Simu ipi kati ya Samsung S Series from S10+ na Iphone kuanzia XR inakaa sana na Chaji?

Vipi kwenye Maduka ya K/Koo
 
Vipi kwenye Maduka ya K/Koo
Ngumu sana Mkuu hasa kwa hizo s20 FE na iphone 11 Na hawaaminiki hata kidogo.

Kama umewahi nunua refurb online zinakuwa na ratings tofauti unakuta simu moja inauzwa Dola 100 mpaka 300 kutegemea na ukubwa wa tatizo, hivyo wabongo sisi tunapenda bei rahisi rahisi atanunua hio ya dola 100 aje akupige.

kama una mtu unamjua uhakika kariakoo unaweza kujaribu bahati yako.
 
Mkuu achana na refurbished.... kwa pesa hiyo tafuta samsung mpya amabayo sio refub ..


Niliwahi tumia Samsung galaxy A30 charge siku nzima inakaa na matumizi ni heavy kabisa! Na kama nikitumia wifi bila kuwasha data huwa inakaa zaidi,

Kuna samsung mpya zimetoa hivi karibuni zifualtilie mkuu...

Unaweza ukachukuwa simu ya bei kubwa sana lakini kumbe specifications unazozihitaji ni za kiani

Achana na hizi iphone refurb!!
 
Ahsante Mkuu. Ngoja nifanye online purchase kwa Amazon. Japo ikitokea wakaniletea simu ikasumbua ndani ya mda mfupi sijui ntaipeleka wapi!!
 
Nilichojifunza kwenye ununuaji wa simu ni kwamba, raha ya simu nunua mpya. Mambo sijui ya Refurbished au Used ni kulazimisha matatizo na gharama zisizo na msingi. Kama unataka kitu na huna pesa ya kutosha kwa wakati huo ni bora usubiri tuu au nunua kipya kulingana na budget yako.
 
Yaani unakuta watu wanaongelea simu wewe unataja A30 are you serious?
 
Kwa bajet yako iyo chukua Motorola edge utakuja kuniunga mkomo na utaleta mlejesho
 
Mkuu kwa hiyo return policy, maana ake hata kama simu ni mbovu hairudi. Na mbona shipping cost ni kubwa sana. Mfano hiyo ni bei ya Renewed S10+ $268 lakini shipping cost ni $101 jumla ni Abt $371. Is it fair mkuu. Nipe final advice
 
Au hiyo return policy ni kwa options ya hzo accessories tu, cyo cm!!!
 
Yes walivyo andika hapo huwezi kuirudisha hio simu kama ni mbovu.

Na unapo nunua vitu USA huwa tunatumia service za ku forward mzigo, unatoka Amazon unaenda kampuni ya ku forward then wao ndio wanakuletea huku Tanzania.

Zipo kampuni Nyingi mitaani unaweza hata ukamtumia Mwl humu jukwaani kama huna uzoefu. Mimi natumia Aramex wapo karibu na ocean Road Mjini pale unaweza watembelea, cost yao ni kama $15 nusu kilo toka USA mpaka Hapa Tz.
 
Mkuu hivi hakuna namna ya kujua Refurbished lakini OG nikachulia hapa hapa Bongo kwetu. Maana wengi wanakubali ku-install app ya kucheki info. Au nazo tiyari zishachakachuliwa kiasi kwamba zitaleta same info kama za GSMArena but fake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…