Wingu Jeusi
Member
- Aug 9, 2017
- 18
- 10
"Ni hatari mno kuukabidhi uongozi wa kitu nyeti kama nchi mikononi mwa mtu mwenye uchu, ujivuni na ubinafsi unaoweza kumfanya aamini yeye anapaswa kuwa juu ya kila kitu bila kujali misingi na taratibu tulizojiwekea. Kwani hili ni taifa linalopaswa kuongozwa kwa misingi ya DEMOKRASIA".
Kwa! Kwa! Kwa!
Yanasikika makofi mara baada ya msemaji huyo kuhitimisha. Ni mwanamume anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 57 hadi 60, amevalia kanzu nyeupe, mawani na baraghashia huku miguuni pake makubadhi yanayoonekana aghali kidogo yakiwa yamejituliza vema. Anaonekana ni mtu anayeijua vema historia na mambo mbali mbali ya ki-nchi.
Makofi yanapokoma, anatoa noti ya shilingi elfu kumi mfukoni mwake halafu anatoa maelekezo kuwa kila mmoja aliyeko katika kibanda kile apewe kikombe cha kahawa na kashata.
Kwa! Kwa! Kwa! Makofi yanamiminika kwa mara nyingine tena. Muuza kahawa anabeba birika lake na kuanza kuwapimia kahawa watumiaji wale mmoja baada ya mwingine.
Wakati wanaendelea kufurahia ladha ya kahawa, mwanaume yule mtoa ofa, anajikohoza kidogo na watu karibia wote wanageuza nyuso zao na kumakinika naye. Naam! Tajiri anakohoa....
Kwa utulivu wa hali ya juu kabisa anawatazama kwa zamu halafu anauliza iwapo wanafahamu asili haswa na maana ya lile neno Demokrasia, swali lile linafanya kijiwe kile kuvamiwa na ukimya wa muda mfupi na kisha anaendelea kwa kusema, "Demokrasia ni neno ambalo limetokana na muunganiko wa maneno mawili ya kigiriki. Demos na Kratein!
Demos haimaanishi kupiga domo, na wala haimaanishi mfano kama ambavyo mtu anaweza kutafsiri akiamua kuiweka katika lugha ya kiingereza. Neno hili linasimama likimaanisha Watu, na Kratein likiwa na maana ya Uongozi. Hivyo Demokrasia kwa maelezo mafupi ni uongozi wa watu kwa ajili ya watu".
Maelezo yale yanaonekana kumsisimua zaidi kijana mmoja aliyevalia jezi ya timu moja maarufu ya mpira wa miguu eneo lile, anaweka kikombe chake cha kahawa chini na kusimama. Anakunja kiganja chake katika mtindo wa ngumi, halafu anaelekea kugongesha na mkono wa tajiri yule ambao nao sasa uko katika mtindo kama wake. Ishara ya kuvutiwa na maelezo yale. Wanapeana tano!
Anapokwisha kumaliza kutoa tano, tajiri yule anaendelea. "Taifa lolote linaloongozwa kwa Demokrasia lazima lifuate misingi yake. Misingi ambayo imegawanyika katika nyanja mbalimbali.
Kwanza ni uchaguzi, demokrasia inasisitiza uchaguzi wa huru na haki. Nchi inayoongozwa kwa misingi ya demokrasia inalazimika kutoa nafasi kwa wananchi kumchagua kiongozi wanayemhitaji bila udanganyifu wowote ule na hii ndio haswa inayoleta tafsiri sahihi ya uongozi wa watu".
Maelezo yale yanamletea mshawasha muuza kahawa ambaye anaamua kumkata kauli tajiri yule na kuuliza, "Mzee, unaukumbuka ule mwaka ambao mvua zilikuwa nyingi sana?," tajiri yule anatikisa kichwa kama ishara ya kukubali. Halafu Muuza kahawa anaendelea tena, "Je unakumbuka namna chama cha NIOMBEE kilivyoshinda kwa kutumia maguvu na ulaghai hata kuweka rekodi iliyopitiliza ya ushindi wa kura nyingi kushinda idadi ya wapiga kura katika baadhi ya majimbo yake katika nchi ya Waendeni?" Mzee yule anatikisa kichwa tena akiashiria kukubali. "Hii inakuaje sasa? Maana si inasemekana nchi ya WAENDENI inaongozwa kidemokrasia?"
Muuza kahawa anakaa kimya mara baada ya kuuliza swali akingojea jibu lake kutoka kwa Bwana yule. Mzee yule tajiri anatikisa kichwa kwa masikitiko na uso wake unaonyesha fadhaa kidogo halafu anatoa jibu fupi tu. Anamwambia, "Chini ya rais Kichwa, Waendeni ilikuwa ikiendeshwa chini ya kivuli cha demokrasia tu. Lakini hakukuwepo na demokrasia thabiti katika uongozi ule, hii ndio sababu ya kwanini haswa matukio yale yalichukua nafasi na hakuna aliyenyanyua angalau kinywa chake na kukemea". Anamtazama muuza kahawa ambaye sasa ni kama anayefanya tafakuri juu ya maneno yale na anaendelea kusema.
"Mbali na hilo, msingi mwingine wa Demokrasia ni Bunge". Kabla hajaendelea, muuza kahawa anamdaka kauli yake tena na kupachika swali. "Kwa hiyo Waendeni ilikuwa inaongozwa kidemokrasia ama laa, maana si wana bunge wale?" Swali hili linamfanya tajiri yule atoe tabasamu hafifu huku akionyeshwa dhahiri kukerwa na mtindo ule wa uulizaji anaoutumia muuza kahawa. Lakini anajitahidi kuficha hisia zake halafu anafafanua. "Demokrasia inasisitiza juu ya kuwa na bunge huru na sio bunge tu. Bunge linalopaswa kusimamia matakwa ya wananchi, Waendeni haikuwa hivyo. Maamuzi mengi yalifanyika kwa ajili ya kumridhisha rais Kichwa. Hivyo bado utawala wa Waendeni licha ya uwepo wa Bunge, inaendelea kutazamwa kama nchi inayopelea kuvikwa kofia ya uwakilishi wa mataifa yenye uongozi wa kidemokrasia".
Kufikia hapo, kama walioambizana, wasikilizaji wale kwa pamoja wanatikisa vichwa kutokea juu kwenda chini kwa kurudiarudia kama wachezao ngoma ya asili ya Kikurya, yaani ritungu. Wanakubali...
"Ukiachilia mbali hayo mawili, uhuru wa vyombo vya habari ni eneo lingine lenye uzito linalopaswa kupewa kipaumbele katika kuhakikisha demokrasia inaishi. Vyombo hivi vinatakiwa kuwa na uwezo wa kuripoti hata taarifa zinazowagusa viongozi kwa ajili ya kuhabarisha, kuonya ama hata kuelimisha bila kuingiliwa", anaongezea...
"Dah! Ndio naelewa sasa Faza kwanini unasema unasema Waendeni haikuwa ikiendeshwa kwa misingi ya demokrasia". Anasema kijana mmoja ambaye kwa mtazamo wa haraka, unaweza kumuita msanii wa muziki katika miondoko ya kizazi kipya. Amevaa suruwali ya kubana, mkufu shingoni na hereni katika sikio lake la kushoto.
"Umenikumbusha" anasema tena. "Ni kweli kuna vyombo viliwahi kufungiwa kwa kuandika madudu yaliyokuwa kwenye moja ya wizara za serikali ya raisi Kichwa, mfano mzuri ni lile gazeti la Mwan..''
Kabla hajaendelea mzee wa ofa, mzee tajiri anasimamisha kidole chake cha shahada mbele ya midomo yake kama ishara ya kumnyamazisha. Halafu anamnanga, "bwana mdogo, uko sahihi lakini siku nyingine ujifunze kwanza kuomba nafasi wakubwa wanapokuwa wakiongea..."
Hili linamnyong'onyeza kijana yule, anaamua kukaa kimya na kumuachia mzee yule ulingo wake.
Nyong'onyeo la barubaru yule halidumu sana. Kelele za vijana wanaozomea na kupiga miluzi kutokea upande wa pili wa barabara zinavuta hisia za wengi wao bandani pale. Wapo wanaosimama na kuelekea huko, na wengine wanaamua kuangazia upande ule kutokea katika maeneo waliyoketi ili kujua ni kipi haswa kinaendelea. Anaonekana binti aliyevaa suruali nyepesi iliyoushika vema mwili wake na kiblauzi kidogo kilichoshindwa kumpatia stara ya kutosha na kuacha sehemu kubwa ya maungo yake wazi. Vya siri vimeletwa hadharani wacha washangilie...
Shangwe lile linadumu kwa dakika zisizozidi tatu. Na linapokwisha, tajiri yule anakikusanya tena kijiji chake Halafu anaongezea..
"Msingi mwingine muhimu kwenye demokrasia ni mgawanyo wa madaraka, mihimili mikuu inayojenga serikali inapaswa kufanya kazi kwa uhuru bila kuingiliana kimajukumu. Bunge liunde sheria na kutimiza majukumu yake mengine bila kuingiliwa, mahakama vilevile na hata upande wa uongozi nao usimamie katika mstari wake wenyewe. Je, naeleweka vyema?" Anaweka tuo kwa swali, na wakati huo huo mtoto wa muuza kahawa ambaye alikuwa bize kuosha vikombe vilivyokwisha kutumika huku akiwa kimya muda wote. Anafungua kinywa chake katika namna ya kuunga mkono hoja. Anakiri kumuelewa halafu anamtupia swali. Anauliza, "Mzee vipi kuhusu siasa ya vyama vingi. Hii pia ni sehemu kati ya misingi ya demokrasia? Maana kuna mahala nimewahi kusikia wakisema kitu kama hicho".
Kabla ya kumjibu, tajiri yule anaruhusu usoni pake pachomoze tabasamu pana. Halafu kwa namna ya ujivuni kidogo anamjibu kijana yule huku akitikisa mguu wake wa kushoto uliobebwa na ule wa kulia. "Hilo ni sahihi, kwa sababu uwepo wa vyama vingi unatoa nafasi kwa raia kushiriki kikamilifu na kwa upana zaidi katika kuamua aina ya uongozi wanaouhitaji. Uongozi unaokandamiza uanzishwaji wa vyama vingi, ni dhahiri unaiminya demokrasia".
Anapomaliza kueleza hayo, mzee yule aliyejizolea sifa ya utajiri katika kijiwe kile anamkazia macho kwa muda mtoto yule wa muuza kahawa ambaye haonekani kuwa na swali la nyongeza. Anatoa mawani yake, na kuyafuta kwa leso yake kisha anayarudisha tena usoni pake. Haieleweki alikuwa anafuta kitu gani maana hakuna mabadiliko yoyote yanayoonekana katika mawani yale. Anaendelea tena..
"Ndugu zangu, tunatakiwa kuwa sehemu ya harakati za kukemea unyonywaji na uminywaji wa misingi ya kidemokrasia mahala popote pale. Tusipofanya hivyo yatatukuta kama yaliyowakuta raia wa Waendeni. Kubanwa na kukandamizwa kwa demokrasia kumepelekea vifo vya wanafunzi kutokana na risasi za maaskari waliopaswa kuwalinda, kumepelekea uwepo wa unyang'anyi wa viongozi dhidi ya wananchi chini ya mwavuli wa maelekezo kutoka juu, kumepelekea uwepo wa migogoro isiyokwisha, na zaidi kumepelekea kukosekana kwa uhuru wa kujieleza na kuchangia udumavu wa maendeleo ya nchi na mwananchi mmoja mmoja kiuchumi na kijamii. Tukiruhusu hili, itakuwa ni palizi rasmi ya anguko letu kama taifa. Tuko pamoja?"
Wiu.. Wiu... Wiuu.. Wiuu.... Kabla hawajamjibu ving'ora vinasikika na magari yaliyoongozana yanafunga breki na kisha wanashuka watu waliovaria sare za jeshi la polisi na mitutu yao mikononi. Kwa fujo wanavamia banda la muuza kahawa na kumbeba juu juu, tajiri yule aliyekuwa akiendesha mazungumzo yale yasiyo rasmi. Baadhi ya wazee na vijana waliokuwa hapo tayari wametimua mbio! Birika liko chini huku mfuniko wake haujulikani ulipokimbilia. Muuza kahawa kajibanza pembezoni mwa mtaro uliopo jirani na banda lake huku pumzi zake zikishindana kuingia na kutoka puani. Ana hofu kuu!
Maaskari hawaonekani kuwa na shida na mtu mwingine yeyote tena tofauti na yule tajiri ambaye tayari wamembeba msobemsobe. Wanapomfikisha katika magari yao wanambwaga mithili ya mzigo wa kuni. Puuu! Hawasemi kitu...
Wakati huo huo mwanamama mmoja mwenye haiba ya uchamungu na uungwana, anatoa kichwa kupitia dirishani kutokea ndani ya moja ya magari yaliyofika eneo lile. Anaonyesha tabasamu pana, kisha taratiibu anainua mkono wake na kuupunga hewani. Anapomaliza, anarejesha kichwa chake ndani ya gari na dereva wake anapiga rivasi na kuligeuza gari halafu analiondoa kwa kasi huku akiacha vumbi nyuma yake.
BADO TUKO WAENDENI!!
Inasomeka plate number.

Upvote
2