figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
HOTUBA YA MBUNGE WA JIMBO LA KISESA, MHE. LUHAGA JOELSON MPINA (MB) ALIPOFANYA ZIARA YA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UJENZI WA SHULE YA UFUNDI MWANDOYA MEATU SIMIYU TAREHE 11 JANUARI 2025
Serikali ilileta fedha kiasi cha Tsh. Milioni 584 mwezi Juni 2024 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Ufundi Mwandoya iliyopo Jimbo la Kisesa Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu ambapo Sekondari ya Mwandoya iliteuliwa kusimamia mradi huo kwa njia ya Ununuzi wa kutumia raslimali za ndani (Force Account).
Kuanza utekelezaji wa Mradi
Taratibu za kumpata Fundi wa Ujenzi wa Mradi huu na Mzabuni wa vifaa vya ujenzi, kufunga Mkataba na kuanza ujenzi imechukua zaidi ya miezi 4 tangu fedha hizo zifike ambapo Fundi ujenzi SHEVA Hardware wa Kinondoni Studio Dar es Salaam aliingia Mkataba na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu tarehe 24 Oktoba 2024 baada ya kushinda zabuni hiyo iliyotangazwa kupitia Mfumo wa NeST.
Katika ziara yangu ya Tarehe 11 Januari 2025 nimejionea hatua ya ujenzi ipo katika uchimbaji wa msingi na usombaji wa mchanga hivyo ni sawa na kusema kuwa utekelezaji wa mradi huu haujaanza zikiwa zimepita siku 77 kati ya siku 90 za utekelezaji wa mkataba wa mradi huu.
Tangu Serikali ilete fedha kiasi cha Tsh. Milioni 584 katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu na Sekondari ya Mwandoya miezi 6 iliyopita ujenzi haujaanza.
Njia i!iyotumika kumpata fundi ujenzi na mzabuni wa vifaavya ujenzi
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kupitia mfumo wa NeST ilimpata fundi na mzabuni wa vifaa vya ujenzi katika miradi 3 ya Shule ya Sekondari ya Ufundi Mwandoya, Shule ya Sekondari Kabondo na Shule ya Sekondari Mbushi ambapo Local Fundi SHEVA Hardware wa Kinondoni Studio Dar es Salaam alikuwa mshindi wa zabuni zote 3 na kusaini mkataba wa thamani ya Takriban Tsh. Bilioni 1.7 wastani wa Tsh. Milioni 584 kwa kila mradi.
Njia ya Ununuzi iliyotumikani matumizi ya raslimali za ndani (Force Account) kwa miradi yote mitatu, Hii ni kinyume na Kifungu cha 76 (3) (b) cha Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 10 ya Mwaka 2023 ambacho kinakataza kutumia raslimali za ndani (Force Account) endapo gharama za mradi zitavuka ukomo wa thamani kwa kazi ya ujenzi iliyoainishwa katika Kanuni.
Ambapo Kanuni ya 167 (2) ya Kanuni za Ununuzi wa Umma za mwaka 2024zinakataza kutumia raslimali za ndani (Force Account) endapo thamani ya ujenzi iliyokadiriwa inavuka kiasi cha Tsh. Milioni 100. Local Fundi SHEVA Hardware amepewa zabuni ya Tsh. Bilioni 1.7 wastani waTsh. Milioni 584 kwa kila mradi hii ni zaidi ya ukomo uliowekwa kisheria wa Tsh. Milioni 100.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu alichukua jukumu la kusimamia ununuzi hadi kutoa tenda kwa kuchagua mzabuni bila kuzishirikisha Taasisi nunuzi ambazo ni Shule ya Sekondari Mwandoya, Shule ya Sekondari Ng'hoboko na Shule ya Sekondari Mwanjolo, Taasisi nunuzi hazikuitwa kuridhia mkataba DED MEATU alichukua jukumu hilo kinyume na masharti yaliyowekwa katika matumizi ya raslimali za ndani (Force Account)
Uhakiki wa sifa za Fundi
Local Fundi SHEVA Hardware ni wa Kinondoni Studio Dar es Salaam na hajawahi kufanya kazi za ujenzi Wilaya ya Meatu na Mkoa wa Simiyu na hivyo katika mazingira ya aina yoyote si rahisi kujua uwezo na ubora wa miradi anayotekeleza au aliyowahi kufanya maeneo mengine. Pia SHEVA Hardware hajasajiliwa na Bodi ya Makandarasi (ERB) hivyo siyo rahisi kujua kama ana sifa za kisheria, uwezo na raslimali za kumwezesha kutekeleza kwa ufanisi mkataba. Uamuzi wa kutoa tuzo bila kufanya uhakiki wa kina wa sifa za mzabuni ni kinyume na Kifungu cha 55 (1) cha Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 10 ya mwaka 2023.
Utoaji wa Tuzo kwa Local Fundi SHEVA Hardware
Local Fundi SHEVA Hardware alishinda zabuni zote 3 na kuingia mkataba na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kujenga miradi hiyo, kumlundikia kazi fundi mmoja na bila hata kufanya tathmini za athari hasi kunapelekea fundi huyo kuelemewa na kazi na kushindwa kukamilisha kwa wakati.
Lakini pia Local Fundi SHEVA Hardware ni wa Kinondoni Dar es Salaam na hafahamiki Meatu wala Mkoa wa Simiyu kwa ujumla na hivyo isingetarajiwa kuaminiwa na kupewa zabuni ya miradi mitatu mikubwa yenye thamani ya Tsh. Bilioni 1.7 kwa pamoja.
Pia bado zabuni aliyopewa Local Fundi SHEVA Hardware ni zaidi ya ukomo uliowekwa na sheria wa Tsh. Milioni 100.
IJamuzi wa utoaji wa zabuni hizi 3 uliofanywa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Ndugu Athumani Hamisi Masasiunaleta mashaka makubwa ya uwepo wa udanganyifu, upendeleo na Rushwa na hii ni kinyume na kifungu cha 107 cha Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 10 ya mwaka 2023.
Malipo ya awali
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu tarehe 8 Novemba 2024 aliagiza taasisi nunuzi kufanya malipo ya awali kwa SHEVA Hardware wakati taasisi nunuzi kupitia kamati za ununuzi zinayo mamlaka kamili zilizokasimiwa kisheria kwa utaratibu wa Force Account kukubali au kukataa kumlipa mzabuni au mkandarasi au fundi baada ya kujiridhisha na mpango wa ununuzi ambapo vifaa vya ujenzi hununuliwa kwa kuendana na mahitaji na vipimo vilivyoidhinishwa na Meneja wa Mradi.
Local Fundi SHEVA Hardware tarehe 25 Oktoba 2024 aliomba malipo ya awali (Advance payment) ya vifaa vya ujenzi kiasi cha Tsh.100,689,400 kwa kila mradi hivyo ni jumla ya Tsh. ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu aliidhinisha malipo hayo licha ya kuwa dhamana ya Benki iliyokuwa imewasilishwa ilikuwa na thamani ya Tsh. 30,206,820 kwa kila mradi ambapo kwa miradi 3 ni Tsh. 90,620,460 tu kutoka Guaranty Trust Bank (Tanzania) Ltd.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu alikubali kuidhinisha malipo ya awali ya Tsh. 211,447,740 bila kuwepo dhamana ya Benki wala Bima kutoka kwa mzabuni. Hii ni kinyume na Kifungu cha 67 (2) cha Sheria ya Ununuzi wa Umma na Kinyume na Kanuni ya 315(4) (c) ya Kanuni za Ununuzi wa Umma za mwaka 2024 zinazotaka malipo ya awali yatakayofanyika yasiwe zaidi ya thamani ya dhamana iliyowekwa.
Malipo ya awali ya Tsh. 100,689,400yalifanyika tarehe 26 Novemba 2024 katika mradi wa Shule ya Sekondari Mbushi na Tarehe 20 Novemba 2024 malipo yalifanyika ya Tsh. 100,689,400 kwa ajili ya mradi wa Sekondari ya Kabondo na hivyo jumla ya Tsh. 201,378,800 zililipwa kwa Local Fundi SHEVA Hardware kama malipo ya awali.
Ambapo tathmini ya awali ya gharama za ujenzi alizotumiafundi kwa ununuzi wa vifaa na ufundi ni takribani Tsh. 60,000,000 kwa miradi yote mitatu tangu alipwe miezi miwili iliyopita na hivyo kiasi cha Tsh. 141,378,800 kutumika kwa matumizi mengine tofauti na miradi aliyopewa hii ni Kinyume na Kanuni ya 315 (7) ya Kanuni za Ununuzi wa Umma ambayo inakataza muuza bidhaa kutumia malipo ya awali kwa kazi nyingine tofauti na kazi zilizoanishwa katika nyaraka za mkataba.
Haieleweki kwanini Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu alikubali kuweka sharti la malipo ya awali kwenye mkataba wa ununuzi wa vifaa huku akijua kuwa malipo ya ununuzi wa vifaa hufanyika baada ya vifaa vya ujenzi kufika eneo la mradi ambapo TAX Invoice na Delivery Note hupokelewa na kusainiwa.
Kazi ndogo za Local Fundi hazihitaji malipo ya awali na hivyo hii ni kinyume Kifungu cha 96 (1) kinachokataza kazi za ujenzi, bidhaa au huduma kulipiwa kabla hazijatekelezwa, kuwasilishwa au kutolewa.
Dhamana ya Mzabuni iliyowasilishwa
Tarehe 5 Novemba 2024 Local Fundi SHEVA Hardware aliwasilisha dhamana za Benki zenye thamani ya Tsh. 30,206,820 kwa kila mradi katika miradi mitatu sawa na jumla ya thamani ya Tsh. 90,620,460 pia tarehe 22 Novemba 2024 SHEVA Hardware aliwasilisha dhamana zenye thamani ya Tsh. 100,689,400 kwa miradi miwili ya Kabondo na Mbushi sawa na jumla ya Tsh. 201, 378,800.
Dhamana (Tender Security Bank Guarantee) hizi zote hakuna uthibitisho kama Halmashauri ya Wilaya ya Meatu ilifanya uhakiki wa dhamana iliyotolewa na Benki ya Guaranty Trust Bank (Tanzania) Ltd kabla ya kuingia mkataba na kuanza kufanya malipo ya awali jambo ambalo ni Kinyume na Kanuni ya 315 (4) (b) ya Kanuni za Manunuzi ya Umma inayotaka dhamana inayowasilishwa iwe imethibitishwa uhalali wake na Benki inayotoa dhamana hiyo.
Malipo ya awali katika Shule ya Kabondo na Mbushi ya jumla ya Tsh. 201,378,800 yamefanyika bila uthibitisho wa uhalali wa dhamana zilizowasilishwa na Local fundi SHEVA Hardware.
Dhamana za Benki ya Tarehe 5 Novemba 2024 na Dhamana ya Benki ya 22 Novemba 2024 haieleweki ni dhamana gani hasa iliyotolewa kwa ajili ya miradi kwani hakuna Maelezo kama dhamana ya Tarehe 5 Novemba 2024 ilifutwa na Benki, kuwepo dhamana 2 kwa pamoja na kwa tarehe tofauti tofauti kwa miradi hiyo hiyo kunaleta mashaka makubwa juu ya uhalali wa dhamana hizo na pengine kuna udanganyifu umefanywa.
SHEVA Hardware malipo yake yanafanyika kupitia Benki ya NMB lakini Benki iliyomdhamini ni Benki ya Guaranty Trust Bank (Tanzania) Ltd jambo hili pia linaleta mashaka ya uhalali wa dhamana zilizowasilishwa.
Hatua zilizochukuliwa na Serikali
Fundi na Wakuu wa Idara kukamatwa
Taarifa zilizopo baada ya utekelezaji wa miradi hii kusuasua Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Fauzia Hamidu Ngatumbura aliagiza kukamatwana kuwekwa rumande katika Kituo cha Polisi Meatu kwa muda mfupi na kuachiliwa huru na kuendelea na majukumu yao ya kazi kama kawaida.
Waliokamatwa na kuwekwa rumande ni pamoja na Local Fundi SHEVA Hardware na Maafisa 4 wa Halmashauri akiwemo Ndugu Ambakisye Mwakabana, Afisa Mipango na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meatu, Ndugu Antony Luyeye, Kaimu Afisa Elimu Sekondari, Ndugu Fatuma Mohamed, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi na Ndugu Saguda Kidanha, Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Miundombinu.
Watumishi hao wa Umma walikamatwa kimya kimya na kuachiwa huru kimya kimya bila wananchi kujulishwa kupitia vyombo vya Habari wala mitandao ya Kijamii ikiwemo ukurasa rasmi wa Instagram wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu jambo ambalo limezua sintofahamu kubwa juu ya usiri huo na ni kinyume na Misingi ya Utawala bora inayotaka uwazi na Uwajibikaji katika kutekeleza shughuli za umma.
Swali kubwa la kujiuliza kwanini akamatwe Kaimu Mkurugenzi na wakuu wa Idara lakini Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu hajakamatwa, hajawekwa rumande wala kufunguliwa mashtaka Mahakamani. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ndiye Afisa Masuuli aliyekabidhiwa dhamana ya kusimamia fedha na mali katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.
(ii) Malipo ya fidia ya ucheleweshaji (Liquidated Damages)
Pamoja na ucheleweshaji wa mradi huu kwa zaidi ya siku 77 Halmashauri ya Wilaya ya Meatu haijafanya mchakato wa kudai fidia ya ucheleweshaji wa utekelezaji wa mkataba ambapo mkataba huo ulitakiwa kukamilika tarehe 24 Januari 2025 tangu uliposainiwa tarehe 24 Oktoba 2024 lakini hadi sasa siku 13 zimebaki kwisha muda wa mkataba huu hatua iliyofikiwa ni uchimbaji wa msingi na hivyo ni dhahiri kuwa mradi huu hautakamilika kwa muda uliopangwa na hadi sasa ninavyo ongea umechelewa kwa siku 77 tangu kusainiwa kwa mkataba.
Hii ni kinyume na Kanuni ya 318 (1) (2) (a) za Kanuni ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2024 zinazotaka taasisi nunuzi kutoza fidia ya ucheleweshaji kati ya 0.10% hadi 0.20% ya thamani ya Mkataba kwa siku za ucheleweshaji.
Hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Meatu pamoja na Taasisj nunuzi zilipashwa kudai faini ya ucheleweshaji ya takribani Tsh. Milioni 261 kwa Local Fundi SHEVA Hardware jambo ambalo halijafanyika hadi sasa.
(iii) Madai ya fedha ambazo zimetumika tcfauti na miradi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu hajachukua hatua ya kudai fedha Tsh. Milioni 141 ambazo SHEVA Hardware amezitumia kwa shughuli tofauti na mkataba. Aidha Halmashauri haijadai kulipwa na mdhamini wa SHEVA Hardware ambaye ni Benki ya Guaranty Trust Bank (Tanzania) Ltd.
Mwisho
Kwa kifupi utaratibu uliotumika kumpata Local Fundi na Mzabuni wa Vifaa, uwasilishaji wa dhamana, malipo ya awali ni uvunjifu mkubwa wa Sheria za nchi, kinyume na Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 na ni hujuma kwa Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Mhe. Rais Dk. Samia SuluhuHassanambayo imejipambanua kuboresha mazingira ya elimu na kupigania ajira kwa vijana.
Kashfa ya Halmashauri ya Wilaya ya Meatu ni mfano mdogo tu wa namna fedha za umma zinavyotafunwa kila upande wa nchi na kama ambavyo tulivyoshuhudia yaliyotokea Halmashauri ya Bunda ambapo baadhi ya watumishi wasio waaminifu walibeba mafurushi ya fedha zaidi ya Tsh. Milioni 200 kupeleka Makao Makuu ya TAMISEMI kwa watu binafsi.
Pia Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika na kuonya mara kwa mara juu ya Usimamizi dhaifu wa mikataba, miradi kuchelewa kukamilika na kutelekezwa, kulipa zaidi ya dhamana, ongezeko la gharama (Variations) na faini na adhabu ya ucheleweshaji malipo. Hali inayopelekea Serikali kupoteza fedha nyingi za umma nakuchelewa kutoa huduma kwa wananchi iliyokusudiwa.
Ushauri na Mapendekezo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu kusimamia kufanyika kwa Ukaguzi wa Kiuchunguzi (Forensic Audit) ili kubaini udanganyifu katika mikataba hii baina ya SHEVA Hardware na Halmashauri ya Wilaya Meatu na kuchukua hatua stahiki za kisheria na kiutawala kwa wote waliohusika na kashfa hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wasimamie SHEVA Hardware kurejesha fedha za Umma alizotumia kwa matumizi yake binafsi kiasi cha Tsh. Milioni 141 pamoja na kulipa fidia ya ucheleweshaji ya Tsh. Milioni 261 jumla ya madai yote ya Tsh. Milioni 402.
(iii) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu kusimamia kuvunja mkataba baina ya Halmashauri ya Wilaya ya Meatu na Local Fundi SHEVA Hardware wa Kinondoni Studio Dar es Salaam.
Pia kuajiri local fundi 14 ili kila jengo liwe na Local Fundi wake ili kuharakisha utekelezaji wa miradi hii kwa maslahi mapana ya umma.
Asanteni kwa Kunisikiliza,
Kazi lendelee
Luhaga Joelson Mpina(Mb) Mbunge wa Jimbo la Kisesa