LGE2024 Simbachawene: Watumishi wa umma msipuuze kupiga kura kesho

LGE2024 Simbachawene: Watumishi wa umma msipuuze kupiga kura kesho

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amewasisitiza Watumishi wa Umma na Watanzania wote waliojiandikisha kupiga kura kujitokeza kufanya uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 Tanzania bara.

Simbachawene ametoa rai hiyo leo akiwa ofisini kwake katika Mji wa Serikali, Mtumba, Jijini Dodoma, akieleza kuwa zoezi la kesho ni la kihistoria nchini hivyo kila Mtanzania mwenye sifa wakiwemo Watumishi wa Umma wote, ni muhimu wakashiriki katika kuwachagua wenyeviti wa Serikali za Mitaa, wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.

“Kwa kuwa zoezi hili ni la kikatiba, nikiwa ndiye Waziri mwenye dhamana ya kusimamia masuala ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ninatoa rai kwa Watumishi wote wa Umma na wananchi wote waliojiandikisha kujitokeza kupiga kura ili kuchagua viongozi bora kwa maendeleo ya taifa letu.” Amesisitiza Simbachawene.

Soma pia: Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu aamua kutembelea ofisi mbalimbali kuhamasisha Watu wakajiandikishe katika Daftari la Kupiga Kura

Ameongeza kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza siku ya kesho kuwa ni siku ya mapumziko ili kutoa nafasi kwa watumishi wote kwenda kupiga kura.

Kufuatia hatua hiyo, Simbachawene amewasisitiza Watumishi hao kwenda kupiga kura bila kupuuza kwani ushiriki wao kwenye mambo muhimu ya kikatiba ni kutekeleza majukumu ya kiutumishi.
Screenshot 2024-11-26 165609.png
 
katika utaratibu wa uandishi barua rasmi, tarehe ya kutolewa kuandikwa ni muhimu sana.
 
Back
Top Bottom