Simiyu: Ajiua baada ya kudaiwa kushindwa kuizima kesi ya ubadhirifu iliyochonguzwa na TAKUKURU

Simiyu: Ajiua baada ya kudaiwa kushindwa kuizima kesi ya ubadhirifu iliyochonguzwa na TAKUKURU

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Karani wa Chama cha Msingi cha Ushirika amedaiwa kujinyonga kwa kinachoelezwa ni kukosa msaada wa kuzimwa kwa kesi yake ya ubadhirifu wa fedha za wakulima wa pamba licha ya kuhonga rushwa mara kwa mara.

Kamanda wa Mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda amesema: “Alikuwa na kesi TAKUKURU, ameacha ujumbe ulioeleza kuwa ameamua kujiua kwa sababu ametoa hela mara kwa mara kupunguza ili kuondoa kesi hiyo, lakini hakuna mafanikio.”

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila ameagiza uchunguzi ufanyike kujua kilicho nyuma ya pazia kuhusu kiufo hicho
 
Hiyo barua aliyoiacha angewataja kwa majina hao maofisa wote wa Takukuru,lakini uamuzi wa kujiua ni wa kiboya...poleni wafiwa.
 
Ndio maana tunaaswa tumpinge shetani,yani umeiba halafu unajiua,unjiadhibu mwenyewe kwa kosa lako mwenyewe...
 
Karani wa Chama cha Msingi cha Ushirika amedaiwa kujinyonga kwa kinachoelezwa ni kukosa msaada wa kuzimwa kwa kesi yake ya ubadhirifu wa fedha za wakulima wa pamba licha ya kuhonga rushwa mara kwa mara...
Sasa Mtu unapigaje deal huku huna kifua cha kupambana na Matokeo ya hilo deal Kama deal litavurugika!!??

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
aise watu mbona wanawahi sana viwanja huko akhera madukani ?

si tutakuta pamejaa sasa ?🤔
 
Ndio maana tunaaswa tumpinge shetani,yani umeiba halafu unajiua,unjiadhibu mwenyewe kwa kosa lako mwenyewe...
Hii ni nzuri, kuliko kuiba bila ya adhabu yoyote. Inamfanya mtu afikirie ubaya wa wizi.
 
Isije kuwa kauliwa na walioshirikiana kuiba. Hapo uchunguzi lazima ufanyike.
 
Police hao, waongo, wanakula hela, mwishowe mahakaman unaenda!
 
Back
Top Bottom