SoC04 Simba, Yanga wameamua kulala, waamke sasa wawe matajiri

SoC04 Simba, Yanga wameamua kulala, waamke sasa wawe matajiri

Tanzania Tuitakayo competition threads

Jabali Jiwwe

Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
7
Reaction score
8
SIMBA, YANGA WAMEAMUA KULALA, WAAMKE WAWE MATAJIRI

Binafsi nimekuwa mpenzi wa moja wa timu zetu pendwa hapa Tanzania. Nimekuwa mmoja wa wanunuzi na wachangiaji wazuri wa kununua bidhaa pamoja na kwenda uwanjani kusapoti timu yangu!

Lakini pia nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa mifumo na taratibu zingine za timu ambazo wanatuzidi hasa ulaya hasa kwenye uendeshaji wa timu kama biashara.

Timu zetu hizi bado zimelala na punde watakapoamka kwa kumaanisha timu zetu zinautajiri wa ajabu

Nimekuja leo jamvini hasa kwenye jukwaa hili la STORIES THE CHANGE, Nikitaka kupendekeza njia moja au mbili ili timu zetu hizi ziinuke kiuchumi

Kuinuka kiuchumi kwa timu zetu ni wazi kwamba zitachochea maendeleo makubwa kisoka, michezo mingine na kijamii kwa ujumla ndani ya taifa letu..

Viongozi wetu inatakiwa waende mbali zaidi hasa namna gani inatakiwa kuboresha uchumi wa timu hizi, kuinua uchumi kwa vilabu vyetu kutapunguza lawama nyingi za mashabiki hasa katika miundombinu ya timu hasa viwanja, kambi, hostel na 'facilities' zingine zinazohusu timu

Timu zetu hizi mbili kubwa nchini, hazina hostel kwa zaidi ya miongo nane sasa, hazina viwanja ikiwa zinazidiwa na timu ndogo hata zinazo panda daraja ambazo hazina mtaji wa watu lakini vinamiliki viwanja safi kabisa.

Wanajukwaa nina mapendekezo makubwa mawili ya namna ya kufanya kuimarisha uchumi katika vilabu hivi ili sasa viweze kujenga hostel, viwanja hata kununua wachezaji wa maana wa gharama bila kutegemea wawekezaji.

1. Kuwe na mfumo wa kiungozi kuanzia ngazi ya mtaa/ kijiji
Utaratibu huu uanzishwe kwa malengo makuu mawili

Mosi, Club kupata wanachama hai wanaochangia na kulipa ada ya uanachama. Hivi mnajua kama kila club itaanzisha mfumo huu, itapata mwakilishi au mwenyekiti wa club kuanzia ngazi ya kijiji/ mtaa mpaka kata, wilaya, mkoa hadi ngazi ya taifa kote nchini na kina Mangungu watapata kazi ya kufanya, watatembelea kijiji au mtaa kwa mtaa kisha kata hadi mkoa

Pili, kufanya club kuwa mali hasa ya watu 'wananchi' na 'wenye nchi' wanachama na mashabiki wajione kuwa wamiliki hasa wa club zile 51% kwa wanachama za umiliki zitajionesha kwa vitendo

Leo unaangalia uchaguzi ukumbi fulani jijini Dar es Salaam huoni kama nawe mwananchi wa kijiji cha nyakibimbili au kule ibutamisuzi kama mkutano ule unakuhusu, kiufupi wanachama na mashabiki maarufu wa jijini Dar es Salaam tunaona ndio wamiliki wa ile 51%, ukifuatilia hata lawama wanazopewa yanga au simba wakifanya vibaya wanalaumiwa hata mashabiki maarufu kuwa nao wamehusika.

2. Timu ziwe na mfumo wa kieletroniki wa kusajili wanachama na kuhakikisha wanachama wanalipa ada yao na kununua bidhaa za timu husika, ngazi ya taifa wawe na timu inayohamasisha wanachama kununua bidhaa za timu hasa jezi za timu kila msimu( hapa wanaweza kuweka limit kwamba kila mtaa nchini kupitia mwenyekiti wa club ngazi ya kijiji/mtaa wananua jezi(kwa idadi fulani na iwe lazima) achilia mbali wale watakaowiwa kununua kwa hiari yao

Kila mwanachama ashawishike kutoa ada, na ada iwe ndogo tu angalau 500/= kwa mwezi
Timu hizi zina watu wengi sana nchini katika idadi ya watu nchini (60M kwa mujibu wa sensa 2022)
Club zetu hizi zinao uwezo wa kusajili angalau wanachama milioni tano kote nchini, ukipiga hesabu wanachama millioni tano mara mia tano ni kiasi cha 2.5 billion kwa mwezi, chukulia katika mwaka kuna miezi 12 hivyo zidisha kwa 2.5 billion utapata 30billion kwa mwaka.

Ni jambo linalotekelezeka, nchi yetu leo imefunguka, teknolojia imekuwa mno hilo linawekana kabisa......

Kupitia mpango huu nashauri pia, kuwe na magari na maafisa maalumu watakaogombea au kuteuliwa kupitia mkutano mkuu wa vilabu hivi.. wao watahusika na yafuatayo

a. Kuwa na gari maalumu kutoka makao makuu ya klabu kitembelea kijiji kwa kijiji kwa kila mkoa kusajili ada ikiwa Tsh 6000 kwa mwaka au Tsh 3000 kwa miezi sita na watawaingiza kwenye mfumo wa club kama wanachama hai na kuwapa kadi

b. Kuwapa elimu wanachama katika mambo yote yahusuyo klabu na mipango yote ikiwemo ratiba, almanac ya klabu kwa mwaka husika pamoja na kuafanya matamsha ya burudani katika kuafanikisha majukumu yao kwa mafanikio

c. Vilabu kufanya matembezi, friendly match kwenye baadhi ya mikoa, kufanya klabu kuwe karibu na wanachama

Kwa mahesabu hayo hapo juu, mambo mengi sana ya kimaendeleo yatafanyika ikiwemo

i. KUJENGA VIWANJA
Mapato ya 30b kutoka kwa wanachama pekee ni wazi bajeti ya kujenga kiwanja cha timu kizuri na chenye hadhi itawezekana achilia mbali "endorsement" zingine za klabu.

ii. JENGO LA UTAWALA NA HOSTEL
Hostel & na jengo zuri la klabu itawezekana kabisa kijengwa au kukarabati majengo yaliyopo sasa..

iii. MISHAHARA NA USAJILI
Bajeti ya 30b kina 'injinia' wanaweza kuleta mchezaji yeyote africa hii na atalipwa kiasi anachotaka kwa nguvu ya 'JERO' ya wanachama..tunakwama wapi????

iv. TIMU ZA VIJANA NA WANAWAKE

U 17, U18, U19, U20 &QUEEN na PRINCESS

Usajili wake, hostel za kuishi zitakuwepo maradhi na chakula

Yote haya yatawezekana na kupitia timu hizi tutakuwa na timu bora za taifa katika nyanja zote hizo

Nawasilisha[emoji120]
 
Upvote 0
Back
Top Bottom