Simba yatia aibu usajili wa Yusufu Mhilu, inategemea tena TFF iibebe kama kwa Morrison

kwenye hili unamsikiliza mchambuzi au kiongozi wa Kagera?
Kagera wangekua wasafi hivyo katika hili suala wasingesema hatutoshitaki kokote,

Pia mimi nimeelezea nilivyosikia, na mwisho nimetoa mawazo yangu, ila wewe kwakua ni mwana Yanga unataka tuongelee vibaya upande usioupenda, sidhani kama ukija katika mtazamo huo tutafika kokote katika kujadili
 
Mwizi ni mwizi TU sio lazima akamatwe na aliyemuibia. Ilipofikia hata mimi kwa niaba ya mpira naweza kuishitaki Simba TFF na FIFA kwa kosa la kumtambulisha mchezaji mwenye mkataba na timu yake.
 
Kosa limeshatendeka kilichobaki ni kosa la kumtambulisha mchezaji mwenye mkataba na timu yake adhabu yake ni ipi? Nothing more nothing less.
 
Hapa kwa kweli Simba wamepepesa na iwapo Kagera wakiamua kusimama kidete bila kuchoka mpaka FIFA watapata haki yao na ziada kidogo. Huwezi kumtangaza mchezaji ambaye bado ana mkataba halali na timu yake bila kwanza kumalizana na hiyo timu yake. Na kitendo walichofanya Simba ni kosa kubwa na kukosa weledi hasa kwa timu inayojua taratibu za uhamisho mpaka wa kimataifa na inayojinasibu kila siku kuwa inataka kuwa klabu kubwa Afrika kama Al haly, Mamelodi, n.k.

Lakini yote kwa yote ni vyema Simba na mchezaji mwenye Mhilu wakajirudi wakawafuata Kagera wakazungumza nao na kufikia makubaliano ambayo yatazinufaisha pande zote tatu Simba, Mhilu na Kagera katika hali ya "win win situation". Mazungumzo siku zote huondoa sintofahamu zote na kuleta maelewano ya kudumu lakini kesi inapofika mwisho huacha makovu na huzaa uadui wa kudumu kati ya aliyeshinda na aliyeshindwa.
 
Hata kama Simba na Mhilu wakienda Kagera Sugar kulimaliza bado hakufuti kosa la kumtambulisha Muhilu kabla ya wakati. Fanya utakavyofanya kosa limeshatendeka. Hata mwenyekiti wa Simba Mzee Mangungu amevuliwa nguo, maana nae hajui cha kusema na pengine hawakumshirikisha kwenye upuuzi huu.
 
Kagera wamesema mpaka sasa bado wanajadiliana na Simba na hawajaamua kushitaki lakini vichambuzi uchwara na utopolo wameshaanza kuishutumu TFF wachukue hatua, hivi TFF inaweza kuchukua hatua bila klabu husika kulalamika? Mbona hao wachambuzi hawazungumzii Plujim kutaka kwenda FIFA kutookana na pesa anazoidai yanga wamebaki kukomalia mambo ya Simba au wanafikiri wakiikomalia Simba nafasi ya ubora ya utopolo itaongezeka.
 
makosa ya kutolipa wachezaji na makocha mbona huyazungumzii
 
Mhilu alikwenda tff kudanganya hana mkataba na Kagera ili uweje?
 
Ukiinflate soko la ndani automatically utaua vilabu vidogo kwa sababu vitashindwa kabisa kusajili wachezaji.

Kagera Sugar siku zote they have issues with Simba toka wapande ligi kuu sijajua ni kwanini
 
Ni kweli hata mimi siungi mkonona hamna namna Simba wanaweza kuficha hii aibu. Ila nimetoa ushauri tu namna ya kulimaliza hili suala kiungwana kabisa bila kumuacha Mhilu akiwa majeruhi. Washauri wabovu inaonekana wameshauri Mhilu aende akavunje mkataba TFF lakini wanashindwa kujua kuwa suala la kuvunja mkataba lilipaswa kuanza kabla ya kutambulishwa na si vinginevyo. Kosa limeshatokea Simba na Mhilu wamechemsha wazi wazi ndio maana nikashauri kiutu uzima waende wakakae chini na Kagera wayamalize kiustaarabu na sio kijanjanja kwa Mhilu kununua mkataba kwani ndio wanazidi kuharibu kabisa.
 
Muhilu katambulishwa au hakutambulishwa na Simba kama mchezaji wao? jibu hilo kwanza acha umbayuwayu!! Kwa maslahi ya mpira, kama Kagera hawatalalamika mtu yeyote anaweza kulalamika.
 
Uto bhana mambi ya Simba mnaimba nyie.

HIVI KESI YA MORRISON CAS INASIKILIZWA LINI MBONA ENG. ANAWACHEZEA KAMA PAKAπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Ilishasikilizwa kitambo, suburi kitu kizito muda si mrefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…