Kwanza kabisa nampongeza mto mada,suala hili ni la msingi lijadiliwe tena kwa kina na sio kulipapasa jujuu.Katika soka letu hapa TZ bado kuna tatizo kubwa ambalo halijatafutiwa ufumbuzi.Taifa star kafungwa Kenya,Simba kafungwa,Yanga nao ndio walewale.
Hivi wasomi tulionao wameshindwa kufanya tafiti juu ya suala hili?Kwa sababu hapa lazima kuna tatizo.Haya kama Taifa Star walipelekwa mpaka Bungeni,Wameleta makocha wakigeni lakini mambo naona ndio yanazidi kuwa mabaya.Na suala hili lakuleta makocha wa kigeni nadhani washika dau katika soka wamekulupuka lakini naamini hawakufanya tafiti kwanza kabla ya kuwaleta hawa wazungu.
Kocha unaemleta hajui kiswahili,yeye anajua kiingereza tena sio kile original,namaanisha sio lugha yao ya awali,mchezaji kiingereza hajui,hapa unategemea nini kitafanyika kama sio mparaganyiko wa mambo.
Kuwachukua makocha wa kigeni mimi sidhani kama itatusaidia kupandisha soka letu,haya mawili ningependekeza yafanyike kwanza,(i)makocha hawa wakifika TZ,wapelekwe shule kwanza wajifunze kiswahili hivyo itasaidia kufundisha kiswahili,mchezo kidogo unaweza kunoga,(ii)kama hiyo itakua haitoshi wachezaji wetu wafundishwe kiingereza kwanza,mimi naona lugha ni tatizo.Nasema hivyo kwa sababu kiingereza tusidanganyane ni kigumu,wewe chuku hata wanaomaliza mlimani wasikilize kiingereza chao ndio utaona lugha hii WATZ bado tuko nyuma,sembuse hawa Form 4,hapa tunadanganyana,soka haiwezi kupanda kwa mfumo huu.Tutabakia kichwa cha mwendawazimu kama alivyosema mzee wa Ruksa.LUGHA JAMANI.
Au kwa nini tusiwapeleke makocha wetu wakaenda kusoma huko halafu wakaja kutufundishia vijana wetu?Hii kasumba ya wageni mbona tunarudi kwenye ukoloni?Naliacha kwenu wadau na mseme.