Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Sunzula B, Wilaya ya Itilima Mkoa wa Simiyu, Bahati Suguti amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh5 milioni kwa kosa la kufanya udanganyifu katika mtihani la darasa la nne mwaka 2023.
Katika kesi hiyo iliyotolewa hukumu leo Februari 2, 2025 na Mahakama ya Wilaya ya Itilima, mahakama imewaachia huru washitakiwa wenzake watano ambao ni walimu baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao.
Hii ni baada ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Robert Kaanwa, kueleza kuwa ushahidi uliotolewa unaonyesha washitakiwa hao watano ambao walikuwa ni wasimamizi wa mitihani, hawakuhusika kutenda kosa hilo.
Source: Mwananchi