Simulizi: For You

FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Luteni Jenerali Weisiko anaanza kufumbua macho yake taratibu, naye anatambua kwamba yuko ndani ya chumba fulani chenye giza kiasi. Anahisi kizunguzungu kichwani, naye anapojaribu kujishika kichwa, anatambua kwamba mikono yake imefungwa nyuma ya mgongo wake. Akakisawazisha vizuri zaidi kichwa chake na kuanza kuhisi vyema hali aliyokuwa ndani yake. Sasa akatambua kuwa alikuwa ameketi kwenye kiti cha chuma, mikono na miguu yake ikiwa imefungwa kwa kamba nene na ngumu sana, na chumba alichokuwemo kilikuwa ndani ya jengo kubwa lililoonekana kama "godown" au "warehouse." Alipozoesha macho yake vizuri ndani hapo, aliona mbao nyingi pembezoni mwa jengo hilo na vifaa mbalimbali vya ujenzi, naye akawa anajaribu kujivuta kwa nguvu sana lakini ikawa kazi bure.

Akaanza kupiga kelele akiita wale waliomfanyia hivi wafike kumfungulia haraka sana, naye akashtukia anapondwa na kopo dogo la bati la soda ya sprite, bila kumwona aliyemponda.

"Nani wewe? Jitokeze mpumbavu wewe! Unaogopa nini? Njoo!" Weisiko akasema.

Lakini hakujibiwa, bali kopo la namna hiyo hiyo likamponda tena kichwani.

"Mnataka kucheza mchezo na mimi washenzi nyie? Najua tayari kwamba ni nyie Mess Makers... hamna haja ya kujificha. Tena nawashangaa mmenifunga halafu bado mnajificha. Gut zenu zilibumbwa kwa kutumia roho za kuku, au?" Weisiko akauliza kwa kujiamini.

Akapondwa tena na kopo kama awali, naye akakasirika sana. Aliona alikuwa anafanyiwa mchezo wa kitoto, na angefanya yote awezayo ili kuukomesha.

"Mnajua nini? Hapa mnajisumbua tu aisee. Hamjui kama kunileta huku ni matatizo kwenu, kwa sababu hata kama mkifanya nini, bado mtavurugwa tu. Na ninawahakikishia, huko kuvurugwa kumeshaanza," Weisiko akasema.

"Nani avurugwe, malaya wewe?"

Weisiko akaisikia sauti hiyo ikiuliza. Ilikuwa ya mwanaume, na ilitokea sehemu ya mbele zaidi kutokea alipokuwa amekaa, na kwa sababu kwa huko palikuwa na giza zaidi, hakuweza kumwona.

"Unaogopa nini sasa kaka? Kama unaniona malaya kweli, nifate. Ukikaa huko utakulaje utamu?" Weisiko akasema kwa kejeli.

Sauti za hatua zikaanza kusikika zikimfata Weisiko, na hapo akaanza kumwona mwanaume fulani ambaye alimtambua kwa uharaka. Ilikuwa ni Victor. Akawa anamfata taratibu, huku mikononi akiwa ameshikilia makopo mengine mawili ya sprite, naye akasimama mbele yake huku akimtazama kwa makini. Weisiko akawa anamwangalia kwa hasira sana, naye Victor akamponda na kopo moja kichwani huku akitabasamu kwa kejeli.

"Ningetarajia mzee mtu mzima kama wewe uwe na hekima ya kutosha kutocheza michezo ya kitoto namna hii. Unajitafutia kifo chenye maumivu sana," Weisiko akasema kwa utulivu.

"Malaya wangu, si umeniita nije kula utamu? Nimekuja halafu unasema nacheza kitoto tena?" Victor akasema kwa dharau.

"Nifungulie basi nikupe huo utamu," Weisiko akamwambia.

"Hakuna haja ya kukufungulia. Nakuja tu kwa nyuma," Victor akasema.

Akazunguka mpaka sehemu ya nyuma alipoketi Weisiko na kuanza kumshika-shika sehemu ya makalio, naye Weisiko akaanza kumtukana huku akijaribu kujinasua.

"Ahahahahah.... utamu wenyewe wa kubabaiiisha..." Victor akamkejeli Weisiko na kuanza kumtekenya.

Weisiko akawa anatukana huku akijivuta huku na huku, na hii ikasababisha aangukie upande mmoja pamoja na kiti chake.

Victor akaendelea kucheka tu na kusema, "Hapo sasa ndiyo umejiweka vizuri. Yaani kama ni utamu nitaula wote."

Akasogea karibu na mwili wa Weisiko na kuanza tena kumtekenya na kumkandamiza makalioni.

"Naona unapata some fun," sauti ya Mensah ikasikika.

Victor akaacha kumchezea Weisiko na kusimama, akimwona Mensah anaingia.

"Yeah, ilikuwa kidogo tu upitwe. Karibu ujiunge nami, nimeahidiwa kupewa utamu hapa," Victor akasema.

"Well save that for later," Mensah akamwambia.

"Mbona umerudi?" Victor akauliza.

"Lexi amenipigia, kasema boss na akina Torres wameshamkamata Jacob kabla hawajafika kule, kwa hiyo wanarudi pia. Wanakuja huku," Mensah akasema.

Weisiko akashangaa kiasi.

"About time. Lakini... mbona kama vile wamefanya upesi sana?" Victor akasema.

"Inaonekana jamaa aliwahi kupita pale wakamnasa... tutajua wakifika," Mensah akamwambia.

Mensah akasaidiana na Victor kunyanyua kiti alichofungwa Weisiko na kukiweka sawa tena, naye Weisiko akawa anapumua kwa hasira sana.

"Mzee wa jeuri, imekupata fresh?" Mensah akamuuliza Luteni Jenerali Weisiko.

Weisiko akamwangalia kwa hasira sana, na ni hapa ndiyo watatu hawa wakaanza kusikia hatua za watu wengine wakija. Weisiko akatazama kwa makini sana mlangoni kule pasikoonekana vyema, na hapo akaanza kuwaona watu wawili aliowafahamu vizuri sana. Lakini alitambua kwamba kulikuwa na mtu wa tatu ambaye alibaki sehemu ile ya mlangoni, na hawa wawili hawakuwa wengine ila Lexi pamoja na Nora. Wakafika mbele yake na kusimama, wakiwa wanamtazama kwa umakini sana. Weisiko akaachia tabasamu la kiburi, lakini kihalisi alikuwa bado anastaajabishwa na ukweli wenyewe wa kuwa "mwanamke" huyo alikuwa hai muda wote huo ambao alifikiri hakuwepo tena duniani.

"Ama kweli... ukistaajabu ya Musa, utayaona ya mfiraji wake. Yaani sasa naamini kuna miujiza kwenye hii dunia," Weisiko akawaambia.

"Na bado," akasema Victor.

"Alexandra Casmir! Aah! Mama la mama. Umerudi kutoka kuzimu hata salamu tu ukashindwa kutuma?" Weisiko akasema.

Hakuna mtu aliyemjibu, bali wote wakabaki kumwangalia tu.

"Ahah... kikundi chenu mlichounda kwa kweli naweza kusema ni kizuri sana. Mmetupa shida, lakini mnapaswa kujua bado hamjashinda. Hata kama mtaamua kuniua mimi, bado hamtaweza kutoka ndani ya haya yote salama," Weisiko akaongea.

"Umekuwa ukisaidiana na Jenerali wako kuharibu maisha ya watu wengi. Miaka yako yote uliyotumiwa kama mbwa imekufikisha wapi Weisiko?" Nora akauliza.

"Sehemu nyingi ambazo haungeweza kuwazia binti. Na wewe hauna lolote. Ni mnafiki mkubwa, msaliti, usiyestahili kubeba jina la baba yako," Weisiko akamwambia.

"Ninafurahi sana kujua matendo ya huyo mwanaume, kwa sababu kuliondoa jina lake kwenye langu Imekuwa justified hata zaidi sasa," akasema Nora.

Weisiko akamtazama sana Lexi, akiona ni jinsi gani alimwangalia kwa chuki kali.

"Unaangalia nini? Nimejinyea?" Weisiko akamuuliza.

"Ni nini kilichokufanya ukamchukua mdogo wangu na kumwekea vitu vingi vya kipuuzi kwenye akili na maisha yake?" Lexi akamuuliza.

"Ahah... ahahahah... nilidhani ungenishukuru kwa kuahirisha kumuua mdogo wako lakini kumbe na hilo hujapenda? Unge-prefer kama ningekuwa nimemuua?" Weisiko akaongea.

"Nikushukuru kwa lipi? Kuwaua wazazi wangu na dada zangu kulikupa faida gani ambayo ni ya kudumu?"

"Kwani hujui? Kwa mambo mengi we si unajifanya mjuzi sana, unashindwa vipi kujua kuhusu hilo? Halafu... Mary nilimgeuza kuwa kile ambacho alitakiwa kuwa sikuzote, na akawa kamili zaidi tofauti na vile yeyote angetazamia..."

"Jina lake ni Azra... siyo Mary..."

"Yeye ni Mary! Ni mwanangu, na atabaki kuwa mwanangu tu!" Weisiko akafoka.

"Huyu jamaa mpumbavu sana," Mensah akasema.

"Mpumbavu ni wewe," Weisiko akamwambia.

Mensah akamsogelea na kumtandika ngumi mbili nzito usoni, naye Weisiko akahisi maumivu lakini akawa anacheka huku mdomo wake ukidondosha damu nzito.

"Ahahahah... ssss... yule siyo mdogo wako tena. Yule ni silaha yangu. Hata kama mngemfanya nini, hangeweza kamwe kukubali wewe ni dada yake. Hajui mtu yeyote zaidi ya mimi, na itaendelea kubaki hivyo upende usipende," Weisiko akamwambia Lexi.

"Kwa hiyo haukumwokoa kwa sababu ya hisia, ila tu kumfanya awe kama mwanasesere wako. Ulikuwa radhi kujiaminisha kwamba unamlea kama binti yako, ila yale yalikuwa ni majuto tu kwa sababu ulishindwa kumlea binti yako wa kumzaa mwenyewe," Nora akasema.

"Chunga maneno yako," Weisiko akasema.

"Au utamfanya nini? Yeye ndiyo alikutuma umuue wa kwako halafu uchukue wa mwingine kumlea baada ya kuwaua wazazi wake?" Victor akamuuliza.

"Mshenzi wewe! Nani amekwambia nilimuua? Nifungue hapa nikuonyeshe!" Weisiko akafoka huku akijivuta-vuta.

Victor akacheka.

"Mary mmemweka wapi? Niambieni!" Weisiko akauliza.

"We unafikiri tumemweka wapi?" akauliza Victor.

"Anajifanya anamjali sana," Mensah akaongea.

"Ulifanya nini mpaka ukaharibu kumbukumbu zake?" Lexi akauliza.

"Haikuhusu. Tambua kwamba yule hakufahamu tena, na wala hawezi kamwe kukukumbuka tena kwa sababu nilihakikisha chembe zozote zile zilizobaki za kumbukumbu kuwahusu nyie nimeziondoa kichwani kwake... kwa hiyo...."

Kabla Weisiko hajamaliza kuongea, yule mtu mwingine aliyekuwa amesimama kule kwenye mwingilio wa jumba hilo akawa ameanza kuelekea upande wao, na taratibu Weisiko akatambua ilikuwa ni Azra. Aliishia kumwangalia tu usoni kadiri alivyowasogelea, na wasiwasi ukamwingia kwa kuwa alijua kila kitu alichokisema, mwanadada huyu alikisikia. Azra akasimama usawa wa Lexi na kumwangalia Weisiko kwa hisia tata, huku Weisiko akijaribu kutabasamu.

"Ahah... Mary... Mary help me. These sickos want to kill me (Mary nisaidie.. hawa wagonjwa wa akili wanataka kuniua)," Weisiko akamwambia.

"You're such a sicko yourself not realizing how huge of a fool you're making yourself look (we ndiyo mgonjwa wa akili kutotambua ni jinsi gani unavyojionyesha kuwa mpuuzi mkubwa)," Mensah akamwambia.

"Mary nisikilize. Don't listen to whatever these people have told you... I'm..."

"Hatujamwambia lolote mjinga wewe. Ametoka tu kuthibitisha ukweli yeye mwenyewe kwa kila kitu ulichokisema," Victor akamwambia.

"Mary... Mary... Mary please..." Weisiko akaendelea kuomba.

"No. I'm not Mary. My name is Azra," Azra akasema.

Weisiko akakunja sura kimaswali, akiwa kama mtu ambaye haamini kile alichosikia.

"Mary, I'm your father. Umesahau... have you forgotten all the time we spent together? Usiwasikilize hawa, I'm the one who raised you (mimi ndiyo niliyekulea)," Weisiko akamwambia.

"To be your weapon? To be... a killer? (Ili kuwa silaha? Kuwa.. muuaji?)" Azra akauliza.

Lexi alikuwa anamwangalia Weisiko kwa hasira kuu.

"I took care of you because I love you. You... you're my daughter... (Nilikutunza kwa kuwa nakupenda. Wewe ni binti yangu...)"

"F(...) you," Azra akamkatisha.

Mensah na Victor wakacheka.

"You know... I put up with all of your shit all that time because I really thought I had only you. You... you killed my parents, and then fed me all the lies, made me into a weapon to kill for you... and now you admit that you erased my memory. You think I care a damn about what you did to keep me alive? Ahah... it would've been better if you just killed me that night, because now I'm gonna make sure you never see tomorrow's light," Azra akaongea kwa hisia.

Weisiko akawa anamtazama kwa hasira sana. Azra akarudisha mkono wake nyuma ya kiuno chake na kutoa bastola yake, kisha akaikoki na kuendelea kuishikilia kiganjani.

"Mary... kweli... unaweza kufikiria kuniua mimi?" Weisiko akauliza.

"Just give me the word, I'll be more than happy to put a hole in his head (naomba uniruhusu tu, itakuwa ni zaidi ya furaha kwangu kukitoboa kichwa chake)," Azra akamwambia Lexi.

"Wait, we shouldn't do that yet (subiri, tusifanye hivyo kwanza)," Nora akasema.

"Kinachowafanya msubiri ni nini? Kama mnataka kuniua, niueni sasa hivi," Weisiko akasema.

"Tulia nyau wewe, utakufa tu," Mensah akasema.

"Why wait? If you want to kill me dear, go ahead, do it now," Weisiko akamwambia Azra, akimshurutisha amuue.

Lexi na Azra wakawa wanamtazama kwa hisia kali sana.

"Ahahahah... hii dynamic duo inawapendeza. Wazazi wenu wangekuwepo sasa hivi, wangekuwa proud. Too bad niliwaondoa duniani mapema sana," Weisiko akamwambia Lexi.

"Ah..."

Lexi akatoa sauti hiyo na kunyoosha kiganja chake kumwelekea Azra, naye Azra akampatia bastola yake na hapo hapo Lexi akainyoosha kuelekea kichwa cha Weisiko kwa hasira sana.

"Wait, wait, wait, wait, subiri, Lexi..." Nora akasema haraka kumzuia.

Lexi alikuwa amekasirishwa sana na maneno ya mwanaume huyo. Kila kitu kuhusu jinsi mwanaume huyu alivyowaua wazazi wake kilirudi kwenye akili yake, na tamaa kubwa ya kutaka kumuua pia ilikuwa imemlemea sana. Weisiko akawa anamwangalia kwa jeuri huku bastola ikiwa katikati ya usawa wa macho yake.

"Lexi... please, tuwasubiri wengine kwanza... then tutaamua cha kumfanya," Nora akamwomba.

Lexi akawa bado ameielekeza bastola kwa mwanaume huyo huku amekaza meno yake kwa hasira.

"Mhm... ni bora kama ungeniua sasa hivi tu mpenzi, maana mkikaa kusu...."

Kabla ya Weisiko kumaliza kuongea, Lexi akafyatua risasi mbili haraka sana, naye Nora akashtuka na kurudi nyuma!

Zilifuata kelele za maumivu kutoka kwa Weisiko, kwa kuwa sasa hakuwa na sehemu za nje za masikio yake mawili. Lexi alizifyatua zote kwa kasi sana, naye Weisiko akawa analia kwa maumivu huku damu zikiruka kutokea pande mbili za kichwa, na sikio moja lilinyofoka kabisa, huku lingine likining'inia usawa wa taya. Azra akang'ata meno yake na kushusha pumzi kwa kuhisi mridhiko kiasi baada ya Lexi kumnyamazisha kiaina mwanaume huyo, huku Mensah na Victor wakitabasamu kwa kufurahia jambo hilo.

"Omba Yesu ashuke akurudishie hayo," Victor akamwambia Weisiko.

Jamaa akawa anaugulia maumivu huku amekaza macho yake na kupiga-piga miguu chini, naye Lexi akamgeukia Nora na kumwona jinsi alivyomtazama kwa hofu kiasi. Akamgeukia tu Azra na kumrudishia bastola yake, kisha akamsogelea karibu zaidi Luteni Jenerali asiyekuwa na masikio tena.

"Unakumbuka nilichokwambia usiku ule? Nilikwambia ningekuua kwa mikono yangu mimi mwenyewe. Usijali. Sijaisahau hiyo ahadi," Lexi akasema na kusogea nyuma.

Azra akasogea karibu na Weisiko na kumtemea mate usoni, kisha akamwangalia Lexi kwa hisia machoni. Lexi akakishika kiganja cha mdogo wake ili kumtuliza hisia, naye Azra akamkumbatia. Nora hakupendezwa kwa kadiri fulani na jambo lililokuwa limetokea, naye akageukia upande mwingine na kuziba mdomo wake kwa kiganja. Moyo wake ulidunda kwa kasi, kwa kuwa masuala ya ukatili yalimhofisha sana, hata ingawa aliyefanyiwa hivyo wakati huu alikuwa mkatili kupitiliza. Lexi akamwachia Azra taratibu, kisha akamfata Nora na kumshika mabegani kutokea kwa nyuma, na Nora akitambua ilikuwa ni yeye, akavishika viganja hivyo kama njia ya kuonyesha ameikubali pole hiyo isiyo ya moja kwa moja.

Wakati huu sasa Weisiko alikuwa akiguna tu kwa maumivu, huku damu zikiendelea kutiririka taratibu, na ni hapa ndipo wote wakahisi hatua zikija kutokea kule kwenye mwingilio wa jengo hilo. Upesi Mensah na Victor wakatoa bastola zao na kuzielekeza upande huo, naye Nora akatoa yake pia na kuielekeza upande huo huo. Ni Lexi na Azra pekee ndiyo waliobaki kusimama wakiwa wanatazama upande huo bila kutoa silaha zao, na hatimaye hatua hizo zikafika mwanzoni mwa mlango na mtu huyo kuingia.

Ni baada ya kuona kwamba ilikuwa ni Kevin, ndiyo wengine wakashusha silaha zao. Akasimama tu huko huko huku akiwatazama wenzake kwa umakini, na jambo hili likampa Lexi hisia fulani mbaya.

"Oya vipi? Mmepitwa na uhondo huku," Victor akamuuliza.

"Bila shaka mambo yamekwenda vizuri upande wenu. Huyo bwege mlimkamata kwenye saa ngapi? Kabla hata giza halijaingia?" Mensah akauliza huku akianza kumfata Kevin.

Lexi akamzuia Mensah kwa kuweka mkono wake usawa wa tumbo lake ili asiendelee kwenda. Azra kuona hivyo, akatoa bastola yake na kuiweka mikononi kwa utayari. Jambo hili likafanya umakini wa Nora upande pia.

"Vipi?" Mensah akamuuliza Lexi.

Kevin akawa amesimama tu pale pale huku akiwatazama kwa mkazo.

"Kevin... boss yuko wapi?" Victor akauliza, naye akiwa amehisi kuna jambo haliko sawa.

"Usijali, tuko naye..."

Sauti hiyo iliyotoa hilo jibu, ilitokea nyuma yake Kevin, nayo iliwafanya wengine pale waitikie haraka sana kwa kutoa silaha zao na kunyoosha upande wa Kevin, isipokuwa Lexi, ambaye ingawa alikuwa amebeba bastola, hakuitoa kwa sababu ya kushangazwa na jambo hili. Ijapokuwa Weisiko alikuwa amekatwa masikio yake, bado aliweza kupokea mawimbi ya sauti vyema kutambua kuwa hiyo ilikuwa ni sauti ya Jenerali Jacob.

Kutokea nyuma yake Kevin, Jenerali Jacob alifika hapo na kusimama pembeni yake, akiwa anatabasamu kwa hila sana. Wengine wote wakawa wanashangaa sana kuona jambo hilo, wakiwa hawaelewi nini kinaendelea.

"What is this Kevin? Unafanya nini hiki?" Mensah akamuuliza kwa hasira.

"Itakuwa bora mkishusha silaha zenu ikiwa mnataka kuwaona wenzenu tena," Jenerali Jacob akasema.

"Itakuwa bora kama utafunga hilo domo la sivyo nitaumwaga ubongo wako!" Mensah akafoka kwa hasira.

"Huyu ndiye ambaye huwa hakosi shabaha?" Jenerali Jacob akamuuliza Kevin.

Kevin akatikisa kichwa mara moja kukubali.

"That son of a bitch is nothing but a backstabber! (Huyo mtoto wa malaya ni msaliti mkubwa sana!)" Azra akaongea kwa hasira, akimaanisha Kevin.

Nora alikuwa akimwangalia baba yake kwa hasira kuu machoni mwake.

"Uncle Kendrick yuko wapi?"

Swali hilo likatoka kinywani mwa Lexi hatimaye. Alikuwa akimuuliza Kevin, lakini jamaa akanyanyua tu kidevu juu huku anamtazama kwa kiburi.

"Binti ya Casmir. Nimesikia mengi kukuhusu. Kiukweli unanikumbusha wakati ule ambao...."

Mensah akafyatua risasi iliyopita usawa wa bega la kulia la Jenerali Jacob na kuchana sehemu ndogo ya koti alilokuwa amevaa, akikatisha maneno yake ambayo hayakuwa na maana yoyote.

"Ahahah... show off," Jenerali Jacob akasema huku anajiangalia begani.

"Ameuliza swali, jibu swali. The next shot I swear napasua kichwa chako!" Mensah akasema kwa hisia kali.

"Kuwa makini na unachoniambia kijana. Huenda ni hicho hicho ndiyo kikakupata wewe," Jenerali Jacob akasema.

Papo hapo wote wakashtushwa sana baada ya kichwa cha Mensah kutobolewa kwa kupigwa na risasi! Hakukuwa na mlio wa risasi, lakini upande wa juu wa jengo hilo kwenye kuta za pembeni kilipasuka kioo kimoja, na ni hapo ndipo risasi hiyo iliyopigwa kwa shabaha ya mbali ilipopita. Mensah akadondoka chini huku kichwa chake kikiwa kinatoa damu nyingi, na jambo hilo liliwahofisha sana wenzake. Jenerali Jacob akawa anatabasamu kwa sifa sana, naye Victor akataka kumfyatulia risasi, lakini papo hapo naye pia akapiga kelele za maumivu baada ya kupigwa kwa risasi kifuani, kisha kichwani!

Wengine walipotaka kutoa itikio la haraka, Jenerali Jacob akasema kwa sauti, "Msijaribu kufanya action yoyote kutuelekea, kwa sababu hizo ni drone, mkijongea tu, mmekwisha!" akasema Jenerali Jacob.

Nora, Azra na Lexi ndiyo waliokuwa wamebaki kusimama, na kilichokuwa kimewapata Mensah na Victor ni kitu ambacho kiliwaumiza sana. Weisiko akawa anatabasamu kwa kiburi huku bado akisikilizia maumivu ya masikio.

"Tupeni hizo silaha chini," akasema Jenerali Jacob.

Hapo hapo wakaanza kuingia wanaume wale wa Jenerali Jacob, wakiwaelekea wanawake wote kwa kuzingira. Idadi yao ilikuwa 11, na hatimaye wakawazunguka watatu hao huku wakiwaelekezea bunduki.

"Hakuna trick zozote zilizobaki kwenu tena, kwa hiyo fuateni ninachowaambia ikiwa bado mnataka kuendelea kupumua," Jenerali Jacob akasema.

"Ni afadhali kufa lakini siyo kukuomba wewe unusuru maisha yetu," Nora akasema kwa ujasiri.

"Siyo wote wanafikiria kama wewe mwanangu," Jenerali Jacob akasema, kisha akageuka nyuma.

Hatua zingine zikaanza kusikika zikija kutokea mlangoni, na baada ya kufika usawa wa Jenerali Jacob, Lexi akaingiwa na hofu kubwa. Ilikuwa ni Kendrick pamoja Torres, wakiwa wameshikiliwa na wanaume wawili-wawili. Walionekana kuchoka sana kwa kuwa walilegea haswa, huku sura zao zikiwa na vimbe ndogo-ndogo na michirizi ya damu, kuonyesha walikuwa wamepigwa mno. Walifungwa kwa gundi za karatasi midomoni, lakini hawakufungwa mikono wala miguu kwa sababu hawakuwa na nguvu mwilini kutokana na kupigwa sana, kutia ndani na risasi zilizokuwa zimetoboa miguu yao.

Lexi akakunja ngumi kwa nguvu akihisi hasira sana, kwa sababu aliona ni makosa yake kutotambua aina ya mtu Kevin aliyekuwa, na kuendelea kumwamini ilikuwa imewaponza wenzake, na sasa wote kwa ujumla.

"Ninatumaini... ingawa sote tunajua jinsi hii itakavyokwisha, angalau utataka kutumia muda kidogo na hawa wapendwa wako waliobaki badala ya ikiwa nitawaua tu haraka. Nadhani umeshachoka kuona watu unaowapenda wakifa mbele ya macho yako, siyo?" Jenerali Jacob akamsemesha Lexi.

Nora na Azra wakamwangalia Lexi kwa hisia, naye akatazama chini kwa huzuni.

Jenerali Jacob akatabasamu na kutoa ishara kwa vidole vyake, na wale wanaume waliowazunguka wanawake wakawafuata na kuwanyang'anya silaha zao. Walipoanza kulazimisha kuwafunga, Azra akaweka kipingamizi na kuanza kuwapiga wanaume hao kwa mitindo yake ya haraka, lakini mmoja wao akamtandika kwa chuma la bunduki nyuma ya kichwa chake, naye Azra akapoteza fahamu. Lexi alikuwa amevunjika sana moyo. Alikuwa amekazwa na wanaume wawili walioanza kumfunga, huku Nora naye wakimfanyia hivyo hivyo. Wanaume wengine wakaanza kumfungulia Luteni Jenerali Weisiko pale alipokuwa amefungwa, naye akanyanyuka hatimaye akiwa bado anahisi maumivu makali sehemu za masikio yake, lakini akajikaza kiume na kumsogelea Lexi alipokuwa ameshikiliwa. Jenerali Jacob pamoja na Kevin wakaanza kuelekea hapo pia, huku Kendrick na Torres wakikokotwa nyuma yao.

"Eti nilikwambia nitakuua kwa mikono yangu mimi mwenyewe! Yako wapi?" Weisiko akamwambia Lexi kwa kejeli.

Kisha akampiga ngumi kwa nguvu sana tumboni iliyofanya Lexi ahisi maumivu makali mno. Lakini hata hakutoa sauti, bali akajikaza tu na kuendelea kutulia huku Nora akilia na kusema wamwache. Jenerali Jacob akawa amefika karibu na binti yake, naye akamtazama kwa hisia kali sana, na Nora vilevile akamwangalia kwa hasira. Jenerali Jacob akamwasha Nora kofi zito usoni, na wanaume wale wakaendelea kumshikilia kwa nguvu.

"Nimekutendea kwa fadhila toka mama yako alipoamua kujiondoa duniani na hii ndiyo shukrani yako kwangu? Haujui ni jinsi gani kila kitu ulichofanya kinavyonikumbusha maumivu aliyoacha mama yako," Jenerali Jacob akamwambia.

Nora akawa anapumua kwa hasira sana huku mdomo wake ukitiririsha damu.

"Lakini mimi bado ni baba yako. Hiyo mishipa yako bado ina damu yangu. Ni hicho tu ndiyo kinachofanya mpaka sasa uendelee kuwa hai," Jenerali Jacob akasema.

"Sihitaji unusuru maisha yangu. Nitakuwa na furaha zaidi ikiwa utaniua, kwa kuwa maumivu aliyopitia mama kwa sababu yako sijayasahau. Lakini nakuonya. Ukiendelea kuniacha mzima I swear... nitakuua mimi mwenyewe," akasema Nora.

"Ahahahah.... empty threats my love..."

Jenerali Jacob akiwa anasema hivyo, Weisiko akachukua bastola moja iliyokuwa chini na kuielekeza kwenye kichwa cha Lexi, akiwa na nia ya kukipasua haraka sana. Lexi alikuwa anamwangalia tu bila hofu.

"Weisiko... subiri," Jenerali Jacob akamzuia.

"Nimesubiri sana General. Hhh... niruhusu kusahihisha makosa niliyofanya miaka mingi iliyopita," Weisiko akamwambia.

"Usijali jembe langu. Kama ni kifo tu, atakipata. Lakini nataka kiwe kifo ambacho hakuna yeyote kati yao anaweza kutarajia," Jenerali Jacob akasema.

Akamsogelea Lexi karibu kabisa na uso wake.

"Kujisumbua huko kote kwa faida gani mwanangu? Mwisho wa siku umerudi tena kule kule ulikotoka. Ila kwa wakati huu... utatamani ingekuwa bora kama ungekufa kipindi hicho," Jenerali Jacob akamwambia.

"Hakuna kingine zaidi nitakachopoteza maishani kuliko kile ambacho ulikichukua kutoka kwangu... na unachotaka kuchukua sasa. Hata kama nitakufa, tayari nina amani moyoni, lakini hicho ni kitu ambacho kamwe wewe hautaweza kupata. Tokea mwanzo Mungu amekuwa pamoja nami, na mpaka wakati ambao pumzi yangu itakata ndiyo atakuwa amemalizana nami. Usifikiri wewe ni mkubwa kwa kila kitu. Mwisho wako unakuja. Na utakuwa mbaya kuliko unavyoweza kufikiria," Lexi akasema huku chozi likimtoka.

Jenerali Jacob akaanza kucheka sana, kisha akasema, "Umenikumbusha mambo mengi kuhusu baba yako. Alikuwa na maneno mazuri pia, lakini hayakumfikisha popote. Ninataka upate glimpse ndogo ya kile ninachoweza kufanya, na finally utambue kwamba kiburi chako hakijawaletea manufaa yoyote yale, kwa sababu sikuzote nitaendelea kuwa mkubwa... kuliko hata huyo Mungu wako."

Maneno ya mwanaume huyo yalijaa kufuru sana. Lexi alikuwa akimwangalia kwa hisia nzito, kisha Jenerali Jacob akarudi nyuma kidogo kuwapisha wanaume wengine wawili waliokuwa wameshikilia kamba, nao wakaifunga mikono na miguu ya Lexi. Kisha, wakatoa gundi ya karatasi nao wakaanza kuizungusha mwilini mwake Lexi, wakisaidizana na wale waliokuwa wamemshika ili kumfunga mwili mzima kuanzia mabegani mpaka miguuni. Akawa amebanwa kwenye mwili wake mwenyewe, asiweze kabisa kujongea kama vile sanamu, huku wanaume hao wakiendelea kumshikilia.

Kisha Jenerali Jacob akawaamuru wengine, yaani Weisiko na wale waliomshikilia Nora warudi nyuma mpaka usawa wake, nao wakatii. Bado Azra alikuwa amepoteza fahamu pale chini, na sasa wale wanaume wanne waliokuwa wamewashikilia Kendrick na Torres wakawasogeza mbele yake Lexi na kuwaachia, wakidondoka chini kwa kishindo. Wakawabandulia gundi mdomoni, nao wakawaacha hapo chini na kutoka kabisa ndani ya jengo hilo.

Lexi alikuwa anawatazama wenzake hao kwa hisia sana, huku akihisi hatia nyingi moyoni, kwa sababu alielewa walikuwa wanaandaliwa kwa ajili ya nini. Jenerali Jacob akatoa bastola kutoka kiunoni kwake na kuishikilia kiganjani.

"Unahitaji tiba mzee. Ni nani aliyekukata masikio?" Jenerali Jacob akamuuliza Weisiko.

"Huyo malaya," Weisiko akamwambia.

"Ahahah... mtoto wa moto huyu! Asingekuwa upande huo angependeza sana kuwa moja ya mikono yangu," Jenerali Jacob akasema.

"Lexi... my dear..."

Maneno hayo yskasikika kutoka kwa Kendrick, akiwa ameyasema kiuchovu sana. Lexi akamtazama chini hapo na kuendelea kudondosha machozi.

Kendrick akajitahidi kuunyanyua uso wake ili amtazame, kisha akamwambia, "Its okay. Tume... tumefika mbali pamoja. Angalau umefanikiwa kusaidia watu... wengi. I'm proud of you..."

Torres, bila kuweza kunyanyua shingo yake vizuri, akasema kwa sauti iliyokwaruza, "Lexi... I'm sorry..."

Jenerali Jacob akamkabidhi Kevin bastola hiyo, naye Kevin akamtazama kwa njia yenye maswali.

"Kill them," Jenerali Jacob akamwambia.

Kevin akatoa tabasamu lenye kuonyesha wasiwasi, naye akaipokea na kumwelekezea Torres.

"Kevin... why? Kwa nini umeamua kuwasaliti watu ambao walikuwa tayari kufa pamoja nawe kwa kupigania haki?" Nora akamuuliza kwa hasira kutokea nyuma yake.

Kevin akawa anasitasita kuvuta kifyatulio cha risasi, kwa sababu kuna sehemu fulani ya dhamiri yake ilikuwa inamsumbua kuhusiana na yote aliyokuwa amechagua kuyafanya. Akamwangalia Jenerali Jacob kwa hofu kiasi kutokana na jinsi yeye na wanaume wake walivyomtazama kwa hila. Akakikaza kiganja chake na kufyatua risasi iliyompiga Torres sehemu ya mgongo wake, naye akalegea zaidi na kulala chini kwa kutulia. Lexi alifumba macho na kuinamisha uso wake akihisi huzuni iliyoambatana na hasira kali sana, naye akafumbua macho na kumwangalia Kevin kwa hasira zaidi.

"Lexi..."

Lexi akashusha macho yake na kumwangalia Kendrick, aliyekuwa ameita hivyo huku amepiga magoti chini sasa.

"Its okay. Hii ikiwa ni mara ya mwisho kukuambia maneno haya... nataka tu ujue kuwa ninakupenda sana... sana Lexi. Hhh... ninajivunia sana kwa kutumia muda wote niliokuwa nimebakiza hapa duniani nikiwa nawe. Na ninafurahi sana, kwa sababu huu nauona kuwa ushindi. Nakupenda sana binti yangu. Ahah... nimejisahau. Nakuchukia sana binti yangu," Kendrick akamwambia kwa hisia.

Jenerali Jacob na Weisiko wakaanza kucheka kwa dharau kwa kuwa waliona maneno ya Kendrick kuwa ya kipuuzi.

Lexi akawa analia kwa kwikwi, naye akamwambia, "Nakuchukia pia uncle Kendrick."

Kendrick akatabasamu kwa kufarijika moyoni.

Jenerali Jacob akazungusha macho yake kwa dharau na kumwambia Kevin, "Well?"

Kevin akaelekeza bastola yake kwa Kendrick, na hapo hapo akafyatua risasi iliyompiga mwanaume huyo mgongoni na kumwangusha chini. Lexi akatoa sauti ya kilio mara moja na kubaki mdomo wazi tu, akilia kwa hisia sana. Nora alikuwa analia sana pia huku akimwangalia mpenzi wake, asijue la kufanya ili kumsaidia. Kwa sifa, Weisiko akaanza kuipiga risasi nyingi sana miili ya Kendrick na Torres huku akimwangalia Lexi na kucheka kwa sifa sana, naye Lexi akageukia pembeni huku akifumba macho kwa nguvu mpaka Weisiko alipomaliza risasi kwenye bastola yake.

"Unajisikia vizuri sasa?" Jenerali Jacob akamuuliza Weisiko.

"Ningefurahi zaidi kama ungeniruhusu niutie matundu mwili wa huyu malaya pia," akasema Weisiko.

"Usijali. Dawa yake inakuja," Jenerali Jacob akasema.

"Wewe ni mpumbavu! Haustahili kuitwa mwanadamu kwa ukatili huu unaofanya!" Nora akamwambia baba yake.

"Na huyu tumwiteje? Au umesahau kama na yeye aliua watu wengi pia?" Weisiko akamuuliza.

"Alimuua nani bila kuwa na sababu? Wewe na wenzako mliua mamia ya watu kwa sababu ya tamaa..."

"Funga domo lako we mtoto! Haujui ni kiasi gani baba yako amejitoa kwenu halafu wewe uje kusema maneno hayo yasiyo na shukrani," Weisiko akamwambia.

"Nimshukuru kwa lipi huyu? Pamoja na yote ambayo mmefanya bado mnajiona kuwa sahihi kabisa? Sikuwahi kukuomba fadhila yoyote, na wala sikuzihitaji. Lakini kama ni kitu nachotaka unipe sasa hivi, basi ni kifo nikiwa pamoja na Lexi. Niue nikiwa pamoja naye, ni hapo tu ndiyo nitakuwa na shukrani kwako," Nora akaongea kwa hisia sana.

Jenerali Jacob akashusha pumzi na kufumba macho yake kwa nguvu.

"Hebu mfungeni mdomo huo," Weisiko akawaambia wanaume waliomshika Nora, nao wakatii na kuuziba mdomo wa Nora kwa gundi ya karatasi. Inaonekana walikuwa nazo nyingi.

Wanaume wale wanne waliokuwa wametoka jengoni hapo dakika chache nyuma, wakarejea pamoja na mwanaume mwingine pia, yule yule Sniper wa Jenerali Jacob. Wenyewe walikuwa wamesaidizana kubeba sanduku refu na kubwa la mbao, lililoonekana kuwa zito mno, likiwa ndiyo lile lile ambalo walimletea Jenerali Jacob kama "mzigo wake" wakati ule yuko nyumbani. Sniper wa Jenerali Jacob ndiye aliyewaua Victor na Mensah kutokea nje muda mfupi nyuma, na wala hazikuwa "drone" kama Jenerali Jacob alivyodai. Wale wanaume wanne wakaliweka sanduku hilo mbele ya Jenerali Jacob, huku Nora, na hata Weisiko na Kevin wakijiuliza kulikuwa na nini ndani yake. Jenerali Jacob akatabasamu kwa hila sana huku akimwangalia Lexi, wakati huo Lexi akiwa ameinamisha tu uso wake kwa kupoteza matumaini.

Luteni Jenerali Weisiko alikuwa wa kwanza kutambua kuwa Azra alianza kurejesha fahamu zake muda huo. Akamtazama jinsi alivyoanza kujigeuza taratibu, na baada ya Kevin kuona ameanza kujongea, yeye pamoja na wanaume wa Jenerali Jacob wakaelekeza silaha zao kwake ili wampige na risasi, lakini Weisiko akawazuia.

"Mfungeni tu huyo. Msimuue," Weisiko akawaambia.

"Lakini... lakini...." Kevin akawa haelewi.

Jenerali Jacob akamwangalia Weisiko kimaswali pia.

"General... unajua umuhimu wake. Popote tutakapoenda nitahakikisha tunaendelea kumtumia," Weisiko akamwambia.

"Lakini huyu ameshajua kila kitu... atawasaliti..."

"Kaa kimya dogo. Huyu ana umuhimu mara mia zaidi yako hapa. General... nitaziondoa tena kumbukumbu zake... nita...."

Jenerali Jacob akamkatisha kwa kunyanyua kiganja chake.

"Fanya jinsi moyo wako unavyotaka Weisiko. Hata mimi nafanya kile moyo unachotaka, siyo kichwa tu," Jenerali Jacob akasema hivyo huku amemwangalia Nora.

Wanaume watatu wakasaidizana kumfunga Azra kwa kamba, ambaye alianza kufurukuta huku akipiga kelele sana pasipo kufanikiwa kujinasua, na akihisi maumivu kichwani kwake pia. Wakamnyanyua na kumsogeza mpaka usawa wa Luteni Jenerali Weisiko, naye akamwangalia kwa ufupi, kisha akawapa ishara wanaume hao wampeleke kwa nyuma. Sasa wakawa wamebaki wanaume wawili waliokuwa wamemshikilia Lexi aliyefungwa mwilini, akiwa anamtazama Nora kwa hisia sana wakati huu.

"This is going to be incredible. You're gonna f(......) love this!" Jenerali Jacob akamwambia Weisiko kwa shauku.

Akatoa ishara kwa vidole, na wale wanaume waliokuwa wamemshikilia Lexi wakamwachia na kusababisha adondoke chini mzima mzima, akiwa wima lakini uso wake ukiangalia juu ili aone kile ambacho Jenerali Jacob alikuwa anataka kumfanyia. Jenerali Jacob akaanza kupeleka mkono wake taratibu kwenye sanduku hilo kubwa, lakini kabla hajalifungua, mmoja wa wanaume wake akamsogelea karibu na kumnong'oneza jambo fulani. Akasimama vizuri na kumwambia yeye na wengine wachache waelekee nje kuyaandaa magari upesi ili waondoke haraka. Weisiko alipouliza tatizo, Jenerali Jacob akasema kwamba wale waliokuwa wakiwasaka walikuwa karibu kuwafikia, hivyo wangetakiwa kuharakisha kuondoka hapo na kutoroka nchi haraka sana.

"Usjie kufikiri kwamba umepata tiketi ya kunusurika my dear, no, no, no... ni kwamba tu tunakuacha u-enjoy some quality time na rafiki yetu hapa," Jenerali Jacob akamwambia Lexi.

Akatoa ishara kwa wengine kwamba waanze kurudi nyuma, na kiukweli hofu iliwaingia wale wote ambao hawakuelewa alichokuwa anataka kufanya, na baada ya Weisiko, Kevin, Azra, Nora, na wanaume wengine kusogea nyuma, Jenerali Jacob akalifungua sanduku hilo na upesi kurudi nyuma pia mpaka usawa wa wengine.

Lexi alikuwa bado chini hapo akitazama kwa uzito sanduku hilo, na hangeweza kuzuia hofu yake kubwa kupanda baada ya kuona kichwa cha chatu kikitangulia kutoka nje ya sanduku hilo! Nora na Azra walishtuka sana, hata Weisiko na Kevin hawakuwa wametarajia hilo, huku Jenerali Jacob akitabasamu kikatili sana. Nora akaanza kupiga kelele za kilio zilizozibwa kwa karatasi ya gundi mdomoni mwake, huku Azra naye akilia kwa hisia ndani ya kiziba mdomo chake alichokuwa amewekewa pia.

Chatu huyo akawa anatoka taratibu kwenye sanduku hilo, na kadiri alivyozidi kutoka ndivyo wengine walivyozidi kuona jinsi alivyokuwa na mwili mnene sana uliokuwa na nguvu kubwa. Lexi akaanza kujiviringisha kwa kurudi nyuma, akijitahidi kukikimbia kifo hicho ambacho alielewa wazi kwamba hakukuwa na namna ya kukiepuka.

"Ohohooo... hapo ndiyo anamwalika vizuri zaidi. Wanapenda movement, na jamaa ana njaa kichizi," Jenerali Jacob akasema kikejeli na kuanza kucheka, lakini bila kutoa sauti.

Chatu yule akaendelea kumfata Lexi taratibu, kama hana haraka vile. Jenerali Jacob akamwangalia Nora machoni kama kumwambia kwamba kama hakuujua ukatili wake vizuri, hiyo ndiyo ingekuwa somo kwake. Kisha akaanza kuondoka hapo haraka na kutoa ishara kwa wengine waondoke pamoja naye. Nora na Azra walijitahidi kujinasua sana lakini ikawa kazi bure, nao wakakokotwa mpaka nje na kuelekea upande ambao kulikuwa na magari sita meusi na kila mmoja kuingizwa kwenye magari mawili tofauti. Nora alishangaa sana baada ya kuingizwa ndani ya gari na kumkuta mdogo wake, yaani Asteria. Akawa anataka kumuuliza nini kilimpata, lakini hawakuweza kusemeshana kutokana na wote kuwa wamezibwa midomo yao, na hivyo kubaki wanatazamana kwa huzuni sana, huku Asteria akionyesha wazi kwamba aliogopa mno kwa kulia sana.

Nora pia alilia sana, sana, sana. Alimwonea huruma sana Lexi, kumwacha akipambana na kifo kibaya sana ambacho hakuwa na hali yoyote ambayo ingemsaidia kukishinda. Lakini pia hali ambayo baba yake alikuwa amemwingiza Asteria ndani yake ilikuwa mbaya mno, kwa sababu binti huyo hakustahili kupitia mambo haya. Azra pia aliumia moyoni kupita maelezo, kwa sababu alielewa kwamba Lexi alikuwa ndiyo mtu wa mwisho kubaki kwenye familia yao, hivyo kumpoteza kulimaanisha anaachwa akiwa peke yake kwa mara nyingine tena na kwenda kuendelea kutumiwa kama silaha. Magari yote yaliondoka eneo hilo upesi na kuanza kuelekea upande mwingine kabisa.

Kule ndani ya jengo, Lexi alikuwa amejitahidi sana kujivuta-vuta na kujiburuza ili kumwepuka mnyama huyo mbaya sana, na kila mara alipotazama lilipokuwa, aliona jinsi lilivyojongea kwa njia ya umendeaji, kana kwamba lilikuwa linafurahia "kumwinda" kwa njia hiyo, ikionekana kama mchezo. Lexi alielewa wazi kwamba mbio zake kwenye sakafu hiyo zingeishia tu hatimaye kwenye ukingo, na hili likathibitika kuwa kweli baada ya kuufikia ukuta mwishoni kabisa kwenye jengo hilo. Alikuwa akihisi maumivu mengi, siyo mwilini, siyo moyoni. Alichoka sana. Akatulia tu hapo hapo, ikionekana kama vile amekubali kile kilichokuwa mbele yake, naye akaendelea kumtazama chatu huyo alipozidi kumkaribia.

Akafumba macho yake, naye akajisemea maneno haya moyoni: "Sandra... nimejitahidi kukimbia kwa muda mrefu, lakini nahisi huenda huu ndiyo utakuwa muda ambao natakiwa kusimama. Niliamua kuchukua maisha mapya ili nitimize ulichoniomba, lakini nimekuangusha pacha wangu. Nimewaangusha wote. Labda kusimama kwangu sasa itakuwa bora... ili niweze kupumzika pamoja nanyi."

Lexi aliweza kuhisi kitu fulani chenye umajimaji kikitekenya pua yake, naye akafumbua macho na kukutana uso kwa uso na chatu huyo, akiwa karibu zaidi na uso wake, huku ulimi wake ukitoka nje ya kinywa chake kilichofunga na kuilamba-lamba pua yake. Lexi aliogopa sana, na kwa kuelewa kwamba mnyama huyo alikuwa anajipa muda kujiburudisha na windo lake, yeye akaamua tu kufumba macho tena na kutulia, na labda hiyo ingesaidia kifo chake kisiwe chenye kuhofisha zaidi ya alivyodhani.

Ghafla, mlio mkali sana ukasikika kwenye ngoma za masikio yake, uliomshtua sana, lakini hakufumbua macho baada ya kuhisi vitu kama vimiminika vyenye ugumu fulani vikimwagika usoni mwake kwa njia fulani kama mtu aliyemwagiwa maji kwa nguvu. Viliambatana na sauti za vishindo kwenye sakafu ya hapo, na mapigo ya moyo wake Lexi yaliendelea kudunda kwa nguvu sana akiwa bado hajafumbua macho yake. Mwili wake uliokuwa umebanwa ulitetemeka sana, na taratibu akafumbua macho yake hatimaye.

Mbele yake sasa aliweza kuona mwili wa chatu huyo, ukiwa unajinyonga-nyonga taratibu bila mpangilio, na ilimchukua sekunde kadhaa kutambua kwamba sehemu ya kichwa cha mnyama huyo mbaya kilikuwa kimepasuka. Ilikuwa hali yenye kuhofisha sana! Hakuelewa ni nini kilikuwa kimetokea mpaka aliponyanyua macho yake na kutazama mbele zaidi, na hapo akamwona mtu akisogea upande wake taratibu huku ameelekeza bunduki upande wake.

Lexi akakaza macho yake kwa mtu huyo, na sasa sura yake ikaanza kuonekana vyema hata zaidi. Ilikuwa ni Luteni Michael!



★★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★★

WHATSAPP +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Asubuhi ya siku hii, siku ambayo ukweli wote kuhusiana na matendo maovu ya Raisi Paul Mdeme na waandamani wake ulifichuliwa, utakumbuka kwamba Bobby na Luteni Michael ndiyo waliokuwa pekee jengoni kwao na kuziangalia video zote kutoka kwa Mess Makers zilizofichua mambo yote hayo. Baada ya kuwa wameziangalia, Bobby alimuuliza Luteni wake ni nini ambacho wangetakiwa kufanya, lakini Luteni Michael akaondoka tu bila kujibu lolote, akionekana kuudhika sana.

Aliondoka jengoni hapo upesi na kuchukua gari lake, kisha akaelekea mpaka sehemu aliyokuwa akiishi mwenyewe na kuingia tu ndani. Akaelekea kwenye kabati lake na kuvuta droo moja, naye akatoa "album" ndogo na kuiangalia kwa umakini. Akaifungua taratibu, kisha akaanza kufunua picha moja baada ya nyingine, akiziangalia kwa hisia nyingi za huzuni. Hapo kulikuwa na picha za ndugu zake na marafiki wengi, lakini zilizovuta hisia zake zaidi zilikuwa picha alizopiga pamoja na mama yake mzazi, binamu zake wa kike, na marafiki wachache aliokuwa amewakumbuka sana.

Hao walikuwa ni kati ya watu wengi waliouawa kwa mashambulizi ya "Demba Group" miaka nane iliyopita, watu waliokuwa wa karibu sana kwake. Utata kuhusiana na Demba Group mpaka inafikia siku hii hakuwa ameweza kuutatua, na sasa ikawa wazi kwake kwamba aliyefanya yale yote ilikuwa ni Jenerali wake. Alihisi hasira kali sana. Tena kujielekea yeye mwenyewe. Yaani leo ndiyo aliona sasa kweli maneno ya Lexi kwamba yeye alifuata tu amri kwa kupelekwa kama mbwa, yalikuwa ni ukweli mtupu.

Kwa muda mrefu, ingawa alijitahidi kuficha mambo haya kuhusu familia yake kisiri, alikuwa amejitahidi kutafuta njia za kuwakamata watu wale ili kuwalipa kwa waliyofanya, lakini haikuwezekana. Sasa akiwa ametambua msababishi mkuu alikuwa nani, hiyo ikamaanisha alikuwa ni adui yake, haijalishi alikuwa ni Jenerali Jacob. Kuanzia sasa, akaamua kuacha kuwa kama mbwa tu, naye angetekeleza haki kwa njia yake mwenyewe.

Akaweka picha hizo kando na kuvua nguo zake zote za kazi. Akachukua nguo nyingine ngumu za mapambano, zenye rangi nyeusi, naye akazivaa na gloves nyeusi mikononi, pamoja na mabuti yasiyo mazito sana miguuni. Akakivalisha kiuno chake mkanda uliobeba silaha na vifaa kama bastola, vyuma vilivyobeba risasi, mfuko wenye mabomu ya kurusha, visu, na darubini, kisha akatoka upesi na kuelekea kwenye gari lake. Sasa alikuwa ameamua kuchukua maamuzi magumu sana, yaani, kwenda kumuua Jenerali Jacob yeye mwenyewe, haijalishi nini kingempata baada ya hapo. Sikuzote alijiahidi kwamba wakati tu ambao angempata muuaji wa familia yake, angefanya jambo hili, na ndiyo huo wakati ulikuwa umewadia.

★★

Luteni Michael aliendesha gari kwa spidi zote, akipita sehemu nyingi ambako aliona jinsi watu mbalimbali walivyokuwa wameanzisha ghasia ndogo ndogo, naye hakukazia fikira hilo na badala yake kuhakikisha anakamilisha mpango wake. Hakujali angekutana na nani mbele; angefanya kila awezalo ili kumuua Jenerali Jacob, full stop. Aliendesha mpaka pande alizojua kabisa kwamba ndiko Jenerali huyo alikuwa, na kwa umakini akaliegesha gari lake sehemu salama, kisha akashuka na kusogea karibu na kichaka ili kuanza kuyasoma mazingira ya kule, akiliangaza eneo hilo kwa darubini yake kwa umakini.

Hazikupita dakika nyingi sana, naye akaona magari fulani matatu meusi, yenye muundo tata sana kama magari maalumu ya jeshi, yakitokea upande huo na kupita hapo kwa kasi sana. Alikuwa amekwishayaona kupitia darubini kwenye eneo hilo la Jenerali yakiwa tuli tu, lakini sasa ndiyo yakawa mwendoni. Kwa fikira za haraka Luteni Michael akadhani kwamba huyo alikuwa ni Jenerali Jacob akitoroka bila shaka, naye akarudi upesi kwenye gari lake ili aweze kuyafuatilia. Yaani alikuwa ameshajiwekea lengo la kumkamata iwe isiwe, na baada ya kuingia kwenye gari lake akaanza mwendo kufuatilia yale magari yalikokuwa yanaenda.

Lakini magari yale hayakuwa yamembeba Jenerali Jacob, bali wale walikuwa ni wanaume wake maalumu ambao aliwaagiza mapema sana kwenda sehemu ili kufanya jambo fulani. Hawa ndiyo walioagizwa kwenda kule Arusha kuilipua nyumba ya Mess Makers kama vile Jenerali Jacob alivyokuja kumwambia Torres baadae. Kevin alipomtafuta Jenerali Jacob na kuwasaliti wenzake, alimpa maelekezo ya ni wapi walikokuwa wakijifichia, hiyo ikiwa ni uhakikisho wa kwamba Jenerali Jacob angeweza kumwamini. Hivyo baada ya kumweleza mpango wao wa kumkamata Jenerali Jacob, ndiyo Jenerali huyu akaagiza watu wake hawa waende kule kuiharibu ile nyumba, ili kusiwe na jambo lolote kwa ajili ya Mess Makers tena endapo wangefikiria kurudi kule. Lakini Jenerali Jacob hakuwa amemwambia Kevin kuhusu hilo.

Kwa hiyo sasa Luteni Michael alikuwa akiwafuatilia watu ambao wangempeleka moja kwa moja mpaka kwenye nyumba ya Mess Makers. Kwa kuendesha magari yale kwa kasi sana, watu hao hawakutambua kuwa walifatiliwa, kwa sababu lengo lao lilikuwa kuharakisha kukamilisha kazi yao, kisha nao waondoke haraka kutoka nchini humu.

★★

Ilifika mida ya saa 7 hivi mchana, naye LaKeisha alikuwa amekaa kule "chini" akisubiri kupewa signal na Torres endapo kama kuna shida ingetokea. Yeye pia alijua vizuri sana jinsi mpango wao ulivyotakiwa kwenda, na akijua ingekuwa mpaka kwenye mida ya jioni, akaona kutulia tu na kuangalia filamu chache kungesaidia kukata muda haraka.

Isiminzile yeye alikuwa sehemu ya jikoni wakati huu akitengeneza chakula kwa ajili yake na LaKeisha, na kwa kadiri fulani bado aliendelea kufikiria kuhusu jinsi Lexi alivyokasirika sana baada ya yeye kumwambia ukweli. Alihisi ni kama asingewahi kuja kufanya jambo lolote ambalo lingemsaidia kuupata msamaha wa kijana yule. Lakini akajipa tu matumaini kwamba mambo yangekaa sawa, kama tu jinsi Nora alivyomtia moyo. Alipomaliza kupika, mwanaume akaamua kwenda kumuuliza LaKeisha ikiwa angependa kula wakati huu ili amwekee chakula. Akaenda mpaka chumbani kwake na kumwona LaKeisha kupitia mlango akiwa amejilaza kitandani, akiwa amevalia T-shirt nyepesi na kikaptura chekundu, na akiwa bado anatazama filamu.

Ni baada ya Isiminzile kuusukuma mlango wa kioo wa chumba hicho, ndiyo LaKeisha akamgeukia na kumtazama kwa umakini. Isiminzile akasimama huku anatabasamu, naye LaKeisha akatabasamu pia.

"Nimemaliza kutengeneza msosi, ungependa nikuletee?" Isiminzile akamuuliza.

"Kwa nini uniletee?" LaKeisha akauliza.

"Aam... yaani... kama unaona uvivu kushuka...."

"Ahah... asante. Nitafata tu mwenyewe..."

"Sawa..."

"Umetengeneza nini?"

"Omelette... nzito..."

"Ahahahah... kumbe unajua kupika?"

"Ahah... kidogo..."

"Ndiyo maana sijavuta harufu yoyote nzuri. Siyo kwamba ulikuwa tu unachanganya kemikali odorless?" LaKeisha akatania.

Isiminzile akacheka kidogo na kuangalia upande wa milango ya dirisha pana chumbani hapo.

"Halafu hatukuwahi kuongea unajua. Hivi unafanya kazi gani?" LaKeisha akauliza.

Lakini Isiminzile hakujibu. Alikuwa ameendelea kutazama upande huo wa dirisha, na hii ikavuta umakini wa LaKeisha. Yeye pia akaangalia huko, lakini hakuona kitu kwa sababu alikuwa amejilaza kitandani.

"Vipi?" LaKeisha akamuuliza.

"Aaaa... hiyo... hicho ni kitu kizuri?" Isiminzile akaongea huku amenyooshea kidole huko dirishani.

LaKeisha akanyanyuka na kusogea hapo upesi, na sasa akaweza kuona kile alichoona Isiminzile. Kutokea kule chini kabisa yalionekana magari yale matatu ya watu wa Jenerali Jacob, yakiwa yanaelekea upande wa nyumba hii kwa kasi. Ilikuwa mbali, lakini kwa sababu ya kuwa juu kwenye ghorofa hili, wawili hawa waliweza kuyaona. Kisha magari yale yakafika usawa fulani usiokuwa mbali sana na jengo hilo, na yote yakasimama ghafla. LaKeisha akaingiwa na hofu kiasi kwa sababu hayo hayakuwa aina ya magari ambayo wenzake waliondoka nayo, na hata bado muda wa kukamilisha mipango yao haukuwa umefika. Ikawa wazi hao walikuwa ni maadui. Akawaona watu sita wakishuka, na wakianza kama kupeana masanduku fulani marefu kwa kupokezana, kisha wakaonekana wakitoa vitu fulani virefu ambavyo LaKeisha hakuvitambua kwa usahihi.

Upesi akatoka hapo na kuanza kuelekea kule chini, huku Isiminzile akimfuata kwa nyuma. Alifika mpaka kwenye mitambo ya Torres na kuangalia kama kuna taarifa yoyote ilikuwa imetumwa, lakini hakuona lolote lile, na ndipo wazo la kumtafuta Torres au Lexi likamjia. Lakini tena, kifaa chake cha kuwasiliana nao akawa amekiacha chumbani, hivyo ikambidi aanze kupandisha tena ili akakifate kuwaambia wenzake yaliyokuwa yanatokea.

Kule nje, nje kabisa, wanaume wale walikuwa wanatoa silaha fulani za kulipua kutoka kwenye masanduku, zinazofahamika kwa jina la "Rocket Launcher." Hizi hufanana na bunduki, isipokuwa zenyewe huwa na muundo kama wa roketi ndogo, na huwekwa begani, kisha mbebaji akifyatua tu, zinakwenda kulipua sehemu iliyowekewa shabaha. Tayari wawili kati ya wanaume hao walikuwa wameshaiwekea nyumba hiyo shabaha kwa Rocket Launcher, nao wakafyatua ya kwanza iliyokwenda moja kwa moja mpaka kwenye sehemu ya ukuta wa mawe uliozunguka nyumba hiyo na kupaharibu vibaya.

LaKeisha ndiyo alikuwa anaelekea kule juu pale tikisiko lililosababishwa na kulipuliwa huko lilipomfanya adondoke na kuanza kuogopa sana. Wakati huu, Isiminzile alikuwa bado kule chini, naye alisikia jambo hilo lililomhofisha, hivyo akatoka upesi kwenda kuangalia ikiwa LaKeisha alikuwa sawa. Alikwenda mpaka sehemu za ngazi na kumkuta akiwa amekaa chini, naye akamsaidia kunyanyuka na kuuliza ni nini kilikuwa kinaendelea. Papo hapo tena, nyumba ikatikiswa kwa nguvu sana baada ya roketi nyingine kufyatuliwa, na zamu hii ilipiga juu kabisa ya ghorofa hili na kusababisha vioo na matofali mazito yaanze kuanguka chini. LaKeisha akamvuta Isiminzile na kuelekea naye mpaka sehemu ya jikoni, na sasa vumbi lilikuwa limeanza kutawala sehemu hiyo na vitu vingi kuharibiwa mpangilio.

"Keisha... tufanye nini?" Isiminzile akamuuliza kwa sauti ya juu yenye hofu.

LaKeisha akajiuliza ni kitu gani kingekuwa cha muhimu kufanya kwanza, na upesi akafikiria kuhusu zile nguo zao maalumu za mapambano. Wengine wote leo waliondoka bila kuzivaa za kwao, kwa kuwa waliona kwamba wangekamilisha mipango yao haraka na kurudi huku bila kukwaruzwa. Kwa hiyo mwanamke huyu akaona kwamba huenda hiyo ingekuwa njia ya kwanza ya kuilinda miili yao, hivyo akamwambia Isiminzile ajikinge kwenye kona ya ukuta wa humo jikoni, naye akamwacha na kuelekea kwenye chumba cha Lexi. Alikuwa anaharakisha sana, na baada ya kuchukua vazi la ziada la Lexi, akaenda mpaka kwenye chumba chake za zamani, ambacho kwa wakati huu alikuwa akikitumia Azra, naye akalichukua la kwake. Alihisi haingechukua muda mrefu na mlipuko mwingine ungetokea, hivyo akavaa lake haraka mpaka na kificha uso, na ni hapa ndipo roketi nyingine ikapiga!

Wakati huu ililipua pande za pembeni mwa jengo hilo mpaka kukifikia chumba alichotumia Kendrick, na hii ikamwambia LaKeisha kwamba watu wale walikuwa wakiilipua hii nyumba kwa kuzunguka. Akatoka hapo na kushuka mpaka kule chini, chini kabisa kwenye handaki lao pana, naye akafungua sanduku la kieleketroni lililokuwa limetunza zile dhahabu ambazo yeye na wenzake walimwibia Mdeme kutoka kwenye treni, kisha akaweka kiasi kingi kwenye fuko kubwa na kuanza kupanda juu. Alijitahidi kutembea kwa umakini mpaka alipofikia usawa wa jikoni, naye akamwita Isiminzile, ambaye bado alikuwa hapo, na kijana akaitika na kumfata.

Wakatoka kwa pamoja mpaka nje, na walipoifikia nyumba ndogo ambayo Zelda alikuwemo, wakasikia sauti kama ya mluzi mkali ikitokea kule nje kuja ndani, naye LaKeisha akamshika Isiminzile na kumwinamisha, kwa sababu hiyo ilikuwa ni roketi nyingine ikija. Wakati huu ikapiga katikati kabisa ya jengo hilo, na wawili hawa walitetemeshwa sana na hata kupigwa na baadhi ya mawe yaliyopasuka-pasuka kwa nguvu, lakini hawakuumizwa. LaKeisha akaona muda haungetosha kumpa Isiminzile vazi lile la Lexi la mapambano aanze kuvaa, kwa sababu bado alihitaji kumwokoa Zelda, kwa njia ambayo isingemuumiza Isiminzile endapo mnyama huyo angemwona, kwa hiyo wangetakiwa kufanya mambo kwa uharaka sana.

Jengo lote kuanzia juu likawa limeporomoka kwenda chini na kuzidi kuchafua hali ya hewa, naye LaKeisha akamwambia Isiminzile aende kwenye gari lile aina ya pickup, Ford Ranger XLT, lililokuwa limefunikwa sehemu yake ndogo ya kuwekea mizigo kwa nyuma. Alimwambia kihususa kwamba aingie kwa ndani, kisha apitilizie mpaka nyuma huko kwenye kubebea mizigo kupitia uwazi mdogo uliokuwepo na kukaa humo humo, akihakikisha pia kwamba hanyanyuki. Isiminzile akatii na kukimbilia kwenye gari hilo, halafu akafanya kama alivyoambiwa.

Wakati huo, LaKeisha akawa amefungua mlango wa nyumba hiyo ndogo, na hapo Zelda akatoka akionyesha kuchanganywa na kelele zilizokuwa zikiendelea. LaKeisha akatoa kiziba uso chake na kumtuliza, kisha akaanza kumpeleka mpaka kwenye gari lile. Wakaingia kwa pamoja, naye LaKeisha akaliwasha upesi kwa kuwa funguo zilikuwa humo humo, kisha akaligeuza gari pale roketi nyingine ilipopiga jengo tena. Kuna jiwe liliruka mpaka sehemu ya mbele ya kioo cha gari, nalo likasababisha kipasuke kwa kuacha nyufa nyingi sana, lakini LaKeisha akakomaa kulitoa gari hapo.

Moto ulikuwa umeanza kuwa mkubwa zaidi na moshi mweusi ulifuka juu, lakini ni kama Mungu tu alikuwa anawalinda, naye LaKeisha akaliendesha gari hilo kupitia sehemu ile ya ukuta iliyobomolewa kwa mlipuo. Matariri ya gari hilo yalikuwa makubwa na imara, hivyo yalisaidia lipite juu ya mawe yaliyobomoka kwa nguvu na hatimaye LaKeisha akafanikiwa kulitoa gari ndani hapo, ingawa kwa msukosuko sana. Upande aliotokea ulielekea sehemu zenye miti zaidi kwenye eneo hilo, na wale wanaume wa Jenerali Jacob wakaliona gari hilo. Upesi, wanne wakaingia kwenye magari yao mawili ili walifuatilie gari hilo, wakiwaacha wawili tu hapo wamalizie kabisa kuiporomosha nyumba hiyo.

LaKeisha aliendelea kuliendesha gari lake kupitia mabonde mabonde na miti mingi, na baada ya kuangalia vioo vya pembeni vya gari, akayaona magari yale mawili yakimfuata kwa kasi, hivyo akaongeza mwendo ili aweze kuyakwepa. Lakini yalikuwa na kasi sana, na kadiri alivyoendelea kujitahidi kukimbia, ndivyo yalivyozidi kumkaribia. Mwishowe akaanza kusikia sauti za risasi, na ni gari lake ndiyo lilikuwa likifyatuliwa kutokea nyuma. Sehemu za nyuma kwenye gari lake zilipasuliwa kwa risasi, na kwa jinsi gari lilivyokuwa likiweweseka aliweza hata kumsikia Isiminzile akitoa sauti za maumivu kwa sababu ya kujigonga-gonga kule nyuma. Zelda ndiyo alikuwa amesimama kwenye siti za nyuma, na kama mnyama wa kawaida alikasirishwa sana na mambo yote hayo yaliyokuwa yanamchanganya mno mpaka akawa anataka kuruka kutoka ndani ya gari hilo.

Risasi tatu zilizofuata ziliweza kupiga matairi ya nyuma ya gari hilo, naye LaKeisha akajitahidi kuliendesha kwa umakini ili alisimamishe kwa sababu lilianza kwenda ovyo ovyo. Yaliishiwa upepo kabisa, na hatimaye gari likagonga mti mmoja kwa upande, yaani upande wa milango yake, kisha likatulia hapo huku likitoa moshi mwingi sehemu ya mbele. LaKeisha alikuwa amekigonga kichwa chake kwa nguvu sehemu ya kioo cha mlango wa gari, naye akawa akihisi kizunguzungu kikali sana, akifumba na kufumbua macho yake kivivu. Akaanza kuhisi pumzi nzito karibu na sikio lake, na upande wa shavu lake ukilambwa, naye alielewa wazi kwamba ilikuwa ni Zelda. Akaanza kusikia sauti za magari kwa nje, naye akajitahidi kukisawazisha kichwa chake na kumwambia Zelda atulie, kisha akaivaa mask yake na kuanza kufungua mlango. Akatoka kwa kudondoka chini na kutambua kwamba Zelda alitaka kutoka pia, lakini akawahi kuufunga mlango na kumwacha anaunguruma kwa hasira huku anaruka huku na huko ndani ya gari.

Mwanamke huyu alipogeukia upande mwingine, akawaona wanaume wanne wenye kuvaa viziba uso kama majasusi, wakiwa wamesimama tu huku wameshikilia bunduki mikononi. Akasimama ili kuwaangalia vizuri, ingawa kizunguzungu chake kilimfanya ayumbe kiasi, lakini akajitahidi kusimama wima. Wanaume hao walijua kwamba kwa sababu ya ajali hii ndogo, mtu huyo hangekuwa na nguvu za kutosha, ndiyo maana walikuwa kama wanamsikilizia tu. LaKeisha hakuwa na silaha yoyote, lakini alitaka kuwafuata wanaume hao na kujaribu kuwanyang'anya bunduki moja ili awamalize wote haraka. Akaanza kupiga hatua kuwaelekea, na mmoja wao akacheka kidogo na kuanza kumfata pia.

Walipokaribiana, LaKeisha akarusha ngumi, lakini mwanaume huyo akaikamata na kumpiga kwa ngumi pia tumboni. Hii ikamuumiza mwanaume huyo, kwa sababu hakujua kama nguo aliyovaa LaKeisha ilikuwa ngumu sana, na hapo hapo LaKeisha akaikamata bunduki yake na kuifyatulia risasi kuelekea mguu wa jamaa! Akatoa yowe la maumivu na kuangukia pembeni, na hapo ndipo wenzake wakatahadharika na kuzinyoosha bunduki zao kumwelekea LaKeisha, wakati huo LaKeisha ameanza kuwafuata na wao. Wakamtandika risasi sehemu za chini za mwili, naye LaKeisha akadondoka chini, kisha akaanza kunyanyuka tena. Wakashangaa sana! Ile mmoja wao alipojiongeza na kukilenga kichwa cha LaKeisha, hapo hapo wote wakashtushwa na sauti ya gari lililounguruma kwa nguvu kutokea upande mwingine, na ile tu wameangalia upande huo, gari hilo likatokea kwa kasi na kuwapitia wanaume hao watatu, waliorushwa kwa nguvu hewani na kudondokea pembeni kwenye miti.

LaKeisha akapiga goti moja chini akiwa ameshtushwa na jambo hilo, huku mwanaume yule mwingine aliyetandikwa risasi mguuni akishangaa pia baada ya kuliona gari hilo ambalo hakutambua limetokea wapi ghafla. Wakati sauti ya mngurumo wa gari iliposikika, yeye na wenzake walidhani ilikuwa ni wale wenzao wawili waliowaacha nyuma, lakini sasa ikawa wazi huyu alikuwa adui. Mlango wa gari hilo ukafunguka, na hapo LaKeisha akamwona aliyefika kuokoa maisha yake bila kutarajia, yaani Luteni Michael. Luteni Michael akatembea upesi kumwelekea LaKeisha, naye akamnyanyua na kuanza kumvuta kuelekea gari lake, lakini mwanamke huyu akajitoa mikononi mwake kwa nguvu na kurudi nyuma huku akipumua kwa kasi.

"Relax... mimi sitakuumiza..."

Luteni Michael akaongea kwa utulivu, naye LaKeisha akabaki kumwangalia tu huku bado uso wake ukifunikwa kwa mask ya nguo yake ya mapambano. Mwanaume yule aliyekuwa amepigwa kwa risasi mguuni, aliweza kuiona bunduki yake ambayo iliangukia usawa na alipokuwa amekaa sasa, hivyo akaisogelea na kuiokota, akiwa na lengo la kumtandika LaKeisha kutokea nyuma. Luteni Michael akaona hilo, naye akatoa bastola yake na kuielekeza kwa mwanaume huyo, kisha akamtandika risasi mbili kifuani kabla ya yeye kufanikiwa kumpiga LaKeisha kwa risasi. LaKeisha akageuka na kuona kwamba adui yake ndiye aliyekuwa amemalizwa kwa risasi hizo, naye akamwangalia tena Luteni Michael.

"Twende... siyo salama tena huku, watu watafurika," Luteni Michael akamwambia.

"Twende wapi?" LaKeisha akauliza.

Luteni Michael akajibu, "Kwa Jenerali Jacob."

"Kufanya nini?"

"Nisikilize dada. Ikiwa bado unataka kukaa hapa, ni sawa, mimi sikuja kwa ajili yako..."

"Basi ni kwa nini uko hapa?"

"Nilikuwa nimewafuata hawa nikidhani walimbeba Jenerali Jacob, lakini ndiyo nimefika na kuona wanailipua hiyo nyumba.... na wale wa kule nyuma hawakuwa na Jenerali. Sijui ikiwa ni wewe tu au kuna wenzako wamebaki, lakini niliona nije kusaidia kwa sababu najua Nora yuko nanyi...." Luteni Michael akamwambia.

"Kwa nini unamtaka Jacob?" LaKeisha akauliza.

"Ameharibu maisha ya watu wengi... kutia ndani na yangu," Luteni Michael akasema.

"Hawa watu wamejuaje kuhusu hii sehemu?" LaKeisha akauliza kwa sauti ya chini.

"Mimi sijui. Hayo yote mliyofanya kwa ajili ya wanyonge na crap, mnajua wenyewe. Ninachowashukuru tu ni kunisaidia kumtambua mbaya wangu, kwa hiyo linalobaki kufanywa sasa kwa wewe ni uamuzi wako... mimi ninamfata mbaya wangu," Luteni Michael akamwambia.

LaKeisha akabaki kumtazama tu, naye Luteni Michael akageuka na kuanza kulielekea gari lake. Alipofika usawa wa gari hilo, akawaona wanaume wale watatu wakihangaika kunyanyuka kutokana na kuumia mwilini, naye akawatandika risasi wote bila kusita. Kisha akafungua mlango na kutaka kuingia, lakini LaKeisha akamwita.

"Hey..."

Luteni Michael akageuka na kumwangalia, naye LaKeisha akatoa mask yake usoni.

"Utajuaje Jacob alipo sasa?" LaKeisha akauliza.

"Nimeshajua anapoenda. Nimeongea vizuri na wale wawili waliokuwa nyuma," Luteni Michael akamwambia.

LaKeisha akacheka kimkato na kutikisa kichwa chake kidogo, akiwa ameelewa kwamba mwanaume huyu aliongea kwa kejeli, kisha akaanza kumsogelea mpaka karibu.

"Nitakuja nawe, lakini tutahitaji kuchukua hayo magari," LaKeisha akasema.

Alikuwa amemwonyesha Luteni Michael magari yale ya wanaume hao wa Jenerali Jacob, naye Luteni Michael akamwangalia na kumuuliza, "Kwa nini?"

"Nina mtu mwingine kwenye hilo pickup... na mnyama mkali pia," LaKeisha akasema.

Kwa kuwa Luteni Michael hakuelewa vizuri, LaKeisha akamweleza kiufupi kwamba mnyama huyo ni kama simba, na hakuwa amezoea mtu mwingine hapo zaidi yake. Hivyo, Luteni angepaswa kuchukua gari moja na kuliendesha akiwa pamoja na Isiminzile, halafu yeye LaKeisha angeendesha lingine akiwa na Zelda. Kwa kuwa walihitaji kuwahi, Luteni Michael akaanza kuingia ndani ya gari moja na kukaa kwanza, akisubiri LaKeisha alipomtoa Zelda kwenye pickup na kumwingiza kwenye lile lingine. Alikuwa akishangaa sana ni jinsi gani mwanamke huyo aliweza kumwongoza mnyama huyo mwenye nguvu na kasi nyingi, na baada ya LaKeisha kumweka Zelda ndani ya gari, Luteni Michael akaenda kumsaidia Isiminzile kutoka kule nyuma ya pickup. Isiminzile alikuwa ameumia kiasi sehemu ya ubavu wake na kichwani, lakini akasema alikuwa sawa, na baada ya kutambulishwa kwa Luteni Michael, wawili hao wakaingia kwenye gari na kuanza kuondoka hatimaye.

Kulikuwa na vifaa vya mawasiliano kama redio ndogo ndani ya magari hayo yenye kasi sana, na baada ya Luteni Michael kujaribu cha kwenye la kwake kumsemesha LaKeisha, mwanamke huyu akajibu kwa kusema alimsikia. Wakatumia njia tofauti ili kuweza kutoka pande hizo kwa kuzungukia sehemu ya mbali kiasi kisha kuendelea na safari ya kurudi Dar es Salaam. LaKeisha akawa amemwambia Luteni Michael kwamba kundi lake liliondoka leo hii na kwenda Dar ili kuwanasa majenerali wale wawili. Yeye Luteni Michael alikuwa ameambiwa na wale wanaume wengine waliobaki kumaliza kuilipua nyumba, sehemu ambayo Jenerali Jacob alidhamiria kwenda kwa ajili ya mpango wake wa kutoroka nchi.

Kwa kuwa LaKeisha alifahamu kule ambako kundi lake lilidhamiria kuwapeleka Jenerali Jacob na Luteni Jenerali Weisiko baada ya kuwakamata, kwenda huko moja kwa moja ndiyo likawa lengo kuu la safari hii, ili aweze kuwajulisha wenzake yaliyotokea kwenye nyumba yao ya maficho, na hata Luteni Michael aweze kumwona mbaya wake.


★★★★


Kuendesha magari hayo yenye kasi kwa masaa kadhaa hatimaye kuliwafikisha Dar es Salaam, na sasa ilikuwa ikielekea kufika mida ya saa 2. Mpaka inafikia wakati huu, bado LaKeisha alifikiri kwamba mipango ya kundi lake ilikuwa imekwenda vyema, hivyo akafikiri ni yeye tu ndiye ambaye angepeleka taarifa mbaya kule walikokuwa. Walikuwa wamejitahidi sana kupita maeneo yasiyokuwa na ghasia nyingi sana, na LaKeisha akiwa ndiyo anaongoza mbele, wakafikia usawa wa mbali wa jumba lile la godown ambako alijua bila shaka wenzake wote wangekuwepo.

Lakini ni kwa usawa huo ndiyo LaKeisha alianza kuona magari fulani meusi, sita, yakiwa yameegeshwa si mbali sana na jengo hilo, kwa njia fulani kama yamefichwa. Ikabidi asimame na kumwambia Luteni Michael, ambaye naye akasema hapo bila shaka kulikuwa na jambo fulani lenye nuksi. Akamwambia wayaegeshe magari yao sehemu za pembeni zilizokuwa na vichaka zaidi, kisha washuke na kwenda kwa umakini kuangalia kama kulikuwa na shida yoyote ili watoe msaada.

Baada ya kufanya hivyo, Luteni Michael, Isiminzile na LaKeisha wakashuka kwenye magari yao, Zelda akiachwa kwenye lile moja, nao wakasogea kwa kuvizia mpaka sehemu iliyowaruhusu kuona mambo vizuri kiasi, ingawa kulikuwa na giza sana. Waliweza kuwaona wanaume wachache hapo nje, wakisimama usawa wa magari yale, na hakukuwa na jambo lolote lenye kushtua waliloona. Lakini watatu hawa wakashtushwa na sauti ya mlio wa risasi ya kwanza kutokea ndani ya jengo lile, na baada ya kutulia kwa sekunde kadhaa, wakasikia ya pili tena. Kisha zikaanza kusikika sauti nyingi sana za risasi, zikipigwa mfululizo na kwa fujo!

LaKeisha akaogopa sana. Akamwambia Luteni Michael kwamba ikiwa watu hao walikuwa wa Jenerali Jacob, basi hiyo inamaanisha rafiki zake walikuwa kwenye matatizo, kwa hiyo wangepaswa kuharakisha kwenda ili kutoa msaada. Lakini Luteni Michael akamwambia atulie, kwa sababu aliona ni kama vile mambo yote pale yalikuwa yamepangwa kwa njia fulani tata sana, hasa kama kweli ni Jenerali Jacob ndiye aliyekuwa anayaongoza. Akamuuliza LaKeisha ikiwa kweli walikuwa na uhakika kwamba mipango waliyoifanya leo ingefanikiwa, na mwanamke huyu akamjibu kwa kusema kwamba kwa asilimia zote, ndiyo, ingefanikiwa. Basi mambo yangekuwa yameharibikia wapi? Ikiwa risasi hizo zilipigwa kwenye miili ya rafiki zake, LaKeisha alihofia kwamba huenda ni yeye pekee na Zelda ndiyo walikuwa wamebaki sasa, na roho ikamuuma sana.

Luteni Michael aliweza kuwaona wanaume watano wakiingia ndani kule tena, huku wanne wakiwa wamebeba sanduku fulani kubwa, naye akabaki kujiuliza afanye nini. Mwanzoni alipotaka kumuua Jenerali Jacob yeye mwenyewe, ilikuwa ni jambo la kibinafsi, lakini sasa tena akajikuta akiwa na vijana hawa wengine ambao aliona kama kuna umuhimu fulani wa kuwawajibikia, na pia ikiwa kulikuwa na uwezekano wa yeyote kati ya rafiki zao kuwa hai, basi angepaswa tu kutulia maana hangeweza kujua nini kiko ndani kule. LaKeisha akawa analia kichinichini, naye Isiminzile akaanza kumbembeleza kwa kumshika begani huku akimtikisa taratibu kwa huruma.

Hazikupita dakika nyingi, naye Luteni Michael akamwona Jenerali Jacob na Weisiko wakitoka ndani kule hatimaye. Hasira ilimwingia na upesi kuitoa bastola yake, akiielekeza huko kana kwamba alikuwa na shabaha tulivu ambayo ingeweza kuwapata wanaume hao ikiwa angefyatua risasi. Ndipo yeye, pamoja na LaKeisha na Isiminzile, wakawaona Nora na Azra wanavutwa kwa nguvu huku wakiwa wamefungwa, nao wakapelekwa kwenye magari yale, kisha baada ya wanaume wale wote kuingia, magari hayo yakaondoka upesi sana. Ilikuwa ni kama watatu hawa wamebaki kupigwa na butwaa zito kupita maelezo, kwa kuwa kufikia hapo ilikuwa wazi hata zaidi kwamba MAMBO YALIKUWA YAMEHARIBIKA.

Luteni Michael akawaambia Isiminzile na LaKeisha wabaki hapo ili yeye aende kwenye jumba lile kuangalia yaliyokuwa yametokea, lakini LaKeisha akakataa kubaki hapo na kusema wangekwenda pamoja. Isiminzile akamwambia Luteni Michael kwamba amkubalie tu, halafu yeye ndiyo angebaki hapo nje kuwasubiri. Hivyo, wawili hao wakatoka hapo na upesi kuwahi kwenye jengo lile, kwa kuwa walielewa kwamba wote walikuwa wameondoka.

Walipoingia huko ndani, Luteni Michael ndiye aliyekuwa ametangulia huku ameelekeza bastola yake mbele, naye alipofikia usawa wa miili ya Kendrick na Torres, akasimama kidogo baada ya kusikia sauti za mburuzo kwenye ardhi kutokea kule mbele. Akaanza kuelekea mbele zaidi kwa tahadhari, naye akaweza hatimaye kumwona chatu yule aliyekuwa akielekea mwishoni mwa jengo hilo, na kwa macho makali Luteni Michael aliweza kutambua kwamba kulikuwa na mtu anayewindwa hapo. LaKeisha alikuwa amebaki usawa wa miili ya Victor, Mensah, Kendrick na Torres, na kwa kutambua ilikuwa ni wao, akaanza kulia huku ameufunika mdomo wake.

Luteni Michael akajitahidi kunyata kwa umakini sana ili aweze kusogea kwenye sehemu ambayo ingempa nafasi nzuri ya kumuua chatu huyo kwa mpigo wa kwanza wa risasi, lakini akatambua kwamba kiumbe huyo aligundua kuna hatua nyuma yake, kwa sababu alikuwa ameukaribia uso wa windo lake lakini akageuza kichwa chake kwa nyuma huku akinyanyua shingo juu. Luteni Michael hakuona sababu ya kuendelea kusubiri tena maana tayari alikuwa ameonwa, hivyo hapo hapo akafyatua risasi iliyomtandika kiumbe huyo kichwani na kumfanya aanze kuupiga mwili wake mkubwa sakafuni kwa nguvu.

Jambo hilo lilimtia kinyaa sana Luteni Michael, lakini akajikaza na kuendelea kusogea karibu zaidi ili aweze kumsaidia mtu ambaye alikaribia kumezwa muda mfupi nyuma. Ndiyo baada ya kuhakikisha zaidi kwamba mtu huyo alikuwa ni Lexi, Luteni Michael akashusha pumzi kama vile amepata kitulizo fulani moyoni mwake. Akaendelea kusogea taratibu kumwelekea Lexi, huku LaKeisha akiwa anamfuata kwa nyuma, naye pia akapata kumwona rafiki yake.

Mwili wa chatu ukawa umetulia sasa, naye Luteni Michael akaupiga kwa mguu mara mbili lakini haukujongea. LaKeisha alikuwa amefunika mdomo wake huku akilia kwa huzuni sana baada ya kumwona Lexi katika hali aliyokuwa nayo. Luteni Michael akamfata mpaka karibu na kuchuchumaa, na wawili hawa wakawa wanatazamana kwa umakini. Uso wa Lexi ulijaa damu nzito baada ya kichwa cha yule chatu kupasukia karibu yake, hivyo Luteni Michael akaanza kumpangusa kwa kutumia nguo yake mwenyewe usawa wa kiwiko chake, kisha akambeba mikononi na kuanza kuelekea upande wa LaKeisha. Alimfikia mwanamke huyo na kumwambia waelekee nje upesi sana, na kwa haraka LaKeisha akatangulia mbele yao na kutoka ndani ya jengo hilo.

Walipofika nje, walielekea upande mwingine wa jengo hilo mpaka kwenye ile sehemu walikoyaacha magari yao, na baada ya Isiminzile kuwaona, akatoka sehemu ile ya kichaka alipojificha na kwenda kusaidizana na Luteni Michael kumbeba Lexi. Luteni Michael na Isiminzile wakamshusha Lexi usawa wa gari, na Lakeisha akachomoa tu kisu kimoja kutoka kiunoni kwa Luteni Michael na kuanza kuzikata kamba na gundi zilizoufunga mwili wake. Midomo ya Lexi ilikuwa ikitetemeka sana, naye LaKeisha alikuwa anazikata kamba huku akilia kwa sauti ya chini, huku wanaume wakimwangalia Lexi kwa huruma. Alipomaliza kuzikata, LaKeisha akamkumbatia Lexi kwa nguvu huku akiendelea kulia sana, naye Lexi akidondosha machozi bila kutoa sauti.

Luteni Michael alikuwa wa kwanza kutambua kwamba kuna magari ya maaskari na wanajeshi yaliyokuwa yamefika upande huo, hivyo akawaambia wote waingie kwenye magari upesi ili waelekee sehemu tofauti na hapo. LaKeisha na Isiminzile wakamsaidia Lexi kunyanyuka, kisha wakaelekea mpaka kwenye gari aliloendesha LaKeisha, Zelda akiwa kwa ndani bado. Isiminzile akarudi upesi kwenye lile lingine naye akaingia pamoja na Luteni Michael na kuanza kuliondoa hapo. LaKeisha akafungua mlango wa gari lake, naye Lexi akaingia ndani ya gari akipokelewa na Zelda, aliyeanza kumlamba usoni kuonyesha jinsi alivyomkosa sana. Lexi akawa anayachezea manyoya ya mnyama wake kipenzi huku akijitahidi kutabasamu, wakati huo LaKeisha akiwa ameshazungukia upande wa usukani na kuingia, kisha akawasha gari na kuanza kuliondoa pia.

Waliyaendesha magari yao kutoka eneo hilo bila kuwasha taa za mbele ili kutovuta uangalifu wa maaskari na wanajeshi, ambao tayari walikuwa wamesimama eneo la jengo lile matukio ya muda mfupi yalipofanyikia. Wakafanikiwa kuondoka na kuelekea sehemu tofauti bila kutumia barabara kuu; LaKeisha akilifuata gari la Luteni Michael kwa ukaribu, na sasa wakiwa wamewasha taa kumulika njia. Wakiwa mwendoni, LaKeisha alimuuliza Lexi kama alihisi maumivu makali sehemu yoyote mwilini, lakini Lexi akawa anamjibu kwa kichwa tu kwamba hakuhisi maumivu. LaKeisha alimwangalia sana Lexi na kuona ni jinsi gani alivyokuwa ameghafilika mno, na kiukweli hata yeye alihisi kufadhaika sana kwa kutoelewa yaliyokuwa yametokea.

Kuna vitu vingi sana ambavyo vilipita kwenye akili ya Lexi. Ilikuwa ni kama maisha yake yalijawa na laana mbaya sana, lakini sikuzote alipokuwa uso kwa uso mbele ya kifo, kuna njia fulani tu ilijitokeza ambayo ingeokoa maisha yake. Alifikiria kuhusu usiku ule familia yake ilipouawa kikatili. Kendrick alifanya yote aliyoweza kuuokoa uhai wake. Aliwaza kuhusu usiku ule alipokamatwa na wanajeshi na kupangiwa safari ya kwenda kwa Jenerali Jacob. Msaada mdogo tu aliopatiwa na Nora ulimwezesha kutoroka. Na leo hii tena, ilipoonekana kabisa kwamba hakukuwa na njia ya kuokoka, msaada usiotarajiwa ukafika kwake.

Hapana. Hizi hazikuwa bahati tu. Kuna kitu ambacho bado alitakiwa kutimiza. Kuna kitu ambacho kilizuia uhai wake kukoma, kwa sababu hiyo yote kwake ilianza kuonekana kama miujiza. Hakuamini kuhusiana na masuala ya roho za watu waliokufa kumlinda, lakini alihisi kwamba bado alikuwa hai ili kumaliza kile alichokianza, kwa kuwa kuna mtu alikuwa anamlinda. Watu wote wa muhimu kwake waliuawa vibaya, na wale waliobaki hawakuwa kwenye hali nzuri hata kidogo, kutia ndani yeye pia. Hivyo kazi bado ilitakiwa kukamilika, na wakati huu angehakikisha inamalizika. Kama ni kitu cha muhimu zaidi kwake alichokuwa amebakiza kufanya kwa sasa, ilikuwa ni kuwaokoa Nora na Azra kutoka kwa wabaya wake. Hangejali lolote lile ambalo lingetokea pembeni yake, hicho ndiyo kilichokuwa cha muhimu zaidi kwake kwa wakati huu.

Luteni Michael alisimamisha gari sehemu fulani iliyokuwa na nyumba ndogo, naye LaKeisha akasimamisha lake hapo vilevile. Akashuka na kuzunguka upande wa mlango wa Lexi, kisha naye Lexi akashuka, akimwacha Zelda ndani ya gari ingawa mnyama huyo alitaka kushuka pia. Luteni Michael akiwa pamoja na Isiminzile akawasogelea wanawake na kuwaambia waelekee kwenye nyumba hiyo, akisema ilikuwa ni jengo la mashine za kusaga nafaka, hivyo wote wakaelekea ndani huko. Walifika ndani, na Luteni Michael akawasha tochi ya simu yake ili kuangaza ndani hapo. Kulikuwa na mashine zenye vumbi na kutu, huku ardhini kukiwa na vumbi kali mpaka kwenye madirisha. Kuta zilijaa tandu za buibui, na kulikuwa na magunia mengi yaliyozagaa chini. Ilikuwa wazi sehemu hii haikutumiwa kwa muda mrefu.

Isiminzile alikuwa ameshikilia chupa yenye maji ya kunywa, ambayo aliitoa kwenye gari lile walilokuwemo, naye akampa Lexi ili anywe. Lexi akabaki kuyaangalia tu huku akipumua taratibu, kisha akapokea na kuanza kunywa taratibu sana. LaKeisha alikuwa amesimama kando yake huku anamwangalia kwa hisia, naye Luteni Michael akawa anamwangalia pia mpaka alipoacha kunywa maji.

"Lexi... what happened?" LaKeisha akaanza kuongea, akimuuliza Lexi ni nini kilikuwa kimetokea.

"Ni Kevin. Kevin ametugeuka Keish..." Lexi akajibu kwa sauti ya chini.

"What?" LaKeisha akashangaa.

"Ametusaliti... akatutupa mikononi kwa Jacob... amesababisha Victor na Mensah kuuliwa... na amemuua Torres na uncle Kendrick mbele yangu..." Lexi akamwambia huku chozi likimtoka.

LaKeisha akafunika mdomo wake kwa kushangaa sana. Isiminzile alikuwa ameshangaa pia, naye Luteni Michael akatazama chini.

"Why... kwa nini amefanya hivyo?" akauliza LaKeisha.

Lexi akabaki kimya tu.

"I'm... so sorry Lexi. I'm so sorry..." LaKeisha akasema huku akiusugua mgongo wa Lexi taratibu.

Lexi akashusha pumzi na kumuuliza, "Ulikuwa pamoja na uncle Kendrick walipomkamata?"

"No. After you left... Torres alibadili plan. Aliniacha chini na Isiminzile akisema kumchukua Jacob wangeweza wakiwa watatu tu..." akasema LaKeisha.

"Unamaanisha nini kubadili plan?" Lexi akauliza.

"Alisema kama kuna jambo lingekwenda down vibaya, basi ningekupa taarifa maana inaonekana alihisi hivyo... labda alimhisi Kevin, lakini hakuwa na uhakika bado. So... nilibaki, then watu wa Jacob wakaja pale tulipokuwa wakiwa na lengo la kuiangusha nyumba yetu yote. Lakini Michael akafika na kutusaidia kuwatoroka watu wake kabla... kabla hawajaniua," LaKeisha akasema kwa huzuni.

"Ku... kuiangusha nyumba?" Lexi akauliza kwa sauti ya chini.

"Wameilipua yote," Isiminzile akamwambia.

Lexi akaangalia chini kidogo, kisha akamtazama Luteni Michael.

"Tumebaki sisi tu Lexi. Yaani... its over. What are we going to do now?" LaKeisha akamuuliza.

"Wamemchukua Nora na Azra. Nataka kuwarudisha," Lexi akasema.

"Tunawarudisha vipi Lexi? Unaelewa kwamba sasa hivi hatuna chochote tulichobakiza?" LaKeisha akamuuliza.

"Sijasema tunawarudisha... nimesema NINAWARUDISHA," Lexi akaongea kwa mkazo.

Wote wakamwangalia kimaswali.

"Lakini Lexi... hautaweza kufanya kazi hiyo peke yako. Na... haujui wako wapi..." Isiminzile akamwambia.

Lexi akawa ananawa uso wake wakati huu, kisha akatupa chupa pembeni na kunyoosha kiganja chake kumwelekea Luteni Michael.

"Nipe bastola yako," Lexi akamwambia.

Luteni Michael akabaki kumtazama tu.

"Lexi please, don't be stupid. Nikisema its over namaanisha its over kweli! Acha kutenda kama mtu asiye na akili, haitakuwa rahisi kushinda sasa," LaKeisha akasema kwa ukali.

"Nimesema nipe bastola yako," Lexi akamwambia Luteni Michael.

"Na akishakupa? Utafanya nini? Utatoka tu, uende kuwarudisha mwenyewe, halafu mambo yote yatakuwa sawa eti?" LaKeisha akamuuliza.

"Whatever it takes!" Lexi akamwambia kwa uzito.

"Unaelewa kwamba unadili na watu wanaokuzidi kila kitu kwa wakati huu..."

"I don't care! Kila sekunde inayopita nikiendelea kuwa hapa ndiyo jinsi Nora na mdogo wangu wanavyozidi kupelekwa mbali nami. Nipe bastola ili nikamalize haya yote... kwa sababu yalianza na mimi," Lexi akaongea kwa hisia kali.

LaKeisha akamshika usoni kwa viganja vyake na kumwambia, "Lexi... please sikiliza. Kila kitu sasa kimepotea. Kutimiza unachotaka... tena kwa hali hii... haiwezekani tena. We've lost. Do you hear me? Tumepoteza huu mchezo. Najua ni ngumu lakini... unapaswa kukubali hilo..."

Lexi akaitoa mikono ya LaKeisha usoni kwake na kurudi nyuma.

"Kwa hiyo mnataka nifanye nini? Mlikuwa na lengo lipi kuja kunisaidia? Kwamba ningeingia tu mafichoni, niwaache watu pekee muhimu waliobaki na walio kwenye taabu? Nisingesita hata kama ingekuwa ni wewe LaKeisha, kwa kuwa nyie wote ni muhimu kwangu. Mensah... Victor... Torres... uncle Kendrick... wote wameuliwa mbele yangu... na sababu ilikuwa ni mimi kutoona mapema kwamba kulikuwa na nyoka katikati yetu...." Lexi akaongea huku machozi yakimtoka.

"Hapana Lexi... siyo makosa yako...." LaKeisha akawa anampoza.

"No... ni makosa yangu. Na sasa nimepewa nafasi ya kusahihisha makosa hayo, siwezi kuiacha ipite. Nitafanya kila kitu kuwatoa wawili hao mikononi mwa Jacob... hata kama usiponipa bastola," Lexi akaongea na kumtazama Luteni Michael.

Watatu hao wakawa wanamwangalia kwa umakini sana, naye Lexi akakwapua funguo za gari kutoka kiganjani kwa Lakeisha na kutaka kuondoka.

"Lexi!"

LaKeisha akataka kumfata lakini Lexi akamnyanyulia kidole kumzuia asimfate. Alikuwa makini sana, na hiyo ikamwacha LaKeisha akiwa amesimama tu, hivyo Lexi akageuka na kuanza kuelekea mlangoni tena.

"Nimeelewa... na ninaomba unisamehe..."

Lexi akasitisha kupiga hatua zaidi na kusimama tuli. Maneno hayo yaliyoka kwa Luteni Michael, naye Lexi akageuka na kumwangalia, akiwa haelewi anamaanisha nini. Wote sasa wakawa wanamtazama Luteni Michael.

"Maneno yako yalikuwa sahihi. Nilikuwa nikifuata tu amri kama mbwa, kama kipofu, bila kutambua kwamba nilikuwa nikitumikia upande mbaya..." Luteni Michael akaongea.

Lexi alikuwa anamtazama kwa makini tu, akihisi maneno ya mwanaume huyo yalielekea sehemu ya muhimu zaidi.

Luteni Michael akaanza kutembea kumwelekea Lexi huku akisema, "Nimeelewa vizuri ni kwa nini ulipigana nami usiku ule, na kwa kila jambo baya nililosema juu yako, ninaomba unisamehe. Mimi pia nilipoteza ndugu zangu sita kwa sababu ya Demba Group, kutia ndani mama yangu mzazi, na sasa naelewa hata zaidi kwamba maneno yangu yalikuumiza sana. Niombe tena samahani kwa hilo..."

Akawa amefika mbele yake sasa na kusimama huku anamwangalia usoni.

"Ni wewe pamoja na wenzenu ndiyo mmenisaidia kujua ukweli kuhusu watu waliosababisha maovu yale. Ninataka sana kuwakamata na kuwaua pia, hivyo ninaelewa unavyohisi. Sitakwambia maneno yoyote kukuzuia kufanya unachotaka kufanya. Sitakuzuia. Ila kama unataka kwenda huko, basi jua niko pamoja nawe. Sitakuacha uende mwenyewe, nitakusaidia kumkomboa Nora na mdogo wako... whatever it takes," Luteni Michael akasema.

Lexi akawa anamtazama kwa umakini sana.

LaKeisha akatazamana na Isiminzile kwa ufupi, kisha akamfata Lexi na kusimama karibu yake.

"Ninajua jinsi ilivyo ngumu kukuzuia kufanya unachotaka, you're just so stubborn!" LaKeisha akamwambia Lexi.

Luteni Michael akatabasamu kidogo.

"Una nafasi kubwa ya kufanikiwa kama tutashirikiana, so am coming with you too... na tafadhali... usiniambie hapana. Na mimi nimeamua kufanya nachokitaka," LaKeisha akasema kwa uhakika.

Lexi akatikisa kichwa kukubali.

Isiminzile akasogea karibu zaidi na kusema, "Sifahamu mambo mengi sana hapa lakini... sitaki kusema kwamba nina hamu ya kurudi nyumbani. Uliniambia mimi ni mmoja wenu sasa, na ninataka kupambana kama mmoja wa timu yako kweli, kwa hiyo niko pamoja nawe katika hili pia... kwa njia yoyote nitakayoweza kusaidia."

Lexi akatikisa kichwa kidogo, lakini akihisi tumaini na imani nyingi sana.

"Tunahitaji kujua watakuwa wanaelekea wapi sasa hivi ili kuwapata Azra na Nora kutoka kwao. Michael..." LaKeisha akasema.

"Ndiyo, hiyo haitakuwa na shida. Wanaelekea sehemu fulani kusubiri ndege binafsi iliyopangiwa kumpeleka Jacob Madagascar. Tunachopaswa kuangalia ni NJIA gani tutakayotumia kuwatoa huko na kuhakikisha tunawakomesha Jacob na Weisiko," Luteni Michael akasema.

"Ndiyo... ni kweli," Isiminzile akaongea.

Luteni Michael akamwangalia Lexi, na kisha akauliza, "Kwa hiyo... mpango ni nini?"

Lexi akavuta pumzi na kuishusha huku akimwangalia Luteni kwa umakini.....



★★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★★

WhatsApp +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA HAMSINI NA TATU

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Jenerali Jacob na Luteni Jenerali Weisiko walikuwa wameshafika sehemu ambayo Jenerali alifanya miadi ya kuletewa ndege ambayo ingempeleka nchini Madagascar (kwa wengine ni kisiwa), alikokuwa amepanga kutorokea. Eneo hilo lilikuwa ni kiwanja kipana sana ambacho hakikuwa na makazi ya watu kutokana na kumilikiwa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mdogo wa ndege, na kwa sehemu kubwa hakukuwa na miti mpaka kufikia upande ambao barabara ya lami iliishia. Yaani, barabara ya lami iliachwa mbali sana mpaka kufikia hapo, hivyo Jenerali na wenzake walikuwa wamefika kwenye kinyumba kidogo kilichojengwa muda fulani nyuma kwa ajili ya wafanyakazi waliokuwa wakisafisha uoto mwingi wa asili wa eneo hilo kwa majuma kadhaa.

Ikiwa ni saa 3 usiku sasa, bado ndege hiyo haikuwa imefika, kwa hiyo wanaume wa Jenerali Jacob wakawa sehemu ya nje wakilinda, huku kwenye nyumba ile ndogo wakiwemo Jenerali Jacob, Weisiko, yule Sniper, Nora, Azra, na Asteria. Wanawake hao walikuwa wamefungwa mikono na miguu yao, nao walikuwa wamekalishwa chini huku Majenerali wakiketi kwenye viti vidogo kutokea usawa wa mlango wakipata mazungumzo. Sniper wa Jenerali alikuwa amesimama tu pembeni akiwaangalia wanawake, na Kevin alikuwa sehemu ya nje ya nyumba hiyo.

"Ilikuwa inatakiwa ifike saa mbili?" Luteni Jenerali Weisiko akauliza.

"Yeah," Jenerali Jacob akajibu.

"Huku kuchelewa General... siyo ishara mbaya? Unajua tunakaribiwa sasa hivi..."

"Aagh... we punguza hofu Weisiko. Jali masikio yako hayo, ndege inakuja," Jenerali Jacob akamwambia kwa kukereka.

Weisiko alikuwa ameyaziba masikio yake kwa tishu laini na gundi ya karatasi, lakini bado aliweza kusikia kwa kadiri fulani. Jenerali Jacob akawa anamwangalia sana Nora, ambaye alikuwa amefungwa mdomoni kama wenzake, akimwangalia baba yake kwa macho yaliyoonyesha uchovu. Asteria akaanza kugeuza kichwa chake huku na huko, kama vile anapata shida fulani, naye Nora akamwangalia kwa wasiwasi. Akaanza kuongea ndani ya kiziba mdomo chake, lakini sauti zikawa zinasikika kama miguno tu. Alikuwa akimwambia jambo fulani baba yake, naye Jenerali Jacob akamwonyesha ishara Weisiko aende kumfungulia mdomo ili amsikie.

Baada ya Weisiko kunyanyuka, akamsogelea na kuivuta gundi kwa nguvu kutoka mdomoni mwa Nora, naye akaanza kupumua kwa nguvu.

"Mfungulie Aste, mpe maji, anahisi kiu!" Nora akafoka.

"Tuliza sauti hiyo mama, mimi siyo kijakazi wako," Weisiko akamwambia.

"F(...) you! Tuliwaambia mtulete huku? Wewe mshenzi, fanya ufanyalo lakini mpatie mtoto maji," Nora akasema na kuelekeza maneno hayo kwa Jenerali Jacob.

"Unajua Nora, nilidhani una akili sana, kumzidi hata mtu yeyote mwenye akili ambaye niliwahi kukutana naye. Wewe kwenda kinyume na mapenzi ya baba yako aliyekuzaa ndiyo kitu ambacho kinasababisha sasa hivi mdogo wako apitie shida hii. Au huoni kwamba haya yote ni makosa yako?" Weisiko akamwambia.

"Yaani wewe... na swagger zote na majivuno yote, bado tu unaburuzwa kama mbwa kwa kila kitu afanyacho huyo mwanaume... utaendelea kuwa malaya wake mpaka lini?" Nora akamwambia Weisiko.

"Una bahati sana kuwa mtoto wake, kwa sababu nisingesita kukipasua kichwa chako hiki kilichojaa utumbo tu," Weisiko akamwambia.

"Basi Weisiko, inatosha," Jenerali Jacob akaongea kutokea kule alipokaa.

Weisiko akasogea pembeni, naye Jenerali Jacob akanyanyuka na kuanza kumfata Nora taratibu mpaka alipomfikia na kuchuchumaa karibu yake. Nora akawa anamwangalia kwa hasira.

"Kile ambacho nimekupa, kile ambacho naenda kukupa, yule mwanamke kamwe hangeweza kukupatia. Sihitaji unionyeshe shukrani yoyote, lakini sitaacha kuwa baba kwako, na hii ndiyo njia yangu... upende usipende," Jenerali Jacob akasema kwa utulivu.

Nora akamtemea mate usoni, naye Jenerali Jacob akajifuta kwa nguo usawa wa mkono wake.

"Najua hizo zote ni hasira kwa kilichompata "baby" wako, lakini hiyo ingempata tu kwa njia moja au nyingine, kwa sababu she had it coming. Ishapita... move on my dear," Jenerali Jacob akamwambia.

Nora akaanza kutokwa na machozi, akiwa amekumbukia hali waliyomwacha nayo Lexi kule kwenye lile jengo muda fulani nyuma. Akainamisha kichwa chake chini, naye Jenerali Jacob akamsogelea Asteria na kutoa gundi yake ya karatasi mdomoni.

"Sorry mpenzi, nilikuwa nimesahau kwamba huku hata mkipiga kelele hazitasaidia kitu hmhmm.... Pole kwa kiu, na usijali. Ndege inafika sasa hivi. Utapata kila kitu, okay?" Jenerali Jacob akamwambia Asteria.

"Mimi... sitaki ndege baba... nataka unirudishe nyumbani. Umenitoa huko tangia asubuhi na kunifungia kama mnyama, kwa nini?" Asteria akaongea kwa hisia.

"Mwanangu... ni ili twende sehemu nzuri zaidi..."

"Sitaki kwenda. Unaniteka mimi na dada ili kuki..."

"No, no, no. Sijawateka. Aste... ninawalinda," Jenerali Jacob akasema.

"Kutulinda na nini?" Nora akamuuliza.

"Kwa sababu ya upuuzi wako kuna watu sasa hivi watataka kumuumiza mdogo wako! Nisingekaa kuangalia hilo," Jenerali Jacob akamwambia.

"Ndiyo umfanyie huyu mtoto hivi? Alikutuma uchague hayo maisha uliyoamua kuchagua?" Nora akauliza.

"Nisikilize Asteria. Utakuwa sawa. Madagascar tutaenda sehemu ambayo hakuna mtu atatusumbua, na baada ya muda mfupi utaenda sehemu yoyote ile unayotaka, I promise," Jenerali Jacob akasema.

"Vipi kuhusu Flora? Na yeye utamtoa Marekani umpeleke huko?" Asteria akauliza.

Jenerali Jacob akabaki kimya.

"Unajua kwamba hakuna mtu yeyote kutokea sasa ambaye atakupenda, ndiyo maana unalazimisha kujionyesha kwamba unatupenda. Huu siyo upendo, ni ubinafsi na ulimbukeni. Angalau ulikuwa umebakiza upendo wa Aste na Flora, lakini sasa hata huo umepoteza. Tena Flora... ahah... yaani ujue ndiyo umempoteza kabisa, maana sasa kila kitu kibaya nilichomwambia kuhusu jinsi ulivyomtendea mama... alivyokuwa anapinga... ujue ndiyo imezidishwa mara mbili kwa yeye kujua haya yote uliyofanya. Upendo wake kwako utakuwa chuki tupu akijua umetutendea hivi. Hauna chochote ulichobakiza tena. Hauna... chochote... tena."

Aliyekuwa akiongea maneno hayo yaliyomchoma sana Jenerali Jacob ni Nora.

Jenerali Jacob akang'ata meno yake kwa kuhisi hasira, lakini akanyanyuka tu na kumgeukia Weisiko. Maneno ya Nora kweli yalikuwa yamemkata sana amani yoyote iliyokuwa ndani yake, kwa sababu kati ya binti zake wote watatu, Flora aliyekuwa Marekani ndiye aliyekuwa wa karibu zaidi kwake; zaidi hata ya Asteria. Lakini sasa Nora kumkumbusha kwamba na Flora angekuwa ameshaona matendo ya baba yake, kukamnyima raha kiasi kwamba akasogea pembeni na kuanza tu kuvuta sigara huku akitafakari vitu vingi. Weisiko akamsogelea Azra na kumtolea gundi ya karatasi mdomoni kwake, akiwa anamwangalia kwa umakini, kisha akazishika nywele zake laini kwa njia ya kuzilaza, lakini Azra akageuzia kichwa chake pembeni kwa kasi sana.

Weisiko akasimama na kumfata Jenerali Jacob pale alipokuwa, na wakati huu, Jenerali Jacob alikuwa ameweka kifaa kidogo cha mawasiliano karibu na mdomo wake, naye Weisiko akamsikia aliposema kwamba ndege ishushwe upesi sana kwa kuwa muda haukuwa rafiki kwao. Jenerali aliposhusha kifaa hicho, Weisiko akauliza vipi, naye akasema ndege ingetua hapo ndani ya dakika tano, hivyo wawaandae wanawake hao watatu kutoka nje upesi ili ikishuka tu wapande haraka. Weisiko akaelekea nje na kuwaita wanaume wanne ili waje kuwachukua Nora, Azra, na Asteria, nao wakaingia upesi na kwenda kuwanyanyua, kisha wakaanza kuwasukuma kuelekea nje ya nyumba hii. Azra ndiye aliyeshikwa na wawili kutokana na kuwa hatari zaidi, lakini hakuwa na mpango wa kujinasua kutokana na matumaini yake kupotea.

Wakatoka nje na kuanza kuelekea sehemu ile pana zaidi huku Jenerali Jacob akiongoza mbele, nao wakaiona ndege ikiwa angani na ikianza kushuka taratibu kuelekea eneo hilo mpaka chini. Jenerali Jacob akaendelea kuwaongoza wengine kwa kutembea upesi kuelekea pale ndege ilipotua na kusimama, na ndiyo hapo wakashtushwa na sauti ya mlio wa risasi kutokea nyuma yao!


DAKIKA KADHAA NYUMA....


Lexi pamoja na Luteni Michael walikuwa wameunda mpango mzuri wa kile ambacho wangefanya baada ya kumfikia Jenerali Jacob. Hakukuwa na mambo mengi sana, kilichokaziwa hasa ilikuwa kuhakikisha wanafanya mambo kwa akili ili Nora na Azra wasiumie kabla ya kuwaokoa, na ili kuwamaliza maadui wao. Jambo la kwanza ingekuwa ni kuhakikisha wanaume wa Jenerali wanapunguzwa haraka kwa njia mbili; aidha kimya kimya, au moja kwa moja, ikitegemea na ni hali ya aina gani wangeikuta eneo hilo kwa sababu hawakuwa na njia ya kujua jinsi ambavyo maadui wangekuwa wamejipanga, kutia ndani na jinsi giza lilivyokuwa zito.

Lakini, kwa msaada wa darubini ya Luteni Michael, wangeweza kuona sehemu za huko hata zikiwa na giza, kwa kuwa kifaa hicho kilitengenezwa kwa mfumo unaowezesha kuona vitu vya mbali hata gizani, vikiwa vya rangi ya kijani. Lexi akasema kwamba cha kwanza kuondoa kwenye kundi la Jenerali ingekuwa ni yule Sniper wake, kwa hiyo wangetakiwa kutambua angekuwa amekaa wapi ili yeye awe ndiyo shabaha ya kwanza kabla hawajaanza kushughulika na wengine. Luteni Michael aliweka wazi kwamba bila shaka mtu huyo angekuwa sehemu ambayo kama angeona adui anakuja, basi angehakikisha anaondolewa, kwa hiyo wangetakiwa kufika maeneo yale lakini kwa umbali fulani kutokea huko ili magari yao yasionekane yakienda, kisha ndiyo wao wangeelekea huko ili kushughulika nao.

Baada ya kukubaliana, Luteni Michael alikwenda na Isiminzile ndani ya gari na kutangulia, na kabla Lexi na LaKeisha hawajaondoka kwenye nyumba hiyo, LaKeisha akamwambia amsubirie ili akamfatie kitu fulani. Akatoka na kurudi akiwa amebeba vazi lile la Lexi la mapambano la ziada, naye Lexi akaonyesha shukrani kwa kulichukua na kulivaa. LaKeisha akamkumbatia na kumwambia kwamba wanakoenda, wanakwenda kushinda, na si vinginevyo, naye Lexi akatia maanani maneno yake, kisha wakatoka na pamoja kwenda kuchukua gari.

Wakiwa mwendoni ndani ya gari, Lexi aliendelea kukumbukia vifo vya wapendwa wake wote waliokufa kikatili kutokana na ubaya huu wote uliokuwa umesababishwa na Jacob Rweyemamu, naye akakaza ngumi kwenye usukani akiwa na nia, tamaa, na dhamira ya kuhakikisha kwamba usiku huu, basi ingekuwa basi.



Luteni Michael alilifikisha gari pande zile ambako alijua ndiyo Jenerali Jacob alikuwepo, naye akaliegesha usawa wa mti mmoja na kushuka pamoja na Isiminzile. Eneo hilo halikuwa na gari hata moja lililopita, na wawili hawa wakaelekea kwenye mwinuko mdogo, na kisha Luteni Michael akatoa darubini yake na kuanza kuzungusha macho kuelekea kule uwanjani. Alitafuta kwa umakini sana kuona mtu yeyote akijongea, na hatimaye akawaona wanaume wawili wa Jenerali Jacob wakiwa wamesimama na bunduki mikononi. Akaendelea kufatilia taratibu eneo la hapo, akimtafuta yule Sniper, lakini hakuweza kumwona sehemu yoyote hapo.

Lexi na LaKeisha wakawa wamefika usawa huo, naye Luteni Michael akawafata na kuwaambia aliyoona. Akasema kiukweli haingekuwa rahisi kujua ikiwa nafasi ya kwenda kwa umakini bila kuvuta uangalifu wa wanaume hao ingetokea na kuwezekana, na njia iliyokuwepo ni kwenda moja kwa moja mpaka huko kwa sababu eneo lote hilo lilikuwa la wazi; kitu ambacho kilikuwa hatari. Kutokea mbali sana, sauti za ving'ora vya magari ya polisi zilisikika, bila shaka wakizunguka sehemu hizo katika uchunguzi wao kutokea kwenye jengo lile la godown walikotoka. Lexi akawaambia wengine kwamba sasa angefanya mambo kwa njia yake, akimaanisha kwamba angekwenda mwenyewe. Wote watatu wakakataa, wakisema hili ni jambo ambalo wangelifanya pamoja na si vinginevyo.

Kwa kuwa Lexi alitambua kwamba wenzake wasingekubali kitu kama hicho, akasema sawa, wasogee pale kwenye mwinuko na kuangalia mazingira upesi ili kubuni chochote kile haraka, kisha wangekwenda pamoja. Wote walipogeuka ili kwenda kufanya hivyo, Lexi akaikwapua bastola ya Luteni Michael kutoka kwenye mkanda wake na kuwanyooshea watatu hao. Walibaki kumshangaa! LaKeisha akauliza nini Lexi alikuwa anafanya, naye akasema asingejiruhusu kuendelea kupoteza muda namna hii, kwa sababu hakukuwa na njia "salama" ya kumaliza mambo haya yote, kwa hiyo angekwenda mwenyewe.

Wenzake walikuwa wanamwangalia tu, na kwa kujiamini LaKeisha akataka kumfata lakini Luteni Michael akamzuia kwa kumshika mkono, kama kusema wamwache tu Lexi afanye anavyotaka. Lexi akaelekea mpaka kwenye gari alilokuja nalo Luteni Michael na Isiminzile, naye akalichukua na kuliondoa hapo upesi sana kuelekea kule kwa wabaya wake, yaani moja kwa moja. LaKeisha akabaki kulalamika, akimwambia Luteni Michael kwamba hicho ni kitu cha kipuuzi walichokuwa wamemwacha Lexi afanye, na wangepaswa kwenda huko pia ili kumsaidia.

Luteni Michael akasema bila shaka wangekwenda kumsaidia, haijalishi nini kingetokea. Akasema Lexi alifanya vile akiwa ana lengo la kuhakikisha hakuna mwingine kati yao atakayeumia, lakini wasingeacha kwenda hata kama haikuwa salama, kwa sababu hili lilikuwa pambano lao pia. Akamwambia Isiminzile kwamba angetakiwa kubaki hapo kwenye ile sehemu ya barabara, ili wanajeshi na maaskari wakipita hapo, awaambie kule ambako Jenerali Jacob na Luteni Jenerali Weisiko walikuwa ili waende haraka pia. Yeye na LaKeisha wangekwenda kufanya chochote kile ili kumsaidia Lexi kuwakomboa Nora na Azra.

Kwa hiyo, ikambidi LaKeisha ashike usukani wa gari alilokuja nalo pamoja na Lexi ambalo Zelda alikuwa ndani, naye Luteni Michael akaingia kwenye sehemu ya nyuma ya buti ili kuwa salama. Ilikuwa ni kama vile wamemwachia tu Mungu kwa ambayo yangefuata baada ya hapo, nao wakaanza kuelekea kule hatimaye na kumwacha Isiminzile anawasindikiza kwa macho.

★★

Wakiwa ndiyo wametoka sasa ndani ya nyumba ile ndogo na kuanza kuelekea sehemu ile pana zaidi, Jenerali Jacob na wengine walianza kuiona ndege ikiwa angani na ikionekana kushuka taratibu kuelekea eneo hilo. Weisiko, Kevin, na wanaume wengine walikuwa wanafurahia sana, kwa kuwa sasa wangeweza kuondoka kiaina bila kusumbuliwa, naye Weisiko akawa anamsifia sana Jenerali Jacob. Ndege Ilifika mpaka chini na kuanza kupunguza mwendo, na ilikuwa kubwa kuzidi hata ndege za kibinafsi, lakini siyo kuzidi zile kubwa za abiria. Jenerali Jacob akawa anawaongoza wengine kwa kutembea upesi kuelekea pale iliposimama, na ndiyo hapo wakashtushwa na sauti ya mlio wa risasi kutokea nyuma yao.

Walipogeuka, wote waliona kwamba mmoja wa wanaume wa Jenerali alikuwa amebaki nyuma zaidi, akifyatua risasi kuelekea upande ambao gari fulani jeusi lilikuwa likija kwa kasi sana. Gari hilo likiwa limekaribia hapo, likapita na mwanaume huyu aliyekuwa akilifyatulia risasi nyingi zaidi wakati huu na kumgonga vibaya sana, kisha likatulia mbele ya wengine. Wote walikuwa wameelekeza bunduki zao kulielekea, lakini Jenerali Jacob akawaambia wasifyatue risasi. Ni kwamba alitambua gari hilo kuwa moja ya magari wanaume wake maalumu waliyotumia, na alikumbuka kwa leo alikuwa amewaagiza kwenda kwenye nyumba ya kundi la Kendrick ili kuisambaratisha. Kwa hiyo alitaka kujua ni kwa nini liko hapa wakati huu, na kwa nini mmoja wa wanaume hao angediriki kumgonga vibaya mtu mwingine aliye upande wake.

Nora na Azra walikuwa wakitafakari kuhusu ni nini kilikuwa kinaendelea, kama kujiuliza ikiwa kuna mtu alikuwa amefika kuwasaidia, basi angekuwa nani. Kwa kuwa ilikuwa giza na vioo vya gari hilo vilikuwa vyeusi, mtu aliyendani asingeonekana, naye Weisiko akamuuliza Jenerali Jacob kwa nini alitoa amri kwa wanaume wake kutofyatua risasi. Jenerali Jacob akabaki kimya tu, akisubiri mtu au watu walioko ndani mule watoke, na ndipo mlango wa gari hilo ukafunguka na mtu huyo kutoka, yaani Lexi. Alitoka tu na kupiga hatua chache mbele, kisha akasimama kwa kutulia.

Wote waliokuwa wakimwangalia walishangaa. Nora na Azra walitoa macho kwa kutoamini kabisa waliyemwona hapo mbele. Jenerali Jacob, Weisiko, Kevin, yule Sniper, na wanaume wengine walishindwa kuelewa iliwezekana vipi Lexi kuwa hai baada ya kumwacha mbele ya kifo cha mnyama mkali. Lexi akawa anawatazama tu jinsi walivyopigwa na butwaa, naye Nora pamoja na Azra wakaanza kucheka-kulia kwa furaha kubwa waliyohisi moyoni mwao.

"Hivi... nahitaji kuliua hili litoto mara ngapi ili life?" Jenerali Jacob akauliza kwa hasira.

Kevin alikuwa ameingiwa na hofu, asiamini kabisa kwamba Lexi ni mzima. "Mnasubiri nini... muueni!" akaongea kwa presha.

Lakini katikati ya maneno hayo, tayari Lexi alikuwa amerudisha mikono yake kwa nyuma na kuivuta mask ngumu ya nguo yake ya mapambano iliyoziba mpaka kichwa na kisha kukivalisha, na hapo akaitoa bastola yake kwa kasi. Wote walikuwa wameanza kumfyatulia risasi, lakini kwa sababu zilidunda akajitahidi sana kumlenga kwanza Sniper wa Jenerali Jacob. Huyo Sniper alikuwa amefikiri kwamba risasi zile zingemuua Lexi, ndiyo sababu yeye hakumnyooshea bunduki. Kwa hiyo Lexi alipofyatua tu risasi hiyo, moja kwa moja ikamtandika kifuani na kumfanya adondoke chini kwa kishindo.

Jenerali Jacob na Weisiko walishangaa sana, na ndipo Kevin akawaambia kwamba nguo ya Lexi ilikuwa ngumu mno wasingeweza kumuua kwa kumpiga risasi, hivyo akawasihi wakimbilie kwenye ndege upesi. Kufikia sasa, Lexi alikuwa akijibizana risasi na wanaume wa Jenerali Jacob, na alikuwa anawadondosha tu chini kwa kuwa za kwao hazikumdhuru sana, ingawa alihisi maumivu mengi mwilini kwa jinsi zilivyokuwa zinaipiga nguo yake ngumu. Jenerali Jacob, Weisiko na Kevin wakawa wanaikimbilia ndege, huku Nora, Azra na Asteria wakivutwa kwa nguvu na wanaume waliowashikilia. Lexi akawa amewamaliza wale wengine wote, na alihisi ni kama mwili wake unaunguzwa na joto kali lililomchoma-choma sana, na pia, sehemu ya chini ya mdomo wake ilikuwa imechunwa kwa risasi, kwa hiyo alihisi maumivu sana lakini akajikaza tu na kuanza kuwafata.

Jenerali Jacob na wengine walikuwa wameifikia ndege wakati huu, na kutoka ndani yake walikuwa wameshuka wanaume wengine wawili waliokuwa wamebeba bunduki huku wakizielekeza kwa Lexi, aliyekuwa akiwafata kwa nguvu zake zote alizobakiza, na wakati huu hakuwa ameshika bastola kwa kuwa ile aliyokuwa nayo iliishiwa risasi.

"Kill her!"

Jenerali Jacob akafoka namna hiyo huku akianza kupanda ngazi fupi za kuelekea ndani ya ndege, na wengine wakimfata, na hapo hapo wanaume wale wawili wakaanza kufyatua risasi kumwelekea Lexi. Akageuza mwili wake na kuwa kama amewapa mgongo, kwa sababu nguvu ya nguo yake ya kuzuia risasi kwa upande wa mbele ilikuwa imepungua, na papo hapo Lexi akasikia kishindo cha nguvu kutokea nyuma yake. Akageuka, na hapo akapata kuona gari lile alilowaachia akina Luteni Michael likiwa limeigonga ndege hiyo sehemu ya tairi la kushoto kwa nyuma, nayo ikakosa mhimili na kuangukia upande mmoja, ingawa bawa refu la upande huo lilizuia yote isianguke chini.

Jambo hili lilifanya Jenerali Jacob na wengine waliokuwa naye mule ndani ya ndege waangushwe kwa upande mmoja, na hili likamkasirisha sana kwa kuwa sasa mpango wao wa kutoroka ulikuwa umevurugwa. Azra ndiye aliyejigonga vibaya, na kwa mara nyingine tena akapoteza fahamu, hasa kwa sababu bado kichwa chake kilimsumbua kutokana na kupoteza fahamu muda fulani nyuma. Weisiko, akiwa amekasirishwa pia, akachukua bastola na kujitahidi kutoka nje ili aende kummaliza Lexi yeye mwenyewe, kwa kuwa alichoshwa sana na mambo yote haya.

Lexi, pamoja na wale wanaume wawili, wakawa wanalitazama gari hilo jinsi lilivyokuwa limeharibika upande wa mbele baada ya kuigonga ndege, na hapo hapo ikasikika sauti kutokea upande wa nyuma wa gari hilo ikisema, "Lexi, get down!" yaani Lexi aende chini, na kwa kasi sana Lexi akajitupa chini upande mwingine. Ilikuwa ni Luteni Michael ndiye aliyesema maneno hayo, na ilikuwa ni muda huo huo alipomaliza kuyasema ndiyo akawa amerusha bomu dogo la funguo kuwaelekea wanaume wale, nalo likawalipukia walipokuwa wamesimama kwa kuwa hawakuliona vizuri wakati limerushwa. Masikio ya Lexi yalipatwa na maumivu makali kwa sababu hayakutarajia mlio wa bomu, na kwa upande aliporukia, kiasi fulani cha udongo mzito uliochimbika baada ya bomu hilo kulipuka ukaufunika mwili wake.

Baada ya Luteni Michael kuwa amerusha lile bomu, akatoka usawa wa nyuma wa gari lake na kwenda kumwangalia LaKeisha, ikiwa alikuwa sawa. Lakini ingekuwa ngumu sana kujua kama alikuwa sawa kwa sababu kama tu angefungua mlango, basi Zelda angemuumiza ikiwa angemwona. Hivyo, akafikiria kwenda kumfata kwanza Lexi pale chini kuona ikiwa na yeye alikuwa sawa, kisha wamsaidie LaKeisha; aliyekuwa amechukua maamuzi magumu ya kuigonga ndege ili kumzuia Jenerali Jacob kutoroka.

Luteni Michael akaanza kuelekea sehemu aliyomwona Lexi amerukia muda mfupi nyuma, na ile alipokaribia tu hapo, akapiga kelele ya maumivu baada ya kutandikwa risasi kutokea nyuma, ikiwa imempata sehemu ya chini ya bega lake la kushoto, naye akadondokea chini na kuviringika, kisha akatulia kidogo na kuangalia upande wa ndege. Hapo akamwona sasa Weisiko akiwa anamwelekea huku ameshikilia bastola, na nyuma yake alifuatwa na Kevin pamoja na wanaume wawili waliokuwa wamemshikilia Azra kabla hajapoteza fahamu.

"Yuko wapi huyo malaya?!" Weisiko akafoka namna hiyo huku akimwelekea Luteni Michael.

Luteni Michael alihisi maumivu makali mgongoni, lakini akajikaza na kupitisha mkono wake mpaka sehemu ya kiuno chake, naye akatoa kisu kidogo na kukishikilia kwa nguvu kwenye kiganja chake huku akimwangalia Weisiko kwa hasira na maumivu.

"Nimeuliza yuko wapi? Nyie washenzi wote ni wasaliti tu!" Weisiko akaendelea kufoka.

"Wei... mheshimiwa... tunatakiwa kutafuta njia ya kuondoka maan...."

"Kaa kimya!" Weisiko akamkatisha Kevin alipokuwa anaongea hivyo.

"Maaskari wanakuja! Tunatakiwa kuondoka! Muue tuondoke!" Kevin akamwambia kwa sauti ya juu.

Weisiko akamgeukia na kumshika shingoni kwa nguvu huku akikandamiza bastola yake kwenye shavu.

"Wewe kama nani unanisemesha hivyo?" Weisiko akamuuliza kwa sauti tulivu, lakini kikatili.

Kevin akawa anamwangalia kwa hofu na hasira kiasi.

Ni wakati huu ndiyo Jenerali Jacob alikuwa ametoka ndani ya ndege ile kwa msaada wa wanaume wale wengine wawili ambao walikuwa wamewashikilia Nora na Asteria, lakini sasa wakawa wamewaacha tu ndani huko. Kule ndani ya ndege, Nora alikuwa akijitahidi sana kutafuta chochote cha kumsaidia kuzikata kamba zilizokuwa zimemfunga ili ajinasue na kuwasaidia wenzake, na rubani wa ndege hiyo alikuwa amepoteza fahamu kwa sababu ya kujigonga vibaya ndege ilipoangukia upande mmoja. Kwa hiyo sasa hapo nje, Jenerali Jacob akawa anamwona Weisiko alipokuwa amemshika Kevin kama anataka kumpiga kwa risasi, naye akaita kwa sauti ya juu na kumuuliza kilichokuwa kinaendelea.

"Anataka tu kuniua General... me hata sijamfanya kitu!" Kevin akapaaza sauti.

"Unasemaje wewe?!" Weisiko akaongea kwa hasira.

"Weisiko! Hebu acha hayo mambo... tutafute njia ya kuondoka hapa haraka!" Jenerali Jacob akafoka.

Weisiko akamsukuma Kevin na kusema, "Hapa kilichobaki ni kuwamaliza tu hawa... ona, hadi na huyu jamaa... Luteni ushenzi ametusaliti," Weisiko akamwambia.

"Aliwahi kuwa kwenye mipango yetu kwani? Muue kama unataka, tuondoke!" Jenerali Jacob akafoka.

Weisiko alikuwa amemgeukia Luteni Michael ili amwongezee risasi nyingine tena, lakini ndiyo hapo Luteni Michael alikuwa ameweza kuusawazisha mwili wake vizuri kiasi na kukirusha kisu kile, kilichomponda Weisiko mkononi na kufanya adondoshe bastola yake. Hakikumchoma, kiliponda tu sehemu ya mkono wake kwa kumkata kiasi usawa wa sehemu ya kuvalia saa, na maumivu yakamfanya aidondoshe bastola. Wale wanaume wawili waliokuwa wamesimama usawa wa Kevin, hawakuwa na silaha, kama wenzao tu ambao walikuwa wamewashikilia wanawake muda mfupi nyuma, hivyo wakatoka kwa kasi walipokuwa na kumfata Luteni Michael pale chini ili wamuue wenyewe, wakati huo Weisiko anaugulia maumivu mkononi.

Wanaume hao wawili wakiwa wamemfikia Luteni Michael, papo hapo rundo la michanga likaruka kwa nguvu kutokea chini, ikiwa ni Lexi ndiye aliyenyanyuka upesi namna hiyo! Wakiwa wameshtushwa na jambo hilo, wanaume hao wakazubaa kiasi, lakini Lexi hakujichelewesha na kuitumia nafasi hiyo kuwarukia na kuwatandika kwa nguvu sana vifuani kwa mateke sambamba, na mwili wake ukadondokea pembeni huku wanaume hao wakianguka chini pia. Jambo hilo lilikuwa limefanya Kevin ashtuke na kuanza kurudi nyuma, ikionekana ni kama mfu ametoka kaburini baada ya Lexi kufanya vile, naye Weisiko akasimama wima huku akimtazama.

Lexi akajisawazisha na kusimama pia, kisha kwa ustadi akawarukia tena wanaume wale wawili na kuanza kuwapiga kwa njia zenye kuwatia maumivu makali sana ili wakianguka, wasinyanyuke. Jenerali Jacob akiwa amesimama usawa wa ndege ile, akawa anaangalia hayo yote kama anasubiri kuona ni yapi yangefuata, akiwa anahisi kukerwa sana kutokana na jinsi ambavyo mtoto huyo wa Casmir alionyesha kutokata tamaa ingawa alimvunja moyo kwa njia nyingi.

Wakati hayo yalipokuwa yakiendelea muda huo huo, kule ndani ya ndege Nora alifanikiwa kuzifungua kamba za mikono yake kwa kuzisugua katikati ya kioo kilichopasuka, na upesi akaifungua miguu yake, kisha akaanza kuzikata na zile zilizomfunga Asteria. Alipomaliza, akamwambia mdogo wake amsaidie kuzifungua za Azra na akae naye humo humo ili kumwangalia mpaka atakapoamka, halafu yeye aende nje kumsaidia Lexi. Asteria alikuwa anaogopa, lakini dada yake akamtia moyo awe jasiri kwa kumwambia alikuwa imara kuliko alivyofikiri.

Baada ya Asteria kukubali na kuanza kumfungua Azra kamba, Nora akajivuta na kuufikia mlango wa kutokea pale kati, na alipoangalia pale nje, akawaona wanaume wale wawili wakipigwa na Lexi upande wa mbele zaidi, na hapo karibu walikuwa wamesimama wanaume wawili wa Jenerali na Jenerali Jacob mwenyewe. Kulikuwa na kopo la wastani la kuzimia moto (fire extinguisher) lililotundikwa usawa huo wa mlango, likiwa la chuma, naye Nora akalibandua na kulishika mkononi kwake, kisha akaruka kutoka hapo mpaka pale chini.

Kishindo alichotua nacho kikawashtua wanaume wale wawili, ila walipogeuka tu, Nora tayari alikuwa amejinyanyua na kulipeleka kopo hilo kwa nguvu sana kuelekea kichwa cha mmoja wao na kukipiga kwa nguvu mno, na mwanaume huyo akaweweseka na kudondokea pembeni. Yule mwingine alipojaribu kumkamata, Nora akavuta sehemu inayofungua hewa kuruhusu madawa ya kuzima moto yatoke, yakiwa kama moshi mzito wa poda, nayo yakamrukia usoni mwanaume huyo na kusababisha aumie macho na kushindwa kuona vizuri. Alipoona amemkengeusha vya kutosha, akamsogelea na kumpiga kwa chuma hicho pia, na jamaa akaanguka na kupoteza fahamu. Nora alipokuwa anataka kumwangalia baba yake, akashtukia anapigwa kofi zito lililomfanya aanguke chini, na chuma kile kikapigwa kwa mguu kutoka mikononi mwake. Nywele zake zikashikwa nyuma ya kichwa naye akaanza kuvutwa juu huku akijitahidi kujinasua.

Muda huo huo, tayari Lexi alikuwa ameweza kuwamaliza kabisa wanaume wale wawili kwa kuwanyonga shingo zao, na sasa akawa amesimama na kumwangalia Weisiko huku akipumua kwa nguvu. Weisiko akatabasamu na kuangalia pale bastola yake ilipokuwa imedondokea, na haikuwa mbali naye sana. Kevin akageuka nyuma na kumwona Jenerali Jacob akiwa anamwokota Nora kutoka chini kwa kuzivuta nywele zake, na ni hapo ndiyo akaanza kusikia sauti za ving'ora vya magari ya maaskari kutokea mbali zikija eneo hilo. Hapa hakuona tena haja ya kujiweka upande wowote ule, kwa sababu alichotaka ilikuwa ni kutoroka tu, na wazo la kwanza likawa ni kuelekea sehemu ile walikoyaacha magari yale sita ili achukue moja na kukimbia.

"Nafikiria kukuua tu kwa risasi, lakini hiyo itakuwa rahisi mno. Nataka hii sasa tuizime kwa njia isiyo mpya hata kidogo..."

Weisiko ndiye aliyekuwa akisema maneno hayo kumwelekea Lexi, naye akaisogelea bastola ile pale chini na kuipiga kwa teke mbali zaidi, kisha akamwonyesha Lexi ishara ya "njoo" na kukunja ngumi huku anamwangalia kwa ukatili.

Lexi akaivua mask yake na kuitupa pembeni, na uso wake mweupe ulionekana vyema kwenye usiku huo mchanga, na alikuwa akitiririkwa na damu kutoka upande mmoja wa kichwa chake. Alipotazama nyuma ya Weisiko, akamwona Kevin akiwa anaanza kuelekea upande mwingine ili awazunguke na kukimbia, naye Lexi akatoka alipokuwa na upesi kuanza kumfata. Weisiko akabaki kushangaa, na pale Kevin alipogeuka akakutana na teke la nguvu lililopiga sehemu ya taya yake ns kumfanya adondoke chini.

Weisiko akaona amfate yeye mwenyewe, kwa sababu kwa kiburi alidhani kwamba Lexi anamwogopa, lakini alikuwa amekosea sana. Kevin akanyanyuka huku akiwa na hasira, naye akamfata Lexi akiwa na lengo la kumpiga, lakini Lexi akamkwepa na kumtandika kwa nguvu sana tumboni. Kevin alipoinama kidogo, tayari Weisiko alikuwa amefika hapo, naye akampiga Lexi kwa nyuma, lakini hakumuumiza kutokana na ugumu wa nguo yake. Kwa hiyo Weisiko akatambua kwamba angepaswa kulenga uso na kichwa cha "mwanamke" huyo zaidi, naye akaanza kumrushia ngumi akilenga kichwa chake, lakini Lexi akawa anayapinga mapigo yake na kumtandika yeye hapa na pale kwa kasi. Kevin naye akajikaza na kuanza kumshambulia Lexi, hivyo ikawa ni wanaume wawili dhidi ya "mwanamke" mmoja.

Kupigana huku kulipokuwa kunaendelea, Jenerali Jacob alikuwa anamvuta Nora kuelekea kule ambako waliyaacha magari yao walipofika eneo hilo, kwa kuzungukia upande wa mbele wa ndege, na Nora alikuwa akihisi maumivu sana tumboni kwa kuwa baba yake alimpiga ili kumlegeza. Akawa anamtukana, akimwambia pia kwa lolote analotaka kufanya asingefanikiwa, na ndipo Jenerali Jacob akachoka na kuamua kumtupa chini kwa nguvu. Nora alipomwangalia baba yake, akakuta ametoa bastola yake na kumnyooshea, ikionekana dhahiri kwamba alitaka kumuua. Nora akatabasamu kidogo na kuanza kusimama, huku bado Jenerali Jacob akielekeza bastola kwake.

"You don't got the balls, do you?"

Nora akauliza hivyo kikejeli, akimwambia baba yake hana nguvu za kiume kufanya jambo kama hilo. Jenerali Jacob alikuwa anajitia ugumu kwenye moyo wake kumfanya afikiri kwamba angeweza kumuua binti yake, lakini akawa anashindwa. Pamoja na maovu aliyofanya, kihalisi, alimpenda sana Nora. Alikuwa anataka njia ya mkato na ya haraka kukimbia matatizo, na hapa alikuwa akijishawishi kwamba hii ndiyo ingekuwa ya haraka, lakini upendo wake kwa damu yake ukamfanya awe dhaifu. Akiwa bado anajishauri, hapo hapo akahisi hatua zikija nyuma yake, naye akageuka haraka ili ammiminie risasi aliyekuwa akija, lakini akashtukia anapigwa kwa kasi sana mkononi na kuidondosha bastola kabla hajamwona adui. Alipomwangalia sasa, akatambua ilikuwa ni Azra.

Binti alikuwa amerejesha fahamu muda fulani nyuma, naye akajitahidi kutoka kwenye ile ndege baada ya Asteria kumweleza yaliyotokea, na yeye Azra kwenda kumsaidia Nora. Jenerali Jacob akakasirika sana na kuanza kumfata ili wapigane, lakini binti huyo alimchanganya sana kwa mapigo yake mengi yaliyomuumiza mkuu wa jeshi. Hata hakutumia mtindo wake wa kumaliza mwili nguvu ili ampe mwanaume huyo maumivu mengi sana mwilini, ikiwa ni njia yake ya kuitoa hasira yake kwa sababu ya mambo yote mwanaume huyu aliyowafanya wapitie. Nora akawa amebaki kutazama tu Azra alipoendelea kumtandika baba yake.

"Go and help Lexi... I'll handle him."

Azra akasema maneno hayo bila kumtazama, naye Nora akatoka upesi ili kwenda kumsaidia Lexi kweli.

Upande wa Lexi, kufikia sasa alikuwa amejitahidi sana kwa uwezo wote aliokuwa amebakiza kupigana na wanaume wale, na Kevin ndiye aliyekuwa chini akiugulia maumivu baada ya kupigwa sehemu za siri, huku Weisiko akiendelea kumpa shida Lexi kutokana na yeye kuwa na mwili imara sana. Ingawa nguo ya mapambano ya Lexi ilisaidia asipatwe na maumivu mengi kupita kiasi, bado uchovu aliohisi ulimruhusu Weisiko amtawale na kumrusha huku na huko. Mwanaume huyo alikuwa na nguvu sana, na alipenda mtindo wa kumnyanyua adui na kumbamiza chini, kitu kilichofanya Lexi azidi kutokwa na nguvu. Luteni Michael alikuwa ametokwa na damu nyingi sana, na maumivu ya risasi yalifanya iwe vigumu kwake kunyanyuka na kutoa msaada; hiyo ilikuwa risasi ndefu, siyo pini. Akawa anatazama jinsi Weisiko alivyoendelea kujifanya anatamba kwa kumburuza Lexi huku na huko, naye akajitahidi kujikaza na kuchomoa kisu kingine kidogo kutoka kwenye mkanda wake, kikiwa ndiyo cha mwisho, kisha akaanza kujiburuza kwa ubavu mmoja akielekea walipokuwa.

Sasa, Lexi alikuwa amepiga magoti chini na kuweka mikono yake ardhini pia, huku akipumua kiuchovu, na uso wake ukitokwa na damu na yeye kuhisi kizunguzungu. Weisiko alikuwa amesimama karibu yake huku naye akitokwa na damu sehemu za masikio zilizotoneshwa, na puani pia, kisha akazishika nywele za Lexi kwa nguvu na kumvuta juu akiwa ameikaba shingo yake mpaka alipousogeza uso wake karibu naye. Akazidisha nguvu kwenye kuikaba shingo ya Lexi, na maumivu yakamwingia kwa kukosa hewa.

Damu zikaanza kumtoka Lexi mdomoni kwa sababu ya mishipa midogo ya kooni kupasuka, lakini ni hapa ndiyo Luteni Michael akawa amefikia karibu zaidi na kujitahidi kukirusha kisu kile kilichomfikia Weisiko na kumchoma nyuma ya mguu. Kwa kuhisi maumivu, akamwachia Lexi huku akijikaza asitoe sauti za maumivu, naye akageuka na kumwona Luteni Michael pale chini akimwangalia. Lexi alikuwa amelala chini sasa, huku akiwa amejishika shingoni na kukikaza kichwa chake kusitiri maumivu, na alikuwa akikohoa kwa shida sana. Weisiko akakichomoa kisu kile kutoka mguuni kwake na kuanza kumfata Luteni Michael, akiwa na lengo la kutaka kwenda ili amchome nacho, lakini ndiyo hapo hapo Nora akawa amefika na kumrukia Weisiko mgongoni mpaka wote kuangukia chini.

Kwa kuona sasa kwamba Lexi alikuwa ameishiwa nguvu, Kevin akajinyanyua na kumfata ili ammalizie hapo hapo chini, na wakati huo huo Weisiko alikuwa amejigeuza na kuurusha mkono wake ulioshika kisu kwa kasi kumwelekea Nora, nacho kikamkata sehemu ndogo ya begani, kikiwa kimemkosa shingoni, naye akaangukia pembeni akihisi maumivu makali sehemu hiyo. Kevin akafika juu ya Lexi na kuanza kumkaba pia, akitumia nguvu nyingi kumkandamiza hapo chini ili asijinasue, na wakati Luteni Michael alipoona hilo akataka kujaribu kujivuta zaidi ili aende kumsaidia, lakini Weisiko akamwona na hapo hapo kupeleka mkono wake wenye kisu hadi tumboni kwake na kumchoma kwa nguvu!



★★★★★★★★★★★★★

ITAENDELEA

★★★★★★★★★★★★★

WHATSAPP +255 787 604 893
 
FOR YOU

Story by Elton Tonny

Familia, Urafiki, Mapenzi, Tamaa, Hila, Usaliti, Unyanyasaji, Uhalifu, Mauaji, Visasi, Vita, Mambo yasiyotazamiwa

R-rated 18+

Enjoy!

★★★★★★★★★★★★★★★★★★

SEHEMU YA HAMSINI NA NNE

★★★★★★★★★★★★★★★★★★


Luteni Michael alikaza kichwa na koo yake kwa kuhisi maumivu makali kupita kiasi, hata sauti haikutoka kwenye mdomo wake ulioachama baada ya Weisiko kufanya hivyo. Kisha Weisiko akakichomoa kisu kwa nguvu kutoka tumboni kwa Luteni Michael na kusababisha maumivu mara mbili zaidi kwa mwanaume huyo. Nora aliona hilo, naye akasema kwa sauti ya chini, "No... Michael..." huku akijitahidi kuyasitiri maumivu ya begani na kunyanyuka. Luteni Michael akalala chini akihisi nguvu nyingi inamtoka, na ni giza la angani pamoja na nyota zake ndiyo vitu alivyoweza kuona tu wakati huu.

Kevin alikuwa anaendelea kutia jitihada za kumkaba zaidi Lexi ili ammalize mwanzo na mwisho, lakini hapo hapo akashtuka baada ya kupamiwa kwa kasi sana na sauti ya mngurumo mkali ikisikika! Weisiko na Nora walipoangalia huko, wakamwona Kevin akiwa chini huku akipiga kelele sana kwa sababu Zelda alikuwa juu yake, akimrarua kwa makucha na kumtafuna kwa meno kwa ukatili wake akiwa kama mnyama. Kevin alipiga sana kelele huku Zelda akiendelea kumrarua namna hiyo, naye Nora alipoangalia kule mbele kwenye ndege, akamwona LaKeisha, na kwa haraka alitambua kwamba alikuwa ameumia sana kwa jinsi alivyotembea huku akianguka.

Wakati huo wote tokea gari aliloendesha kuigonga ndege, LaKeisha alikuwa mbali sana na fahamu baada ya kukigonga kichwa chake vibaya, na hata alipoamka alimkuta Zelda akiwa amelala pembeni yake, na mnyama huyo alikuwa ameumia kiasi pia. Hakutambua kilichokuwa kinaendelea nje, lakini akajipa tu matumaini na kuufungua mlango, ingawa ilikuwa kwa shida, na ndipo Zelda akatoka na kufikia kumrarua Kevin hapo nje.

Weisiko aliingiwa na hofu baada ya kuona jinsi mnyama huyo mkali alivyomrarua binadamu mzima mzima, naye akasimama upesi na kuanza kuelekea sehemu ambayo alikumbuka muda mfupi nyuma aliipiga bastola yake kwa teke huko, ili aitafute na kumuua mnyama huyo. Alipoelekea huko, Lexi akamwona, na wakati huo Nora akajitahidi kuondoa hofu aliyokuwa nayo kumwelekea Zelda na kumsogelea Luteni Michael ili aone kama angeweza kumsaidia kunyanyuka. Akakuta bado yuko hai, lakini alikuwa amepoteza damu nyingi sana, na isingekuwa rahisi kumsaidia anyanyuke akiwa na maumivu yote hayo. Weisiko alipokuwa ameenda pale hakuiona bastola yake, na wazo lingine likaja alipokumbuka bunduki za wanaume wa Jenerali waliouliwa na Lexi muda fulani nyuma, naye akaanza kukimbilia huko ili achukue bunduki upesi.

Lexi akakusanya nguvu zote alizobakiza na kusimama, naye akaanza kumfata Weisiko. Nora akawa anamwita kwa hofu, lakini Lexi hakumwangalia hata kidogo na kuendelea kumfata mbaya wake pamoja na kuhisi maumivu mengi. Weisiko akawa amefika sehemu ile yenye bunduki na kuokota moja, lakini alipogeuka tu akakutana na kipigo cha ngumi usoni kutoka kwa Lexi, naye akarudi nyuma, kisha akataka kumpiga Lexi kwa chuma la bunduki, lakini Lexi akamkwepa kwa kumzungukia mpaka mgongoni, kisha akaupiga mkono wa Weisiko kwa nguvu sana akitumia teke, naye Weisiko akadondosha bunduki chini.

Kwa hasira, Weisiko akamtandika ngumi usoni, lakini Lexi akatulia tu kwa kusimama, akimwangalia kwa hasira. Weisiko akampiga nyingine tena, lakini Lexi akageuza tu uso wake na kumwangalia, ikionekana kama vile hakuumizwa kabisa na ngumi hizo. Weisiko akashangaa sana. Ilikuwa ni kama vile anapiga sanamu, lakini kwa wakati huu ni kwamba Lexi hakuwa akijali maumivu aliyohisi tena, naye akavuta ngumi moja ya nguvu na kumtandika Weisiko puani, na hii ilimuumiza sana jamaa mpaka kumvunja pua. Akarudi nyuma akihisi maumivu makali mno, na hapo sasa Lexi akaanza kumpa kipigo cha aina yake.

Weisiko alitumia mbinu zake zote za kijeshi kujaribu kumwangusha kijana huyu lakini zikawa zinagonga mwamba. Kila pigo alilorusha, Lexi aliliwahi na kuligeuza kwa Weisiko kwa njia zilizomuumiza zaidi. Ilikuwa ni kama ameingiwa na nguvu mpya tena, na sasa akazidi kufanya kichwa cha Weisiko kitangetange kwa kukosa mbinu zingine za kupambana. Weisiko alipodondoka chini, Lexi akaukamata mkono wake mmoja na kuuvunja nyuma ya mgongo wake, na kisha akafanya namna hiyo hiyo na ule mwingine. Jamaa alipiga kelele nyingi sana za maumivu, huku Lexi akiwa amepiga magoti chini karibu yake akipumua kwa nguvu.

Hayo yakiwa yanaendelea, Azra alikuwa amefanikiwa kumdhibiti Jenerali Jacob na kumfanya atulie kwa kuishiwa nguvu, na wakati huo alikuwa ametoka huko na kwenda walipokuwa wengine. Alimfikia LaKeisha, aliyekuwa amelegea kwa kuumia sana kichwani, na baada ya kumwona Zelda akiwa anamrarua Kevin pale chini, akaamua kumsaidia LaKeisha kunyanyuka na kumwongoza mpaka usawa wa ndege; yeye arudi ndani ya ndege kutoa kitu chochote ambacho kingemsaidia mwanamke huyu kupunguza ukali wa maumivu yake.

Pale chini ambapo Nora alikuwa amemshikilia Luteni Michael, mwanamke huyu hakuzisikia sauti za kelele kutoka kwa Kevin tena, kwa kuwa sasa mwanaume huyo msaliti hakuwa hai. Kifo kibaya sana ambacho Torres alimwambia kingempata, kikawa kimempata. Ni baada ya Zelda kuhakikisha ameuondoa uhai wake ndiyo akaachana naye na kuanza kumwelekea Nora. Nora aliingiwa na hofu, na wakati huu Luteni Michael alikuwa amefumba macho na kutulia, lakini bado alikuwa hai kwa sababu upumuaji wake haukukoma.

Zelda akamsogelea Nora mpaka karibu zaidi, kisha akatulia mbele yake huku macho yake ya njano yaking'aa gizani hapo. Nora alikuwa anamtazama tu machoni, naye Zelda akaunguruma kwa njia ya kumwogopesha Nora, lakini mwanamke huyu hakuacha kumwangalia machoni. Baada ya Zelda kuacha kunguruma, Nora akameza mate kujipa utulivu, kisha akanyoosha kiganja chake taratibu kumwelekea Zelda mpaka alipokifikisha karibu na mdomo wake, naye Zelda akaunguruma tena, lakini Nora hakukishusha. Akajipa ujasiri zaidi na kupeleka kiganja chake mpaka kwenye manyoya yake ya shingoni, na mnyama huyo akawa anamwangalia huku akipumua kwa nguvu. Mdomo wake ulionekana kujaa damu nyingi kutokana na uraruaji wake kwenye mwili wa Kevin. Nora akatabasamu kidogo kumwonyesha hisia ya urafiki, naye Zelda akanyanyua macho yake na kutazama upande ule alikokuwepo Lexi.

Lexi sasa alikuwa juu yake Weisiko, yaani, Weisiko alikuwa amelala chini, huku Lexi akiwa juu yake akimtandika ngumi usoni bila kuacha. Alikuwa anampiga, na kumpiga, na kumpiga, na mkono wake uliuma sana mpaka hakuuhisi tena, lakini akaendelea kumpiga.

"Kwa... mikono... yangu... mwenyewe... kwa... mikono... yangu... mwenyewe..."

Lexi akawa akimpiga ngumi huku akisema maneno hayo kwa sauti tetemeshi namna hiyo.

Zelda akaruka kutoka alipokuwa amesimama na kumpita Nora bila kumdhuru, akielekea kwa Lexi upesi. Nora akageuka pia na kumwona Lexi akiwa anatandika tu mtu ngumi, na kutokea upande wa mbele zaidi aliweza kuyaona magari mengi ya wanajeshi na maaskari yakifika maeneo hayo na kuanza kulizunguka haraka. Lexi akawa anapiga tu uso wa Weisiko mpaka Zelda alipofika nyuma yake na kumgusa kwa mguu mmoja. Akashtuka huku akiwa ameweka ngumi hewani bado, naye akabaki kumwangalia Zelda huku akipumua kiuchovu.

Habari ya Weisiko ikawa imeishia hapo. Alikuwa amepigwa usoni na kuharibika kiasi kwamba isingekuwa rahisi kutambua ikiwa ilikuwa yeye kweli. Zelda akaanza kuunguruma kwa hasira kuelekea magari yale yaliyokuwa yamefika hapo, na wanaume wengi wanajeshi na maaskari kushuka wakiwafuata huku wamewaelekezea bunduki. Zelda, akiwa kama mnyama mkali asiyetaka maadui wamdhuru Lexi, akawa anawaelekea kwa hasira, lakini Lexi akamwahi na kumshika shingoni kwa mkono wake, huku mwingine akiunyoosha juu kuwaelekea watu hao kuonyesha kwamba wasimdhuru yeye na mnyama wake.

Magari hayo yalikuwa yanatoa mwanga uliomulika sehemu yote vizuri, na wote waliweza kuona jinsi watu walivyozagaa chini kutokana na mauaji yaliyofanyika. Nora akamwachia Luteni Michael na kuanza kunyanyuka huku amenyoosha mikono juu, naye akaanza kuwaambia maaskari waliokuwa upande wake kwamba Luteni wa jeshi alikuwa ameumia vibaya sana hapo chini, hivyo wampe msaada kwa uharaka.

Wakati huu, tayari Azra alikuwa akimpatia LaKeisha huduma ya kwanza kwa dawa za kupunguza maumivu na kufunga kichwa chake kwa bendeji kutoka kwenye boksi dogo la huduma ya kwanza alilotoa kule ndani ya ndege, na Asteria alikuwa ameshashuka kutoka ndani ya ndege pia akimsaidia. Kwa hiyo Nora alipoomba msaada kwa maaskari, Azra akamwacha LaKeisha chini hapo akiangaliwa na Asteria ili yeye aende na boksi hilo la huduma ya kwanza kwa Luteni Michael. Maaskari na wanajeshi walionyesha ukali kwa kumwambia Azra atulie, lakini akalionyesha sanduku hilo juu huku akitoa ishara kwamba anataka kumsaidia yule aliyeumia pale chini, na Nora akamtetea pia kwa kuwaambia ingekuwa muhimu kama wangeruhusu Luteni Michael apatiwe msaada huo kwanza.

Kwa kuwa Luteni Michael alifahamika kwa wengi wao, wakachukua boksi hilo dogo na kwenda kuanza kumpatia huduma ya kwanza. Azra akawaambia wanajeshi wale kule ambako alimwacha Jenerali Jacob akiwa ameishiwa nguvu, na baadhi wakatoka hapo kwenda kumfata, huku wachache wakiwazunguka yeye Azra, na pale alipokuwa Asteria na LaKeisha.

Pale ambapo Lexi alikuwepo, bado alikuwa amenyanyua mkono wake juu kuwaonyesha wanajeshi wasipige risasi, na ndipo mmoja wao akawa anatembea kumwelekea taratibu. Lexi akamwona, na Zelda alikuwa ameanza kujivuta kutoka kwake ili amshambulie adui huyo aliyemwona akija.

"Subiri... hhh... usisogee... atakurukia..."

Lexi akatoa onyo hilo kumwelekea mwanaume huyo, naye akasimama kwa kutulia. Alikuwa mrefu na mwenye mwili mkubwa kiasi, naye alishikilia bastola mkononi lakini hakuielekeza kwa Lexi.

"Mnataka kunikamata... sawa... lakini msimuumize... nawaomba mnipe nafasi ya kumweka sehemu..."

Lexi akawa anaongea huku akijitahidi kumdhibiti Zelda aliyekuwa akiunguruma kwa njia ya kuwafukuza watu hao wengi mbele yao. Wakati huo, Nora alikuwa akitembea taratibu kuelekea sehemu aliyokuwepo Lexi huku amenyoosha mikono yake juu.

Mwanaume huyo aliyekuwa amesimama mbele akarudi nyuma kidogo, kisha akaongea kwa sauti ya juu, "Tufanye nini kwa ajili ya mnyama wako?"

Lexi akatulia kidogo, kwa sababu alishangazwa kiasi na swali hilo. Ilikuwa ni kama mwanaume huyo anamwambia kwamba anataka kumsaidia, siyo kumkamata.

"Mruhusu amweke ndani ya gari..."

Lexi akageukia upande ambao sauti hiyo ilitokea na kumwona Nora, akiwa ndiyo amesema maneno hayo.

"Tunafanyaje hivyo?" mwanaume huyo akauliza.

"Sogezeni gari moja mbele... mliache... mrudi nyuma ili nimweke..." Lexi akamwambia.

"Na ukikimbia?" mwanaume huyo akauliza.

"Sitakimbia. Liwekee pancha kama ukitaka," Lexi akasema.

Mwanaume huyo, akiwa ndo sauti kuu ya wanajeshi hao, akawaamuru wafanye kama Lexi alivyosema. Mmoja wao akawa anauliza kwa nini aliamua kufanya jambo hilo kwa ajili ya mwanamke huyo mhalifu, lakini mwanaume huyo akasema amri yake ifuatwe upesi.

Basi, mmoja wao akachukua gari na kulisogeza usawa wa alipokuwa amekaa Lexi na Zelda, kisha akashuka na kuyatia matairi mawili pancha. Muda wote huu, Lexi alikuwa anajitahidi sana kumdhibiti Zelda kwa sababu alitaka kumlinda asiumizwe endapo angewashambulia maadui, na Nora alikuwa amesimama pembeni kidogo akiangalia hayo yote. Kisha, mjeshi huyo aliyesogeza gari akarudi kwa wenzake, na yule mwanaume aliyewapa amri akawaambia vijana wake wasogee nyuma ili Lexi afanye kama alivyodhamiria.

Walisogea kwa umbali mfupi, lakini bado walikuwa wamezingira sehemu hiyo huku wakielekeza bunduki zao kumwelekea, hivyo Lexi akajitahidi kunyanyuka huku akimsemesha Zelda kwa kiingereza kuwa amfate. Nora alikuwa akimwangalia kwa huruma sana, jinsi alivyoonekana kuwa na maumivu makali, lakini akajikaza na kutembea taratibu mpaka kulifikia gari, kisha akaingia huku Zelda akimfuata pia. Wanajeshi na maaskari wengi walikuwa wakishuhudia jambo hilo kama vile ni sinema iko matengenezoni, na baada ya Lexi kuufunga mlango wa upande walioingilia kwenye gari hilo, baadhi ya wanajeshi wakamsogelea zaidi Nora kuhakikisha anakuwa chini ya ulinzi zaidi.

Lexi, akiwa ndani ya gari, akawa amekishika kichwa cha Zelda kwa ukaribu huku akilia kwa hisia. Hii ilikuwa ndiyo "hatimaye" ambayo sikuzote alijua ingefika tu. Alikuwa ameweza kuwalipizia kisasi wapendwa wake waliouwawa kikatili kwa kumuua muuaji wao kwa mikono yake yeye mwenyewe, na hilo likawa limetimia, ingawa na wakati huu alikuwa amepoteza wengine wengi waliokuwa muhimu sana kwake. Akiwa amemshika Zelda, akawa anamkumbukia Sandra, pacha wake, naye akafumba macho na kusema maneno machache kwa hisia sana.

"This was for you Sandra."

Baada ya hapo, akatumia mlango mwingine wa gari hilo kutoka nje na upesi kuufunga kabla Zelda hajatoka naye pia. Akawa ameweka paji la uso wake sehemu ya kioo, huku akimwona Zelda kwa ndani akiwa kwenye kioo hicho pia akitaka kutoka ndani humo kwa kuunguruma kwa nguvu sana, naye Lexi akageuka nyuma na kukuta wanajeshi na maaskari wamekwishasogea karibu yake, na mwanaume yule aliyewaongoza akiwa karibu zaidi. Nora, Azra, LaKeisha, na Asteria wakaletwa sehemu hiyo pia, naye Luteni Michael alikuwa amefungwa kwa bendeji tumboni na begani na kubebwa mpaka kwenye gari moja ili awahishwe hospitali.

Nora akawa anamwangalia Lexi kwa hisia sana, na hata LaKeisha na Azra walikuwa wakimtazama kwa huzuni mno. Kutokea upande ule mwingine, wote waliweza kumwona Jenerali Jacob akiwa anavutwa na wanajeshi wawili kuelekea kwenye gari, akiwa amedebweda hasa baada ya kipigo alichopokea kutoka kwa Azra. Wanajeshi na maaskari wengine wengi walikuwa wakishughulika na miili ya wote waliouawa iliyokuwa pale chini, na wengine walikwenda kuichunguza ndege ile iliyopindukia upande mmoja. Lexi akamwangalia mwanaume huyo aliyekuwa amesimama tu akimtazama kama vile anasubiri afanye jambo fulani, naye Lexi akanyoosha mikono yake mbele kwa njia iliyoonyesha kwamba alikuwa tayari kufungwa kwa pingu.

"Major... tafadhali..."

Nora alikuwa ameanza kuongea maneno hayo, lakini mwanaume huyo akanyoosha kiganja chake juu kumzuia asiendelee. Nora alimfahamu mwanaume huyo kuwa ndiyo Meja Jenerali Sebastian, yule yule aliyeweka msimamo wa kuwatafuta majenerali wale wawili na viongozi wa siasa waliosababisha matatizo kwa wengi. Akawa anamwangalia Lexi kwa umakini, kisha akatoa ishara kwa wanaume wake, ambao wakaja mbele na kuanza kuifunga mikono ya Lexi kwa pingu.

Nora, Azra, LaKeisha, na Asteria wakafungwa kwa pingu pia, kisha Meja Jenerali Sebastian akaanza kuongoza mbele kuelekea gari lake la kijeshi, huku wanaume wake wakiwatembeza wanawake hao kumfata pia. Wakawapeleka mpaka kwenye gari moja aina ya Defender lakini likiwa ni kubwa zaidi na lenye muundo mgumu sana, nao wakawaingiza kupitia milango ya nyuma, nyuma kabisa, na hapo wote wakamkuta Isiminzile akiwa ameketi pia huku mikono yake ikifungwa kwa pingu.

Baada ya milango hiyo kufungwa, Isiminzile akaanza kumuuliza Lexi na wengine ikiwa walikuwa sawa, na ni Nora tu ndiye aliyemjibu kwa kusema wangekuwa sawa. Mwanaume huyo akawapa pole na kuanza kuwaelezea jinsi ambavyo wanajeshi wale walimkuta barabarani na kumkamata, kisha akawaelezea hali halisi ilivyokuwa na kuwaeleza yale ambayo Luteni Michael alimwambia aseme, ndiyo akawekwa ndani ya gari hili na kufikishwa sehemu hiyo. Gari hilo likaanza mwendo, na kila mmoja wao alielewa kwamba hii ilikuwa ni safari ya moja kwa moja kuelekea vifungoni.

Nora alikuwa ameketi karibu zaidi na Lexi, akimwangalia jinsi alivyokuwa ameumia sana usoni, na akitazama chini kwa uchovu mwingi. LaKeisha alikuwa ameketi upande ambao alimtazama Lexi uso kwa uso, naye alikuwa analia bila kutoa sauti kwa kuhuzunishwa na yote yaliyotokea, na ni Asteria ndiye aliyekuwa anambembeleza kwa kumsugua mgongo taratibu kwa mikono yake yote iliyofungwa kwa pingu. Nora akakishika kiganja cha Lexi huku akimwangalia kwa hisia, naye Azra akanyanyuka kutoka alipokuwa ameketi na kuchuchumaa karibu na ndugu yake, kisha naye akaweka kiganja chake juu ya viganja vya wawili hao.

Lexi akaanza kudondosha machozi huku akimtazama mdogo wake, na Nora akalaza kichwa chake kwenye bega la Lexi. LaKeisha akasogea hapo pia na kuweka viganja vyake pale pale kwa wengine, na Isiminzile na Asteria wakafanya hivyo hivyo pia, kuonyesha wanamuunga mkono Lexi na kumpatia faraja kwa njia hiyo katika huzuni yake nyingi.

★★

Gari hilo liliendelea na mwendo kwa takribani dakika 30 hivi, kisha likatulia hatimaye. Wakiwa wanajiandaa kutolewa ndani ya gari, Nora akawatia moyo wengine kwa kuwaambia wasiogope, kwa sababu hata kama nini kingewapata, cha muhimu ni kwamba walikuwa hai bado, na Mungu angeendelea tu kuwapigania haijalishi nini kingewapata mbele ya safari ya maisha yao. Milango ikafunguliwa, na wanajeshi watatu wakiwa wamesimama hapo nje wakawaambia washuke. Wote wakaanza kushuka, lakini baada ya kufika nje, hali waliyoikuta ikawashanganza.

Kwanza, magari mengine yote yaliyokuwa pamoja na kundi hilo la Meja Jenerali Sebastian hayakuwepo, yaani yote yaliyokuwa yamefika kule walikotoka hayakuwepo, isipokuwa hili walilobebwa na lingine moja ambalo Meja Jenerali Sebastian alitumia. Eneo hilo lilikuwa kama kiwanja kidogo cha mpira, na hakukuwa na majengo yoyote kuzunguka hapo. Walipotazama mbele zaidi, wakaona helicopter kubwa sana ikiwa imetulia tu chini, na ndipo gari lingine kubwa likawa limefika hapo. Gari hilo lilikuwa la kubeba mizigo, na lilikuwa limebeba gari lingine dogo. Kwa kuliangalia, Lexi akatambua ndiyo lile lile gari ambalo alimwacha Zelda ndani yake.

Wote wakawa wanatazamana kimaswali sana, wasielewe kilichokuwa kinaendelea, na ndipo Meja Jenerali Sebastian akawasogelea karibu zaidi. Lexi akiwa katikati, akawa anamwangalia mwanaume huyo kwa njia ya kawaida tu, naye Meja Jenerali Sebastian akatoa ishara kwa wanajeshi wake, nao wakaanza kuzifungua pingu kutoka mikononi mwa vijana hao wote. Hiki ni kitu kilichowaacha wakiwa wamechanganyikiwa, kwa sababu hawakuelewa walikuwa wanaandaliwa kwa ajili ya nini.

Meja Jenerali Sebastian akasogea karibu zaidi na kusimama mbele yake Lexi, kisha akasema, "Mko huru kuondoka."

Maneno yake yakawafanya wabaki kumwangalia tu kimaswali.

Nora akauliza, "Unamaanisha nini... kuondoka?"

"Mtachukua helicopter hiyo, kuna rubani humo ambaye atawavusha kufikia Eldoret. Nimefanya mipango, kwa hiyo hamtasumbuliwa. Baada ya kufika huko, natumaini mtatumia akili na skill zenu kujua mtakapopaswa kwenda, lakini mnatakiwa mpotee... milele," akasema Meja Jenerali Sebastian.

Bado maswali mengi yalipita kwenye vichwa vya watu hawa.

"Major... nini kinaendelea?" Nora akamuuliza.

"Ninawapa nafasi ya kwenda kuanza maisha mengine, msijulikane tena. Mtapaswa kuishi kama mmekufa, la sivyo mnajua mtakufa. Tunamweka mnyama wenu kwenye hilo kontena dogo, mtalibeba humo humo kwenye helicopter. Oh na...."

Meja Jenerali Sebastian akiwa anaongea hivyo, akawaonyesha kumwelekea mwanajeshi wake mmoja, ambaye alikuwa ameshikilia mfuko fulani mkubwa na kuusogeza karibu yake.

"...hizi tumezikuta kwenye gari lililogonga ndege. Nafikiri zitawasaidia," Meja Jenerali Sebastian akamalizia.

Akampatia mfuko huo Lexi, naye akaupokea na kuangalia ndani yake. Hapo akaona mabamba mengi ya dhahabu, na ni zile zile ambazo LaKeisha alikuwa ameziweka humo baada ya kutoroka kule kwenye nyumba yao iliyobomolewa. Lexi akamtazama LaKeisha, naye LaKeisha akamwonyesha kwa ishara ya kichwa kukubali kwamba ni yeye ndiye aliyezibeba, lakini hata yeye bado hakuelewa ni kwa nini na jinsi gani Meja Jenerali huyo alikuwa akifanya haya yote.

"Ninafanya hivi kwa ajili ya nyie watano, lakini huyu atapaswa kubaki," Meja Jenerali Sebastian akasema.

Alikuwa akimaanisha Asteria, kwa sababu tayari alielewa kwamba binti aliingizwa tu kwenye kisa hicho bila kutarajia.

"Hapana... mimi sitaki kubaki. Nataka kwenda na dada yangu," Asteria akasema.

"Usiogope. Hatutakufunga. Wewe utakuwa salama zaidi kubaki, na dada yako wa Marekani atakuwa pamoja nawe. Lakini kwa nyie... mnajua..." Meja Jenerali Sebastian akasema.

Asteria akawa anamwangalia Nora kwa njia iliyoonyesha hakutaka jambo hilo, naye Nora akamshika mkono kumtuliza.

"Kwa nini unafanya hivi?"

Swali hilo likatokea kwa Lexi hatimaye, akiwa ameuliza kiutulivu na akimwangalia Meja Jenerali Sebastian kwa umakini sana.

Meja Jenerali Sebastian akashusha pumzi, kisha akasema, "Nilifahamiana na Kapteni Kendrick pamoja na Meja Casmir, baba yako. Walikuwa ni watu wazuri sana. Kwa kipindi kirefu nilikuwa najua kuhusu matendo ya Jacob na Mdeme, lakini sikujiona kuwa na nguvu za kutosha kusimama dhidi yao. Ulichofanya binti yangu, ni zaidi ya kile ambacho jeshi zima la nchi hii linaweza kufanya, na kwa sababu ya ujasiri wako na wa wenzako... nimeweza kusimama ili kufanya lililo sahihi..."

Lexi akawa anamtazama kwa umakini, na wengine walikuwa wanamsikiliza kwa umakini pia.

"Sijaona ikiwa itakuwa fair kama utapelekwa kifungoni, ndiyo maana nikafanya huu mpango mdogo wa kukuua kwa mara nyingine... ikiwa unaelewa namaanisha nini," Meja Jenerali Sebastian akasema.

Lexi akatazama tu chini.

Asteria, akiwa hajaelewa, akamuuliza Nora, "Anataka kutuua?!"

"Ha..pana... yaani... anamaanisha..."

"Anataka kufanya ionekane kwamba Lexi na sisi tumekufa... ili tusahaulike," Isiminzile akamalizia maneno ya Nora.

"Ndiyo. Lakini hiyo ni ikiwa tu utakubali msaada wangu. Ni uamuzi wako," Meja Jenerali Sebastian akamwambia Lexi.

Wengine wakamtazama Lexi kwa umakini. Akiwa bado ameangalia chini, Nora akakishika kiganja chake na kuunganisha vidole vyake hapo kwa nguvu kiasi. Lexi akamtazama kwa hisia, akiwa anatafakari vitu vingi, kisha akamgeukia Meja Jenerali Sebastian na kutikisa kichwa kukubali........



★★★★★★★★★★★★



MWAKA MMOJA BAADAE.....


Miezi mingi ilipita kutokea wakati ule wa machafuko yaliyotembezwa nchini kutoka kwenye kundi maarufu kwa jina la Mess Makers. Ilifikiriwa kwamba kundi lao lote liliuawa katika mapambano baina yao na watu wa Jenerali Jacob, lakini ukweli wa kwamba wachache walitoroka na kwenda kusikojulikana haukufahamika kwa wengi. Sasa, nchi hii ilikuwa na Raisi mwingine, ambaye alikuwa amechaguliwa na wananchi walioona alifaa zaidi kuitumikia nchi kwa njia ambayo ingewaletea mabadiliko mengi. Huyo hakuwa Raisi kutoka kwenye chama chochote kile chenye kupiga domo sana. Tena, alikuwa ni mwanamke. Mwanamke wa kwanza kabisa kuwa Raisi. Huyo hakuwa mwingine ila mwanamama Emiliana Ngoyi. Ulifikiri nani?

Kutokana na jinsi alivyokuwa shupavu na mwenye bidii katika kufichua na kuondoa maovu na ufisadi akisaidizana na viongozi wengine, cheo hicho kilimwangukia yeye baada ya muda mfupi wa nchi kuongozwa na jeshi kupitia kwa Meja Jenerali Sebastian. Kwa wakati huu, Sebastian ndiye aliyekuwa Jenerali Mkuu wa Jeshi, naye alihakikisha anasafisha aina zote za uonevu kwenye jamii kutoka kwa watu wa usalama, na kuwatumikia wananchi kwa njia iliyo sahihi zaidi.

Luteni Michael Mwakasiba, alikuwa amepona kabisa jeraha lake la kisu tumboni baada ya kutibiwa miezi michache nyuma, na sasa alikuwa vizuri kiafya na aliendelea na kazi, wakati huu akitumikia kama Kanali wa Jeshi la Nchi. Yule ambaye alikuwa Kanali mwanzoni, yaani Oswald Deule, kwa sasa alikuwa akitumikia kifungo gerezani baada ya matendo yake maovu kufichuliwa pia, hasa na Michael. Vijana wa timu ya "Kanali Michael" nao walikuwa bado pamoja naye, na walikuwa wakifanya kazi sambamba naye kwenye vitengo maalumu ndani ya jengo la Usalama wa Taifa.

Asteria kwa wakati huu alikuwa akiishi Marekani pamoja na dada yake, Flora, naye alikuwa akifanya kazi kwenye taasisi fulani kubwa iliyohusiana na masuala ya utunzaji wa miti na mimea. Dada yake alikuwa mwanasheria katika kampuni kubwa, na wakati huu alikuwa akikaribia kufunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu. Asteria pamoja na Flora, wote walijua kwamba kuna sehemu ambayo Nora alikuwepo, akiwa hai mpaka wakati huo, lakini wasingeweza kujua alikuwa wapi kwa sababu hakuwahi kuwatafuta tokea yeye na wengine walipotoroka baada ya Meja Jenerali Sebastian kufanya ionekane ni kwamba Mess Makers wote walikufa.

Paul Mdeme, Raisi aliyepita, kwa wakati huu alikuwa gerezani pia akitumikia kifungo cha maisha yake yote yaliyobaki huko. Hakuishi vizuri gerezani kwa sababu kule alikutana na njemba zilizokuwa na hasira naye kutokana na yote aliyoyafanya, na hivyo akawa amegeuzwa kuwa "mke" wa gereza. Alifanyishwa kazi ngumu, alionewa, alipigwa, na hata kuingiliwa kinyume na maumbile yake mara nyingi sana. Yote yalikuwa ni malipo kwa maovu aliyofanya, naye angeendelea kuishi maisha yake yote namna hiyo hiyo.

Jacob Rweyemamu, a.k.a Jenerali aliyepita, alikuwa hai bado, lakini katika sehemu mbaya sana ambayo hakustahili kuwekwa mwanadamu. Hata yeye ilidhaniwa kwamba alikufa kwa wengi, lakini alikuwa amefungiwa kwenye sehemu iliyo kama shimo, lililokuwa chafu sana na lilifunikwa kwa juu kuacha sehemu ndogo tu kwa ajili ya hewa. Alitendewa kama mnyama asiye na thamani. Alitupiwa chakula humo kwa mida isiyoeleweka, alijisaidia humo humo, alipewa maji kwa kumwagiwa kutoka juu, na wakati mwingine watu waliomweka huku walimkojolea na kutupa takataka ndani ya shimo hilo ambazo ziliozea humo humo pamoja naye.

Waliomweka huko hawakuwa watu wa Jenerali Sebastian, bali watu waliotaka kufanya maisha yake yawe mabaya kwa sababu ya kujua kwamba alimuua Salim Khan. Ndiyo, watu wa Salim Khan, Mafia wale. Waliingia kwenye makubaliano na Sebastian kuwa awape mtu huyo kwa sababu hata kama angempeleka wapi, wangefanya tu yote wawezayo ili kumfikia, naye Sebastian hakuwa na neno ila kuwapatia Jacob tu, na ndiyo wakamweka huko ili aishi maisha yake kwa shida sana.

Kwa hiyo mambo nchini kwa ujumla yakaanza kunyooka taratibu. Mifumo mingi ya kisiasa na kijamii iliboreshwa kwa sababu wananchi walichangia katika ujenzi wa maendeleo ya nchi, na maisha ya wale wote waliokuwa wamenyonywa kwa muda mrefu sana na Mdeme yakawa yameboreka zaidi shukrani kwa msaada ambao Mess Makers waliwapatia.


★★★★


Siku fulani, mida ya mchana, kulikuwa na mjumuiko wa marafiki kadhaa wa muda mrefu ndani ya jiji la Dar es Salaam, ambao walipanga kukutana kwenye hoteli ya kujivinjari, iliyokuwa na muundo hasa kwa ajili ya watu wenye maisha ya juu na watalii.

Marafiki hawa walikuwa watatu, lakini wote walikwenda na familia zao hapo ili kufurahia muda wa wiki moja kwa pamoja sehemu hiyo, kwa sababu kwa wote ilikuwa ni wakati wa likizo. Marafiki hao watatu walikuwa ni wanawake, na walifahamiana kwa miaka mingi, lakini hawakuwa wameonana kwa muda mrefu. Hivyo mpango huo wa matembezi ungekuwa fursa nzuri ya kukumbushia enzi za zamani na kufurahia urafiki wao ambao uliwafanya wawe kama dada wa kimwili.

Wanawake hao watatu walikutana siku hiyo huko kwenye hiyo hoteli, wote wakiwa na waume zao pamoja na watoto. Mmoja wao aliitwa Joaris, naye alikuwa pamoja na mume wake na watoto wawili wa kike kwenye miaka kati ya 12 na 7. Mwingine aliitwa Irene, naye alikuwa pamoja na mume wake na mtoto wao mmoja wa kiume mwenye miaka 10. Wa mwisho alikuwa ni mwanamke aliyekwenda pamoja na mume wake na binti yake wa kike, mwenye miaka 9, na huyu alikuwa ni Valentina. Ndiyo. Yule yule madam Valentina.

Baada ya kumaliza kupangilia mambo yao, familia hizi zilianza kufanya mambo mengi yenye kuburudisha, na wanaume wa marafiki hao walipatana vyema. Wote walikuwa na maisha ghali sana, hivyo wangefanya mambo kama vile wazungu. Mida ya usiku baada ya kuwa wamemaliza kupata mlo, watoto wakawa wamepelekwa vyumbani kwao pamoja na wazazi wao, lakini ni wanawake hao watatu ndiyo waliotoka na kwenda kukaa sehemu ya kujiliwaza ili kupatana hata zaidi (catch up). Waliongelea vitu vingi kwa njia ya masihara na utani huku wakipata vinywaji mpaka inafika saa 6 usiku.

"Halafu unajua mimi nadhani walifanya mbaya sana..." akasema Joaris.

"Kwa nini?" akauliza Irene.

"Ilipaswa waiweke hiyo siku. Tusherehekee hao watu maana walikuwa ni magwiji..." akasema Joaris.

"Ahahahah... hiyo ingezua utata. Can you imagine siku ya namna hiyo watu wangekuwa wanafanya mambo gani?" Valentina akasema.

"Oh ingekuwa ni kuibiana tu, hamna kingine. Wale jamaa kilichokuwa mbele ya pua zao ni kunusa mamilioni tu..." akasema Irene.

"Hamna bwana. Wangepewa hiyo heshima. Me naona haikuwa fair kutowapa siku ya kuwakumbuka. Ingeitwa "Mess Makers Day." Ina ring nzuri eeh?" akasema Joaris.

Wenzake wakacheka.

"Kama Independence Day?" akauliza Valentina.

"Exactly," Joaris akajibu.

"Hmmm... ingekuwa siyo poa. Ila kiukweli hata mimi wale jamaa niliwakubali sana. Wameacha historia ambayo ilifunika hata ile ya Demba Group," akasema Irene.

"Mwenzangu! Si mimi nikapokea milioni 46 kwenye akaunti yangu bwana! Heheee... walinifaidi sana wale jamaa," akasema Joaris.

"Mmmm... milioni 46 wapi? We mwongo kweli," akasema Irene.

"We kama hukupokea hata senti ni kivyako shosti, sisi wengine zilifika. Tina we ulipokea ngapi?" Joaris akaongea.

Valentina alikuwa anatafakari kitu fulani, kisha akasema huku akitabasamu, "Trilioni moja."

Wenzake wakaangaliana, kisha wakaanza kucheka sana. Valentina akaangalia chini tu huku akitabasamu.

"Hapo umeenda mbali sana aisee, mpaka nimemwamini Jo, ila wewe, mm-mm..." akasema Irene.

"Trilioni moja labda kama angekuwa anatoka na yule mmoja wao... me nilimpenda yule kaka mwenye rasi jamani alikuwa mkali!" akasema Joaris.

"We! Ntamwambia Albert umesema hivyo!" Irene akamtania.

"Ahahaaa... ili umfanye aone wivu kwa mtu mfu? Hanaga hizo pigo," akasema Joaris.

"Zake ni zipi kumfanya aone wivu? Au ndo' kusema ulipopata milioni 46 sijui ndiyo akawa mpole na kukunyenyekea kwa kila kitu?" Irene akamuuliza kiutani.

Joaris akacheka kidogo na kumwangalia Valentina, ambaye alikuwa tu ameshikilia glasi yake yenye kinywaji akionekana kutafakari kitu fulani. Irene akambonyeza Joaris huku akimwangalia kwa njia ya kuuliza mwenzao ana nini, na ndipo Joaris akamgusa Valentina kiganjani. Valentina akamtazama kama ameshtuka.

"Vipi we dem? Unawaza nini?" Joaris akamuuliza.

"Aa... hamna kitu," Valentina akajibu.

"Tumekuja huku ku-enjoy, kwo' usilete stress zako hapa," Irene akamtania.

Valentina akatabasamu tu. Joaris akaona kwamba kuna umakini fulani ulikuwa umemwingia rafiki yake, naye akataka kujua mengi zaidi.

"Tina... ni kweli wewe ulitumiwa Trilioni moja?" Joaris akauliza.

Valentina akatikisa kichwa kukubali. Irene akawa makini pia.

"Wow! Ina maana ulikuwa umepoteza pesa hizo zote... la, haiwezekani," akasema Joaris akiwa haamini.

"Ahah... hapana, sikupoteza hela wala. Walinitumia tu hizo," akasema Valentina kwa unyoofu.

"Ongea ukweli shosti," akasema Irene.

"Ni kweli," akasema Valentina.

"Yaani kumbe hapa tumekaa na bonge moja la tajiri?" akasema Irene kwa shauku.

"What... kwa nini walikutumia pesa hizo zote? Willy anajua?" Joaris akauliza.

"Ni... hapana, hajui. Nime... ni mambo mengi, ni story ndefu..."

"Oh, kwani kuna sehemu yoyote tunaenda babe?" akauliza Irene.

Valentina akashusha pumzi, kisha akasema, "Ni kitu ambacho sijaongea na yeyote yule kabla. Najua mnafahamu kwamba Alexandria siyo mtoto wa William..."

"Ndiyo, tunajua. Kila mtu anaweza kuona hilo, hawafanani hata kidogo, na hatukuwahi kuku-pressure kutuambia baba yake ni nani ijapokuwa mara kadhaa tulizokuuliza ulikuwa una...."

"Irene, Irene... mwache basi aongee jamani! Tina, em' sema unachotaka kusema," Joaris akamwambia Valentina.

"Aliyenitumia hizo pesa ni baba yake," Valentina akawaambia.

Rafiki zake wakabaki kushangaa.

"Alikuwa mmoja wao... wa hao Mess Makers," Valentina akasema.

"Mh! Mbona hukuwahi kutuambia?" Irene akauliza.

"Ningewaambia nini? Maisha yetu yalivurugwa sana, aliniacha nikifikiri amekufa, ndiyo baadae nikajua nina ujauzito wake. William nimekutana naye tayari nina Alexa, na kama mnavyojua yeye hawezi ku..." Valentina akaishia tu hapo.

"Yeah, yeah, tunajua..." akasema Joaris.

"Kwa hiyo nilikuja kukutana naye mwaka jana, nikashangaa sana kumwona tena. Nilifikiri amekufa. Nikamwachia namba lakini hakunitafuta... ndiyo baadae nakuja kumwona akitangazwa kuwa mara muasi, mara nini sijui... Mpaka wakati huu bado sielewi kwa nini alijiingiza kwenye hayo mambo, hata kama alikuwa anapigania wanyonge... bado nilitaka kumtambulisha kwa Alexa... properly," Valentina akaongea kwa hisia sana.

Wenzake wakaangaliana, naye Valentina akanywa tu kileo chake.

"Val... unataka kusema kwamba bado ulikuwa unampenda huyo mtu?" akauliza Irene.

"Ndiyo. Ndiyo bado nili... nampenda William. Ninampenda mume wangu, ni mtu mzuri na baba bora kwa mwanangu. Lakini bado nilikuwa na hisia kwa yule mwingine, sitakataa. Hilo halina faida yoyote sasa lakini... ahah..." akasema Valentina.

Joaris akashusha pumzi na kusema, "Girl... leo umeangusha bomu kali kuliko lile la benki kuu."

Valentina akacheka.

"Kwa hiyo alikutumia Trilioni moja kama... nini yaani?" Irene akauliza.

"Alituma na ujumbe. Aliomba samahani kwa sababu hangewahi kuja karibu na binti yake tena... alimwona mara moja tu. Lakini akasema pia kwamba anajua nitamtunza vizuri, kwa hiyo pesa hiyo ingenisaidia kumpa mwanangu maisha mazuri hata zaidi," akasema Valentina huku chozi likimtoka.

Joaris akamfuta chozi lake, naye Valentina akachekea kwa chini na kujisawazisha.

"Tumesema hakuna stress, kwa hiyo nafurahi kwamba hilo nimeliweka pembeni kwa wakati huu. Nafikiri itakuwa bora tukirudi kwa..."

"Yeah, yeah, yeah, kabisa..." Joaris akamkatisha Valentina, akiwa ameelewa alimaanisha kurudi kwa familia zao.

"Lakini nawaombeni msije mka..." Valentina akaishia hivyo.

Irene na Joaris wakamhakikishia kwamba mambo aliyowaambia yangebaki kuwa siri, nao wakaendelea kumtania kwa kusema kwamba kwa sababu sasa hivi walijua ana hela nyingi kupita maelezo, ndiyo ingekuwa nafasi ya kuomba kununuliwa chochote walichotaka na kwenda sehemu zozote walizotaka, eti kama njia ya kumnyonya pia.

Baada ya maongezi hayo, wote wakarudi vyumbani kwa familia zao, huku Valentina akiwa amemkumbuka sana "Xander," baba ya mtoto wake, aliyefikiri kwa mara nyingine tena kwamba hakuwepo duniani. Lakini akaendelea tu kuwa na shukrani moyoni kwamba aliachiwa zawadi nzuri na kijana yule, yaani Alexandria binti yake, naye angeendelea kumtunza kwa upendo maisha yake yote akiwa na urithi mkubwa sana alioachiwa kutoka kwa baba ya mtoto huyo.


★★★★


VISIWA VYA SANTORINI, UGIRIKI


Moja kati ya sehemu bora zaidi kwenye uumbaji wa kipekee duniani, Visiwa vya Santorini ni sehemu yenye kuvutia sana. Ni sehemu nzuri sana ambayo huvutia watalii wengi, na wale waishio huko wamejitahidi kuboresha zaidi sehemu kubwa ya kisiwa kufaana na mahitaji ya wengi ambao huenda kutembelea. Ni sehemu yenye tamaduni mbalimbali kutoka kwa watu wa huko, na pia eneo la bahari kukizunguka hufanya papendeze hata zaidi kutokana na mandhari yake yenye fukwe kubwa zilizo na shughuli mbalimbali za watu wengi. Ni kisiwa kisifiwacho kuwa namba moja duniani kwa sababu ya umaridadi wake, na wengi kutoka nchi mbalimbali hupenda kwenda hasa kwa lengo la kujivinjari na fungate.

Kuna hoteli za kifahari zilizojengwa kuzunguka kisiwa hicho, na nyingi ndiyo sehemu za kufikia wageni kutoka nje katika masuala ya utalii. Moja kati ya hizo ni Grace Hotel, iliyo kubwa na pana sana na yenye mwonekano kama wa mahekalu ya kale, lakini kwa njia ya kisasa zaidi. Kuna vyumba vikubwa sana, swimming pool pana mno (mita zaidi ya 22 kabisa), vyumba vya shughuli za urembo (spa), migahawa na bar kadhaa kwa viburudisho, na madarasa maalumu kwa ajili ya mazoezi na upishi pia.

Kulikuwa na wageni wawili kwenye hoteli hiyo, walioishi hapo kwa karibia miezi 10 sasa, na walijiweka karibu na wengi na kushiriki katika mambo mbalimbali kwa muda mrefu kufikia hatua ya kutoonwa kuwa wageni tena. Hawa waliitwa Sia na Bella. Wakiwa siyo wazawa, walionwa kuwa watalii wa muda mrefu, lakini kwa waliowazoea hapo ilifanya waonwe kuwa wenyeji.

Kwa kipindi cha miezi michache, Sia alijiunga na madarasa ya upishi na kuweza kusaidiana na mwalimu mkuu kufundisha wengine pia aina mbalimbali za upishi wa vyakula kutoka nchini kwao, na hii ikampatia nafasi nzuri ya kama ajira kwa njia ya ujitoleaji. Bella yeye alijihusisha zaidi katika madarasa ya mazoezi, akisaidiana na makocha katika kuwafundisha wageni wengine waliokwenda hapo kufuata taratibu za mazoezi fulani ili kuboresha afya za miili yao; hasa kwa wanawake ili kuishepu miili vizuri.

Baada ya kujihusisha na shughuli za hapa na pale na kuchangamana na watu kwenye hoteli hiyo, Bella na Sia wangekutana na kufurahia uhusiano wao mzuri kwa matembezi na kupumzika pamoja pia. Waliyaendesha maisha yao kwa ustaarabu sana na kufanya amani na kila mtu, hivyo kwa muda wote walioendelea kuwa hapo walikuwa na furaha sana.

Siku fulani, Sia aliombwa na kiongozi wa darasa la upishi, aliyekuwa mwanamke mzee, kwamba amsaidie na kazi za ziada kwa ajili ya maandalizi ya darasa lake kwa siku ambayo ingefuata. Hakukataa. Akatumia muda mwingi pamoja na mwanamke huyo mpaka inafika saa 3 usiku, ndipo akaagana naye ili arudi kwenye chumba alichoishi na Bella. Alipofika ndani, akamkuta Bella akiwa anasoma karatasi fulani kwenye meza ndogo iliyokuwa na kifaa kinachotoa mwanga kumulika kwa ajili ya usomaji, naye akamfata na kumshika kichwani kwenye nywele zake ndefu.

Bella hakugeuka hata kumwangalia, naye Sia akamuuliza kwa sauti ya chini, "Have you eaten?"

Bella akatikisa kichwa kukubali kwamba alikuwa ameshakula, na hata hapo hakugeuka kumwangalia. Kwa kuelewa karatasi hiyo Bella aliyokuwa ameshika ilikuwa ni kwa ajili ya nini, Sia akambusu tu nyuma ya kichwa chake na kuamua kwenda kujimwagia kwanza halafu ndiyo arudi kukaa pamoja naye. Chumba hiki kilikuwa kipana, na kilikuwa na mwonekano uliopendeza. Upepo ulipuliza mapazia marefu yaliyokuwa kama yamekatwa-katwa kwa pande zote zenye uwazi mkubwa wa madirisha.

Zikapita kama dakika 10 hivi, naye Sia akawa amerudi; akiwa amevalia sweta lililofunika mpaka viganja, na kikaptura chepesi cha rangi ya njano. Nywele zake nyeusi na laini zilionekana kulowana bado, naye akaketi karibu na Bella, ambaye wakati huu alikuwa amemaliza kusoma yale yaliyoandikwa kwenye karatasi ile, hivyo akawa anamwangalia pia.

"How's yaya? (bibi yukoje?)" Bella akamuuliza Sia.

"She's good. Just recently been having back aches, think you should help her with some exercises (Yuko vizuri. Amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo, nafikiri utapaswa kumsaidia kwa mazoezi kiasi)," Sia akasema.

"Naah... I don't think she'd go for that (hapana.. sidhani atafikiria kufanya hivyo)," akasema Bella.

"She hates exercises... almost forgot (anachukia mazoezi... ilikuwa kidogo nisahau hilo)," akasema Sia.

"Yes, so technically she hates me (ndiyo, kwa hiyo kihalisi ananichukia mimi)," Bella akatania.

Sia akacheka kidogo.

"I met a guy on the Caldera today. He was hitting on me (Nimekutana na mwanaume fulani kwenye Caldera leo. Alikuwa ananitongoza)," Bella akasema.

"Ahahah... you sure get that a lot (...unapatwa na hilo jambo sana)," Sia akamwambia.

"Yeah... makes me wish for a change of the environment sometimes (ndiyo.. inanifanya nitamani kubadili mazingira nyakati nyingine)."

"Guys will keep on hitting on you, no matter where you go (Wanaume wataendelea kukutokea tu haijalishi utaenda wapi)."

"Yeah, might as well start living in a nun costume (Ndiyo, itakuwa bora kama nikianza kuishi ndani ya nguo za ma-sister)."

"They still won't stop (bado hawataacha)."

Bella akatabasamu kidogo na kuiangalia karatasi ile.

"Is that her? (huyo ni yeye?)" Sia akauliza, akimaanishia aliyeandika karatasi hiyo aliyoshika Bella.

"Yeah..." Bella akajibu.

"This is like... the third time she's sent you a letter In one week. Isn't that gonna be a problem? (Hii ni kama mara ya tatu amekutumia barua ndani ya wiki moja. Hiyo haitakuwa tatizo?" Sia akauliza.

"I'm thinking she can't help it. She's lonely (Nafikiri anashindwa kujizuia. Yuko mpweke)," Bella akasema.

"We all are. I don't know what she's said this time, but you know staying out of reach is what's helping us still be safe... (Sisi wote ni wapweke. Sijui wakati huu amekwambia nini, lakini unajua kutowasiliana ni kitu kinachosaidia tuendelee kuwa salama)" Sia akasema.

Bella akamwangalia, kisha akasema, "She wants us to meet. She wants to see me (Anataka tukutane. Anataka kuniona)."

"But... that's dangerous (lakini hiyo ni hatari)"

"Don't you think that it is already dangerous that you and I have been together this all time? (Kwani haufikiri kwamba tayari ni hatari mimi na wewe kuwa pamoja muda huu wote?)" Bella akamuuliza.

Sia akabaki kumtazama tu, kwa njia ya kawaida, lakini iliyojaa mshangao. Bella akainama na kufumba macho.

"I'm sorry," Bella akasema.

Sia akakishika kiganja chake huku akimwangalia kwa hisia, kisha akasema, "Lexi..."

Bella akamwangalia. Huyu alikuwa ndiyo Lexi wa Mess Makers.

"Lexi nisikilize. Naelewa jinsi unavyohisi kwa sababu imekupasa ukae mbali na mdogo wako. Mimi pia roho inaniuma kwa kuwa wadogo zangu bila shaka wanajua niko hai, lakini wanapaswa kuishi wakiigiza kwamba nimekufa. Najua unatamani kumwona pia, lakini tulikubaliana kukaa mbali mbali na kubadili utambulisho wetu ili kubaki salama. Ukikutana naye, najua itakuwa ngumu kwako kumwacha tena... hata yeye pia," Sia akasema.

"Ndiyo uko sahihi. Najua uko sahihi. Lakini kuna ile... hisia fulani yaani..."

"Unajiona kuwa mbinafsi kwa sababu mimi na wewe tuliamua kubaki pamoja ilhali wengine wanafikiri sote tumekwenda sehemu tofauti?" Sia akamwambia.

"Azra amekuwa mwenyewe kwa kipindi kirefu sana Nora. Hizi barua anazotuma kwangu... ananihitaji. Anaogopa kwamba anaweza kufanya kitu fulani kitakachomsababishia ajulikane, kwa hiyo anahitaji niwe naye ili...." Bella/Lexi akaishia hapo.

"Naelewa ni ngumu. Naelewa pia kwamba unammiss sana. Ila mifumo mingi sasa hivi iko tight. Angalau tulibahatika kufika sehemu za mbali na kujificha lakini bado unajua ilikuwa kwa shida. Azra... naelewa ni mdogo na ana uhitaji wa familia... lakini ni ngumu sana Lexi kuishi namna hiyo tena..." Sia/Nora akamwambia.

"Kwani Nora... hatuwezi kumleta huku, tukakaa naye kama sisi tulivyoweza kuishi pamoja kwa muda huu wote..."

"Lexi..." Sia/Nora akamkatisha kwa sauti yenye kubembeleza.

Bella/Lexi akaangalia tu pembeni.

"Isiminzile yuko Liverpool. Azra yuko Mumbai. LaKeisha yuko Jakarta na Zelda. Ningetakiwa kuwa sehemu nyingine, lakini nikaja pamoja nawe bila wenzetu kujua ingawa nilielewa hatari iliyopo. Siyo kwa sababu sisi ni wabinafsi Lexi... ni kwa sababu tunapendana. Najua unampenda Azra pia, na singetaka kufanya ionekane ni kama vile ninaugawanyisha upendo wako, lakini hata wewe unajua kilicho sahihi kufanya ili kumlinda mdogo wako. Anyway... sitakiwi sana kuwaza kwamba mambo yanaweza yakaharibika maana, tuko mbali, na watu wanafikiri tumekufa. Ni kwamba tu...." Sia/Nora akaishia hivyo baada ya kusema hayo yote.

"Nora... ninakuelewa. Tulichojenga huku mimi na wewe ni special sana. Lakini usijali. Nina njia za kuhakikisha kwamba Azra atakuwa salama hata ikiwa atakuwa pamoja nami tena," Bella/Lexi akamwambia.

"I know. Samahani nina... nina-panick sana..."

Lexi, a.k.a Bella, akavishika viganja vya Nora, a.k.a Sia.

"Hapana, najua uko sahihi. Lakini Azra, ni muhimu nikimweka karibu yangu, karibu nasi. Atatulia zaidi tukiwa pamoja maana... kama ujuavyo, ana shida sana kwenye kushughulika na watu ndiyo maana anaogopa. Na ingawa amejitahidi kukaa mwenyewe kwa hiyo miezi yote, bado anahangaika sana," akasema Lexi.

"Okay. Ni sawa. Sasa ndiyo naelewa hata zaidi wewe kufikiria kubadili mazingira ilikuwa hasa kwa sababu yake na siyo kwamba some guy hit on you..." Nora akatania.

Lexi akatabasamu na kusogea karibu ya uso wake Nora zaidi.

"Asante kwa kunielewa Sia wangu," Lexi akamwambia.

"Ahahah... always Bella wangu," Nora akasema.

Lexi akatabasamu kwa hisia.

"Kubadili majina ni step ya kwanza. Azra akifika huku atapaswa kubadili utambulisho wake wote tena," Nora akasema.

Lexi akatikisa kichwa kukubali, kisha akasema, "I'll deal with that."

Nora akashusha pumzi, kisha akauliza, "So... nini kinafuata sasa?"

"Nataka nikufundishe style mpya nimeipata kwenye yoga za leo," Lexi akajibu kiutani.

"Basi unasubiri nini?" Nora akauliza kiutani pia.

Lexi akatabasamu, naye akaanza kumpiga busu laini mdomoni.

Wawili hao, kwa sasa wakitambulika kama Bella na Sia, wakaendelea kuonyeshana upendo mpaka walipokwenda kulala pamoja. Hii ndiyo ingekuwa aina ya maisha ambayo yangeendelea kuwazunguka, wakiwa mbali na bara lao, na wakiwa wamekufa kama Lexi na Nora. Bila shaka, hadithi yao ya mambo yaliyopita wangejitahidi kuiweka nyuma ya migongo, nao wangeendelea kuijenga hadithi yao mpya ya mambo ambayo yangefuata kwenye maisha yao kwa njia bora hata zaidi.





★★★★★★★★★★★★★★★


MWISHO


★★★★★★★★★★★★★★★
 
Well! Well!
You had me speechless bro,
Kazi nzuri sana mwanzo mwisho
Salute sana mwamba
I hope kuna season two unatuandalia
 
Asante sana kwa burudani nzuri sana. Hii ni fasihi andishi inayotengeneza hisia kwa msomaji. Mungu amegawa vipaji hakika. Asante sana kwa burudani nzuri. Kama ukiwiwa wasomaji wako tunangoja kitu kingine ili kituliwaze ktk maisha haya tunatoishi kama watoto wa mama ntilie.
 
Hakika. Niko naandaa pishi lingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…