Simiyu: Ndugu wa damu wahukumiwa Miaka 20 jela kwa kosa la kuzini na kuishi kama Mume na Mke

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Screenshot 2024-08-15 122059.jpg
Mahakama ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela Mussa Shija (33) na Hollo Shija (35) miaka 30 jela kwa kosa la kuzini na kuishi kama mke na mme kwa zaidi ya miaka sita wakijua kuwa ni ndugu wa damu.

Wakazi hao wa Kijiji Cha Mandang'ombe Wilayani Maswa walihukumiwa jana Agusti 14, 2024 na Hakimu mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo Enos Misana, ambapo ilidaiwa mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao walifanikiwa kupata mtoto mmoja mwaka 2022.

Katika jinai namba 26634/2024 iliyokuwa inawakabili watuhumiwa hao ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mashitaka ya Taifa wilaya ya Maswa, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Vedastus Wajanga kuwa walitenda makosa hayo tarehe na miezi tofauti kati ya mwaka 2018 hadi Julai 2024 katika kijiji cha Mandang'ombe wilayani humo.

Chanzo: Habari Leo
 
Hii kesi ndogo sanaaa wapate wakilii mtiifu basii
 
Mambo ya kifamilia hayo wanayaingiliaje? Wamekosa kazi? Kuna mashauli luluki ya kisheria hayajapatiwa hukumu huo muda wa kudeal na family affair za watu wanautolea wapi? Wahead kabisà.

By the way hao vijana ni washenzi mno, ndio wanaletaga laana za familia.
 
Back
Top Bottom