Simulizi: Mji Wenye Shida - 1

Simulizi: Mji Wenye Shida - 1

mastory

Member
Joined
Dec 5, 2018
Posts
18
Reaction score
10
SIMULIZI;MJI WENYE SHIDA
MTUNZI;RAJA SAIDY
WHATSAPP;0756920739.
SMS;0621047841.

SEHEMU YA KWANZA ( 1 )

ANZA NAYO......

Ilikuwa siku ya jumapili,nakumbuka nilikuwa nimejilaza kwenye kijigodoro changu huku mvua kali ikiendelea kunyesha.

Yalikua majira ya saa tatu usiku.Macho yangu muda wote yalikuwa yakitazama juu ya paa la nyumba,yote sababu nilikuwa nikiendelea kutazama tundu za bati zisiozidi tano, zikiendelea kupitisha maji na kukifanya chumba changu kujaa maji.

Maisha yangu yote sikuwahi kulala kwenye kitanda hivyo kijigodoro changu kilikuwa kwenye sakafu ya chumba hicho iliokuwa ya udongo.

Kwakuwa mvu bado iliendelea kunyesha ilipelekea kijigodoro hicho kutapakaa ipasavyo.Baridi kali ilizidi kuongezeka na kujikuta naanza kutetemeka huku meno yakigongana mithili ya nyimbo za kale na hii ni kutokana na baridi kali ilivyokuwa ikizidi kuongezeka.

Matumaini ya mvua kukata yalizidi kufifia kwani kila muda ulivyozidi kujongea ndivyo Mvua ilizidi kuongezeka, nilitamani nipande juu ya paa la nyumba hiyo ili nizibe tundu hizo lakini sikuwa na uwezo huo, nilichokifanya ni kuchukua simu yangu ya nokia niliozawadiwa na Mwalimu Onyango na alinizawadia siku ambayo niliongoza kwenye mtihani wa jaribio la Hisabati pindi nilipokuwa kidato cha pili, nilibonyeza batani nyekundu kwa lengo la kuiwasha.

Baada ya simu kuwaka mtandao ukasoma umejaa.Ghafla jumbe zikaanza kuingia na hii ni kwa sababu niliizima simu hiyo kwa muda mrefu.Kisha nikaamua kufungua jumbe moja baada ya nyingine,nyingi zilikuwa za kampuni ya mtandao ninaotumia zikinisihi nilipe deni nililokopa pindi nilipoishiwa salio, niliamua kuzipotezea kwani sikuwa na pesa ya kulipa kwa wakati huo.Niliendelea kufungua zile ambazo sijazisoma hadi nikafikia jumbe ambayo ilitoka kwa rafiki yangu tuliyemaliza nae kidato cha nne.
ujumbe huo
ulisomeka vyema,
"
VIPI KAKA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YAMETOKA MIMI NIMEFAULU, ILA KWA UPANDE WAKO NIMEONA HUJAFANYA VYEMA ,UMEFELI KAKA UNA "D" MOJA YA HISABATI.”

Ujumbe niliusoma vizuri sana, ulikua unatoka kwa Musa aliyekuwa rafiki yangu wa karibu.

Niliumia sana kwa taarifa zile maana darasani nilikuwa na uwezo sana, ila kilichonichanganya ni mawazo juu ya kifo cha wazazi wangu wawili akiwemo Baba na Mama niliumia sana,baada ya kukumbukua tena kifo cha Mama yangu wa kambo na Baba yangu wa kambo, walionipa malezi bora.

Sababu ya kifo chao ni ajali ya Bus kitu kilichopelekea niishi maisha ya tabu na kuamua kufanya vibarua na kazi ndogo ndogo za hapa na pale na kubahatika kupanga kwenye chumba chenye tundu ambazo zilikuwa zikinitesa hasa katika nyakati za masika, nilijikuta natiririkwa na machozi shavuni na kunifanya niumie zaidi.

Nilitoa betri na kuzima simu, kisha nikaibana mfukoni ili isipatwe kuingiwa na maji
Niliibana kwenye mfuko wa mbele wa jinsi yangu niliyoikata mwenyewe, japo ilikuwa imechakaa sana na ni moja kati ya nguo zangu nilizozipenda mno.

Wakati yote hayo yakiendelea sikutaka kulala maana chumba changu kilikua si imara hivyo nilihofia usalama wangu, nilichokifanya ni kuanza kuandaa vitu vyangu vya muhimu kwa ajili ya safari ya ghafla nilioamua kuifanya.

Baada ya matokeo ya kidato cha nne kutoka ili kuepuka aibu ya kukutana na wenzangu na kuamua kwenda mjini kutafuta maisha maana nilikua natengemea nikifaulu niende chuo lakini ndoto zangu zimeharibika kutokana na ubovu wa matokeo hayo.

Hivyo basi baada ya kuwa nimemaliza kupanga vitu vyangu vya maana na vilikua vichache sana,niliamua kuvunja kibubu changu nilichokuwa natumia katika kuhifadhia fedha nilizokuwa nalipwa kama posho kwa kila kazi niliokuwa naifanya.

Nikiwa tayari nimeshakifungua kibubu hicho, nilikutana na fedha nyinyi kisha nikaanza kuzihesabu.Zilkuwa Elfu arobaini na kujipa matumaini zitatosha kwa safari yangu.

Nilimaliza kujiandaa kikamilifu,bila ya kupoteza muda nilielekea kwenye kijigodoro changu ambacho ukipiga ngumi unaumia kwenye sakafu ya chini maana kilikuwa chembamba sana,na pia baridi haikuacha kuendelea kunitwanga.

Niliendelea kufanya hivyo mpaka usingizi ulivyonipitia kwa shida..
Yalikuwa majira ya asubuhi sikutaka kuchelewa, nikachukua mswaki wangu wa kijiti,kisha nikaanza kujisukutua kwa ajili ya kupunguza harufu mdomoni.

Nilipomaliza kwa kila kitu,nikaweka begi langu la BOB MARLEY mgongoni kwa ajili ya safari na kwenda kwa jirani kwa lengo la kumuomba anitunzie kijigodoro changu maana ndio kitu cha muhimu kilichokuwa kimebaki.Vitu nilivyoviweka kwenye begi ilikuwa ni kandambili zilizitoboka kwa chini na kuacha alama ya visigino vya miguu, pensi zangu nyeusi mbili pia zikiwa na harufu ya oili na shati mbili za mistari ya rangi nyeusi.

Siku hiyo nilivaa shati la mikono mirefu lenye rangi ya pinki na nyeupe, na suruali ndefu ya kitambaa nyeusi yenye vilaka makarioni, sikujali yote hayo na kuamua kwenda kumfuata jirani.

Niligonga mlango wa jirani mara tatu naye aliitikia na kutoka nje,alionekana ya kuwa ameamka mapema sana japokuwa kulikuwa bado hakujapambazuka kwani kulikuwa na kagizagiza.

"Shikamoo??"

"Marahaba ujambo mwanangu???"

"Sijambo...Mzee samahani mimi naenda mjini kutafuta maisha nachokuomba Mzee wangu unilindie ili godoro mungu akinijalia tutaonana sawa Mzee wangu....???"

"Sawa mwanangu hiyo haina shida!!!"

Baada ya kumkabidhi kijigodoro hicho niliondoka, sikujiuliza ni kwanini Mzee huyo hakuniuliza maswali mengi kwani alikuwa sio muongeaji sana na alikuwa anasifika pale mtaani kwa upole, na ukarimu.

Nikaanza kuondoka zangu na kuelekea kwenye chumba changu mahali napoishi maana kilikuwa kimejitenga,niliibana kufuli yangu yenye kutu na kuelekea stendi moja kwa moja.

Mungu akasaidia nikafika stendi bila kukutana na mtu yoyote njiani na kupanda basi kwa ajili ya safari ya kuelekea mjini kutafuta maisha.(Kama unataka muendelezo wa simulizi hii njoo whatsapp namba 0756920739 nikutumie chapu.)

Je,nini kitaendelea...........
1545308289013.jpeg
 
Sasa watsap kufanya nini kama umeamua kuileta hapa?
 
Siyo rahisi ati
Mi nimeangalia kwnza mwisho wa hii adisi nilivyoona whatsup nikacoment na nasepa kma hivi
 
Back
Top Bottom