Simiyu: Mganga wa kienyeji ajenga madarasa ya shule, achimba kisima, aweka solar

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
FQDiyJGXIAAY39W.jpg
Mganga mmoja wa tiba za kienyeji katika Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu amejitolea kwa gharama zake kujenga vyumba viwili vya madarasa ya kisasa, kuchimba kisima cha maji na kuweka umeme wa Sola kwenye shule mbalimbali wilayani humo.

Mganga huyo Ndabagija Katani amesema ameamua kufanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuinua maendeleo ya elimu.

Katika mahojiano yake na Runinga ya East Africa, Mganga huyo amesema suala la kuchangia maendeleo halipaswi kuachwa kwa Serikali pekee, bali kwa kila Mtanzania.

Ndabagija ambaye ni mkazi wa kata ya Chinamili Wilaya ya Itilima, amewashauri waganga wengine wa kienyeji nchini, kushiriki kuchangia shughuli za maendeleo ya Taifa.

MGANGA.jpg
Source: East Africa TV
 
sawa mganga unaakili sana naona na jf unaitumia hongera usiishie hapo.
 
Mganga mmoja wa tiba za kienyeji katika Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu amejitolea kwa gharama zake kujenga vyumba viwili vya madarasa ya kisasa, kuchimba kisima cha maji na kuweka umeme wa Sola kwenye shule mbalimbali wilayani humo.

Mganga huyo Ndabagija Katani amesema ameamua kufanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuinua maendeleo ya elimu.

Katika mahojiano yake na Runinga ya East Africa, Mganga huyo amesema suala la kuchangia maendeleo halipaswi kuachwa kwa Serikali pekee, bali kwa kila Mtanzania.

Ndabagija ambaye ni mkazi wa kata ya Chinamili Wilaya ya Itilima, amewashauri waganga wengine wa kienyeji nchini, kushiriki kuchangia shughuli za maendeleo ya Taifa.

Source: East Africa TV
Umemtambulisha kwa kumkashifu sana.Ungemueleza kuwa ni;MTAALAMU/MGANGA/TABIBU WA TIBA ZA ASILI.
Neno "kienyeji" linamuweka kundi moja na wale wa "tuma kwenye namba hii"!
 
Ilitosha kusema Mwananchi mmoja ajenga madarasa, achimba kisima, aweka solar. Sidhani kama kuna uhusiano kati ya shughuli zake na jambo la kijamii alilolifanya
 
Mganga mmoja wa tiba za kienyeji katika Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu amejitolea kwa gharama zake kujenga vyumba viwili vya madarasa ya kisasa, kuchimba kisima cha maji na kuweka umeme wa Sola kwenye shule mbalimbali wilayani humo.

Mganga huyo Ndabagija Katani amesema ameamua kufanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuinua maendeleo ya elimu.

Katika mahojiano yake na Runinga ya East Africa, Mganga huyo amesema suala la kuchangia maendeleo halipaswi kuachwa kwa Serikali pekee, bali kwa kila Mtanzania.

Ndabagija ambaye ni mkazi wa kata ya Chinamili Wilaya ya Itilima, amewashauri waganga wengine wa kienyeji nchini, kushiriki kuchangia shughuli za maendeleo ya Taifa.

Source: East Africa TV
Akipiga ramli chonganishi watu wakauana mtathubutu kumkamata, anywa maendeleo hayana chama wala imani, yenyewe yanakwenda tu
 
Hata Mwendazake Mwandulami mganga aliuejijengea kaburi pale Kijiji Cha Itunduma Mtwango Njombe nae alijenga madarasa pale Sovi secondary,

Ila waganga Wana Hela Sana aisee sema Ndio hawapendi show off
Au nasema uongo
Ndugu yangu
Mshana Jr?
 
Mganga mmoja wa tiba za kienyeji katika Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu amejitolea kwa gharama zake kujenga vyumba viwili vya madarasa ya kisasa, kuchimba kisima cha maji na kuweka umeme wa Sola kwenye shule mbalimbali wilayani humo.

Mganga huyo Ndabagija Katani amesema ameamua kufanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuinua maendeleo ya elimu.

Katika mahojiano yake na Runinga ya East Africa, Mganga huyo amesema suala la kuchangia maendeleo halipaswi kuachwa kwa Serikali pekee, bali kwa kila Mtanzania.

Ndabagija ambaye ni mkazi wa kata ya Chinamili Wilaya ya Itilima, amewashauri waganga wengine wa kienyeji nchini, kushiriki kuchangia shughuli za maendeleo ya Taifa.

Source: East Africa TV
Huyu jamaa namfahamu aisee.
 
Back
Top Bottom