Simplify your life | Rahisisha maisha yako

Simplify your life | Rahisisha maisha yako

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
5,500
Reaction score
8,060
Je, una malengo?

Kama unayo, basi jaribu kurahisisha maisha yako.

Kivipi?

Jaribu kupunguza mambo ambayo yataathiri hayo malengo yako.

Mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine hayana mchango wowote ule katika malengo uliyojiwekea.

Mambo kadha wa kadha ambayo uwepo wake katika mwenendo wa maisha ya mtu ya kila siku ni kichocheo cha kuyaharibu malengo yake.

Mambo ambayo uwepo wake katika maisha ya mtu ni kisiki cha kujikwaa na hatimaye 'kuanguka' kimaisha.

Mambo hayo ni 'mzigo mkubwa' na 'mzito sana' tena kupindukia kwa sababu muda wote yanapambana na kuhakikisha kwamba unashindwa kuyatimiza malengo yako.

Bila shaka kila mmoja anajua na anayafahamu, ni mambo gani yanayojaribu kuyawinda "kwa udi na uvumba" malengo yake.

Kama unafahamu hilo basi rahisisha maisha yako.



Always
THE GREAT
 
Japo huu ushauri umechelewa sana lakini nitauzingatia huko niendako maana huko nyuma nimeharibu sana
 
Hakuna jambo gumu kuamua kama i.e kununue gari, kununua Iphone XS Max na kujenga nyumba hapo hapo...muda wa kujenga nyumba umefika na kwa wakati huo huo unataka uwe na ndinga kali..ya kulia bata haswa ukizingatia ujenzi wa nyumba waweza chukua mwaka 1-2 kwa wale wenzangu wa kudunduliza hela..
 
Back
Top Bottom