Sharp Observer
Member
- Apr 11, 2011
- 59
- 41
Habari ndugu mwana JF
Katika sayansi ya kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasilianao (ICT), tunapozungumzia SIMULATION tunamaanisha kufanya practical katika mazingira yasiyo halisi (virtual environment). Mfano unaweza kuwa ni kutafiti msongamano wa magari dsm na kutoa ufumbuzi wake kupitia programu za kompyuta kabla ya kuingia barabarani.
Kwa sasa kumekuwa na wimbi kubwa (hapa sina data numerali - quantitaive data) la watu wengi (wakiwemo JF members), vituo vya redio, mapadri, wachungaji, television, tovuti, magazeti n.k.; kuongelea mambo mengi kuhusu ndoa na namna ya kuzidumisha. Pia wanaongelea kuhusu malezi ya watoto.
Katika makundi hayo wapo ambao hawana ndoa (padri/sista), wengine ndoa wamevunja wenyewe (mchungaji maarufu mikocheni), vijana ambao hawajaoa/kuolewa, wanaume/wanawake ambao wameacha wake zao/wameachika kwa waume zao.
Mtu wa namna hii anapoizungumzia ndoa, anajaribu kufanya simulation ya ndoa kwa kuwa anachokihubiri ama kukieleza hakielewi kwa kuwa hakiishi (Virtual marriage). Vilevile mpaka kwenye malezi ya watoto.
Wabongo kwa vitu tusivyoweza, tukae kimya na si kueleza tu ili mradi uonekane kwenye TV, gazeti, tovuti, au tu lazima waumini wako uwaelezee, wala lazima upost hapa JF. Ila kwa wale wenye kuyaishi maisha hayo wanahaki ya kushauri, kuonya kwa sababu wanajua. Wale tusioishi maisha ya ndoa wala kuwa na watoto tuwachie wahusika wazungumze, nasi tutachota hekima toka kwao.
Nakereka sana kumsikia binti, kijana, padri, sista, mchungaji (mikocheni), na wengine wengi wa namna hiyo; kushauri kuhusu ndoa wakati wao wenyewe hawaishi maisha ya ndoa. Hiyo ni marriage simulation na haitusaidii.