Mshambuliaji wa Timu ya Tanzania “Taifa Stars”, Simon Happygod Msuva ameifikia rekodi ya Mrisho Ngassa ya kufunga Magoli 25 katika timu hiyo na hivyo kuwa wachezaji waliofunga Magoli mengi ngazi ya timu ya Taifa.
Msuba amefikia rekodi hiyo kwa kufunga kwa njia ya penati katika mchezo uliomalizika kwa sare ya Goli 1-1 dhidi ya Uganda wa Kundi C katika Michuano ya AFCON inayoendelea Nchini Morocco.
Pia, jumla Msuva ambaye amewahi kupita katika Klabu za Azam FC, Yanga, Wydad C kwa sasa anaitumikia Al-Talaba SC amefunga Magoli matatu Michuano hiyo ya AFCON.