Uchaguzi 2020 Simiyu: Minada yasitishwa kupisha Uchaguzi Mkuu

Uchaguzi 2020 Simiyu: Minada yasitishwa kupisha Uchaguzi Mkuu

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, amesitisha minada na magulio yote mkoani humo siku ya uchaguzi mkuu ya Oktoba 28, 2020, ili kutoa nafasi kwa wananchi kwenda kupiga kura kumchagua Rais, wabunge na madiwani wanaowataka.

RC Mtaka ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Maswa, na kusema kuwa minada na magulio yataendelea siku ya Alhamisi kama kawaida.

"Minada inayofanyika jumatatu na jumanne ni ruksa, Jumatano hakuna mnada, Oktoba 28, 2020, mnada hautafanyika ili Watanzania waliojiandikisha wapate nafasi ya kupiga kura", amesema RC Mtaka.

Kwa upande wake, msimamizi wa uchaguzi majimbo ya Maswa Magharibi na Maswa Mashariki mkoani Simiyu, Fredrick Saganiko, amewaapisha wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi watakaohudumu zaidi ya vituo 500 majimbo hayo, kisha akahimiza uchaguzi ufanyike kwa haki, utulivu na amani.
 
Haswaa,,, tena na Rais atangaze siku ya kupiga kura ni siku ya mapumziko.ili wananchi tukampe kura za kutosha kipenzi cha watanzania John Pombe Magufuli.
 
Safari Watanzania tuna jambo letu juu ya msaliti wa Nchi kutoka ubeligiji.
 
Usaliti wa Lissu ni upi... Mnajua kabisa mlivyomlipua kwa marisasi na kuperekea yeye kwenda kupigania uhai wake huko ugaibuni.. So usaliti wake ni upi
 
Safari Watanzania tuna jambo letu juu ya msaliti wa Nchi kutoka ubeligiji.
Usaliti wa Lissu ni upi... Mnajua kabisa mlivyomlipua kwa marisasi na kuperekea yeye kwenda kupigania uhai wake huko ugaibuni..

So usaliti wake ni upi na kama msingempiga Marisasi asingekwenda nje ya nchi...Mkamnyima matibabu na Kumstipu Ubunge... Tunajua na Mungu anajua mlichomfanyia..
 
Kaka huwezi kutoa hukumu kwa kitu usicho na ushahidi

Pia kutandikiwa risasi sio kigezo cha kuwa kiongoz,ungekuwa hivyo Majambazi yote yangekuwa viongozi kwani nao wamekumbana na hayo majanga
Usaliti wa Lissu ni upi... Mnajua kabisa mlivyomlipua kwa marisasi na kuperekea yeye kwenda kupigania uhai wake huko ugaibuni.. So usaliti wake ni upi na kama msingempiga Marisasi asingekwenda nje ya nchi...Mkamnyima matibabu na Kumstipu Ubunge... Tunajua na Mungu anajua mlichomfanyia..
 
Usaliti wa Lissu ni upi... Mnajua kabisa mlivyomlipua kwa marisasi na kuperekea yeye kwenda kupigania uhai wake huko ugaibuni.. So usaliti wake ni upi
Huo huo usaliti ndiyo uliyopelekea akaripuliwa marisasi.kwani hukumbuki alikuwa aki-mfeed iformation yule mkulima aliyezikamata ndege zetu. Au hukumbuki wakati JPM anakamata makinikia bandarini jamaa alipiga kelele kuwa tutafilisiwa na akawa mstari wa mbele kuwashinikiza Barric watushitaki. Huyo msaliti na shoga mwenzio mpe kura wewe mwenyewe.
 
Kwa hiyo kumbe unawajua walimpiga risasi? ('akaripuriwa marisasi')
Kumbe jeshi linatakiwa linanzie nawe kwani unajua kila kitu!
 
Back
Top Bottom