Simiyu: Miradi ya TASAF yatakiwa kukamilika kabla ya mwezi Machi 2025

Simiyu: Miradi ya TASAF yatakiwa kukamilika kabla ya mwezi Machi 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) umewataka wataalamu wanaosimamia miradi ya kupunguza umaskini kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini awamu ya tatu (TASAF III) Mkoa wa Simiyu kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kabla Machi 2025.

Mbali na miradi hiyo kukamilika, mfuko umewataka watalaamu hao kuhakikisha miradi hiyo inasimamiwa kwa ukaribu zaidi ili iweze kusajiliwa kabla ya muda huo kuisha na kuanza kutumika.
Wito huyo umetolewa na Ofisa Mtalaamu wa Ufuatiliaji kutoka katika mfuko huo, Emmanuel Macha alipowaongoza wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Uongozi wa TASAF kutembelea wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini awamu ya tatu katika mkoa huo.

Alisema kuwa katika taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo kwenye mkoa wa Simiyu, bado kuna baadhi ya miradi ambayo ilibuliwa na wananchi kupitia mpango huo haijakamilika utekelezaji wale pamoja na kutosajiliwa.

Aliwataka wataalamu ambao wanasimamia miradi hiyo hasa kwenye halmashauri kuhakikisha miradi yote inatembelewa mara kwa mara na kusimamiwa kwa ukaribu ili iweze kukamilika ndani ya muda huo.

“ Nitoe wito kwa watalaamu wa mkoa wa Simiyu, ambao baadhi ya halmashauri ili miradi ya kupunguza umaskini ambayo bado haijamilika kabla ya mwezi Machi, 2025 inatakiwa kuwa imekamilika na kusajiliwa,” alisema Macha.
 
Back
Top Bottom