George Betram
JF-Expert Member
- Oct 10, 2015
- 4,672
- 6,272
Harare,Zimbabwe
Dereva wa basi katika hospitali ya vichaa ya Bulawayo Mental Hospital iliyokuwa katika miji wa Bulawayo,Zimbabwe alikua akiwasafirisha vichaa 20 kutoka Harare kwenda Bulawayo,lakini akiwa njiani Dereva huyo anasimamisha basi na kuingia katika baa moja iliyopo mji wa Harare kwa lengo la kupata kinywaji kidogo kisha aendelee na safari yake.
Mara baada ya kumaliza kinywaji dereva anarudi kwenye basi kwa lengo la kuendelea na safari,lakini jambo la kustaajabisha anakuta basi halina mtu hata mmoja,vichaa wote 20 wametoroka na kuingia mitaani kipindi yeye akiwa baa.
Baada ya Dereva kukaa chini na kuwaza nini afanye juu ya tatizo lililotokea,dereva anafanikiwa kuja na maamuzi ya ajabu sana.
Dereva anaamua kuendesha gari mpaka kituo cha mabasi kilichopo karibu,baada ya kufika kituoni Dereva anatangaza usafiri wa bure kwa abiria 20 wanaohitaji kwenda Bulawayo,watu ishirini wanapatikana haraka,kisha wanapanda kwenye basi tayari kwaajili ya safari ya kwenda Bulawayo bila kujua mpango wa dereva.
Baada ya abiria 20 kupanda kwenye basi,dereva anaendesha basi moja kwa moja mpaka hospitali ya vichaa ya Bulawayo (Bulawayo Mental Hospital),baada ya kufika hospitali ya vichaa dereva wa basi anakutana na wafanyakazi wa hospital na kuwakabidhi abiria wale 20 kama vichaa ambao amewatoa katika mji wa Harare.
Bila kujua wafanyakazi wa hospitali ya vichaa wanawachukua abiria wote na kuwaingiza hospitalini tayari kwaajiri ya kuanza tiba ya ugonjwa ya akili,abiria wanagoma na kupiga kelele kwamba wao si vichaa,lakini kelele zao hazikuwasaidia chochote,wafanyakazi wa hospitali waliamini kuwa wale ni vichaa na hawakua tayari kusikiliza kile walichokua wakizungumza.
Ilichukua siku tatu hospitali kugugundua kwamba wale watu ishirini(20) walikua si vichaa,ila kuna makosa yamefanyika.
Wale wagonjwa wa akili 20 waliotoroka hakupatikana hata mgonjwa mmoja.
Kisa hiki ni tukio ambalo lilitokea nchini Zimbabwe mwaka 1997,tangu mwaka huo story hii imekua ikichapishwa katika Magazeti na mitandao mbalimbali nchini Zimbabwe na nchi zingine.Lakini bado kuna mashaka juu ya ukweli wa tukio hili.
Pamoja na kuwa na utata juu ya ukweli wake,lakini story hii inaweza kutusaidia katika kutambua namna ya kufanya au kutofanya maamuzi.