LGE2024 Simiyu: Upigaji kura wasifiwa kwa kwenda kwa amani na utulivu

LGE2024 Simiyu: Upigaji kura wasifiwa kwa kwenda kwa amani na utulivu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Wajumbe wa Kamati ya Amani Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Kaimu Shekh Issa Kwezi, wameeleza kuridhishwa na zoezi la upigaji kura lililofanyika jana Novemba 27, 2024.

Shekh Kwezi amesema kuwa ulinzi na usalama viliimarishwa, na wapiga kura walienda vituoni kupiga kura kwa utulivu bila kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani.

Amesema dosari ndogo zilizojitokeza, kama majina kutopangwa kwa mpangilio wa alfabeti, zimetambuliwa na kuomba zishughulikiwe katika chaguzi zijazo.

Katika hatua nyingine, wajumbe hao wamesifu mazingira rafiki yaliyowekwa kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalumu kwenye vituo vya kupigia kura.

Pia soma: LGE2024 - Special Thread: Maoni ya Wananchi na Taasisi juu ya Mwenendo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa baada ya matokeo kutangazwa
 
Back
Top Bottom