SIMULIZI: KANGA SEASON 01

SIMULIZI: KANGA SEASON 01

Xav Emmanuel

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2018
Posts
215
Reaction score
316
HADITHI FUPI - S01E01
"KANGA" - [Rudisha Kwa Mhusika]
Mtunzi. Xavery Luoga (Mkandarasi)
Na. +255672493994
___________________

Atuganile Chamse, mrembo aliyeshindana na mumewe kwa muda mrefu, muda huu alikua anamalizia kupanga vitu vyake kwaajili ya kumkimbia huyo mumewe. Safari yake ya siri aliyoipanga tokea muda mrefu, ilichagizwa na ukorofi wa kiume kutoka kwa mumewe, pindi amlazimishapo kufanya mambo asiyoyahitaji. Safari yake hii, ni matokeo ya kipigo cha jana, alishoshushiwa na mumewe.

Apangapo vitu vyake kwenye mfuko mkubwa wa plastiki, Atu aliifikia Kanga, vazi ambalo hakuwahi kulivaa tokea aletewe na mumewe, akimthibitishia kuwa ameiokota barabarani. Licha ya mng'ao wa pekee wa kanga hiyo, Atu hakuwahi thubutu kuivaa mwilini mwake, aliikunja na kuhifadhi, na leo anakutana nayo kutokea katika nguo ambazo alizitekeleza muda mrefu bila ya kuzivaa.

Alipitisha mashauri kadhaa kabla ya kuamua kiunganisha Kanga hiyo na nguo anazopaswa kukimbia nazo, bila kumewe kujua. Alikua anatoroka Atu, Atu Chamse, mtoto asiye na baba wala mama aliyemzaa. Wote walitangulia mbele za haki, mapema tu.

Na alipowaza kuhusu mustakabali wa Kanga hiyo, akahisi kuibeba itampa faida nyingi za kumuumiza mumewe kuliko kitu chochote kingine, kwani tokea aolewe miezi sita iliyopita, Kanga hiyo ndio zawadi ya mwisho kutoka kwa Sunubi, mumewe.

Aliunyanyua mfuko ulokwisha vimba kwa nguo zisizopagwa, haukuwa mwepesi, alichagua nguo chache tu, zikiwemo nguo zitazositiri tupu yake, pamoja na baadhi za kujifutia maji atokapo kuoga; magauni manne marefu, likiwemo la satini, pamoja na blauzi zinazofanana rangi karibia na rangi yake ya damu ya mzee; ndala alishazikomea miguu, labda kwenye begi, aliweka viatu vyake pea mbili, ambavyo anaviamini haviwezi kumtia aibu aingiapo Kwenye umati wa watu wengi wasiomzohea.

Atu alifanikiwa kutoroka kwenye nyumba ya mumewe, bila kuacha notisi yoyote mezani, labda kwa ishara ya kutoweka kwa Kanga ambayo alikuwa anashinikizwa kuivaa na mumewe tokea amuokotee pahali, hii itakuwa ishara pekee ambayo Sunubi atakuna nayo na kutambua kuwa, sasa ametalakiwa na mkewe, bila maelezo ya muhimu ya anamuacha kwa sababu gani, tena bila kukumbuka kiapo cha 'Hakuna cha kututenganisha'.

Lo, Atu! Unakwenda wapi wewe?

Gari alipanda na mjini akafika, kwa pesa zake alizowekeza kidogo kidogo kila akifanya tukio la kimaendeleo kwenye kaya yake. Hakutumia pesa ya Sunubi, mumewe aliyemuita Mlevi aliyeshindikana, Malaya mwenye medali... Aliamini Sunubi hana la Mtume wala la Mhazini, ijapokuwa huyo Sunubi, hakujiona hivyo, alihusi ni mume aliyefanya majukumu yake kwa kiwango cha Juu, hasa baada ya kumletea zawadi ya Kanga, mkewe.

"Shaga'ngu! Nimetoka gerezani" Atu alijisifia kwa maneno ya kuponda nyumba ya mumewe, akikaa sawasawa kwenye kochi la mtu mmoja lililojaza chumba kimoja chenye kitanda kikubwa na vitu vingine vichache, chumbani kwa rafikiye.

"Siamini Atu, hivi kweli umefanikisha kumkimbia Sunubi? Ameamua kuondoka kweli Malindi na kuja Mji mwema?" Rafikiye alifurahi. Ni moango waliousuka mpango siku nyingi, ila kutokana na uzito wa Atu kwenye kufanya maamuzi, mpango ulichelewa kutiki.

"Basi nikadhani, Mwane ameshatajirika. Nilitegemea n'takuta mjengo mkubwa mno, kumbe ndo kwaaanza unajipanga mwaya!" Atu hakuficha maneno, alisema yote kwa shoga'ke aliyemtambulisha kwa jina la mwane.

"Usikihukumu kitabu kwa kutazama jalada, mpenzi, katika kundi letu, mimi ndio mtu wa mwisho kuyafikia mafanikio, WAZAWA wote wamefanikiwa, watu wameporomosha majengo Atu. Ni juhudi zako tu, kujituma kwenye kazi."

"Unajua Mwane, bado hujaniweka wazi ni aina gani ya Kazi ambayo nakuja kuungana nawe, mana uliniambia nakuja kuongeza nguvu... Kila kitu umeshakiweka sawa" Atu alisema, macho ya shauku yakimmulika shogaake Mwane, aliyevalia blazia nyekundu na kanga ya rangi ya maziwa, tatoo ya kipepeo iking'aa upande wa kulia wa shingo yake.

"Na hilo jina Mwanu, niite humu ndani tu, huko nje naitwa Mwana, Mwana-mama, Mwana-utamu, Mwana-chitoto, Chochote utachoweza kuongozea. Hebu panga kwanza nguo zako kwa utaratibu, hilo fuko litajaza chumba, kisha nikakutambulishe kwa WAZAWA, mambo yashachangamka shoga'ngu" Mwane, Mwana, kama alivyojitambulisha, aliongea haraka haraka ili kutojenga hofu. Kazi alomwitia Atu si ya kusemeka kwa maneno, inahitajika kushuhudia kwa macho.

Atu alisimama, akazimwaga nguo zake kitandani na kuanza kuzipinga kama zilivyopangwa nguo za Mwane, ila kasheshe ikaanzia ilipoonekana Kanga...

Atu hakuamini macho yake, ile kanga haijuwa ile aliyoichukua Malindi, ilikuwa imebadilika kabisa, awali ilikua na mchoro wa ua jepesi, liliozungukwa na rangi nyeupe huko ua hilo likichorwa kwa rangi nyeusi, lakini kwa sasa, kanga ilikua nyeupe vile vile ila ule mchoro ulibadilika, haukuwa Ua, bali ni ndege, kama njiwa, aliyechorwa kwa rangi rangi nyekundu iliyokorea...

Unashauku? Tukutane wakati mwingine.

Asante kwa Kuwasiliana na,
HADITHI ZA MKANDARASI ✍️

Hizi Hapa HADITHI na BEI Zake.

01 MISSION TANZANIA =
02 NAFSI YA GIZA =
03 USIKU WA MANENE =
04 HISIA ZA MWISHO =
05 MKUKI WA MAPENZI -
06 MACHOZI YA DAMU -
07 INSPEKTA KONYA (S01&S02) =
08. JUMBA BOVU = (kitabu)
09. DAMU BATILI =
10. MHURI WA KIFO - (kitabu)
11. MKOBA WA SIRI =
12. GEREZA LA NDOA
13. MWALIMU WA ZAMU =
14. SITO'KUSAMEHE DAIMA - Bure
15. NGUVU YA UPENDO = Kitabu

Karibu Whasap kwa 0672493994
 
Back
Top Bottom