Simba yanusa ubingwa VPL

Simba yanusa ubingwa VPL

TheGreatASA

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2014
Posts
264
Reaction score
331
USHINDI wa 4-1 waliopata Simba dhidi ya Mbeya City unawafanya klabu hiyo kuhitaji pointi nnetu ili wawe mabingwa wa Ligi Kuu Bara.

Mabao ya Rally Bwalya, Luis Miquissone, John Bocco na Clatous Chama yalitosha kuwafanya mashabiki wa Simba kuweka imani ya ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba mpaka sasa wanaongoza msimamo wakiwa na pointi 73 katika michezo 29, huku Yanga wakiwa nafasi ya pili na pointi 67 katika mechi 31.
Kimahesabu Simba wanatakiwa wawe na pointi nne zingine na kufikisha pointi 77 ambazo hata kama Yanga wakishinda mechi zao tatu zilizobaki hawatowafikia Simba.

Yanga wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 67 katika mechi 31, wakishinda mechi zao tatu zilizobaki watafikisha pointi 76, huku Simba wao viporo vikiwa vinawabeba.

Katika kipindi cha pili Simba walianza kwa kutafuta mabao zaidi kama ilivyokuwa katika kipindi cha kwanza.

Dakika 47 Simba walifunga bao la tatu kupitia John Bocco baada ya kupigiwa pasi na Mohamed Hussein 'Tshabalala' na yeye aliuwahi na kuupiga mpira wavuni.

Dakika 52 Mbeya City walipata bao la kwanza kupitia kwa Pastory Athanas baada ya kiungo wa Simba, Bwalya kufanya uzembe alipokuwa na mpira na Pastory Athanas aliuwahi na kuupiga kwa ufundi ukamshinda mlinda mlango Beno Kakolanya na kwenda wavuni.

Simba walifanya mabadiliko dakika 59 kwa kumtoa Bwalya na kuingia Clatous Chama kwenda kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji.

Dakika 63 mshambuliaji Pastory Athanas alionyeshwa kadi ya njano baada ya kuonekana kujidondosha ndani ya boksi baada ya kuchukua mpira
Dakika 65 Simba walifanya mabadiliko ya kumtoa John Bocco na kuingia Meddie Kagere wakati Mbeya City walimtoa Seleman Ibrahimu na kuingia Samson Madeleke.

Dakika 68 Mbeya City walitaka kupata bao baada ya Kibu Denis kufanyiwa madhambi nje kidogo ya boksi na faulo hiyo ilipigwa na David Mwasa na kwenda moja kwa moja langoni lakini kipa, Kakolanya aliutema na mabeki wake waliondoa na kuwa kona isiyokuwa na faida.

Simba walifanya mabadiliko mengine dakika 76 akitoka Bernard Morrison na kuingia Mzamiru Yassin, mabadiliko hayo yakionyesha wanaenda kuzuia.
Mbeya City katika kipindi cha pili walikuwa wanashambulia zaidi huku mabeki wa simba walionekana wakiwa wamechoka.

Lakini bado walikuwa hawawezi kupenya mabeki wa Simba na badala yake walikuwa wanatumia njia ya kuoiga mashuti nje ya boksi.

Dakika 85 Simba walifunga bao la nne kupitia kwa Clatous Chama baada ya Kapombe kuuwahi mpira mrefu ndani ya boksi na kupiga pasi ya pembeni kwa Chama na kufunga.

MORRISON ATOA KIBWEKA
Mshambuliaji Benard Morrison alitia kali ya wiki alipotolewa, mchezaji huyo alitokea pembeni na kutembea mpaka kwenye benchi la Mbeya City na kukaa.
Tukio hilo liliibua kelele za kushangiliwa mchezaji huyo na yeye mwenyewe alinyanyuka huku akitembea na kucheka.

Benchi la ufundi Simba likiongozwa na kocha msaidizi, Seleman Matola na kocha wa viungo, Adel Zrane walinyanyuka na kwenda kumkumbatia huku wakicheka.

Source


full-pic-1-data.jpg
full-pic-data.jpg
 
Back
Top Bottom