Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,641
- 11,958
SIMULIZI:MPENZI JINI.
MTUNZI:LAMECK PETER
SEHEMU YA 1.
...Kwa Jina Ninaitwa KETARO Ilikuwa Ni Mwaka 2015 Nikiwa Na Umri Wa Miaka 21 Nikiwa Nimezaliwa Mwaka 1994.Nilikuwa Ninaishi Na Bibi Yangu Mzaa Mama Katika Mkoa Wa Rukwa Sumba Wanga.Bibi Yangu Huyo Alikuwa Ni Kabila La Mfipa.Bibi Yangu Alinilea Mimi Tangu Utotoni Hadi Kukuwa Kwangu Hakuwahi Kunieleza Lolote Kuhusu Maisha Yangu Zaidi Ya Kuniambia Yakuwa Wazazi Wangu Walifariki Na Ajali Nikiwa Mdogo Sana Ndipo Aliponichukuwa Nakuishi Na Mimi Nikiwa Na Umri Wa Miaka 4 Hadi Sasa Nikiwa Na Umri Wa Miaka 21. Bibi Yangu Alikuwa Ni Mzee Pia Alikuwa Akijishughulisha Na Shughuli Za Kilimo.Bibi Yangu Jina Lake Halisi Alikuwa Akiitwa LIKANDE.kwa Kweli Nilikuwa Nikimpenda Na Kumjali Sana Bibi Yangu Kwani Nilikuwa Namchukulia Kama Mama Yangu ,Bibi Yangu Alikuwa Akinihaswa Na Mengi Juu Ya Maisha haswa Maisha Ya Kijijini Kwetu Hapo Nakuniambia Mara Kwa Mara Yakuwa Niwe Makini.Katika Maisha Yangu Yote Nilikuwa Makini Na Sikutaka Kujihusisha au Kujiingiza Katika Mambo Yasiyo Faa.Kwa Kweli Watu Wengi Kijijini Hapo Walinisifu Kwa Utii Wangu Na Wachache Wake Wakinisifu Kwa Jinsi Nilivyo Mzuri Kwa Lugha Ya Wageni Wanasemaga Handsome Boy.Wanawake Wengi Walikuwa Wakivutiwa Nami Nakunisifia Hali Iliyonifanya Mimi Mwenyewe Kujishangaa Na Kujitazama Kwenye Kioo Mara Kwa Mara Lakini Hali Ile Ya Kusifiwa Na Wanawake Wengi Yakuwa Ni Mzuri Ili Wachukiza Sana Watoto Wa Kiume Wenzangu.Katika Kijiji Hicho Kuna Dada Mmoja Aliyekuwa Anaitwa LUYANGE Alikuwa Ni Mjukuu Wa Bibi Mmoja Aliyekuwa Akisifika Kwa Uchawi Pale Kijijini.Binti Huyo Alijaribu Kuzielezea Hisia Zake Kwangu Mara Kwa Mara Na Kuniambia Yakuwa Ananipenda Lakini Sikuwahi Kumkubalia Hata Kidogo Kwani Nilikuwa Mwenyekuzingatia Maonyo Ya Bibi Yangu.Karibia Watu Wengi Pia Walikuwa Wakizungumza Maneno Yapembeni Wakisema "Mtoto Huyu Sio Ridhiki " Kwani Sikuonyeshaga Hata Punje Ya Kupapalika au Kudata Kwa Mabinti Wa Kike.Siku Moja Nikiwa Ninaenda Kuchota Maji Kisimani Eneo Tunalochota Maji Ni Mbali Kidogo Na Maeneo Ya Nyumbani Nilipofika Nilichota Maji Yangu Nakuanza Kurejea Nilipotoka ,Wakati Nageuka Nilihisi Mtu Akinigusa Katika Bega Langu La Kushoto Nilishtuka Sana Nakumwaga Maji Yalikuwa Kwenye Mti Nilipogeuza Shingo Yangu...
KETARO:Wewe Luyange Kwanini Lakini.Kumbe Alikuwa Ni Luyange Na Mashoga Zake Wawili Wakienda Mtono Kuchota Maji.Nyakati Hizo Mashoga Zake Wote Walikuwa Wakicheka Isivyo Kawaida.
KETARO:Luyange Sininakuuliza Jamani Kwanini Unanishtuwa Ivyo.
LUYANGE:Samahani Ketaro Ila Lengo Langu Nilikuwa Nataka Kukuona Tu Utafanyaje.
KETARO:Aaah Kwahiyo Umefurahi Sasa Nilivyomwaga Maji Sindio Eenh.
LUYANGE:Hapana Ila Maji Sikitu Kwangu Niwapo Na Wewe Faraja Ya Moyo Wangu Kama Ni Maji Nitakuchotea.Wakati Huo Huo Akamwomba Mmoja Wa Marafiki Aliyokuja Nao Akanichotee Maji.
LUYANGE:MANYA Nakuomba Ukamchotee Maji Shemeji Yako Tafadhali.
MANYA:Usijali Shoga.
KETARO:Luyange Mbona Unanipotezea Muda Wangu Hebu Niambie Unachotaka Kuniambia Basi Fasta Mimi Niondoke Zangu.Nikiwa Ninazungumza Hayo Luyange Alikuwa Akinitazama Usoni.
LUYANGE:Ketaro Kila Ninapokuona Huwa Ninapata Mshtuko Wa Moyo .Sura Yako Naa Jinsi Ulivyo Vinanifanya Nikose Amani Ketaro Wewe Ni Mzuri Sana Sijapata Kuona.
KETARO:Luyange Naona Unanipotezea Muda Hebu Niache Mimi Niondoke Zangu Bibi Anasubilia Maji Nikageuka Ilikuyafuata Maji Yangu Aliyokwenda Kufuata Shoga Yake MANYA Nilipogeuka Tu Alinishika Mkono Nakusema...
LUYANGE:Ketaro Hebu Jaribu Kunielewa Hata Chembe Kidogo Tu Kwanini Unataka Kunijeruhi Moyo Wangu Kwanini Hautaki Kuzielewa Hisia Zangu Kwako Jaman Mimi Nakupenda Ketaro Kwanini Ni Nini Ambacho Sina Mbaka Unanifanyia Ivyo Jaman.Kwa Kweli LUYANGE Alikuwa Ni Binti Mmoja Mzuri Sana Kwani Alikuwa Ni Binti Mwenye Rangi Nzuri Ya Chokreti,Lips Nene Nzuri Laini Zenye Rangi Nyekundu Iliyokolea.Mwenye Umbo Lililodhihirishwa Na Baadhi Ya Sehemu Zilizokuwa Zikionekana Katika Mwili Wake ,Alikuwa Anaumbo Zuri Sana Waswahili Wenyewe Wanasema Namba Nane.Luyange Alikuwa Mwenye Nywele Laini Zenye Kuvutia,Macho Makubwa Yaliyo Legea Yenye Umbo La Duara ,Kidevu Kilicho Jichonga ,Matiti Yake Mazuri Yaliyobinuka Ipasavyo Kama Vile Milima Miwili Iliyopakana Bila Kusahau Miguu Yake Iliyokuwa Imebarikiwa Unene Inayojulikana Kwa Jina La Miguu Ya Bia Kwa Ujumla Luyange Alikuwa Ni Binti Mzuri Sana Isivyo Kawaida Alikuwa Ni Mwanamke Aliyeumbika Mithili Ya Malaika Katika Mabinti Watatu 3 Pale Kijijini Wazuri Ukitafuta Hutoweza Kumkosa Luyange.Luyange Alieleza Hisia Zake Mara Kwa Mara Kwangu Tena Mara Nyingine Alipokuwa Akiwakilisha Kwangu Hisia Hizo Alikuwa Akilia Sana Alikuwa Akinieleza Hisia Zake Hizo Mara Kwa Mara bila Kuchoka Lakini Niliogopa Sana Tena Haswa Bibi Yake Kutokana Na Kusifiwa Na Uchawi Alionao Na Matukio Anayofanya Haswa Ya Mauaji Hali Iliyonifanya Kuingiwa Na Hofu#
ITAENDELEA...