Simu inanidhuru

peri

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
2,579
Reaction score
1,164
Kichwa cha Habari chahusika.

Nikiweka simu sikioni kuongea hatakama ni kwa dakika 2 tu Kichwa kinauma sana na mpaka sikio linauma. Yapata wiki sasa tangu nianze kupata hili tatizo.

Zamani nlikuwa nikiongea kwa muda mrefu kama nusu saa ndio nasikia maumivu ya kichwa japo hayakuwa makali kama sasahivi. Kazi yangu inanilazimu kuongea na simu mara kwa mara hivyo imenilazimu wakati mwingi niwe naweka loud speaker japo wakati mwingine nashindwa kutokana na mazingira na maongezi yenyewe.

Nashindwa kujua hasa sababu ya tatizo hili na namna ya kukabiliana nalo. Sijajua kwasasa niende hospitali gani kwani hospitali nyingi kwa ufahamu wangu hazina utaalam wa mambo ya mionzi.

Naamini ntapata msaada na mawazo mazuri.

Natanguliza Shukran.
 
Wewe ni mpenzi wa earphone? yaani kusikiliza radio na mziki kwa earphones? ni hatari sana hii kitu maana nyingi (sio zote) hazina ubora kabisa.

Pili ili kusaidia hilo tatizo lako kwasaa jitahidi au jifunze kutumia Loudspeaker, au ikishindikana hio hakikiksha simu yako unapunguza sauti. Yaani unapoongea na mtu uwe unasmikia at least kwa mbali kidogo sio sauti kuuuubwa hadi majirani wanasikia kila kinachozungumzwa na upande wa pili huku simu umegandamizia sikioni.

MUNGU akuponye
 
Tumia external loudspeaker yaani kama upo ndani ya chumba basi ukipigiwa inasikika chumba kizima na ukipokea hutakiwi kushika simu wewe unaongea tu na yeye anakujibu, hii ipo pia kwenye magari. Sijuwi bei za hivyo vifaa ila ukiwa interested niambie naweza kukupekulia sehemu
 

mimi sio mpenzi wa earphon japo huwa nazitumia mara chache. Nashukuru kwa kunizindua mkuu, nlikuwa nafikiria kuzinunua ili niwe natumia kama mbadala wa tatizo langu.

Vipi kuhusu Bluetooth devices za kuvaa sikioni, zina madhara au zinaweza kunisaidia?
 

nashukuru mkuu kwa ushauri mzuri, tatizo mazingira ya kazi hayanipi nafasi ya kufanya hivyo.
Napokuwa nyumbani au sehemu private Ndio natumia loudspeaker.
 
pole sana na ni vema wakati unasaka hospitali ya kwenda ni bora ukachukua taadhari ya kupunguza ama kuacha kutumia simu pia inapolazimu kutumia simu tumia kusikiliza kwa sikio la kushoto kwa wanavyoshauri wataalamu
 
pole sana na ni vema wakati unasaka hospitali ya kwenda ni bora ukachukua taadhari ya kupunguza ama kuacha kutumia simu pia inapolazimu kutumia simu tumia kusikiliza kwa sikio la kushoto kwa wanavyoshauri wataalamu

nashukuru kwa ushauri mkuu.
Nilikiwa sijui tunapaswa kutumia sikio la kushoto japo kwangu hata Nitumie sikio la kushoto bado naumia.
 
pole sana mkuu simu zina athari kubwa sana jitahid kuonana na docta
 
Asante mkuu, tatizo Sijajua hata hosipitali ya kwenda.
Mkuu unapaswa kuchunguza simu yako,simu zngne zina kiwango kikubwa cha radiation hivyo huathiri mfumo wa sikio,bonyeza*#06*IMEI number ya katikati ndo kiwango cha ukubwa wa mionz,inatakiwa iwe 0 mpaka 3,zaid ya hapo majanga jaribu kubadilisha simu tumia Nokia za kawaida zenye tochi hizo shida utasahau!
 

mkuu unachosema ni kweli?
natumia Samsung Galax s 2 na Nokia express music zote nimeangalia hiyo kitu unayosema inaonyesha no ya katika ni 4. Kuna ukweli katika HILO?
 

Kuna thread ilikuwa inajadili hivyo vitu, inasemekana bluetooth si salama.
 
Last edited by a moderator:
nashukuru kwa ushauri mkuu.
Nilikiwa sijui tunapaswa kutumia sikio la kushoto japo kwangu hata Nitumie sikio la kushoto bado naumia.

Jizoeshe kutumia message, watu wako wakikuzoea tu itakuwa kawaida sana, simu sikioni ni hatari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…