Kuweka makubaliano na mwenzio namna ya kuandika majina kwenye phone books ni jambo muhimu sana, vinginevyo, matakuwa mnajenga mazingira ya kila mmoja kupata wasiwasi juu ya mwenzie...!
Hayajakukuta wewe mimi simu ya mwenzangu sithubutu kuigusa hata siku moja ila yeye ndio huwa anaigusa niliwahi kuigusa nikalazwa kwa BP so nilishajiepusha siku nyingiiiii
mi hayajanikuta ila sidhani kama ni busara kupekua simu ya mwenzio. Kama nataka kupiga au ku-sms kutumia simu yake namwomba, nampa namba yeye ndo ananipigia. Ila mambo ya kupekua sijui sms, mara phonebook, sijui call directory..... Kwa kweli hayajaniingia bado akilini. Naona ni kama kukosa uaminifu.
We dema amsi unamdanganya huyo jamaa, asipokuwa makini jamaa huyo mke atapeleka pa baya, haiwezekani mama awe na mahusiano nje ya ndoa hadi wanatumiana meseji za mapenzi matamu namna hiyo halafu akae kimpya. Jamaa alikosea kumpa mama simu ajosomee meseji, alipaswa kumsomea huku ameshika amulize huyo jamaa ni nani asipotaka ampigie wakati mama anaona ili amjue mwizi wake. Hatuwezi kuwa na mke mmoja wanaume wawili lazima mmoja abaki naye na ningemkabidhi huyo mke jioni hiyo hapo hapo. Sasa alishakosea namshauri siku nyingine aache upole wake huyo ataletea maradhi nyumbani.
kwa nini watu wanapotosha maana ya ndoa?
sidhani kama kuna haja ya kukubaliana jinsi ya kuandika majina, lakini cha muhimu ni kuwa freee na simu zenu, mimi sioni logic ya watu wanaoishi pamoja, kulala pamoja na kila kitu ni kimoja cha kifamilia, lakini mwisho wa siku kunakuwa na usiri kwenye simu, simu za wanandoa zinatakiwa kuwa free muda wote na kwa yoyte
kaka umeongea point,hivi kweli kama siyo mumeo au mkeo nani mwingine ashike simu yako?Simu haziachanishi ndio bali tabia yako mbovu ndio huachanisha ndoa. Kama hutaki mumeo/mkeo ashike simu yako then kuna tatizo kwako
Sasa jamaa kamuosha nani?Ni vyema jamaa akaelewa ya kuwa mwosha huoshwa........................and what comes around goes around.............
huyu jamaa akisikia hivi leo hii anamuondoa kesha choka,ila kinacho muuma kampa mama mtaji wa hiyo biasharaNyongeza ya hapo kwenye bold AMEKWISHA ibiwa........jamaa aukubali ukweli huu; na sio kujipa tumaini.........na asimame kushughulikia tatizo!
hayajakufika we jisifie tu, yakikukuta hutasemaKituko, siyo kama kuna usiri katika simu. Mfano mimi, hata siku moja mume wangu hajanikataza kushika simu yake, na mara nyingi tu huwa anaiacha sehemu ambayo mimi nipo na yeye akaendelea na shughuli zake. lakini simu yake ikiita, hata kama ipo chumbani na mimi yeye yupo nje, nitaibeba na kumpelekea huko aliko. na kama sms imeingia siwezi kuisoma sababu ile simu siyo yangu......... ni kautaratibu tu nimejijengea, siyo sababu yeye hataki niguse simu yake
Kituko, siyo kama kuna usiri katika simu. Mfano mimi, hata siku moja mume wangu hajanikataza kushika simu yake, na mara nyingi tu huwa anaiacha sehemu ambayo mimi nipo na yeye akaendelea na shughuli zake. lakini simu yake ikiita, hata kama ipo chumbani na mimi yeye yupo nje, nitaibeba na kumpelekea huko aliko. na kama sms imeingia siwezi kuisoma sababu ile simu siyo yangu......... ni kautaratibu tu nimejijengea, siyo sababu yeye hataki niguse simu yake
Mwambie huyo jamaa yako aachane kabisa na mambo ya kushika simu ya mkewe atakufa na presure. Simu ni personal sana aachane nayo. Na akitaka ndoa yake ivunjike ajihusishe na hiyo simu ya mkewe hajasikia kuwa simu zimeachanisha sana ndoa? Aachane nayo kabisa[/QUOTE]
Ndoa zina mambo kwakweli!
Kwa nini simu zinaachanisha ndoa? Ni simu au tabia za watu kutokuwa waaminifu kwa wenzi wao? Ni kipi kilicho cha sili ambacho hutaki mtu ambaye unasema ni mpenzi wa moyo wako au Mke/mume toka kwa bwana hutaki akijue? Kuficha ficha huko ndo kunawafanya wengi wenu kulalama kila siku ndoa zenu zinamatatizo maaana hamna mawasiliano yaliyo ya wazi. Na hayawezi kupatikana kama kila mmoja wenu ana mambo ambayo hataki mwingine ayafahamu.
Kusema huyu ni mke/mume wangu inamaana kuna upendo wa kweli, mnaheshimiana, munajaliana, hutaki kukosea mwenzi wako na unampenda na hivyo vyake ni vyangu na vyangu ni vyake. Unavyosema kuangalia simu ya mwenzi wako utakufa na presure ni kwa sababu miongoni mwenu hamko waaminifu ndo maana unaweaz kufa na hiyo presure. Kwa nini uruhusu message za kipuuzi kuingia kwenye simu yako? Inamaana na wewe hizo message huwa unazituma na umekubaliana na tabia hiyo hata kama ni utani. Kwanini ufanye kitu ambacho mwenzi wako asingekipendelea? Utani unaoingilia masuala ya ndoa au kuyahatarisha ni bora kuliko unavyomjali mwenzi wako?
Kwangu mimi hiyo hapana, kama ni hizo message nazipiga marufuku mtu kunitumia. Utani wa ajabu ajabu huo ndo unasababisha mwishowe watu kuingia kwenye mahusiano mengine nje ya ndoa zenu. Na wengi wa watu wanapiga marufuku wanandoa wao kuangalia au kushika simu zao si waaminifu ndo maana hawataki wapenzi wao kushika simu zao.
Endeleeni kuintatain hizo tabia mtakuta mtoto si wenu tena. Ni mawazo tu
hayajakufika we jisifie tu, yakikukuta hutasema