Simulizi: Masikini Aisha

Simulizi: Masikini Aisha

CK Allan

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2013
Posts
2,781
Reaction score
6,139
Aisha alikuwa binti mzuri Wa uso na umbo ..Aisha alijulikana kwa ukarimu wake na upole..

Siku moja Aisha akiwa na wasichana wenzake walitekwa na kuozeshwa kwa wanaume kinguvu...

Aisha aliishi utumwani kwa tabu akifanyishwa kazi za kila namna..

Wanasema hakuna marefu yasiyo na ncha hatimaye...mwaka 1961 ndugu zake aisha walijitutumua na kumkomboa ndugu yao na Inasadikika hakuna damu iliyomwagika na ndio maana Aisha hakuwa na DOA lolote katika mwili wake....

Aisha alirudi katika ardhi yake akapata mume ambaye hakumtesa Aisha ...alimpenda sana...pamoja na kumlea Aisha mume huyu alikuwa na malengo ya kuunganisha ndugu wote ili wasitekwe tena..Aisha alimpenda mume wake lakini Mungu alimpenda zaidi....akamchukua...

Hata hivyo Aisha aliachiwa Mali nyingi sana na mume wake....na alipewa angalizo kuwa wapo wanaume wakware watakaojitokeza ili wamrithi si kwamba wanampenda yeye Bali Mali zake!..

Hatimaye kweli wanaume wakajitokeza...kila mmoja akatoa Sera zake ...hatimaye akajitokeza Juma! Juma akakubalika machoni pa Aisha na ndugu zake....kwanza Juma alikuwa ni ukoo ule ule Wa mume Wa zamani Wa Aisha kwahiyo Aisha alidhani ataendeleza mazuri ya mumewe kipenzi! hatimaye Juma akapewa mke kwa sherehe kubwa....kipato huleta majivuno...Juma akabadili hati miliki zote zisome jina lake...nyumba,mashamba, viwanja vyote Juma akajimilikisha!!

Na mbaya zaidi juma akaanza tabia nyingine mbaya kabisa ya kumpiga mkewe kila anapodai haki yake!.. Juma akageuka nyang'au Mkubwa... kwa amani kabisa Aisha akaamua kutengana na Juma pamoja na wingi Wa miaka yote walioishi pamoja! hapo sasa akajitokeza mwanaume mwingine akadai yeye atamtunza vizuri Aisha kwa manufaa ya watoto Wa Aisha ..ikiwemo kuwasomesha mpaka watakapochoka wenyewe....kidogo Aisha alivutiwa nae...na kila alipokuja usiku Aisha alimuandalia chakula kizuri sana.

..hatimaye minong'ono ikaanza na kumfikia Juma... Juma akaanza vitisho kwa Aisha alidai kama Aisha akiolewa na bwana mwingine nyumba haitakalika..na Juma akaanza tabia ya kupita kwa ndugu zake Aisha akawashawishi kwa zawadi na bakshishi...kumbuka Juma ana mali nyingi..basi pole pole ndugu zake Aisha wakamshawishi eti arudiane na mumewe kwani amebadilika siku hizi! eti asisikilize porojo..

Kwa uchungu siku hiyo yule bwana mwingine baada ya kupewa mkanda mzima na Aisha alimwambia maneno machache tu..

"Aisha nakupenda sana kumbuka Juma anakulaghai...ni miaka mingapi umeishi nae ? zaidi ya 30 na amekufanyia mangapi Leo hii anakushawishi kwa vijizawadi hivi u akubal? Aisha Mimi nakuacha lakini Ipo siku utanikumbuka...

kweli Aisha akarudiana na Juma!! mwanzoni Juma alionyesha kweli sio Juma yule amebadilika kabisa huku akichapa kazi kwa bidii..

Aisha alifurahi na kuanza kumdhihaki yule bwana kuwa kumbe "angejichanganya" hata hivyo yule bwana alimjibu Aisha huku akitabasamu...

"Aisha Mimi nimekua nimecheza na Juma tangu utotoni utotoni ninamjua Juma vizuri...Juma ni yule yule hajabadilika na hatabadilika..."

mwisho
 
Mbona kama stori inatakiwa kuendelea.....mwisho wa Aisha na Juma ni upi? Au jibu la yule bwana kuwa Juma hawezi kubadilika ni kweli?

Ningekua Mimi Aisha ningewalea tu wanangu kwanza.... Sasa kukuru kakara hizo ataishia kuachwa njiani na watoto huku Mali zote zimetapanywa.
 
Hahaaaaa huyu Aisha huyu. Saivi anazuiwa hata kuongea na ndugu zake. Hela ya matumizi hapewi(tunabana)
 
Wakati nasoma hii hadithi linimuonea huruma sana Aisha, lakini si kiviiile kwa kuwa sikuwa na mfahamu, lakini mwisho wa hadithi nimestuka kumbe ni mtu ninae mjue kabisa, sio tu kumjua ni mtu anae ni husu kabisa, sio tu kunihusu na mimi pia ninahusika katika hii hadithi.
 
Mbona kama stori inatakiwa kuendelea.....mwisho wa Aisha na Juma ni upi? Au jibu la yule bwana kuwa Juma hawezi kubadilika ni kweli?

Ningekua Mimi Aisha ningewalea tu wanangu kwanza.... Sasa kukuru kakara hizo ataishia kuachwa njiani na watoto huku Mali zote zimetapanywa.
Nikweli stori inaendelea, muda wa muendelezo bado kwamaana ni stori isiyo na mwisho.

bheka nawe at amashumi amabini anamabini amawaka amahlanu.
 
Ndo maana serikali haitaki masomo ya sanaa
Mtu unasemwa upo hapo hapo hii haisaidii kuleta viwanda. Sasa nasema tena nyie mikopo ya elimu ya juu mtaisikia kwenye bombedier tu
Hamna namna sasa
 
Nimesoma between lines kuna kitu nimepata na kamwe maisha ya Aisha yatakuwa ya tabu sana
 
vipi? kizulu kinapanda nini?
Naanza kuelewa somo sasa. Kweli Juma kamwe hatobadilika mpaka mauti yatakapo mkuta na bado damu yake aloiacha itazidi kumuendesha Aisha. Pole sana dada Aisha.. Laiti ungeweza kujiokoa unge komboa kizazi chako
 
nikisikia hili jina la AISHA nakumbuka wimbo mmoja wa charanga wa zamani kidogo uliokuwa unatambaga sana sijui umeimbwa na nani? mwenye nao anisaidie jinsi ya kuupata au nani aliuimba
 
Mimi napita tu koment at your own risk...

Aisha.. bado yupo na ndoa yake na bwana juma
 
Back
Top Bottom