Simuelewi

chetuntu

R I P
Joined
Jan 10, 2011
Posts
949
Reaction score
111
Habari wana jamvi la malavidavi. Naombeni mchango wenu katika hili ,niko kwenye mahusiano na kijana mmoja ila haongei ni mkimya sana hajui hata kusema asante. Hata sim zake ni za kikazi tu.marafiki anao akipiga story ni kazi au bizness. Hata kunitöngoza aliongea kidogo tu. Hata marafiki hawamuelewi. Nifanyeje ananipenda sana na me pia nampenda. Naomba mwongozo tafadhali.
 
mwongeleshe kwa nguvu....mpigie story za kutosha umfanye akuzoee....labda anakuogopa
 
Unasema haongei mbona alikutongoza na ukaelewa somo ? unampenda naye anakupenda sasa maneno mengi ya nini ? wanaoongea sana wengi ni waongo.
 
mpeleke akachangamane n watoto....ataongea tu..!!
 
kuna njia za kufikisha hisia kwa mwanamke ni kupapasa na kwa mwaname ni kumuonyesha maumbile ya kike.kwa hivyo tumia njia hiyo utamnasa tu. wengine kuongea sio njia muafaka kufikisha ujumbe tumia njia hizo,unajuaje kama anakupenda ishara imeonyesha au ulisikia kwa rafiki zake.
 
Taratibu Chetuntu,mwanaume kuongea sana si sifa nzuri....Nenda nae taratibu,akikuzoea atakuwa comfortable kuzungumza zaidi na kufanya mambo mengi na wewe.Hata kama asipobadilika,hicho si kilema,unaweza jifunza kuishi nae vile alivyo.Best Wishes!
 
It makes him a good listener. Those who yap alot sometimes do it out of lack of personality.
 
Inategemea na wewe mwenyewe kama humsemeshi unataka aanze kuimba mashairi ya kina Fid Q? anzisha somo uone atakavyojibu!!!!
 
Unatakiwa ufuate hatua... punguza pupa na uata hatua zifuatazo:-

1.Kuongea (Mmeshaanza na hiyo ni tikrti ya ninyi kuingia kwenye michezo)

2. Jua interest za mwenzi wako ( anza kuongea kutokana na interest yake)

3.Hatua muhimu kwenye mahusiano yako ni 4 ring ambazo ni (i) Engagement Ring (ii) merriage Ring (iii) Secret Ring (iv) Suffering Ring

Sasa wewe ulivyo unataka urukie ring ya mbele kabla ya ile ya awali kitu ambacho si sahihi hata kidogo!! jipange upya ili uendane na huyo kaka kama kweli unampenda kama ulivyosema wewe mwenyewe!!
 
nshakutana nae kama huyo,siku akiongea sanaaa na kucheka ujuwe anataka mchezo,mpige chini yaani wanauzi hao
 
Unataka aongee nini??? Longolongo nyingi ni wizi mtupu mkimya ndo poa hana uongo ila kaa chonjo wanakuwa na hasira hao??? Usiombe kusikia maana ataona kosa la kwanza hasemi, la pili hivyo, la tatu hivyo la nne umekwisha kama wewe ni unaongea sana jitahidi kupunguza kurap kuwa kama mwenzio hiyo ndo kusoma weakness za mwenzako!!!
 
Wanaume huwa hatuongei sana dada........... mie sa nyingine huwa nashindwa kujua akina dada hua mnaongea nini muda wote.
Unawezakuta watu wanaongea kuanzia mchana mpaka usiku wa manane. Ukiwauliza mlikuwa mkiongea nani hamna jibu la maada
 
Ukitaka aongee toka na jamaa mwingine kisha jifanye ni rafiki yako wa zamani nadhani utajua anaongea au la!
 
nshakutana nae kama huyo,siku akiongea sanaaa na kucheka ujuwe anataka mchezo,mpige chini yaani wanauzi hao

shosti acha ku generalize bwana, labda wake yupo tofauti,hebu atuambie.
 
Taratibu Chetuntu,mwanaume kuongea sana si sifa nzuri....Nenda nae taratibu,akikuzoea atakuwa comfortable kuzungumza zaidi na kufanya mambo mengi na wewe.Hata kama asipobadilika,hicho si kilema,unaweza jifunza kuishi nae vile alivyo.Best Wishes!

thanx mamaa michelle, ntaufanyia kaz ushauri.
 
Inategemea na wewe mwenyewe kama humsemeshi unataka aanze kuimba mashairi ya kina Fid Q? anzisha somo uone atakavyojibu!!!!

hata ukianzisha somo majibu ni ya mkato mno, story akichek movie tu, hata kusema ucku mwema kwake ni mtihani.
 
nshakutana nae kama huyo,siku akiongea sanaaa na kucheka ujuwe anataka mchezo,mpige chini yaani wanauzi hao

shosti acha tu , sina hata raha. Na yeye hivyo hivyo akimaliza tu busy na compture.
 

thanx kwa ushauri, jaman hata story tu za kawaida tukitoka kazini ni kimya hadi umwambie kuoga au kula . Ukimpigia sim anauliza kuna nini? Mmh jaman.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…