KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Ametoa rai hiyo alipozungumza na watumishi hao katika Mtaa wa Benki Wilayani Bariadi katika muendelezo wa zoezi la kuhamasisha Watumishi wa Taasisi za Serikali na Binafsi Mkoani Simiyu kujitokeza kujiandikisha.
Amewataka watumishi hao kutochanganya zoezi la maboresho ya Daftari la kudumu la Wapiga kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu na Daftari la wapiga kura za viongozi wa Serikali za Mitaa.
Amewataka pia kuwa mabalozi wa kuhamasisha Wananchi kujitokeza katika vituo vya kujindikisha ili waweze kuwa na sifa ya kupiga kura kuwachagua Viongozi wa Serikali za Mitaa.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Rais -TAMISEMI uchaguzi wa Serikali za Mitaa Nchini utafanyika Tarehe 27 Novemba 2024.