simuelewi mwanamke huyu

malande

Member
Joined
Dec 31, 2011
Posts
15
Reaction score
0
wajameni nilikuwa na uhusiano wakimapenzi na mke wa jirani.kila mara huniambia ananipenda sana kuliko mumewe wa ndoa, siku moja nilimwambia kama kweli ananipenda aende akadai talaka ili tuwe pamoja .karudi kwangu anasema tayari kashapewa talaka nimuowe !!!?? simuelewi mwanamke huyu nimchukulie vipi?
 
Wewe si ulimwambia aombe talaka? Amepewa muoe sasa!
 
Yaani JF ni burudani tupu. Nimejikuta nacheka bila kupenda. Duh, hii dunia ina vituko mwanzo mwisho. Unaweza ona kama utani vile! Au story za kutunga hizi? Hata mmewe basi alikuwa hamtaki huyo mwanamke iweje ampe talaka haraka hivyo?
 
nimeingia kwenye mitaa ya akina zembwela nini...
 

>Taraka-talaka,
>Hivi ukipanda daladala k/koo-Mwenge unategemea ushuke airpot kwenye ndege?
 
Sasa huelewi nini?si ulimtuma akaombe talaka,kapewa sasa unajisahaulisha au?
 
Kama wananchi wenyewe ndo hawa, hii inji itaendelea kuongozwa na Magamba milele:A S angry:
 
Wewe ndo mwenye matatizo,unamwambia akaombe talaka anaenda halafu unajiuliza kumuoa huna maana wewe!
 
Dreva anaweza pitisha gari huko hata km ni uchochoroni

ila huweza kutokea mlango wa ndege, best utabanana apo apo mlango wa daladala..na finga za mfukon utapigwa!
Hi Erick!
 
Yani we ujaona wanawake wote duniani isipokuwa mke wa mtu.

Hivi dogo ulipokuwa mtoto ulikuwa ukinywa buluga.
 
Mchumbie tu bro., Kwakuwa amesha achika endelea kusafisha nyota kadri anavyohitaji. Naona amegundua wewe ndiye uliyeumbwa kwa ubavu wake!. pia nadhani anatosheka kuliko kule kwa mtalaka wake.
 
Duh, nimecheka sana. Ngoja niendelee kupiga ndovu zangu maana vioja jf haviishagi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…