Simbu, Giniki na Geay Bungeni

Simbu, Giniki na Geay Bungeni

Melubo Letema

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
416
Reaction score
414
Wanariadha wa Kimataifa wa Tanzania, Alphonce Felix Simbu, Gabriel Gerald Geay na Emanuel Giniki Gisamoda wanatarajia kuhudhuria kwenye kikao cha Uwasilishwaji wa makadirio ya Bajeti ya mapato na matumizi ya wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bungeni jijini dodoma Jumatatu ya Tarehe 6 Juni 2022.

Wanariadha hao , Tayari wamefikia viwango vya kukimbia mashindano Makubwa ya dunia pamoja na mashindano ya Jumuiya ya Madola.

Emanuel Giniki Gisamoda na Gabriel Gerald Geay, wao wanatarajia kuiwakikisha nchi kwenye Mashindano ya Dunia Eugene, Oregon Marekani 15 Julai Hadi 24 julai 2022.

Simbu na wanariadha Wengine watatuwakilisha kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola (Commonwealth Games) yatakayofanyika Birmingham, Uingereza Julai 28 Hadi Agosti 8 Mwaka huu.

IMG_20220604_155602_372.jpg
 
Programu ya mazoezi kwa wanariadha hawa wanaotegemewa kuleta medali kwa Tanzania ktk mashindano haya makubwa kidunia haitavurugika na kuchagia wafanye vibaya ?

Hii ni sawa na vile Simba au Young Africans kufumbuliwa na wazee wa kamati ya ufundi kwa siku mbili mfululizo kuelekea mechi zao kubwa za kimataifa kisha kufanya vibaya ?

Waziri aache kuwatumia wanariadha kipindi hiki muhimu katika siasa za bungeni
 
Nawashauri wakati wakichangia bajeti waomne serikali ipiunguze kodi kwenye mafuta badala ya kutoa ruzuku.
 
Kuna mbunge mmoja aliwapa za uso wake za mawaziri kuwa wanakwenda kuuza sura tu bungeni, hawa nao itakuwaje?
Wanawakilisha Wanariadha wenzao, japo Kocha na watu wake wamemfukuza Mwanariadha wa kike kambini, Failuna alitakiwa na yeye awepo
 
Back
Top Bottom