Simu yangu ya Kichina - naomba msaada

Simu yangu ya Kichina - naomba msaada

nguvumali

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2009
Posts
4,924
Reaction score
1,334
Ninamiliki simu/handset moja ya kichina ina line mbili, ni handset matata sana, sasa mfumo wa sauti umejifunga...naleta kwenu wataalamu mnisaidie naweza vipi ku-restore factory settings, wakati sijui password yake ? Nokia N95....ya kichina.
 
mshikaji wangu hapo ni kununua nyingine tu,si unajua mabo ya kichina ni bomu?
 
Ninamiliki simu/handset moja ya kichina ina line mbili, ni handset matata sana, sasa mfumo wa sauti umejifunga...naleta kwenu wataalamu mnisaidie naweza vipi ku-restore factory settings, wakati sijui password yake ? Nokia N95....ya kichina.

Handset matata halafu imechemsha ??? 🙂
 
mchina jamani mchina kaja kuharibu soko la watu haya mnaojua utaalam msaidieni mwenzenu
 
Password ambayo huwa ni default kwa cmu zote kama haujawahi ku-set ni 12345 kwa simu zenye passwords za digit 5 au ni 0000 kwa simu za password za digit 4, jaribu hizo mbili, endapo utashindwa kabisa aheri uende kwa wataalamu wanaotumia softwares kurekebisha simu.
 
ASANTE KWA MSAADA WAKO wa kiufundi , ingawa haukunisaidia sana,
SASA nimeamini kweli mchina hana maana, hii simu inanitesa tangu siku ya kwanza.
acha nikaone mafundi, ila wito , achaneni na simu za Kichina.
 
asante kwa msaada wako wa kiufundi , ingawa haukunisaidia sana,
sasa nimeamini kweli mchina hana maana, hii simu inanitesa tangu siku ya kwanza.
acha nikaone mafundi, ila wito , achaneni na simu za kichina.

pole sana
 
mchina jamani mchina kaja kuharibu soko la watu haya mnaojua utaalam msaidieni mwenzenu

KIufundi na kiexperience mchina hana kosa ila ni wafanyabiashara wetu ndio wana kosa.
Binafsi nipo China almost miaka kama mitano,ila ninapoenda kununua bidhaa bei ninayonunulia mara nyingi huwa ni mara mbili ya bei ambayo kitu hichohicho kama utakinunua Guangzhou(au Tanzania),ni kwanini? Sababu kwa china kama unataka kitu cha maana lazima ujue wapi unakipata na pili si kwa bei cheap kihivyo.
Kinachotokea ni mawili,either kwa kutokujua ukauziwa kitu feki(vitu vilivyotengenezwa kwa ajili ya mafukara wa kichina wanaohitaji huduma ila hawana kipato) au Wafanyabiashara wetu kwa kutaka faida za haraka ihali wanajua ni bomu ila hawajali wakanunua vitu nya bei rahisi then wakaja kuwabambika.
So wa kuwalaumu sio wchina tu bali na hata wafanyabiasara wetu,ni mara nyingi masela wangu wamekuwa wakiniambia wanitumia pesa niwanunulie bidhaa huku,pindi ninapowaambia bei wakilinganisha na zile bidha za Guangzhou zilizopo Bongo,wanaishia kusema aah,unatuibia.

Bidhaa nilizonunua kwa ajili ya matumizi yangu binafsi kuharibika ni nadra sana na mara kama kadhaa jamaa huniambia mzee mbona hiki kitu ni tofauti na nyingine? kwakuwa najua wapi nipate nini na nalijua nasoko la china lipo vipi.

Tukirudi kwenye mada ya jamaa hapo,kimsingi hakuna NOkia yenye line mbili ambayo ni Genuine kutoka China,So kuanzia leo ukiona Nokia yenye line mbili toka China ni 100% fake,na inatengenezwa na viwanda vya uchochoroni ambavyo sio legal,huku china tunaziita(fan le) wakimaanisha simu zilizofanyiwa Reverseengineering,mfano mzuri kuna siku nilinunu Nokia E66 kwa bei ya 2500Yuan ambayo kama dola 400,na kuna jamaa yangu akanunu hiyohiyo(Fan le) kwa 700Yuan kama dola 100 hivi,Alivyoidondosha tu mambo yakaishia hapo.Kwa wataalamu ukiiangalia tu unatofautisha,ila kwa mwenzangu na mimi ni ngumu.

Wao wenyewe wanasema tunatengeneza circuit kwa ajili ya level zote,so kumbuka China bei ndiyo inayodetermine quality,Kuweni makini na hao wafanyabiashara wetu ambao ndio source ya matatizo.Mchina yupo very flexible.Sio tu kwenye Simu bali hata majengo,barabara nk

Nimeongea hivi kwakuwa ninawafahamu wachina,ninafana kazi na wachina na ninaijua china na si watetei wachina.

Nawakilisha!
 
pole sana ndugu kama unafanya factory setting kwa cm ya kichina ingiza 1122, or 1234 or 0000 ila hiyo ya kwanza ni lazima kwa cm ila itabadilisha lugha kwenda kichina na kama ina display ya touch itabidi uikalabrait ukishindwa usisite kunitafuta kwa 0713280207
 
Simu hiyo siyo genuine hivyo haina features kama simu original na ndiyo maana mnauziwa bei poa, hivyo ikiwa na tatizo lolote la software huwezi kufanya reset yoyote. Dawa ni kutupa ununue nyingine.
 
Ninamiliki simu/handset moja ya kichina ina line mbili, ni handset matata sana, sasa mfumo wa sauti umejifunga...naleta kwenu wataalamu mnisaidie naweza vipi ku-restore factory settings, wakati sijui password yake ? Nokia N95....ya kichina.

tena una bahati kuna jamaa yangu mmoja ilimlipukia mfukoni wee acha tu maka leo hataki simu hata ukimpa ya yapi
 
Wao wenyewe wanasema tunatengeneza circuit kwa ajili ya level zote,so kumbuka China bei ndiyo inayodetermine quality,Kuweni makini na hao wafanyabiashara wetu ambao ndio source ya matatizo.Mchina yupo very flexible. Sio tu kwenye Simu bali hata majengo,barabara nk

Nimeongea hivi kwakuwa ninawafahamu wachina,ninafana kazi na wachina na ninaijua china na si watetei wachina.

Nawakilisha!

Kazi ipo!
 
cm za Mchina ni balaa. jamaa alikuwa na blackberry mchina. kuigonga na mlango wa gari wakati amekaa ndani ya gari basi ikasambaa wino screen nzima. Tena zina kellele za kuudhi sana.
 
Ninamiliki simu/handset moja ya kichina ina line mbili, ni handset matata sana, sasa mfumo wa sauti umejifunga...naleta kwenu wataalamu mnisaidie naweza vipi ku-restore factory settings, wakati sijui password yake ? Nokia N95....ya kichina.
dah hiyo kitu ni rahisi sana kurekebisha, tatizo niko mbali na wewe...ningekuformatia na nikatoa hayo mapasiwedi yao...kukuelekeza kwa mdomo ni riski kwani hizo hazichelewi kuwa bomu...au ukaharibu sistimu zingine...
 
Back
Top Bottom