mchina jamani mchina kaja kuharibu soko la watu haya mnaojua utaalam msaidieni mwenzenu
KIufundi na kiexperience mchina hana kosa ila ni wafanyabiashara wetu ndio wana kosa.
Binafsi nipo China almost miaka kama mitano,ila ninapoenda kununua bidhaa bei ninayonunulia mara nyingi huwa ni mara mbili ya bei ambayo kitu hichohicho kama utakinunua Guangzhou(au Tanzania),ni kwanini? Sababu kwa china kama unataka kitu cha maana lazima ujue wapi unakipata na pili si kwa bei cheap kihivyo.
Kinachotokea ni mawili,either kwa kutokujua ukauziwa kitu feki(vitu vilivyotengenezwa kwa ajili ya mafukara wa kichina wanaohitaji huduma ila hawana kipato) au Wafanyabiashara wetu kwa kutaka faida za haraka ihali wanajua ni bomu ila hawajali wakanunua vitu nya bei rahisi then wakaja kuwabambika.
So wa kuwalaumu sio wchina tu bali na hata wafanyabiasara wetu,ni mara nyingi masela wangu wamekuwa wakiniambia wanitumia pesa niwanunulie bidhaa huku,pindi ninapowaambia bei wakilinganisha na zile bidha za Guangzhou zilizopo Bongo,wanaishia kusema aah,unatuibia.
Bidhaa nilizonunua kwa ajili ya matumizi yangu binafsi kuharibika ni nadra sana na mara kama kadhaa jamaa huniambia mzee mbona hiki kitu ni tofauti na nyingine? kwakuwa najua wapi nipate nini na nalijua nasoko la china lipo vipi.
Tukirudi kwenye mada ya jamaa hapo,kimsingi hakuna NOkia yenye line mbili ambayo ni Genuine kutoka China,So kuanzia leo ukiona Nokia yenye line mbili toka China ni 100% fake,na inatengenezwa na viwanda vya uchochoroni ambavyo sio legal,huku china tunaziita(fan le) wakimaanisha simu zilizofanyiwa Reverseengineering,mfano mzuri kuna siku nilinunu Nokia E66 kwa bei ya 2500Yuan ambayo kama dola 400,na kuna jamaa yangu akanunu hiyohiyo(Fan le) kwa 700Yuan kama dola 100 hivi,Alivyoidondosha tu mambo yakaishia hapo.Kwa wataalamu ukiiangalia tu unatofautisha,ila kwa mwenzangu na mimi ni ngumu.
Wao wenyewe wanasema tunatengeneza circuit kwa ajili ya level zote,so kumbuka China bei ndiyo inayodetermine quality,Kuweni makini na hao wafanyabiashara wetu ambao ndio source ya matatizo.Mchina yupo very flexible.Sio tu kwenye Simu bali hata majengo,barabara nk
Nimeongea hivi kwakuwa ninawafahamu wachina,ninafana kazi na wachina na ninaijua china na si watetei wachina.
Nawakilisha!