Sio Tu Kwa Kuzishabikia Timu Bali Kwa Kuwabadilisha Mashabiki wake Akili Sawa Washabikie Mpira lakini Wafanye na Kazi za Kujiiingiza Vipato Ili Maisha yaende .
Vilabu Vya Simba na Yanga Pia Vimekuwa Sehemu ya Kusahaulisha Watanzania Pale Taifa lipokuwa Katika Hali ya Sinyofahamu ya Katika Kujadili Maswali ya Msingi ya Kitaifa Simba na Yanga Hutumika Kama Chambo Cha Kubadilisha Uelekeo wa Mijadala Ili watu waaache Kuufuatilia Vitu Vya Msingi na Badala yake Kujadili Wachezaji na Usajili na Kamali Hasa Katika Vijiwe Vya Kuuzia Magazeti .
Vitengo Vya Uhamasishaji Katika Vilabu Hizi Siku vitakapoanzisha Falsafa Mpya ya kuhimiza Ushabiki wa Soka na Utendaji Kazi Uchumi wa Nchi Unaweza Kukua na Kuhamasisha uwajibika na Kuwafanya Watanzania wengi Kuacha Kutumia muda Mwingi Kujadili Wachezaji ,Kamali na Jezi Bora na Kuanza Kufanya Kazi kujiingizia Vipato na Kuacha Kutumia Muda Mwingi Kujadili Vitu ambavyo Haziwaingiziii Pesa Wala Faida yoyote kwani Muda wanayotumia Kujadili Vilabu Hivi wangeweza Kutumia Kujiiingizia Kipato na Kubwa kuliko yote watanzania ni watu wanaopenda kuhamasishwa Muda wote wa Maisha Yao Hivyo Kama Hamasa ya Simba na Yanga ingetumika kuwahamasisha watanzania Kufanya Kazi,
Basi Uchumi wa Tanzania Ungekuwa Kuliko Ulivyo Sasa Sababu watu wengi wanatumia Muda Mwingi Kujadili Mambo Ambayo hayawaingiziii Kipato Chochote na Hivyo Taifa Kupata Hasara Kwa Kupoteza Fedha Kwa Kusababisha Watu kufwatilia Simba Na Yanga ambapo Baadhi ya watu Huweka Rehani wake zao na Nyumba Kwa kubashiri kuwa Timu moja ikishinda utachukua Mke wangu au Nyumba yangu au Kuwekeana Mke Kwa Mke au Nyumba Kwa Nyumba na Kuzitia Hasara Familia .
Na mfano Mzuri Kama Klabu Cha Soka Yanga Kilivyotumika Kudai Uhuru ambapo wakoloni Hawakujua Kinachoendelea Klabu Humo na Kuja Kutaamaki Kuwa Yanga Haikuwa Klabu ya Mpira wa Miguuu pekee Bali ilikuwa Ikitumika Kama Sehemu ya Kudai Uhuru .
Lakini Hata Klabu Cha Simba Katika Michuano ya Kimataifa kilivyotumika kuitangaza Tanzania Katika Jezi Zake Kwa Kuandika Maandishi ya "Visit Tanzania " yaani Tembelea Tanzania Ili watu wajioneee Vivutio Vya Utaliii , Ndivyo pia Vilabu Hivi Vinaweza Kutumika Pia kuwahamasisha Watu wakafanya Kazi kuhamasiha Vijana Kuwa Baada ya Simba na Yanga Kuna Maisha Baada ya Timu Hizo .
Mfano Mzuri Mwingine Kama Msemaji wa Simba na Kundi lake Aliweza Kuhamasisha Matembezi ya Kuhamisha Mashabiki wake Kutembea Kuitia Hamasa Klabu Hiyo Baada ya Kufika Hatua ya Robo Fainali Dhidi ya Wydad ya Morocco Inawezakana Kabisa Kuwa Timu Hizi Kutumika Kubadilisha Mawazo ya watanzania ya Kujikita Kufanya Kazi Pia Baada ya Kuzishangilia Timu Hizo .
Hivyo ni wakati wa Simba na Yanga Kubadilisha Mitazamo ya watanzania wavipende Hivyo Vilabu lakini Pia Wafanye Kazi za Kujiingizia Vipato Ili Kuinua Uchumi wa Vijana Wa Kitanzania .
Uhamasiha unaweza kuongeza chachu Mfano katika Awamu Mbalimbali Tumeona Tanzania Ikipiga Hatua Mfano wakati wa Awamu ya Kwanza Serikali ya Mwalimu Nyerere ili Hamasisha sera ya Ujamaa na Kujitegemea Kiasi Kwamba Watanzania Wengi waliitikia Mwito wa Kufanya Kazi lakini Pia kulikuwa hata na Magazeti Mfano Mfanyakazi mifumo ya Uhamasishaji ilisaidia kuwafanya Watanzania kujikita katika kazi mbalimbali hata wakati Huo Idhaa ya Taifa ilikuwa Ikitengeneza Vipindi Mfano Ijue Idm Mzumbe, General Tyre watu walikuwa wakifahamu Vizuri mambo ya Maana nay a Kiuchumi yaliyokuwa Yakiendelea Nchi .
Lakini sasa Simba na Yanga Imefunika mambo yote hayo Kiasi Kwamba muda Huu hakuna Vijana wanaoweza kuilezea hata Rasilimali zilizopo Nchini Mwao kwasababu wao Muda wote wanawza Simba naYanga na kamali Tatizo ambalo limekuwa Msiba kwa taifa kuhamasisha kumeingiza saikolojia kuwa hayo ndio Maisha sahihi ya Kuishi hapa Nchini na Kwengine Hivyo Vilabu vinaweza kutumika Pia kuhamasisha katika Mtazamo Chanya wa Kuwafanya Watu Kufanya kazi na Kuongeza Uwajibikaji .
Picha Kwa hisani ya mitandao ya kijamii
Attachments
Upvote
3