Kwakuwa wewe mwenyewe umeona maranyingi ni rafiki zake wanapiga na hapokei, hapo kunaweza kuwa na mambo kadhaa kama:
1) Kawaahidi rafiki zake wataonana baadae, unajua tena washkaji hivyo akiwa
nyumbani anaghairi kutoka na kutopokea simu.
2) Inawezekana anadaiwa, maana watu wanaodai wanajua kweli kukumbushia
madeni yao.
3) Labda ni mwanamke anapiga ila amehifadhi(save) namba ya simu kwa
kutumia jina la rafiki yake/zake unaowajua.
Mweleze wazi kuwa iyo hali inakukera halafu uone atafanyaje pia mshauri kama hataki kupokea simu akiwa nyumbani atoe sauti.
Ni vizuri kila mtu akawa hana tabia ya kugusa simu ya mwenza wake, maana mara nyingi utahangaika kupekua na kupata presha za bure. Pia simu ya mkononi ni ya mtu binafsi siyo watu.
Hamna kitu kizuri kama wanandoa/wapenzi kutokupekua vilivyoandikwa ndani ya simu ya mwenza wako JAPO ni gumu sana kutekeleza hili.
Za leo wa ndugu, naomba kuuliza je ni fanye nini na tabia ya mume wangu kuhusu simu(mobile phone) Kwa kweli ni jambo lililokuwa likinisumbua kwa mda mrefu sana. My hubby anatabia ya kutopokea simu sometimes, yn cmu yake inaweza kuuita kwa mda mrefu bila yeye kupokea. Then, hasemi ni nani anakaa kimya tuu! Ila kwa investigations zangu mara nyingi huwa ni rafiki zake wa kiume. Je nivema kuwa namuuliza kuwa ni nani au je ni vipi watu huu behave wanapoishi wawili katika maswala ya simu. Maana sipendi kukwazika na sipendi kumkwaza pia.
Asante sana ndugu, yani ushauri wako huo wakutoa sauti nilikuwa sina kabisa. Na kuhusu no. ya demu kusave kama ni jamaa yake, hapo uhakika ni nnao maana hata mimi kabla ya kuolewa (enzi za usichana wangu) nakumbuka niliwahi kumfanyia jamaa mmoja hivyo maana hakuwa na muelekeo wa mapenzi na mimi na akawa na wivu. So that trick is in my finger tips. Stay blessed.
Kwakuwa wewe mwenyewe umeona maranyingi ni rafiki zake wanapiga na hapokei, hapo kunaweza kuwa na mambo kadhaa kama:
1) Kawaahidi rafiki zake wataonana baadae, unajua tena washkaji hivyo akiwa
nyumbani anaghairi kutoka na kutopokea simu.
2) Inawezekana anadaiwa, maana watu wanaodai wanajua kweli kukumbushia
madeni yao.
3) Labda ni mwanamke anapiga ila amehifadhi(save) namba ya simu kwa
kutumia jina la rafiki yake/zake unaowajua.
Mweleze wazi kuwa iyo hali inakukera halafu uone atafanyaje pia mshauri kama hataki kupokea simu akiwa nyumbani atoe sauti.
Ni vizuri kila mtu akawa hana tabia ya kugusa simu ya mwenza wake, maana mara nyingi utahangaika kupekua na kupata presha za bure. Pia simu ya mkononi ni ya mtu binafsi siyo watu.
Hamna kitu kizuri kama wanandoa/wapenzi kutokupekua vilivyoandikwa ndani ya simu ya mwenza wako JAPO ni gumu sana kutekeleza hili.
Hizi simu ni kama shetani hivi,, you will be tempted to scan thro your partners phone just to be sure or kama vijitabia vyake vinakupelekea kumshuku...
Aunty Lao; Hawa wababa ukiwafuatilia sana unaharibu afya yako. Ikibidi na wewe anza kuwa busy na simu yako hasa jioni na usiku, mwambie hata shoga yako awe anakupigia usiku wa manane halafu pokea simu na ukimbilie bafuni kuongelea. Ikiwezekana anza kutoka siku za week end peke yako au na shoga yako (toka mchana) umwonyeshe kwamba huna time naye. Au pale anarudi nyumbani kama ni jioni basi akukute umeulamba na unamwambia unadharula kidogo unatoka, Uone naye kama roho haitamdunda. Hiyo inaweza kumfanya aanze kuwa karibu saana nawewe (jaribu tu). Hakuna dawa mbadala au solution katika haya tunajaribu tu. Nakutakia kila la heri
Masuala ya kujibu simu yanaleta maswali yake. Kwa mfano kama mko na mwenzi wako unakuta simu inaita halafu anakuacha anaenda mbali kidogo kuongea ila ukiwa mdaku ndio matatizo yanapoanzia. Ni vyema ukajifanya huna habari kama alikuwa anaongea na mtu usipate pressure bure. Akipenda atakueleza mwenyewe. Jaribu kutojihusisha sana na simu ya mwenzi wako.
Ndugu yangu, hali hiyo kwangu tayariinafahamiak kwani nami pia some times huwa sipokei simu...lakini kwangu mara nyingi inatokea kama na fahamu issue ni nini na sina hoja za kuwwwweza kumlidhisha mtu, so kwa upande wako nadhani kasumba hiyo ni ya kawa kwa wanaume, wanaphichology wanasemaga kuwa you ladies are more smart na ni wastaarabu zaidi kuliko sisi wanaume, ndio maana inakukela. Namshukuru Mungu kuwa tayari ni mume wako lakini ingekuwa washikaji tu moja anaweza kudhani kuwa jamaa anamshikaji mwingine, so ningekusihi uongee naye tu na kumwambia kuwa ustaarabu wa kupokea simu ni kitu kizuri kwa marafiki au wapenzi. Atakuelewa tu dear, ikiongea naye pole pole
...Huku nilipo norway kwa kweli bado nimgeni sijapata mashoga bado.
...hao mashoga ndio waogope sana tu! Rafiki wa kweli ni yule atayekwambia 'usinyimwe usingizi kwa "kelele za mlango" ' kwani mumeo unaye hapo ndani- nyumbani!
Bora uwe mbogo(mkali) na mashoga zako kuhusu mumeo.
mashoga zako ni rafiki zako tu,wasizoee 'shemeji' wala nini...marafiki wabaya sana!
ukiwapata mashoga huko uwe mwangalifu!
Mbuu ndugu yangu, asante kwa ushauri. Ila methali yako au niseme msemo wako sijui, wala sijauelewa kakangu. Hebu nifafanulie mweee!