Simuelewi Mume wangu

Story nyingine ukizisoma unashondwa kuelewa binadamu wengine akili zao huwa zinafikiria nini. Unatamani kupiga mtu makofi. Wewe unaweka hela hata haujui kama zipo au la, unaendelea kuweka tu. Eti mume wangu...Kweli kina mama kazi mnayo....hata kila siku ikiwa siku ya wanawake dunia, bado itakua ngumu kwenu kuwa sawa na wanaume.

The best way ni kila mtu kuwa na account yake. Mkitaka kufanya kitu ndo mnachangia. By the way ukiona mwanaume anafuatilia pesa za mke ujue anatatizo. Mimi mke wangu ana keep hela zake mwenyewe, anaamua mwenyewe afanye nini, ingawa ananishirikisha katika ushauri na kuboresha wazo lake. Mimi pia hivyo hivyo nafanya mambo yangu kwa uhuru kabisa. Vitu vyetu tunaandika majina ya watoto au yetu wote au kila mmoja mmoja kulingana na kitu chenyewe.
 
Account ipo kwa jina lake tu si unajua kupenda sikuona kama ni shida na isitoshe ni mume.

Pole sana kama account ipo kwa jina lake tu basi huna kitu umebaki na mume. Huyo mume wako atakuwa ameshatumia pesa ukiwa hujui jua sasa wacha kulala usingizi wa kimapenzi.
 
Reactions: Sal
ungekua binti yangu ningekushauri ufungue account yako mwenyewe na ukome kabisa kuweka pesa kwenye hiyo joint account yenu, mwache yeye aweke. Joint account zilipitwa na wakati siku nyingi sababu ya mfumo dume. Najua mnapendana sana sasa hivi ndio maana mkaamua jambo la kiungwana kama hili, lakini kwa maisha ya sasa hivi haifai. mumeo mwenyewe anaweza kukutapeli vilevile. Najua mtanitoa roho hasa wababa maana wanapenda kupewa, lakini sijali maana ukweli ndio huu.

 
Nimeandika kiswahili wewe umeona kizungu.

Step ya kumjua au kutomjua inategemea sidhani wote waliopa hapa hawamjui, kama wewe humjui wengine wanamjua.
labda wewe tu ndio unanijua ila isikupe shida sana tutaonana jioni
 
Inawezekana eeh lol!siamini kabisa kuhusu kabinti teheeee
 
Account ipo kwa jina lake tu si unajua kupenda sikuona kama ni shida na isitoshe ni mume.

Sijui nicheke au nikuhurumie. We unaweka pesa kwenye account ya mtu mwingine unasema account ya pamoja kisa ni mume na mke? Kweli unajua kupenda na hilo nakusifu. Ila ufahamu tu kuwa hiyo sio account ya pamoja ni account ya mumeo na huwezi kumlazimisha kufanya chochote hata kama pesa yote umeweka wewe peke yako. Unachotakiwa ni kumwomba tena kwa kumbembeleza.

Nakushauri kwa sasa acha ku deposit pesa katika hiyo account, fungua account yako uwe unajiwekea akiba humo wakati mnajadiliana matumizi ya pesa za mumeo (account ya mwanzo) au namna ya kubadili na kuwa na account ya pamoja yenye majina yenu wote.
 
Mwali unataka kuvunja ndoa ya mwenzako??????

Si jambo jema sana kwa wenye ndoa kila mmoja kuwa na kitu chake

Hapo ni kushauri jinsi ya kuondoa wasiwasi alionao Mke huyu juu ya account yao

Mama Sema na Mumeo ili kuweka sawa jambo hilo, Uzoefu unanionyesha kwamba Matatizo mengi kwenye ndoa huanzia kwenye PESA
Mshirikishe MUNGU, Kwa maana omba maelaekezo ya jinsi ya kulimaliza hili
 
nimefurahi kwa mara ya kwanza kuona mtu analeta tatizo la ndoa jepesi na lisilohusiana na uaminifu!nikupe tu hongera ndoa yako ni tamu na mdumu na matatizo hayo sio yale ya infidelity!am I sound crazy?
 
As long as unaweka na hela zako kwenye akaunt mwambie akuletee bank statement na ktk hili u need kuwa serious ht kama ni mumeo kwani unaweza ukawa uanaibomoa ndoa yako kwa pesa zako mwenyewe akawa anaspend na small house! Kama ni mumeo na nakupenda kweli kwa nn awe mkali ukiuliza maswala ya fedha? Something is wrong wake up!!! Usiwarudishe nyuma wanawake wenzio wanaopigania haki sawa thn ww ukawa mnyonge kisa MUME!!!
 
ucmwulize ki2 chochote tuna mpango wa kununua dowans.hatutaki m2 yoyote ajibu.mbona mke wangu hajanilalamikia?mambo mazuri hayataki haraka
 
Tupe hint ya hivyo vijisenti, vingapi?

Moja katika fitna kubwa sana ya dunia ni mali. Wacha kuweka pesa kwenye hiyo account na ili iwe salama, unaweza kuwaandikia bank wakawa wanakutumia statements za kila mwezi kwa email, na pia unaweza kuwa ni signatory na zisitoke pesa bila ya wewe kuidhinisha pia, hata kama uko mbali, siku hizi mitandao imerahisisha mambo.

Kuwa makini na mali isije ikawa ni kichocheo cha kuharibu ndoa yenu.
 
Inawezekana eeh lol!siamini kabisa kuhusu kabinti teheeee
Teh najua huwezi na mimi simaanishi kweli anako...Lol
Ila take care na mienendo yake madame...hatuaminiki wanaume
 
Shosti kumpenda sawa na usisahau kua umri unaenda na fanali uzeeni, amka mapema hizo pesa ulizoweka na yeye ziwache kama zilivyo sababu unampenda na hutaki kuliza haki yako sababu utamkera na unampenda sawa, sasa fungua account yako nyengine ufanye mambo yako <sio rahisi kujua moyo wa mtu fafanua shosti...
 
Pole dear,but next time Ujifunze..me huwa kuna baadhi ya Viungo vyangu haviaminiani sembuse mtu!sawa ni Mumeo but hujakua nae,u met with mo than meno32!..muamin Mungu wako tu!do not trust anybody in this world!
Msubir aje na umulize taratibu,na pia uwe tayari kupokea shockin news..n im sure ameshazitumia,and its a very big mistake kumtrust m2 ktk hela that way!! Next time fungua ur own account n dont tel him,hujazaliwa nae,na utakufa kvyako.umheshm kama mume bt jipende wewe kwanza.ok?
"Kiruu kwenye petha tena maee,apana kabithaaa,thimuamini mtu ki ivo kwa jina la Mungu"
 
a

sijui umeelewa mada, mdada ameweka pesa kwenye akaunti ya mmewe ila matumizi ya pesa hizo hayajulikanai, mme akiulizwa anakuwa mbogo,

Mauntana, imekula upende wako hiyo ni akaunti yake na huna access nayo, fungua akaunt nyingine uwe unatunza mwenyewe pesa, kama kuna jambo la muhimu linafanyika basi uwe unatuma kwa kiasi huku ukiulizia inatumika vip, hupati maelezo ya kutosha unasitisha kutuma, pia jitahidi uwe unatembelea nyumbani kwako ili uwe na uhakika wa kile unachokituma na kinavyotumika
 
mbona simple?
si uache kuweka pesa kwenye hiyo akaunti?
mpaka mtakapofikia makubaliano?
usije jikuta wewe unatafuta, yeye anahonga....
 
Duh! Ati pesa umemuwekea kwenye akaunti yake? Utajuaje matumizi ya hiyo akaunti na kumebaki kiasi gani??? Kwa kweli hapo sikamatiki toka nina miaka 5.
 
Mipango hupangwa kitandani mama,
mume kwanza kazi badae.

Acha kumdanganya mkuu, mipango ya maendeleo hupangiwa mezani, kitandani unaweza kujikuta umetoa ahadi hata ya kununua treni na reli yake wakati uwezo huo huna.,epuka sana mipango ya kitandani mara nyingi huwa inakuwa unrealistic
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…