"Simu ya ajabu "

"Simu ya ajabu "

IamBrianLeeSnr

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
2,010
Reaction score
4,179
EDD6781D-33BE-4B4D-A6A7-615C72A592BC.jpeg

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA.

Chapter 1


Kama miezi miwili hivi iliyopita nilikuwa zangu katika mihangaiko yangu nje ya jiji la mbeya.

Usiku mmoja majira ya saa nne na nusu nikiwa chumba cha kulala wageni simu ikaita mie nikajua ni wife labda anataka kunitakiwa usiku mwema kwani nilikuwa sijaongea nae muda huo.

Kucheki nikaona ni namba ngeni, huwa sina mazoea ya kupokea namba ngeni ila nikasema ngoja nipokee pengine ni wenyeji wangu wa eneo lile.

Duu!! Ikatokea sauti moja laini sana ya kike tena inaonyesha alikuwa anajiandaa kulala na anataka kuongea na mpenzi wake zile chati kama wewe unayesoma unazopenda kuongea na mpenzi wako kwenye simu... usijifanye kama hujui...

Basi nikapokea na kabla sijaongea neno akaanza " Hellow Darling siku yako imeishaje, nimekumis sana na baridi hii hope utajilinda?"

Muda huo nikawa nashangaa maana sina kazi za nje kwa muda tangu nilipooa many years ago. Basi nikaona hapa nisijifanye kuuliza jina lake wala anataka kuongea na nani nami nikaanza kula naye sahani moja.

Aiseee yule binti ana sauti yaani dunia nzima, basi tukaongea kama nusu saa na tukaachana huku yeye akilala na mie nikiwa sasa nawaza huyu binti ni wa wapi na anataka nini kwangu au katumwa kupata data kutoka kwangu na wife.

Usiku ule sikupata jibu na asubuhi nilipotaka kumpigia simu ikawa haipatikni. Nikaendelea na kazi zangu na ilipofika usiku mida ile ile simu ikaita tena na sasa nikaongea nae kwa muda mrefu zaidi ya jana yake.

Tuliendelea kuongea kwa siku kadhaa mara nikarudi zangu home na kila ilipofika mida ile ya kuongea nikajifanya natoka kwenda kupata bia moja kumbe ili niisikie ile sauti ya binti wa kwenye simu ambaye hata jina naogopa kumuuliza kwani inaonkena twafahamiana na mie naelewa kuwa ni WRONG namba.

Binti alikuwa mtata na kuwakati unaweza washa TV bila kutarajia hasa sauti na utaalamu wa maneno utafikiri ana kiwanda cha kuchapisha maneno matamu ya mapenzi mdomoni mwake.

Siku moja jioni mida ileile nikiwa najiandaa..........

Itaendelea
 
79F0D12E-D434-4120-AD9D-B21A02FDD2DE.jpeg

Binti alikuwa mtata na kuna wakati unaweza washa TV bila kutarajia hasa sauti na utaalamu wa maneno utafikiri ana kiwanda cha kuchapisha maneno matamu ya mapenzi mdomoni mwake.
Siku moja jioni mida ileile nikiwa najiandaa kupokea simu .......
ILIPOISHIA

MWENDELEZO

kupitia namba yangu nyingine ulikuja ujumbe mfupi wa maneno usemao, " Acha kuipokea simu hiyo na uondoke hapo haraka"

Kweli nikasimama na kuondoka kuelekea nyumbani huku nikiwa na mawazo mengi. Nakumbuka wakati navuka barabara kuna dereva bodaboda mmoja kidogo anikwangue tako lakini nifanikiwa kuruka upande wa pili wa barabara na kusikia sauti ikiniita.


Nikajibana nyuma ya mti ili nijue sauti hiyo inatokea wapi huku nikiwa natetemeka na mkojo ukinibana. Sauti ile ikaita tena "DoonyBi!! DoonyBi!!! mbona umeondoka bila kulipa bili na bia zako umeziacha?"

Aaaah shit, kumbe alikuwa ni dada aliyenihudumia vinywaji nikagundua sikumlipa fedha yake hivyo nikampa na kumdanganya nilikuwa nataka kuongea na simu moja ya siri ili nije huko....

Yule dada akanitania na kusema, " mmmh haya naona kama kawaida yako mzee wa vilongalonga ... mkeo atakufuma iwe noma" sikumjibu kwani muda huo akili ikiwa imejawa na wasiwasi na uoga kutokana na ile meseji.

Nikatembea kama hatua ishirini na kusimama kisha nikajihoji, " Yaani mimi mwanaume wa shoka, mkakamavu niogope sms ???"

Nikaifungua na kuisoma tena kwa ujasiri kisha nikafanya maamuzi magumu na kurudi bar na kuzinywa zile bia na simu nikazima......

Baada ya kutosheka kunywa nikaamua kuanza kurudi nyumbani.
Kwa kuwa sikuwa na saa na nilitaka kujua muda wakati huo ikanibidi niwashe simu ili kujua muda.

Kabla sijamaliza kujua kama ni saa saba na dakika ngapi iliingia meseji moja ya kutisha sana.

Kutokana na ule ujumbe nikatupa simu chini huku nikihema juu juu kama mwizi aliyeponea kiberiti cha moto....

Nikakimbia hatua tatu mbele lakini nikakumbuka thamani ya ile simu yangu nikarudi.

Nikatazama huku na kule nione kama kuna mtu aliniona huku kijasho cha usiku kikinitiririka kisha nikaiokota na kuipukuta simu yangu ili nisome vizuri ile text.
 
7C3BE491-026E-4794-AE74-FB98CF4A3975.jpeg

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Chapter 3

Soma mwendelezo wake


ILE TEXT ILIANDIKWA HIVI, " Unajifanya mjanja?? utaona" kwa kweli nilishtuka sana, moyo wangu ukaanza kwenda kasi kiasi cha kwamba nilihisi muda wowote naweza nikapoteza fahamu..

Nilijiuliza mambo mengi sana kichwani mwangu hivi nipo ndotoni au nipo katika ulimwengu wa kweli?. Fahamu zilipokuja kunirudia nikajikuta karibu na mlango wa nyumbani kwangu.

Ghafla nikasikia sauti kutoka kwa mke wangu ikiniuliza, " Mbona umesimama muda mrefu sana hapo ukiwaza, kuna nini?" Nikajibaraguza kwa kucheka na kumshika mkono na kumvuta karibu na mpaka wa eneo la nyumba yetu.

Nikamwambia, "Unajua nini mke wangu? majirani zetu wote nyumba zao zina mageti, kasoro sisi tu. hili suala linanisumbua sana akili yangu, hasa nikiwaza kuhusu ulinzi.

Unakumbuka kazi niliyoenda kufanya kule Iindi? Pesa nitakazopata kule nitaweka ukuta na geti ili bwana wale wanakumendea mendea niwakomeshe........ Tukacheka na kushikana mikono na kuingia ndani lakini kichwani mwangu nkitafakari kuhusu ile meseji.... " Unajifanya mjanja?? utaona"

Asubuhi yake nikiwa ofisini nikakumbuka kuwa nilitakiwa kujibu email za ofisi hivyo nikaiwasha laptop yangu na kuanza kuzipitia emails kwenye akaunti yangu.

Moja kati ya email niliyokutana nayo wakati nasoma ilinipa mshutko mkubwa sana kiasi cha kwamba sikuweza kuendelea kuzisoma zile email nyingine.

Tumbo la kuhara likanibana na nikakimbia haraka kwenda chooni na kurudi haraka.

Mhudumu wa ofisi akanitania kaka mbona leo shuzi zako kali hivyo? sikumjibu nikajifanya kutabasamu na kuingia ofisini kwangu nakuanza kuisoma ile email vizuri.

Email ile iliandikwa hivi "washa simu yako nakutafuta" nilizidi kuchanganyikiwa kwani hadi nafika ofisini kwangu simu yangu ilikuwa nimeiwasha......!!! sasa nikajiuliza maswali mengi sana simu yangu imejizimazimaje na muda gani ilijizima wakati ilikuwa na full charge?

Pia huyu aliyenitumia email ni nani?na nilipojaribu kureply ile email ilikataa,na nilipo rudi kuiangalia tena ili nisome imetoka kwa nani,cha kushangaza na cha kuogopesha zaidi ile email ilikuwa imetowekaa,kwa kweli kijasho chembamba kilinitoka ingawa ndani ya ofisi kulikuwa na AC.

Sasa nikaamua kuiwasha simu huku nikitetemeka kabla sijakaa sawa simu ya ofisi ya mezani ikaita kwa sauti ya juu sana nikaruka kwa mshtuko safari hii kidogo nianguke na kutaka kugogesha paji la uso kwenye ukingo wa meza.

Sikutaka kuipokea nikamwita haraka mhudumu na kumwambia aipokee, alipoipokea waliongea dakika kama tatu kisha akanipatia na yeye kutoka nje.

Sauti niliyoisikia ilikuwa ya yule dada ambaye mara kwa mara tumekuwa tukiwasiliana naye bila kumjua jina lake. Akasema, sapraiiiz hata nimeku-miss nikaona nikupigie simu nikusalimu sina mengi nitakutafuta usiku kwenye simu yako ya mkononi kuna kitu nyeti nataka tujadili......... hakuongea zaidi akakata simu.

Niliishiwa nguvu na kuanguka chini...................................................................................................................................(nilipoanguka chini nini kiliendelea?...........................
 
895F7B0B-1140-4552-AC86-0A24AF509A6A.jpeg

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Chapter 4

ILIPOISHIA
Sauti niliyoisikia ilikuwa ya yule dada ambaye mara kwa mara tumekuwa tukiwasiliana naye bila kumjua jina lake. Akasema, sapraiiiz hata nimeku-miss nikaona nikupigie simu nikusalimu sina mengi nitakutafuta usiku kwenye simu yako ya mkononi kuna kitu nyeti nataka tujadili......... hakuongea zaidi akakata simu.
Niliishiwa nguvu na kuanguka chini.............................................................

Soma mwendelezo wake

BAADA ya kuzinduka nikajikuta nipo hospitali nikiwa nimezungukwa na ndugu na marafiki. Sikuamini nilichokiona nikafikiri nipo ndotoni.

Mke wangu akanihoji, " nini kilikukuta mme wangu? Maana nilipigiwa simu kuwa umeanguka ghafla na umeletwa hospitali na pia vipimo vinaonyesha ulipatwa na mshtuko mme wangu, Ni mshtuko gani mme wangu?"

Ingawa nilikuwa nimeshaanza kupata nguvu, kutokana na lile swali nikajifanya sina hata nguvu ya kulijibu swali maana ingenipa mshtuko wa pili hata kabla ya kutoa maelezo yake.

Jioni yake nikaruhusiwa kutoka na kurejea nyumbani.
Zilipita takribani wiki tano nikiwa nimeirushia chooni ile laini tena choo cha shimo ili nisiweze kuiona tena.
Hata kama nitapatwa na wasi wasi baada ya kukumbuka enzi za udogo wetu tuliwahi mchukia paka wetu kisha tukamshika na kumtupa katika choo cha shimo ili asiwe taabu tena kwa kunya kitandani na kwenye unga.

Lakini maajabu yake baada ya kumtupa na kuridhika kuwa yuko shimoni muda wa chakula alikuja akiwa na kinyesi yaani wote tuliduwaa na kunifanya kuwachukia kabisa paka 🤯🤣🤣🤮🤮

Lakini kwa hili niliamini kuwa ni suluhu na hata yule mhudumu wa ofisi nilimwambia asipokee simu yoyote ya kunitaka mimi private zaidi ya kuwambia wanitafute bila kuwapa namba yangu na zile za kiofisi ajibu.

Nilichukua likizo ya wiki mbili pale ofisini na kumwambia mke wangu twende nje ya mji tukapumzike na nikatumia mwanya huu kumkumbusha kuwa nilitakiwa kufanya hivyo kwa ushauri wa daktari hasa baada ya lile la shinikizo kuwa nilizidisha kazi mno.

Niliondoka na familia yangu kwenda matema nje kidogo na mji wa Mbeya huku nikiamini sasa lile tatizo limeisha.

Kweli zilipita siku tatu nikiwa pale kwa furaha na familia yangu nikiwa na marafiki wapya na simu nyingi nilizopigiwa zilikuwa ni za ndugu jamaa na marafiki.

Ijumaa mmoja usiku wa saa nne nikiwa nacheza na mwanangu huku napata mvinyo wangu mara simu ikaita kuangalia ilikuwa ni namba ngeni.

Nilipotaka kupokea tu ikakata na kwa kuwa sikuwa na muda wa maongezi na ilikuwa ni usiku nikaachana nayo.

Jumapili usiku nikiwa na mke wangu tumelala pale hotelini, simu ilipigwa tena na wakati huu iliita sana na mtu wa kwanza kuisikia alikuwa mke wangu.

Akaichukua simu na kunipatia, si wajua tena hawa ndugu zetu walivyokua addicted na simu wakijua ni michepuko.

Basi mimi nikaichukua ile simu na kuipokea kwa loudspeaker nikijiamini kuwa sina mchepuko....Ila kwa bahati mbaya mpigaji alisikika hewani ila hakuongea neno nikakata simu na kulala.

Jumatatu mchana nikiwa nimekaa pembezone mwa ziwa napunga upepo nilipokea sms iliyosema "Nitakupigia usiku" kutoka kwenye namba ile ile ya jana yake usiku.

Nikataka kupata uhakika wa kuwa ni nani huyo ambaye hawezi kuongea mchana mpaka usiku. Nikaipigia ile namba ila haikupokelewa basi sikuitilia maanani.

Nikaendea kupunga upepo pale na si wajua tena mandhari ya matema ilivyoyakuvutia? Zilipita dakika 20 nikapokea sms kutoka katika namba ile ile ikisema, " wee endelea kupunga upepo tu, nimeshakuambia nitakupigia. Huelewi nini hapo?"

Nilinyanyuka haraka na kuelekea usawa wa ziwa bila kujua naelekea wapi? Mara ghafla nikashtushwa na sauti ya mwanangu akisema babaa babaa na mimi nije kuogelea?
Ile nageuka tu nilichokiona..............
 
D8FA7FA7-F9F2-4FC7-A2E9-4946B31126BF.jpeg

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Chapter 5

ILIPOISHIA

Nilinyanyuka haraka na kuelekea usawa wa ziwa bila kujua naelekea wapi? Mara ghafla nikashtushwa na sauti ya mwanangu akisema babaa babaa na mimi nije kuogelea?
Ile nageuka tu nilichokiona..............

Soma mwendelezo wake

Ile nageuka tu nilichokiona kilinifanya nibadilishishe uamuzi wa kuelekea ziwani kwani alikuwa mke wangu akiwa na mwanetu mdogo.
Akaniita na kuniuliza, " mbona umenyanyuka haraka na kuelekea ziwani?"

"Nimepata mzuka wa kwenda kuchezea maji mama watoto" nikamjibu huku nikichezea maji ingawa kichwani mwangu akili iliniruka wakati huo.

Basi nikageuza na kuelekea upande aliokuwepo.
Ilipofika saa tatu usiku huku kichwa changu kikiwa na mawazo tele juu ya simu itakayopigwa na hamu ya kula ikiwa imenitoka na baadhi ya vyakula vikinikodolea macho nilijiuliza.

Mimi wa kunywa bia moja saa zima? Kweli mawazo yamenishika.
Muda wote nilikuwa nikiitazama simu ili kuona nini kitajiri.
Muda ulizidi kwenda na ile bia ikanizima na hatimaye kuyafumba macho yangu kwa usingizi mzito.

Asubuhi nililipoamka nikakuta missed call zaidi ya 10 na meseji moja kutoka kwenye ile namba.
Kwa kweli nilitamani nisingeamka na kuelendea na usingizi ulionifariji sana.
Wazo likanijia kichwani "haya mambo nimshirikishe mke wangu?"

Nikaona nijikaze kiume na kutoka kwenda bafuni kuoga bila kuifungua ile meseji.
Bafuni nilikaa zaidi saa moja nikiitafakari ile meseji itakuwa ina nitaka nini mimi?

Niliporudi toka bafuni nikaitazama ile simu juu ya kitanda ila wakati huu nikaifungua chupa yangu ya pombe kali aina ya grants na kuigigida ili kujiongezea ujasiri.

Nikaitazama ile simu ambayo ilikuwa muda huo kiganjani kwangu kisha nikaufungua ule ujumbe.

Ujumbe uliandikwa hivi, " acha kuendekeza pombe wewe wanaume, pombe sio chai ambayo utakunywa na maandazi ili kutatua matatizo yako kuwa wanaume wewe!!"

Duuh!!! Hakuishia hapo mstari ulionichosha zaidi ni huu uliosema hivi, " nitakupigia baadae sasa leo zima simu uone!"

Dakika kama tatu hivi wakati na itafakari hiyo sms nilisikia kelele toka nje. Nilipotoka nje nilimwona mke wangu alikuwa akiniita huku akilia kwa sauti ya kuchanganyikiwa.

Mtoto wetu alidumbukia kwenye maji na kwa bahati nzuri aliweza kuokoka baada ya msamaria mwema kumwokoa.

Hivyo basi tukaelekea hospitali kupata matibabu zaidi.
Ilipofika mida ya saa kumi jioni tukiendelea kumwangalia mwanetu nilipokea ujumbe mwingine.

Kwa kuwa nilikuwa na stress za mwanangu niliufungua ule ujumbe bila kufohia na kuusoma.
Ujumbe ule lisema, " pole baba na mjukuu, mnaendeleaje mbona simu yako haipokelewi?"

Duuuuuh, nilishusha pumzi ndefu baada ya kungundua ujumbe ule ulikuwa wa mama.

Nilipomaliza kuusoma ule ujumbe nikairudisha ile simu na kuelekea wodini kumwangalia mtoto na kumwambia mke wangu juu ya ujumbe ule.

Tukaruhusiwa muda mfupi baadae na kuelekea hotelini ambako tulipofika hotelini mhudumu wa hotel aliniita na kuniambia kuwa nina ujumbe wangu.

Ujumbe huo ulitoka kwenye namba ilele na baada ya kuzisoma zile namba nikagundua ni namba ile ile ambayo hunipigia
Ujumbe ule ulisema hivi, ...................
 
11BABB32-9AB0-468F-9428-A84F16B6442F.jpeg

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

Chapter 6

ILIPOISHIA

Tukaruhusiwa muda mfupi baadae na kuelekea hotelini ambako tulipofika hotelini mhudumu wa hotel aliniita na kuniambia kuwa nina ujumbe wangu.

Ujumbe huo ulitoka kwenye namba ilele na baada ya kuzisoma zile namba nikagundua ni namba ile ile ambayo hunipigia

Ujumbe ule ulisema hivi, .....................................................

Soma mwendelezo wake

UJUMBE usilisema hivi, " Nimekutumia vocha ya shilingi elfu 10, sasa leo naomba wewe unipigie saa sita kamilia.... USIKOSE" Sikutaka yule dada agundue kitu, hivyo nikatabasamu kwa uoga..... nakuanza kuondoka.

Kwa kuwa nimechanganyikiwa na ule ujumbe bila kujua amefahamu vipi namba ya yule mhudumu na kama haitoshi kwanini atume pesa na ni mpigie bila kukosa? na wakati yeye akipiga tu nahisi kuzimia..... nikahisi roho yangu ingeweza kutoweka muda wowote.

Wakati natafakari hayo nikashtushwa na kelele za mlango uliogongwa na mke wangu kumbe nilikuwa nimejifungia na kusahau kama nilikuwa na familia. Nikakimbia haraka na kuufungua mlango na halafu nikarudi kwa spidi kuenda katka eneo ambalo kila habari mbaya ikinikuta huwa mtetezi wangu (chooni).

Mke wangu akaanza kupatwa na mashaka kwani mara kwa mara aliona tabia yangu imebadilika na kwa muda huo nilishaingia chooni kama mara tatu.

Akaniuliza, " kuna kitu nahisi kinaendelea na hutaki kunishirikisha"

Kwanza siku hizi unapigiwa sana simu nyakati za usiku kuanzia saa sita...!!! Na ukipokea akili yako huonekana imechanganyikiwa baada ya kupokea hiyo simu.... Nini tatizo baba Imeldah?

Nikashtuka na wazo la kwanza likanijia kuwa leo saa sita usiku natakiwa kupiga simu na mama imeldah kagundua mida hiyo huwa napokea simu, sasa leo sipokei tena ila natakiwa kupiga na tena sio kwa iyari bali lazima kutokana na uzito wa ile sms na nikizingatia sifahamu ni nani haswa huwa nazungumza na yeye!

Kweli nilizidi kuchanganyikiwa kiasi cha kwamba sikuelewa tena maneno ya mama imeldah aliyoongea ghafla ganzi mwili mzima ilinizunguka.

wakati nikiwa pale Mara nikashtushwa na mlio wa simu bila kujua ni ya nani kati yangu na mama imeldah!

Nikaikimbilia na kuichukua haraka sana kukimba nayo chooni nilipofika chooni nikagundua ni ya mama imeldah nikarudi haraka na kumpa mama Imeldah kumbe ilikuwa ni ya baba mkwe akiulizia hali ya mjukuu wake.

Mama imeldah alikuwa akiongea na simu huku akinitazama na macho yake yalionesha kuwa mama imeldah hakuwa akinielewa tena wakati huo nilikuwa nikizunguka huku na kule bila kujua nini nitamjibu mama imeldah baada ya kuonge ana simu.

Baada ya kukata simu mama imeldah akachukua simu yangu na kusema sasa atakaa nayo kwa ili kujua nini naendelea nacho maana alihisi nimeanza kuchanganyikiwa ingawa hakuwahi kuikuta sms yoyote mbaya kutoka kwa michepuko.

Sikuwaza yeye kuchukua simu lakini hofu yangu ilikuwa ni ifikapo saa sita nini kingejiri.

Mida ikazidi kusogea na ilipofika saa sita kasoro dakika tano......................................................................................................

Je ilipofika saa sita maajabu gani yalitokea?
 
9931E4A0-F03B-4E20-BEE6-AE0B8841F778.jpeg

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Chapter 7

ILIPOISHIA
Sikuwaza yeye kuchukua simu lakini hofu yangu ilikuwa ni ifikapo saa sita nini kingejiri.Mida ikazidi kusogea na ilipofika saa sita kasoro dakika tano......................................................................................................

Endelea

SIKUWAZA yeye kuchukua simu lakini hofu yangu ilikuwa ni ifikapo saa sita nini kingejiri.

Mida ikazidi kusogea na ilipofika saa sita kasoro dakika tano akili ikanituma nichukue kidonge kimoja cha Valium dawa ya usingizi na kumchanganyia kwa siri katika juice yake.

Kwa kweli siku hiyo nilijifanya mwenye mapenzi ya kweli na kumjali ila moyoni mwangu nafamu nini nilikihitaji.

Basi nilimbembeleza na kumpa ile juice na kweli alikunywa na zilipita dakika kadhaa nikagundua alikuwa kalala fofofo.

Hapo nikapata mwanya wa kuichukua ile simu ili niweze kuiweka ile vocha na kuipiga ile namba.

Kweli nikaipiga ile namba ila iliita kwa dakika kadhaa bila kupokelewa na nikaamua kutoipiga tena ila kichwani nikawa na mawazo.

Wakati natafakari kwanini simu haijapokelewa na iweje nimefikia hatua kumwekea mke wangu dawa ya usingizi aina ya valium, na je ni kweli mimi ni mtu wa kuchangaywa na simu ya mtu ambaye simfahamu?

Wakati nayatafakari hayo ilikuwa mida ya saa saba usiku na usingizi ukiwa umenipotea.

Nikaamua kutoka nje na kukaa pembezoni mwa ziwa nikiwa natafakari peke yangu mambo yaliyojitojeza katika maisha yangu pasipo na jibu sahihi.

Nikiwa kwenye dimbwi la mawazo mara nikashtushwa na mkono ulionigusa niliposhtuka alikuwa ni muudumu akisema.
" vipi ndugu mbona uko peke yako usiku huu wa manane hapa nje?"

Nikamjibu kwamba, " nimeamua tuu kuja hapa nje baada ya kugundua ndani kuna joto sana.'

Mhudumu alitabasamu na kuniambia, " hili eneo ulilokaa sio salama, maana mara nyingi nyakati za usiku kuna vitu vya ajabu hutokea hivyo haturusu watu kukaa hapa mida hii"

Wakati tukiondoka kutoka eneo hilo huku tukijadili mambo mawili matatu mhudumu akagundua jambo nakusema pomoja na hayo una matatizo kaka..!!!

Kweli nikatamani nimweleze nini kinachonisibu ili nipate ahueni ila nilishindwa na kubaki kumwambia hakuna shida.

Wakati tukaribia mlango wa chumbani kwangu mara ulisikika mlio wa simu kutoka kwenye chumba cha mhudumu na ule mlio ukanishtusha sana.

Mhudumu akakimbia na kwenda katika chumba chake ili apokee ile simu
Huku nyuma akaniacha nikiwa niko kwenye mawazo sana kuwa nini kitatokea hivyo nikawa nasubiri kuona nini kingejiri kama mgonjwa aliepooza.

Kweli baada ya kupita dakika 3 nikamwona mhudumu akitoka na kuja kwangu kila hatua aliyozidi kuja kwangu tumbo langu nalo likazidi kuvurugika.

Nilitamani nikimbie ila nikavumilia na kumwacha afike. Kweli neno la kwanza alilosema lilinifanya nihisi dunia ikipasuka.
Kwani alisema hivi..............
 
4EE8B32A-6AA0-4607-A12B-8118DD541E7B.jpeg

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Chapter 8

ILIPOISHIA

Huku nyuma akaniacha nikiwa niko kwenye mawazo sana kuwa nini kitatokea hivyo nikawa nasubiri kuona nini kingejiri kama mgonjwa aliepooza.

Kweli baada ya kupita dakika 3 nikamwona mhudumu akitoka na kuja kwangu kila hatua aliyozidi kuja kwangu tumbo langu nalo likazidi kuvurugika.

Nilitamani nikimbie ila nikavumilia na kumwacha afike. Kweli neno la kwanza alilosema lilinifanya nihisi dunia ikipasuka.
Kwani alisema hivi.....................

Endelea

ALIFIKA na kusimama kwa sekunde kadhaa bila kusema neno lolote huku akiniangalia usoni kama abiria aliyebanwa na tumbo la kuhara katikati ya mbuga za wanyama pale mikumi na uwezekanao wa basi kusimama haupo.

Neno la kwanza alilolisema lilisema ,

"Umemfanya nini mkeo?"

kwa kweli nilishtushwa sana na swali hilo na kutaka kujua kapata wapi hizo taarifa?

Imekuaje wakati tukio nalifanya nilikuwa peke yangu?

Ikanibidi nimhoji kama sijui nini kinaendelea muda huo,

" Binti kwa nini umeniuliza swali hilo?

Mbona mke wangu kapumzika muda huu au unajifunza umbea?"

Na wakati huo nilijifanya kucharuka lakini wakati nimebadilisha sura maneno yaliyofuata yalinifanya niwe mpole kama paka aliyemwagiwa maji tena ya baridi sana!

Binti alisema hivi,
" Simu niliyopokea imeniambia kila kitu kuhusu wewe"

Majibu haya yalinishtua zaidi na kunifanya nilegee kama mlenda wa iyunga....!!! basi bwana kila kitu kilinibana kuanzia haja kubwa mpaka haja ndogo na jasho likaanza kulinyemelea paji la uso na kuona pombe zote zilizokuwa kichwani kutoweka.

Binti aliendelea kusema....
" Sauti ya kike ilisema kuwa wewe umemfanya mkeo alale ili wewe ufanye mambo yako kinyume na makubaliano yenu hivyo sasa amesema kuwa mkeo akiamka upige simu na usirudie ujinga uliofanya mbona yeye anakupigia mkeo akiwa macho?" aliongeza kusema binti yule

Daaah!! kwa kweli ukiyastaajabu ya musa utayaona ya DOONY-B basi bwana sikutaka kujadiliana naye nikatimka na kurudi chumbani haraka na kujifunika kitandani gubigubi huku nikitetemeka kama simu ya mchina.

Nilipitiwa usingizi mzito na baada ya kufumbua macho kulikuwa kumekucha na mke wangu akiandaa mabegi kwa ajili ya safari ya kurudi nyumbani.

Sikutaka kamwe kwenda kuaga zaidi ya kumwomba mke wangu aende kuwaaga kwani nilihisi nigepewa ujumbe wa kunifanya nibaki pale jambo ambalo ningeamsha malaria ambayo nilihisi ikininyemelea.

Tulianza safari tukiwa wenye furaha huku nami nikijitahidi kujisahaulisha mikasa yote na kucheza na mwanangu Imeldah huku mama imeldah akituendesha na tulipofika kiwira tulishuka na kufanya manunuzi ya vitu vya nyumbani kwani hatukuwepo kwa muda mrefu na tulihitaji pia kumsalimia rafiki yetu pale.

Muda wote huo nilikuwa nimeizima simu yangu ili kutunza chaji maana ilibaki jiwe moja na nilihitaji nikifika niandike kisa na kuweka nyuzi humu JAMIIFORUMS pamoja na kuchati na marafiki wajue niko maeneo gani.

Namshukuru Mungu tulifika nyumbani salama na huwezi amini nyumba ilikuwa chafu sana tukaanza kushusha mizigo na baadae nikamwacha mama imeldah akifanya usafi nami nikaingia bafuni kuoga na niliporudi nikachukua simu yangu ilikua ikiingia chaji na kuelekea sebuleni ili niwashe simu yangu na kuangalia TV nione yapi yamejiri kwa siku hiyo.

Nilipowasha simu ziliingia meseji kadhaa kutoka kwa marafiki zangu nikawa nazisoma moja moja na kuzijibu, laaah haula!! moja kati ya meseji zilizoingia nashindwa hata kukuambia.............................................................................................................................................

Je ni ni kiliandikwa katika meseji hiyo?
 
148973C3-52F2-4042-927B-61D5101E19CF.jpeg

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Chapter 9

Yaliyomo....

Baba Imeldah ni kijana aliyejaliwa kuwa na mke na watoto wawili na familia yake imekuwa ya furaha na amani kwa muda mrefu.

Pamoja na kuwa na furaha hiyo pia Baba Imeldah amejaliwa kuwa na mafanikio makubwa katika biashara zake binafsi na pia ni mfanyakazi wa kampuni moja maarufu sana yautafiti wa madini.

Siku moja akiwa katika mihangaiko yake binafsi nje ya jiji la Mbeya majira ya usiku akiwa chumbani mwake mara anapokea simu ngeni kutoka kwa mtu asiyemfahamu.

Mara ya kwanza ilionekana kama ni WRONG NUMBER lakini baada ya muda ulivyozidi kwenda ikaonekana kuwa sio WRONG NUMBER tena bali ni mtu anayemfahamu fika ingawa yeye hamtambui na nia yake ikiwa haieleweki.

SIMU HII YA AJABU ikanza kuipoteza furaha ya baba Imeldah na hatimaye furaha ya familia nzima, kazini mpaka jamii inayomzunguka kuanza kumwona kama mtu anayeanza kuchanganyikiwa.

Baba Imeldah anaanza mkakati wa kutatua tatizo lake na mkakati huo unamfanya baba Imeldah kujikuta anapita katika njia zenye visa vya kutisha, majaribu, vioja na heka heka nyingine nyingi zenye maumivu na kuifunza jamii.

ILIPOISHIA...

Namshukuru Mungu tulifika nyumbani salama na huwezi amini nyumba ilikuwa chafu sana tukaanza kushusha mizigo na baadae nikamwacha mama imeldah akifanya usafi nami nikaingia bafuni kuoga na niliporudi nikachukua simu yangu iliyokua ikiingia Chami na kuelekea sebuleni ili niwashe simu yangu na kuangalia TV nione yapi yamejiri kwa siku hiyo.

Nilipowasha simu ziliingia meseji kadhaa kutoka kwa marafiki zangu nikawa nazisoma moja moja na kuzijibu, laaah haula!! moja kati ya meseji zilizoingia nashindwa hata kukuambia...................................................................?

Endelea

SMS ilisema hivi,
Karibu tena nyumbani mpenzi

Macho yalinitoka kama nimeonana ana kwa ana na nyoka aina ya Anaconda, nilitetemekea sana na moyo wangu ulijawa na ghadhabu na hasira nyingi sana.

Nakujiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu, Hivi huyu ni nani na anataka nini kwangu? Katokea wapi? Namba yangu kaijuaje?

Kabla sijamaliza kujihoji vizuri maswali hayo, mke wangu alikuja pale sebuleni na kunipa chakula ambacho nilianza kula bila hata ya kuwa na hamu nacho.

Ilivyofika usiku mida ya saa mbili na nusu nilimuaga mama Imeldah kuwa natoka kidogo naenda kukutana na marafiki zangu bar ya jirani ambayo haikuwa mbali na nyumbani.

Kweli nilitoka ila nia yangu kubwa ilikuwa ni kununua vocha ili nipige ile namba na niweze kutatua tatizo langu huku nikipata nafasi ya kujua ni nani anayenipigia kila siku hata baada ya kubadilisha namba....

Nilifika dukani na kununua vocha ya mtandao mmoja unaojulikana sana kwa kutoa offer kwa wateja wake.
Baada ya kuiweka ile vocha ya shilingi elfu kumi na kujihakikishia kuwa nitapiga simu bila kukatisha maongezi yetu; nikaamua sasa kuanza kuipiga ile namba.

Simu iliita zaidi ya mara tano bila ya kupokelewa, uso wangu ulianza kushamiri furaha na kuona kama ushindi unakaribia kwani nilijua kuwa yule dada anayenisumbua ananiogopa, hivyo kwa ujasiri, kiburi na dharau nikaamua kupiga tena kwa mara ya mwisho.

Safari hii mambo yalikuwa tofauti kabisa na nilivyodhania kwani simu iliita kwa muda kidogo halafu ikapokelewa.

Mwee!! mwee!! mwee!! mwee!! niliachia shuzi moja kubwa kama bomu la nyuklia kwani nilisikia sauti ya yule dada akasema hivi.................................................................................................................

Je dada yule aliongea nini? Na nini hatma ya Baba Imeldah? ...
 
0F7FFD7D-1D8A-413C-9B50-6653E14C4A3E.jpeg

HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Chapter 10

ILIPOISHIA

Safari hii mambo yalikuwa tofauti kabisa na nilivyodhania kwani simu iliita kwa muda kidogo halafu ikapokelewa.

Mwee!! mwee!! mwee!! mwee!! niliachia shuzi moja kubwa kama bomu la nyuklia kwani nilisikia sauti ya yule dada akasema hivi..........................

Endelea

Mwee!! mwee!! mwee!! niliachia shuzi moja kubwa kama bomu la nyuklia kwani nikasikia sauti ya yule dada akasema hivi,

"Haya niambie sasa naona leo umeamua kunipigia kwani niliitegemea sana simu hii kutoka kwako"

Akaendelea kusema,

"We mwanaume umeniudhi sana kwa tabia uliyoifanya na kama utarudia siku nyingine yaani kitu nitakachokufanyia hutokaa usahau maisha yako yote"

Muda wote huo sikujibu hata neno moja nikipumua kwa chini chini mithili ya askari aliyeko vitani na kupata ishara ya adaui kuwepo eneo hilo na sikuweza kukumbuka aliendelea kuongea maneno gani zaidi ya neno la mwisho alilosema

"NAJUA KILA KITU UNACHOKIFANYA NA NITAKUFUATA POPOTE UTAKAPOENDA"

Kwa uoga nilikata simu ile na nikapata wazo la kumpigia rafiki yangu mmoja maana niliona maji yashazidi unga, na nikiendelea kuficha nikakumbuka ule msemo wa vijana usemao mficha maradhi kifo kitamuumbua hivyo nikampigia rafiki yangu aitwaye Dole Gumba Mwakibubu.

Mwakibubu ni moja kati ya marafiki zangu niliosoma nao enzi hizo nikiwa chuoni Tumaini pale iringa na nakumbuka mara baada ya kuhitimu na kupata kazi njombe na kufanya kwa miezi kadhaa alibahatika kupata ufadhili wa kwenda kusoma nje kwa mwaka mmoja.

Kwa kuwa mkewe alikuwa mjamzito wa mwezi mmoja aliamua kutafuta binti wa kazi ili asaidiane na mkewe kwa kipindi atakacho kuwa masomoni na binti yule alipatikana ingawa kwa mwonekano alionekana ni binti wa kawaida sana aliyehitmu masomo ya kidato cha nne na kukosa nafasi ya kujiendeleza.

Akiwa masomoni mwakibubu akaongezewa muda na kukaa mwaka mmoja na miezi kadhaa na siku anarudi mkewe alikuwa kijijini na yule binti wa kazi kabaki nyumbani.

Mwakibubu alishikwa na mshangao kuona jinsi yule binti alivyobadilika na kuwa mtoto mzuri tena mwenye mvuto wa ajabu tofauti na alivyomwacha.

Unajua tena mtoto wa kibongo ambaye ni kuku wa kienyeji apate bahati na akae sehemu yenye rutuba anavyonawiri!!!!.

Basi mwakibubu akamwomba penzi na binti akakataa kwa jinsi alivyokuwa akimheshimu dada yake ambaye ni mke wa mwakibubu ingawa hakuweza kumdhibiti mwakibubu kwani alifanikiwa kumwingilia kinguvu binti yule.

Binti akamwambia mwakibubu akimtahadharisha kuwa angepatwa na mkasa mzito lakini yeye kwa dharau akacheka na kuendelea na mambo yake.

Muda ulipozidi kwenda na bado mkewe yupo kijijini mwakibubu akaanza kugundua boxer zake zinapotea mle ndani kimiujiza na baada ya kushindwa kuvumilia akamuuliza yule binti.

Mwakibubu kidogo azimie baada ya kujibiwa na yule binti kuwa boxer hizo amezichukua na kazituma kwa babu yake huko sumbawanga kwani babu alimkataza asitembee na mtu yoyote mpaka ndoa hivyo atakayemfanya avunje ahadi hiyo lazima afanyiwe mila.

Ilichukua zaidi ya siku tisini za kutolala usingizi na kuchanganyikiwa huku akizidi kukonda bwana mwakibubu na kujikuta akimlipa fedha nyingi huyo binti ili amtumie babu yake na huyo binti ili tu mwakibubu aokoke kukumbwa na janga la kimila na mwishowe mwakibubu akaja kugundua kuwa hakukuwa na mila yoyote zaidi ya binti kufungua duka kubwa la nguo mtaa wa nne kutoka kwao kwa ufupi binti alitumia fursa ya kibunifu kujipatia mtaji.

Kutokana na kisa hicho cha mwakibubu ambacho kilitufanya tumcheke sana na kumwona ni zube lakini wakati huu nikaona kuwa yawezekana visa vyetu vinaendana nimfuate ingawa mimi simwoni adui yangu na mpaka sasa sijui anataka nini na uwezo wake wa kutambua ratiba zangu anautoa wapi na kwa namna zipi?

Nilimpigia simu ili nimweleze yanayonisibu na nakumbuka tuliongea kwa muda kisha tukakubaliana tukutane ili nimweleweshe kwa undani zaidi.

Basi tukakubaliana tukutane maeneo ya forest na kwa kuwa ni jirani na Gracious House of Cakes, tukaona ni vyema tukutane hapo na maongezi yaendelee huku tukitafuna cake na bisi kuyafanya mazungumzo yetu yanoge zaidi ingawa kwangu bado nilikuwa naona kama natazama filamu tena ya kihindi..

Mwakibubu aliwahi kufika pale na nikamkuta akiwa tayari akinisubiri na maongezi yetu yakaanza kwa mimi kumsimulia kisa kizima tangu sekeseke hili linaanza mpaka lilipogeuka na kuwa muvi ya kutisha na kuninyima usingizi.

Alishangaa sana na kunilaumu kwa kukaa kimya kwa muda wote huo na kuniomba nimpe meseji hizo ili azisome mwenyewe na kuhakikisha maana aliona ni kama filamu, eti kudume mimi natishiwa mpaka nanusurika kugongwa tako na bodaboda kisa ujumbe wa simu????

Haikumwingia akilini.
Aliichukua simu ile na alipoifungua meseji ya kwanza alishtuka na kuniambia.............................................................................................................

Je ni nini aliniambia?

Na aliona nini kwenye hiyo meseji?

Je tatizo litatatulika au ndio mwanzo wa safari mpya ya kutisha????
 
View attachment 2460346
HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Chapter 9

Yaliyomo....

Baba Imeldah ni kijana aliyejaliwa kuwa na mke na watoto wawili na familia yake imekuwa ya furaha na amani kwa muda mrefu.

Pamoja na kuwa na furaha hiyo pia Baba Imeldah amejaliwa kuwa na mafanikio makubwa katika biashara zake binafsi na pia ni mfanyakazi wa kampuni moja maarufu sana yautafiti wa madini.

Siku moja akiwa katika mihangaiko yake binafsi nje ya jiji la Mbeya majira ya usiku akiwa chumbani mwake mara anapokea simu ngeni kutoka kwa mtu asiyemfahamu.

Mara ya kwanza ilionekana kama ni WRONG NUMBER lakini baada ya muda ulivyozidi kwenda ikaonekana kuwa sio WRONG NUMBER tena bali ni mtu anayemfahamu fika ingawa yeye hamtambui na nia yake ikiwa haieleweki.

SIMU HII YA AJABU ikanza kuipoteza furaha ya baba Imeldah na hatimaye furaha ya familia nzima, kazini mpaka jamii inayomzunguka kuanza kumwona kama mtu anayeanza kuchanganyikiwa.

Baba Imeldah anaanza mkakati wa kutatua tatizo lake na mkakati huo unamfanya baba Imeldah kujikuta anapita katika njia zenye visa vya kutisha, majaribu, vioja na heka heka nyingine nyingi zenye maumivu na kuifunza jamii.

ILIPOISHIA...

Namshukuru Mungu tulifika nyumbani salama na huwezi amini nyumba ilikuwa chafu sana tukaanza kushusha mizigo na baadae nikamwacha mama imeldah akifanya usafi nami nikaingia bafuni kuoga na niliporudi nikachukua simu yangu iliyokua ikiingia Chami na kuelekea sebuleni ili niwashe simu yangu na kuangalia TV nione yapi yamejiri kwa siku hiyo.

Nilipowasha simu ziliingia meseji kadhaa kutoka kwa marafiki zangu nikawa nazisoma moja moja na kuzijibu, laaah haula!! moja kati ya meseji zilizoingia nashindwa hata kukuambia...................................................................?

Endelea

SMS ilisema hivi,
Karibu tena nyumbani mpenzi

Macho yalinitoka kama nimeonana ana kwa ana na nyoka aina ya Anaconda, nilitetemekea sana na moyo wangu ulijawa na ghadhabu na hasira nyingi sana.

Nakujiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu, Hivi huyu ni nani na anataka nini kwangu? Katokea wapi? Namba yangu kaijuaje?

Kabla sijamaliza kujihoji vizuri maswali hayo, mke wangu alikuja pale sebuleni na kunipa chakula ambacho nilianza kula bila hata ya kuwa na hamu nacho.

Ilivyofika usiku mida ya saa mbili na nusu nilimuaga mama Imeldah kuwa natoka kidogo naenda kukutana na marafiki zangu bar ya jirani ambayo haikuwa mbali na nyumbani.

Kweli nilitoka ila nia yangu kubwa ilikuwa ni kununua vocha ili nipige ile namba na niweze kutatua tatizo langu huku nikipata nafasi ya kujua ni nani anayenipigia kila siku hata baada ya kubadilisha namba....

Nilifika dukani na kununua vocha ya mtandao mmoja unaojulikana sana kwa kutoa offer kwa wateja wake.
Baada ya kuiweka ile vocha ya shilingi elfu kumi na kujihakikishia kuwa nitapiga simu bila kukatisha maongezi yetu; nikaamua sasa kuanza kuipiga ile namba.

Simu iliita zaidi ya mara tano bila ya kupokelewa, uso wangu ulianza kushamiri furaha na kuona kama ushindi unakaribia kwani nilijua kuwa yule dada anayenisumbua ananiogopa, hivyo kwa ujasiri, kiburi na dharau nikaamua kupiga tena kwa mara ya mwisho.

Safari hii mambo yalikuwa tofauti kabisa na nilivyodhania kwani simu iliita kwa muda kidogo halafu ikapokelewa.

Mwee!! mwee!! mwee!! mwee!! niliachia shuzi moja kubwa kama bomu la nyuklia kwani nilisikia sauti ya yule dada akasema hivi.................................................................................................................

Je dada yule aliongea nini? Na nini hatma ya Baba Imeldah? ...
Kila tukio lazima uachie Shuzi au uharishe![emoji1787] Ila story tamu sn mkuu.
 
Back
Top Bottom