Simulizi: Naitwa mume zoba kwa kumpenda mke wangu. (kisa cha kweli cha kusisimua)

Simulizi: Naitwa mume zoba kwa kumpenda mke wangu. (kisa cha kweli cha kusisimua)

Rahidin73

Member
Joined
Oct 25, 2024
Posts
23
Reaction score
30
SIMULIZI: NAITWA MUME ZOBA KWA KUMPENDA MKE WANGU.
SEHEMU: 1
MTUNZI: Madodi ✍🏼
Whatsapp: 0655 969 973
Naitwa Iqram, kijana mrefu, mweusi mwenye tabasamu la kuvutia ambalo lilikuwa na uwezo wa kuwatoa watu wasiwasi hata kwenye hali ya huzuni. Nilikuwa na bahati ya aina yake kwa kumwoa Zuhura, mwanamke mrembo kiasi cha kutikisa nyoyo za wanaume wengi mtaani kwetu. Alikuwa na umbo la kipekee, sura nyororo kama ya malaika, na macho ya kumtoa mtu roho. Kila alipopita, nyuso za wanaume ziligeuka kumfuata, huku wengi wakibaki wakimtamani kwa macho ya dharau na wivu.

Nilikutana na Zuhura katika harusi ya rafiki yangu, na tangu siku hiyo, moyo wangu haukupata amani. Nilijua kwamba niliangukia penzi la kweli. Tabasamu lake la kwanza lilinishinda kabisa, na nilijikuta nikiwa sijielewi kila nilipokuwa karibu naye. Tulipoanza kuzungumza, niligundua kuwa uzuri wake ulikuwa ni sehemu ndogo tu ya uzuri wake wa ndani. Alikuwa na busara za kustaajabisha, upole, na mapenzi ya dhati yaliyonifanya niamini kwamba yeye ndiye aliyekuwa nimemtafuta maisha yangu yote.

Tulipooana, niliapa mbele za Mwenyezi Mungu kwamba nitamlinda kwa gharama yoyote, hata kama ingemaanisha kufa kwa ajili yake. Nilimpenda Zuhura kwa moyo wangu wote, lakini pamoja na hayo, wivu ulianza kunizidi. Uzuri wake ulikuwa baraka na laana kwa wakati mmoja. Ilikuwa ngumu kwangu kudhibiti hisia zangu kila nilipomuona akizungukwa na wanaume waliokuwa wakimtongoza hadharani.

"Nakupenda sana, Zuhura," nilisema nikiwa nimemshika mikono yake tulipokuwa tumekaa kwenye bustani yetu ndogo ya nyumbani. "Lakini wivu huu unanitesa, siwezi kuvumilia kuona macho ya watu yanavyokuangalia."

Zuhura alitabasamu, tabasamu lake lenye kuleta amani. "Mpenzi, najua unanipenda na una wivu, lakini unaamini kweli kwamba ningeweza kukusaliti? Hakuna mtu mwingine anayenivutia kama wewe."

"Lakini siwezi kudhibiti jinsi ninavyohisi," nilimjibu huku nikishusha pumzi ndefu. "Ninaogopa siku moja mambo yatabadilika."

"Nipo hapa kwa ajili yako, Iqram. Kamwe usikubali hisia hizo kuharibu uhusiano wetu. Ni wewe tu unayenifanya niwe na furaha."

Maongezi yetu yalikuwa ya muda mfupi lakini yenye uzito. Niliamua kwamba nitafanya kila linalowezekana kumlinda Zuhura dhidi ya macho ya watu. Lakini haikuchukua muda mrefu kabla ya kugundua kwamba heshima ya mtaa ilikuwa inashuka kila siku. Wanaume walikuwa wakijitokeza kwa ujasiri kumfuata hata akiwa na mimi, na mimi nikaonekana mzembe na dhaifu machoni pao kwa kushindwa kumlinda mke wangu.

Siku moja, nilikuwa nimemsubiri Zuhura nje ya duka moja la mitindo alipokuwa akinunua nguo. Nilipokuwa nimekaa kwenye kiti pembeni ya duka, niliwaona wanaume wawili wakimfuata mara tu alipotoka dukani. Walicheka, wakamwita kwa majina ya kudhalilisha, na hata mmoja wao alijaribu kumshika mkono. Nilijikuta nikikosa uvumilivu, nilisimama na kuelekea walipokuwa kwa hasira.

"Nini mnachokifanya?" nilipaza sauti huku nikiwaangalia kwa macho yaliyojaa ghadhabu.

"Ah, kijana, usijali," mmoja wao alisema kwa dhihaka, "Huyu mrembo hakufai wewe. Unafikiri unaweza kumtosheleza?"

Nilijaribu kutulia, lakini mishipa yangu ilikuwa imechafuka kabisa. "Huyo ni mke wangu," nilisema kwa ukali. "Msinifanye niwafanyie kitu kibaya."

Walicheka tena, wakionyesha dharau zao bila haya. "Mume zoba," mmoja wao alisema kwa sauti ya kebehi. "Mke mzuri kama huyo haleti heshima kwa mwanaume kama wewe."

Zuhura alikuja na kunishika mkono kwa nguvu, akinivuta pembeni. "Iqram, tafadhali, tuondoke hapa. Sio kila mtu anastahili hasira yako."

Lakini sikuweza kuvumilia. Nilijikuta nikiwa nimeshikwa na hisia kali za kulinda heshima yangu na penzi la mke wangu. "Hatuwezi kukubali kudhalilishwa hivi," nilimwambia kwa sauti ya chini.

"Mpenzi, tafadhali..." aliendelea kuniomba huku akionekana kuwa na wasiwasi.

Nilikuwa nimeamua tayari kwamba sikuweza kuruhusu jambo hili liendelee. Niliwatazama wale wanaume kwa mara ya mwisho, macho yangu yakionyesha nia yangu ya kutetea penzi la Zuhura kwa gharama yoyote...................Itaendelea.

Je unawzaje kutetea penzi lako dhidi ya watu wabaya? Karibu usime Simulizi hii, utajifunza na utabirudila.

NUKUU "Mapenzi huanza katika mazingira ambayo haiyatarajii kabisa, yanaingia kwenye damu na mwishoe mmmoja anakua chizi. Unajikuta unamjali mwenzako zaidi ya unavyojijali wewe mwenyewe"

Fanya kusearch hapo Instagram @middotz_ utaona mwendelezo kama hutaki kusubiri kesho hapa
Screenshot_20241009-235220_Add Text.jpg
 

Attachments

  • Screenshot_20241009-235220_Add Text.jpg
    Screenshot_20241009-235220_Add Text.jpg
    272.8 KB · Views: 18
SIMULIZI: NAITWA MUME ZOBA KWA KUMPENDA MKE WANGU.
SEHEMU: 2
MTUNZI: Madodi ✍🏼
Whatsapp: 0655 969 973

Mwaka mmoja baada ya ndoa yetu, furaha yangu ilifikia kilele. Zuhura alikuwa mjamzito, na nilijiona kama mwanaume mwenye bahati zaidi duniani. Kila siku nilipokuwa naye, moyo wangu ulizidi kujazwa na upendo na matumaini kwa maisha yetu mapya. Niliwaza jinsi ambavyo tutakuza mtoto wetu pamoja, jinsi atakavyokuwa nakshi ya familia yetu na kuleta furaha zaidi nyumbani.

Siku ilipowadia, tulikimbia hospitalini. Nakumbuka jinsi mikono yangu ilivyotetemeka nilipokuwa nikimshika, huku akihangaika kutokana na uchungu wa uzazi. Nilikuwa pale kando yake, nikimfariji na kumwambia kuwa kila kitu kitakuwa sawa.

Baada ya saa kadhaa za uchungu, kilio cha mtoto kikasikika. Nilisimama pale kwa mshangao, moyo ukinipiga kwa nguvu. Muuguzi alipoleta mtoto, niliona kiumbe mdogo, lakini kitu kilinifanya nisimame, macho yangu yakakodoka kwa mshangao. Mtoto alikuwa na ngozi nyepesi, yenye rangi nyeupe, macho makubwa ya kiarabu, na nywele za kahawia. Nilijikuta nikitazama kwa mshangao, huku nikiweka akilini kwamba mtoto wangu alionekana kuwa wa asili tofauti kabisa na yangu.

"Zuhura," nilimnong'oneza, macho yangu yakiwa yamejaa maswali. "Mtoto anaonekana tofauti."

Zuhura, akiwa amejaa furaha baada ya kujifungua, alicheka kidogo. "Wewe huelewi nini, mpenzi?" aliniambia kwa sauti ya upole. "Huyu mtoto wetu kachukua asili ya babu yangu. Babu yangu alikuwa Mwarabu, si lazima mtoto afanane na wewe. Watu wanachukua sura za wazazi wa mbali pia."

Nilitabasamu kwa kusita. Maneno yake yalikuwa na mantiki, lakini bado, kitu fulani ndani yangu kilionekana kutokuwa sawa. Niliridhika na maelezo yake, lakini pale pale hospitalini, nilianza kuona jinsi watu walivyokuwa wakiniangalia. Muuguzi mmoja alinitazama kwa macho yaliyojaa mshangao, na nilihisi minong'ono ikianza kuenea.

Baada ya kurudi nyumbani, hali haikufanya tofauti. Familia yangu, mama na baba, walipoona mtoto kwa mara ya kwanza, macho yao yalionyesha maswali mengi.

"Baba, haya ni maajabu gani haya?" Mama aliuliza huku akiwa na mshangao. "Mtoto wa Iqram anaonekanaje hivi?"

Baba yangu, ingawa hakusema chochote mara moja, alinisogelea na kuniambia kwa sauti ya chini,

"Mwanangu, hizi nyakati si za kubeza au kukurupuka. Lakini nakushauri uchukue tahadhari. Huyu mtoto anafanana zaidi na mgeni."......ITAENDELEA.

Instagram imefika EPISODE ya 8 @middotz_
Mtoto katoka mwarabu, Familia na jamii mzima inamshangaaa, Je atachujua maamuzi gani? Usikose.

NUKUU "Ama Kweli Mapenzi ni Upofu,Mapenzi mara nyingi hufanya mtu kufumbia macho ukweli, akivumilia kasoro na makosa ya mpenzi wake. Mtu anaweza kujikuta akiendelea kuamini kuwa mabadiliko yatatokea, licha ya maumivu au dalili za wazi kuwa mambo hayaendi sawa. Hali hii huonyesha jinsi upendo unavyoweza kumfanya mtu kuwa kipofu kwa ukweli wa mambo, akiendelea kushikilia matumaini hata pale ambapo yanapaswa kuachwa. Mapenzi, kwa njia hii, huweza kumfanya mtu kupoteza uwezo wa kutathmini hali kwa uwazi"
 
Hii ni kali, inafikirisha na kuuachagamsha ubongo katika fikra tunduizi, ni kazi ya fasihi iliyoshiba, nataman kuisoma mpaka mwisho
 
SIMULIZI: NAITWA MUME ZOBA KWA KUMPENDA MKE WANGU.
SEHEMU: 3
MTUNZI: Madodi ✍🏼
Whatsapp: 0655 969 973

Maneno yake yalinigonga moyoni kama mwiba. Sikuweza kumwamini mke wangu angeweza kufanya jambo lolote la kunidhalilisha. Nilimpenda, na nilijua jinsi alivyokuwa na heshima katika ndoa yetu. Lakini kwa upande mwingine, maneno ya baba yangu yalinitia wasiwasi.

Majirani walikuwa wa kwanza kuanza kuzungumza. Siku chache baada ya kurudi nyumbani na mtoto, nilianza kusikia minong'ono kila nilipopita.

"Unamjua yule mke wa Iqram?" mmoja alisema akiwa amesimama kwenye kibanda cha mboga. "Mtoto wao ni mzungu kabisa! Huwezi kumwambia huyo ni damu ya Iqram, inawezekana kweli?"

"Nimewahi kumsikia anasema babu yake alikuwa Mwarabu," mwingine alijibu, "lakini bado, si kawaida kwa mtoto kuwa tofauti namna ile!"

Siku moja, nilikuwa nikiketi nje ya nyumba yetu, nilisikia kundi la vijana wakipita wakicheka. "Iqram ni mume zoba!" mmoja wao alisema kwa dhihaka. "Mke wake anachepuka na wanaume wa nje. Ndio maana mtoto kaja na sura za Kiarabu."

Moyo wangu ulishtuka. Nilijaribu kujikaza kiume na kupuuza maneno yao, lakini yalikaa kichwani mwangu kama sumu. Kila siku nilipomwangalia mtoto wetu, nilijikuta nikiuliza, je, ni kweli huu ni damu yangu? Je, inawezekana Zuhura amekuwa akichepuka bila mimi kujua?

Nilijaribu kumzungumzia Zuhura kuhusu hisia zangu, lakini kila wakati alipozungumza, alinifunika na maneno ya busara.

"Iqram, mtoto wetu anafanana na babu yangu. Kwani lazima kila mtoto afanane na baba yake moja kwa moja?" Alisema kwa sauti ya upole, lakini yenye msisitizo. "Tafadhali, acha kusikiliza minong'ono ya watu. Wanafanya hivyo kwa sababu ya wivu tu."

Nilijaribu kumwamini. Mapenzi yangu kwake hayakuwa na kikomo, na sikuweza kufikiria kumwacha. Lakini nilikuwa pia mwanadamu, na udhaifu wangu ulianza kunichosha. Wivu ulianza kuchukua nafasi ya busara, na kila mara nilipoenda kazini au kupita mtaani, nilihisi macho ya watu yakinichoma kwa dhihaka.

"Mume zoba," maneno hayo yaliendelea kunisumbua usiku na mchana.

Lakini nilipomwangalia mtoto, nilihisi kitu cha ajabu. Ingawa nilijaribu kupuuza tofauti zake za kimwonekano, nilihisi kuna uhusiano kati yetu. Alikuwa na tabasamu ambalo lilinikumbusha furaha ya ndoa yangu na Zuhura. Nilijikuta nikimpenda mtoto huyo, ingawa maswali yalikuwa bado yanauma ndani yangu.

Nilihitaji majibu, lakini sikuwa tayari kuharibu amani ya familia yangu. Nilijua kwamba maamuzi yangu yangekuwa na matokeo mazito, lakini bado moyo wangu uligawanyika kati ya mapenzi ya mke wangu na minong'ono ya watu.......Itaendelea.

Je wewe kuweza hayo yote... unaweza kuvumilia manyanyaso ili ulinde Amani.

NUKUU "Iqram anasema 'Bora Kuvumilia Mateso Ila Nilinde Amani ya Penzi Langu' Wakati mwingine, mtu anaweza kuamua kuvumilia mateso na changamoto ndani ya mahusiano kwa lengo la kulinda amani ya penzi lake. Hata kama moyo unalilia maumivu, kufurahia utulivu wa penzi huchukuliwa kuwa bora kuliko kuleta migogoro. Vilio na machozi vinafichwa nyuma ya tabasamu. matumaini ya kurekebisha mambo yakichukua nafasi ya ukweli mchungu. Amani ya penzi inathaminiwa zaidi kuliko faraja ya nafsi.
Screenshot_20241009-235220_Add Text.jpg
 
SIMULIZI: NAITWA MUME ZOBA KWA KUMPENDA MKE WANGU.
SEHEMU: 4
MTUNZI: Madodi ✍🏼
Whatsapp: 0655 969 973

Miaka miwili ilipita haraka sana, lakini mzigo wa aibu na masimango uliendelea kuongezeka juu yangu. Sikuweza kutembea mtaani bila kusikia watu wakinong'ona na kuzungumzia maisha yangu. Maneno ya dhihaka yalikuwa yamekuwa sehemu ya maisha yangu.

"Nimeona Iqram anapita, bado anaishi na huyo mwanamke? Jamaa anaibiwa, anaona lakini haoni!" Kila nilipopita, miguno ya watu ilikuwa kama kisu cha moto moyoni mwangu.

Mtoto wetu Issa alikuwa amefikisha miaka miwili, na kila siku alizidi kufanana na Waarabu. Nywele zake za kahawia zikiwa na mawimbi madogo, macho ya kijani yaliyokuwa na mng'ao wa mbali, na ngozi nyororo iliyokuwa kinyume kabisa na ile yangu ya msukuma mweusi kutoka Mwanza. Issa alionekana kama mgeni kwenye familia yangu, na hilo lilikuwa ni tatizo kubwa zaidi kwa wale waliokuwa karibu nami. Mama yangu, mzee Sadick, na wadogo zangu walikuwa wametupa mkono kabisa.

Nakumbuka siku moja nikiwa nimekaa na baba yangu, mzee Sadick, tulipokuwa nyumbani kwake. Alikaa kimya, lakini macho yake yalikuwa na huzuni ya dhahiri.

"Mwanangu," baba alisema huku akichezesha fimbo aliyokuwa ameishikilia. "Nakuelewa sana. Lakini mimi na mama yako tumekaa tukafikiria, tumeona heri tujitenganishe na haya mambo yako. Huna hata aibu mbele za watu. Unakubali kudharauliwa namna hii, unalea mtoto ambaye kila mtu anasema si wako, na bado unamkumbatia huyo mke wako?"

Sauti yake ilikuwa nzito, ikinikandamiza kama mzigo. "Baba, sina uhakika na haya maneno wanayosema. Zuhura ameniambia kwamba mtoto kafanana na babu yake, na mimi nimempenda mtoto kama wangu. Sihitaji maneno ya watu kuamua uhusiano wangu na mke wangu."

Mzee Sadick alitikisa kichwa, akimwangalia mama yangu, ambaye naye alikuwa amekaa pembeni bila kusema chochote.

"Unamwamini sana huyo mwanamke, lakini dunia nzima inakuambia ukweli. Wewe huoni? Hiyo ni aibu kwa familia yetu, kila mtu anatusema kwa sababu ya mke wako."

Nilikaa kimya, nikiwa na huzuni. Nilijua familia yangu ilinipenda, lakini walikuwa wamekata tamaa kabisa juu yangu. Mama yangu hakusema chochote, aliniangalia tu kwa macho yaliyokuwa yamejaa huzuni, kama vile alikuwa ananiombea mabadiliko niliyokuwa siwezi kuyaona.

***

Mtaani, hali haikuwa bora zaidi. Issa alianza kuwa na wakati mgumu zaidi na watoto wenzake. Kila alipocheza na wenzake, walimzomea, wakimwambia kwamba mimi si baba yake.

"Baba yako ni nani? Mbona wewe una sura ya Kiarabu na baba yako ni mweusi kama giza?" mmoja wa watoto alimzodoa wakati fulani tulipokuwa uwanjani.

Issa alikimbia kwangu huku akilia, moyo wangu ukiuma kwa kumuona mwana wangu akiteseka kwa kitu ambacho hakuchagua. Nilimwinua na kumkumbatia kwa nguvu.........ITAENDELEA. Ingia INSTAGRAM search @middotz_ utaikuta imefika EPISODE YA 10

Matatizo ya Iqram yananza kutesa wasio na hatia... JE KIPI KITATOKEA EPISODE INAYOFUATA.

NUKUU "Kuvumilia mambo yasiyostahili kwa kisingizio cha upendo au amani, wakati mwingine hujenga mazingira ya maumivu kwa wale walio karibu. Wakati mtu anapokubali kukandamizwa, wengine wanaounga mkono au kuhusika nao pia hupatwa na athari za mateso hayo. Hivyo, uvumilivu wa kijinga unaweza kuendeleza maumivu yasiyo ya lazima kwa wote"
 

Attachments

  • Screenshot_20241009-235220_Add Text.jpg
    Screenshot_20241009-235220_Add Text.jpg
    272.8 KB · Views: 8
SIMULIZI: NAITWA MUME ZOBA KWA KUMPENDA MKE WANGU.
SEHEMU: 4
MTUNZI: Madodi ✍🏼
Whatsapp: 0655 969 973

Miaka miwili ilipita haraka sana, lakini mzigo wa aibu na masimango uliendelea kuongezeka juu yangu. Sikuweza kutembea mtaani bila kusikia watu wakinong'ona na kuzungumzia maisha yangu. Maneno ya dhihaka yalikuwa yamekuwa sehemu ya maisha yangu.

"Nimeona Iqram anapita, bado anaishi na huyo mwanamke? Jamaa anaibiwa, anaona lakini haoni!" Kila nilipopita, miguno ya watu ilikuwa kama kisu cha moto moyoni mwangu.

Mtoto wetu Issa alikuwa amefikisha miaka miwili, na kila siku alizidi kufanana na Waarabu. Nywele zake za kahawia zikiwa na mawimbi madogo, macho ya kijani yaliyokuwa na mng'ao wa mbali, na ngozi nyororo iliyokuwa kinyume kabisa na ile yangu ya msukuma mweusi kutoka Mwanza. Issa alionekana kama mgeni kwenye familia yangu, na hilo lilikuwa ni tatizo kubwa zaidi kwa wale waliokuwa karibu nami. Mama yangu, mzee Sadick, na wadogo zangu walikuwa wametupa mkono kabisa.

Nakumbuka siku moja nikiwa nimekaa na baba yangu, mzee Sadick, tulipokuwa nyumbani kwake. Alikaa kimya, lakini macho yake yalikuwa na huzuni ya dhahiri.

"Mwanangu," baba alisema huku akichezesha fimbo aliyokuwa ameishikilia. "Nakuelewa sana. Lakini mimi na mama yako tumekaa tukafikiria, tumeona heri tujitenganishe na haya mambo yako. Huna hata aibu mbele za watu. Unakubali kudharauliwa namna hii, unalea mtoto ambaye kila mtu anasema si wako, na bado unamkumbatia huyo mke wako?"

Sauti yake ilikuwa nzito, ikinikandamiza kama mzigo. "Baba, sina uhakika na haya maneno wanayosema. Zuhura ameniambia kwamba mtoto kafanana na babu yake, na mimi nimempenda mtoto kama wangu. Sihitaji maneno ya watu kuamua uhusiano wangu na mke wangu."

Mzee Sadick alitikisa kichwa, akimwangalia mama yangu, ambaye naye alikuwa amekaa pembeni bila kusema chochote.

"Unamwamini sana huyo mwanamke, lakini dunia nzima inakuambia ukweli. Wewe huoni? Hiyo ni aibu kwa familia yetu, kila mtu anatusema kwa sababu ya mke wako."

Nilikaa kimya, nikiwa na huzuni. Nilijua familia yangu ilinipenda, lakini walikuwa wamekata tamaa kabisa juu yangu. Mama yangu hakusema chochote, aliniangalia tu kwa macho yaliyokuwa yamejaa huzuni, kama vile alikuwa ananiombea mabadiliko niliyokuwa siwezi kuyaona.

***

Mtaani, hali haikuwa bora zaidi. Issa alianza kuwa na wakati mgumu zaidi na watoto wenzake. Kila alipocheza na wenzake, walimzomea, wakimwambia kwamba mimi si baba yake.

"Baba yako ni nani? Mbona wewe una sura ya Kiarabu na baba yako ni mweusi kama giza?" mmoja wa watoto alimzodoa wakati fulani tulipokuwa uwanjani.

Issa alikimbia kwangu huku akilia, moyo wangu ukiuma kwa kumuona mwana wangu akiteseka kwa kitu ambacho hakuchagua. Nilimwinua na kumkumbatia kwa nguvu.........ITAENDELEA. Ingia INSTAGRAM search @middotz_ utaikuta imefika EPISODE YA 10

Matatizo ya Iqram yananza kutesa wasio na hatia... JE KIPI KITATOKEA EPISODE INAYOFUATA.

NUKUU "Kuvumilia mambo yasiyostahili kwa kisingizio cha upendo au amani, wakati mwingine hujenga mazingira ya maumivu kwa wale walio karibu. Wakati mtu anapokubali kukandamizwa, wengine wanaounga mkono au kuhusika nao pia hupatwa na athari za mateso hayo. Hivyo, uvumilivu wa kijinga unaweza kuendeleza maumivu yasiyo ya lazima kwa wote"
@everyone
#highlights
Boss ukiweka mwendelezo tustue wana
Poa mkuu saiv na kesho mapema
 
SIMULIZI: NAITWA MUME ZOBA KWA KUMPENDA MKE WANGU.
SEHEMU: 5
MTUNZI: Madodi ✍🏼
Whatsapp: 0655 969 973
INSTAGRAM @middotz_
"Usiwajali hao watoto," nilimwambia kwa upole. "Wewe ni mwanangu, na nitakupenda daima."

Lakini ndani yangu, huzuni ilikuwa kama jivu lililojaa kwenye moyo wangu. Nilijua mtoto huyu alikuwa hana hatia, lakini dhihaka za watu zilikuwa zikinikumbusha kila siku kile ambacho jamii iliamini.

***

Siku moja, nilipokuwa nyumbani na Zuhura, nilikusanya ujasiri kuuliza swali ambalo lilikuwa likininyemelea akili yangu kwa muda mrefu.

"Zuhura," nilianza kwa sauti ya chini, "unajua watu wanasema nini mtaani, siyo? Wanasema Issa sio mwanangu."

Zuhura aliweka chini kikombe cha chai alichokuwa anakinywa, akaniangalia kwa macho ya kushangaa na kuchanganyikiwa. "Iqram, unamaanisha nini? Hivi una mashaka na mimi na mtoto wetu?"

"Nashindwa kuelewa, Zuhura. Naumia. Kila mahali naposikia maneno hayo, nashindwa kuyapuuza. Familia yangu imejitenga kabisa, mtaani wananikejeli, hata watoto wanamnyanyasa Issa. Niambie ukweli, Zuhura, je, huyu mtoto ni wangu kweli?"

Zuhura alikaa kimya kwa muda mrefu, kisha akainua macho yake, macho yaliyojaa machozi. Hakika huyu Zuhura kule Bongo Movie sijui nimfananishe na nani.

"Iqram, nimeshakuambia mara nyingi, mtoto wetu kafanana na babu yangu. Si lazima afanane na wewe. Naumia kuona jinsi watu wanavyotutenga kwa sababu ya jambo hili. Naumia kuona familia yako imejitenga. Lakini ukweli ni huo; Issa ni mtoto wako. Nifanye nini ili uamini?"

Maneno yake yalikuwa mazito, lakini bado moyo wangu ulikuwa haupo katika amani. Nilimpenda sana Zuhura, lakini shaka iliyoingia ndani yangu haikutaka kutoka.

***

Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi kadri muda ulivyoendelea. Vituko vya Zuhura vilianza kujitokeza polepole. Alianza kunichukulia kawaida, akichelewa kurudi nyumbani, wakati mwingine bila hata maelezo.

"Siku hizi unajichelewesha sana, Zuhura," nilimuuliza mara moja aliporudi nyumbani usiku wa manane. "Ulikuwa wapi?"

Alikuwa na sura ya kutokuwa na wasiwasi, akijibu kwa sauti ya kawaida, "Nilikuwa na rafiki zangu, tumekuwa tukizungumza kuhusu mambo yetu ya kawaida huko kitambaa cheupe"
Screenshot_20241009-235220_Add Text.jpg

"Kitambaa cheupe mke wa mtu usiku wa manane, na ni rafiki gani hao ambao hawajulikani?" nilimuuliza, sauti yangu ikiwa imejaa mashaka.

Lakini bado, niliziba masikio. Nilijua kwamba hali ilikuwa ikienda pabaya, lakini moyo wangu ulishikilia mapenzi yangu kwa Zuhura. Nilimpenda sana kiasi kwamba nilikubali kupuuza kila dalili ya hatari.

Sikuweza kuacha kumwona kama mwanamke aliyenifunga kwa uzuri wake, uaminifu nilioutarajia, na matumaini ya kujenga familia bora. Hata hivyo, nilianza kugundua kwamba nilikuwa pekee yangu katika vita vya kulinda ndoa yetu........ITAENDELEA.

Kitambaa cheupe mke wa mtu🤔🙄 ndio kumbukumbu iliyobaki. Usikose kujua kipi kitampata Zoba.

NUKUU "Wakati mwingine unachagua kufumbia macho makosa na udhaifu wa mke wako, ukijisahaulisha kwa makusudi ili kuendeleza penzi hata kama hilo penzi linatembea katika giza barabarani kama likiona taa nyekundu linajidai halina breki, huku ukitumaini kuwa upendo utashinda changamoto hizo, na kukufikisha salama safari yako"
 
SIMULIZI: NAITWA MUME ZOBA KWA KUMPENDA MKE WANGU.
SEHEMU: 6
MTUNZI: Madodi ✍🏼
Whatsapp: 0655 969 973

Nilipoanza kufanya kazi kiwanda cha dawa kule Mwenge, maisha yangu yalikuwa na changamoto nyingi. Shift za usiku zilikuwa zikinichosha sana, lakini sikuwahi kufikiria kwamba changamoto kubwa zaidi ilikuwa nyumbani kwangu. Zuhura alikuwa mke ambaye uzuri wake ulinifanya nimsamehe kila kosa, lakini hivi sasa nilikuwa nikiishi katika mateso makali ya moyo.

Majibu ya kejeli yalizidi kila siku. "Zuhura," nilimuita mara moja alipoanza kujiandaa kutoka, "Unajua unachofanya si sawa. Unakuwa klabu kila wikiendi, huagani wala kuniambia chochote. Mimi ni mume wako."

Aligeuka, akicheka kwa dharau, na akaanza kuimba kipande cha wimbo wa Rayvanny kwa sauti ya kejeli, "...Ivi una akili wewe... zinachaji kweli yani uko na babe lina minyama tukuachie mwenyewe..." Akamalizia kwa kucheka na kutoka, akiwa hajali kabisa maumivu yangu. Hilo liliniumiza sana. Maneno hayo yalikuwa kama msumari wa moto moyoni mwangu.

Nilijua kwamba mke wangu alikuwa anajitokeza hadharani, akiwa kwenye klabu na matamasha ya wasanii kila wikiendi. Watu walikuwa wanazungumza mtaani, lakini mimi nilikaa kimya, nikijaribu kuamini kuwa pengine hali itabadilika.

***

Niliporudi nyumbani baada ya shift za usiku, nilianza kukutana na vitu ambavyo viliuchoma moyo wangu kama sindano. Siku moja nikiwa na uchovu mwingi baada ya kazi, nilipofika nyumbani, niliona kitu kilichonishitua. Condom zilizotumika zilikuwa zimeachwa mezani sebuleni, bila hata kufichwa. Mikono yangu ilitetemeka nilipovichukua. Nilihisi maumivu makali yakinipitia mwilini, moyo wangu ukipiga haraka kwa uchungu.

Nilimsubiri Zuhura arudi. Aliporudi nyumbani usiku huo, akiwa amevaa nguo nyepesi, macho yake yalionekana kama kwamba hakuwa na shaka yoyote.

"Zuhura," nilisema kwa sauti ya chini, nikimwonyesha hizo condom zilizotumika, "Hizi ni nini? Unanifanyia nini?"

Alinitazama bila hisia, halafu akaanza kuimba tena, "...Kama umechoka tuachie sisi... tumle mpaka mifupa sisi ndio mafisi..." Alimalizia kwa kucheka kama vile hakuna kilichokuwa kibaya.

"Unajua nini unafanya, Zuhura?" niliuliza, sauti yangu ikiwa imejaa huzuni. "Unajua maneno haya yanamaanisha nini kwangu? Yananiua ndani kwa ndani, lakini siwezi kukuacha. Umefanya hivyo mara ngapi? Unanidanganya kwa namna hii hadi lini?"

Lakini hakujali. Alipita mbele yangu, akaenda chumbani bila kusema chochote zaidi. Maisha yangu yalikuwa ni mateso makali; nilikuwa naishi na mwanamke ambaye niliamini bado nilimpenda, lakini alikuwa akinichoma kila siku kwa vitendo vyake......ITAENDELEA.

Kule Instagram imefika 11 fanya kusearch @middotz_

PENZI LIPO MAHUTUTI AISEE... JE TAENDELEA KUVUMILIA? YETU MACHO. USIKOSE SEHEMU YA 7

NUKUU "Wakati mwingine unaishi na mwanamke unayeamini bado unampenda, lakini vitendo vyake vinaendelea kukuchoma kwa maumivu ya kimya. Unajikuta ukivumilia, ukiamini kuwa labda mabadiliko yatakuja, ingawa kila siku inaongeza mzigo wa machungu moyoni mwako. Hata hivyo, upendo unaobaki unakufanya ushindwe kuacha, ukiendelea kumtegemea mabadiliko ambayo huenda yasifike"
 
SIMULIZI: NAITWA MUME ZOBA KWA KUMPENDA MKE WANGU.
SEHEMU: 7
MTUNZI: Madodi ✍🏼
Whatsapp:
👇🏽
Siku moja, nilizungumza na mmoja wa marafiki zangu wa karibu, ambaye alikuwa akijua kinachoendelea. Tulikuwa tumekaa kwenye baa ndogo kule Mwenge, nikinywa chai ya moto.

"Kaka," alinianza kwa sauti ya tahadhari, "hii hali ya nyumbani kwako haijawa nzuri. Watu wengi wanazungumza kuhusu Zuhura. Kuna wanaume ambao wanadai kabisa kuwa na mahusiano naye, na wanafanya wazi kabisa. Inakula kwako kila siku, lakini huonekani kufanya chochote."

Nilijua alikuwa sahihi, lakini nilihisi kama nimenaswa kwenye mtego wa mapenzi. "Siwezi kumuacha, rafiki yangu," nilisema kwa sauti ya chini. "Mke wangu ni mzuri sana. Kila mtu anamtamani. Lakini mimi nilimchagua, na bado nadhani anaweza kubadilika."

Alinitazama kwa huruma. "Lakini kuna wakati, ndugu yangu, mapenzi yanapaswa kuwa na mipaka. Hii ni aibu kwako, kwa familia yako. Mzee Sadick ameishasema kwamba haupaswi kuendelea kuvumilia hili."

Nilinyamaza, nikiwa nimechoka kimwili na kiakili. Kwanza nilichukia nilitaka ushauri lakini sio ushauri wa kumuacha mke wangu. Nilikunywa chai yangu polepole, nikifikiria maneno ya rafiki yangu. Je, nilikuwa na nguvu za kuendelea kuvumilia? Au ningepaswa kuachana na yote na kuanza upya?

***

Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi kadri siku zilivyoendelea. Zuhura alianza kuwa mjeuri zaidi, akiwasha muziki kwa sauti kubwa kila alipopata nafasi, akinicheka kila nilipokemea tabia zake. "Wewe ni mume au mlinzi?" aliniuliza mara moja. "Unafikiria maisha yangu ni ya kukaa ndani tu? Nahitaji kuwa huru kufanya mambo yangu Babu, upo?!"🤐🙄

Nilihisi kama maisha yangu yalikuwa yanaanguka taratibu. Zuhura hakuwa tena yule mwanamke niliyempenda kwa dhati. Vituko vyake vilizidi, na nilihisi kama nilikuwa nimekosa uwezo wa kudhibiti chochote.

Lakini bado, licha ya kila kitu, sikuweza kumuacha. Niliamini ni makosa ambayo kila mmoja anaweza kuyafanya, Uzuri wake ulikuwa ni kitu kilichonifanya nishindwe kuchukua hatua yoyote. Alikuwa mrembo mno; kila alipopita, wanaume walimtazama kwa tamaa. Na kila siku, nilijikuta nikiwa mtegemezi wa uzuri wake.

Zuhura alikuwa amegeuka kuwa mke wa ajabu kwangu, lakini bado nilivuta pumzi na kujaribu kuvumilia. Sijui niliwezaje kufanya hivyo, lakini moyo wangu ulishikilia matumaini kwamba siku moja, labda, hali itabadilika...........ITAENDELEA.

ZUHURA HUYU KABADILIKA ZAIDI YA ZUWENA.

NUKUU "Wakati mwingine mke wako anabadilika na kuwa mtu usiyemjua tena, akifanya vitendo vya ajabu vinavyovunja moyo na kuleta maumivu yasiyovumilika. Kila siku unashuhudia upendo ukiyeyuka taratibu, lakini bado kuna kitu ndani yako kinachokushikilia. Nguvu za kuvumilia zinatoka wapi? Labda ni matumaini madogo yanayobaki kwamba hali itabadilika, au ni hofu ya kuachilia penzi mlilolijenga. Hata pale ambapo penzi linaelekea kuzimu, unashikilia kwa nguvu zile za mwisho, ukikataa kuamini kwamba safari yenu imefika mwisho."

#madodi
#highlights
Screenshot_20241009-235220_Add Text.jpg
 
Lakin mkuu pamoja na kwamba umeweka vipande vitatu, lakin vipande vyenyewe ni vifupi mno, vinakera
 
SIMULIZI: NAITWA MUME ZOBA KWA KUMPENDA MKE WANGU.
SEHEMU: 8
MTUNZI: Madodi ✍🏼
INSTAGRAM: @middotz_

Baada ya vituko vya kila aina, nilijikuta nikifikiria suluhisho la pekee ambalo lingeweza kuziba midomo ya watu waliokuwa wakiniteta vibaya mtaani. Nilihisi kuwa, kama ningepata mtoto mwingine, labda mambo yangetulia na maneno ya watu yangekoma. Hilo lilikuwa tumaini langu kubwa. Nilimwita Zuhura, na baada ya mazungumzo marefu ya usiku, alikubali wazo langu bila kusita. "Tupate mtoto mwingine, ili uone jinsi watu watakavyonyamaza," aliniambia kwa tabasamu. Nilijawa na matumaini, nikiamini kwamba mambo yangebadilika.

Baada ya miezi michache, mke wangu akapata ujauzito. Katika kipindi hicho, Zuhura alibadilika kidogo. Alikuwa mtulivu, hakwenda tena kwenye klabu wala kwenye matamasha. Niliamini labda ujauzito huu ungekuwa mwanzo mpya wa amani nyumbani kwangu. Familia yangu, ingawa walikuwa wamenitenga, walianza kunipa polepole kutokana na taarifa za ujauzito huu. Nilihisi kama hali inarejea kwenye mstari.

***

Siku ya kujifungua ilipowadia, nilikuwa na wasiwasi, lakini pia nilijawa na matumaini makubwa. Hospitalini, nilisubiri kwa hamu na ghamu, macho yakiangalia mlango wa chumba cha kujifungulia. Baada ya muda mrefu wa kungoja, nesi alitoka na kuniita. Niliharakisha ndani, nikamkuta Zuhura akiwa na tabasamu la kawaida, akishika mtoto mchanga mikononi mwake.

Lakini mshangao ukanipata nilipomtazama mtoto wetu. Alikuwa mzungu kabisa! Sura yake ilionekana kama vile anatoka Ulaya, rangi ya ngozi yake ikingaa na nywele zake za dhahabu zikionekana kama za mchezaji maarufu wa Manchester City, Erling Haaland. Sijawahi kuona kitu kama hiki katika maisha yangu.

Nilimuangalia Zuhura kwa macho ya mshangao, nikiwa sijaamini kilichotokea. "Zuhura... huyu mtoto ni wa nani? Hivi mimi na wewe tunafanana na huyu kweli?"

Zuhura alinitazama kwa utulivu na akatabasamu, "Iqram, huyu mtoto amefuata kwa bibi yangu kabisa. Ni damu ya familia yetu hii. Si lazima watoto wafanane na baba au mama moja kwa moja."

Nilishindwa kujizuia, nikiwa na mchanganyiko wa hisia za huzuni na mshangao. "Lakini Zuhura... huyu mtoto anaonekana kama si wa kwetu kabisa. Familia yangu haitakubaliana na hili." Nilihisi huzuni ikingia moyoni, nikijua sasa maisha yangu yangekuwa magumu zaidi.

***

Habari za kuzaliwa kwa mtoto zilisambaa haraka mtaani. Kila mtu alianza kuzungumza kuhusu "Baba Mwarabu Mzungu." Ilikuwa kama vile neno lililozua furaha kwa kila mtu isipokuwa mimi. Watu walikuwa wananicheka kila nilipopita, wakipiga mikogo ya dhihaka na kuninyoshea vidole. Hata watoto wadogo walikuwa wakinizomea. "Baba Idrisa! Baba Haaland!" waliniita, huku wakicheka kwa sauti........ITAENDELEA

Hatimae Kazaliwa Erling Haaland.. Chuma cha kisukuma kimepata mtoto wa kizungu. Saivi mtaani anaitwa Baba Mwarabu Mzungu 🤣🤣🤣

NUKUU "Wakati mwingine unafikia hatua ya uvumilivu ambapo kila mtu anakuona kama umechizika. Marafiki, familia, na hata majirani wanakushangaa kwa jinsi unavyovumilia maumivu yanayoendelea kumaliza nguvu zako. Lakini, licha ya yote, kuna kitu ndani yako kinachokushawishi kubaki na kulinda penzi lako bubu, penzi ambalo maneno hayawezi kuelezea. Unajiambia, labda ni wewe tu unayeweza kuona thamani iliyobaki, na kwa namna fulani, unashikilia matumaini yasiyoeleweka. Hata dunia ikigeuka dhidi yako, moyo wako unakataa kuacha, uking'ang'ania kuamini kwamba penzi hilo, lililo kimya na kiza, linaweza kufufuka tena."
 
SIMULIZI: NAITWA MUME ZOBA KWA KUMPENDA MKE WANGU.
SEHEMU: 9
MTUNZI: Madodi ✍🏼
INSTAGRAM: @middotz_

Wakati mmoja, nilikutana na kijana mmoja mtaani akiniangalia kwa dhihaka. "Kaka, hivi kweli huyo mtoto ni wako? Hata Haaland mwenyewe angekuja leo, singejua tofauti!" alisema huku akiangua kicheko. Nilijaribu kupuuza, lakini maneno hayo yaliniumiza kwa ndani.

Nyumbani, nilikaa kimya, nikiwaza kuhusu maisha yangu na jinsi nilivyokuwa nimefika hapa. Kila mara niliwaangalia watoto wangu, Issa ambaye alikuwa mwarabu kabisa, na sasa Idrisa, mzungu kabisa. Nilipokuwa nao, nilihisi huzuni mchanganyiko na furaha. Nilipenda familia yangu, lakini nilijua kwamba jamii haikunielewa, na hata familia yangu ilikuwa imesha nikata tamaa kabisa.

***

Wakati huo huo, baba yangu, Mzee Sadick, alijitenga kabisa nami. Nilipomtembelea siku moja, alinitazama kwa macho yenye huzuni na kusema, "Iqram, nimefika mwisho wa kuvumilia. Wewe sio tena mtoto wangu. Zoba wa namna yako sijawahi kuona. Umekubali kufanywa kichekesho cha mtaa mzima, halafu unajifanya kama hakuna tatizo."

Maneno hayo yaliniuma sana. Nilimuangalia baba yangu, mzee aliyenilea kwa nidhamu, na nikahisi kama kila kitu kimeniponyoka mikononi. "Baba, tafadhali, usiniseme hivyo. Hawa ni watoto wangu, lazima niwatunze, hata kama wanaonekana tofauti."

Lakini baba yangu hakunisikiliza. "Hata kama ni watoto wako, unafikiria nini juu ya familia yetu? Watu wanatusema kila siku. Hivi kweli, mweusi msukuma kama wewe, unapata watoto wa kizungu? Tafakari, mwanangu."

Nilinyamaza, nikiwa na maumivu moyoni. Hakukuwa na maneno ya kusema. Niliaga kimyakimya na kuondoka, nikijua kwamba familia yangu imeniacha kabisa.

***

Mtaani, minong'ono ilikuwa imepamba moto. Watu walikuwa wananizungumzia waziwazi. Niliposimama kwenye kibanda cha magazeti siku moja, nilisikia wanaume wawili wakiongea nyuma yangu.

"Mzee yule kaamua kuachana na akili kabisa. Mke wake anazaa watoto wa kila rangi, lakini yeye anabaki kimya. Zoba kweli."

"Mwanaume wa namna hiyo ni wa kushangaa sana. Aibu kwa familia nzima, si kwa mtaa tu."

Nilitaka kugeuka na kuwakemea, lakini sikujua pa kuanzia. Hata watu wa karibu walikuwa wameniacha. Nilikuwa nimeshikwa na kitanzi cha mapenzi ya Zuhura, mapenzi ambayo yalinipofusha.

Lakini licha ya hayo yote, bado niliamua kubaki na familia yangu. Nilijaribu kadri ya uwezo wangu kuwatunza watoto wangu, Issa na Idrisa. Nilijua maneno ya watu yasingeisha, lakini sikutaka kuwaacha watoto wasio na hatia. Hata kama sura zao hazikufanana na mimi, niliamini kuwa walikuwa wangu.

Ilikuwa ni safari ya huzuni isiyoisha, lakini nilichagua kuendelea kusimama. Nilikuwa baba wa watoto hawa, na hata kama jamii ilinizomea, nilijua ndani ya moyo wangu kwamba nilikuwa nimefanya chaguo la upendo.......ITAENDELEA.

Je msomaji unaamini hao ni watoto wake kweli.

NUKUU "Wakati mwingine unajikuta katika safari ya huzuni isiyoisha, ukivumilia ukweli unaokuchoma kwamba watoto unaowapigania huenda si wako. Licha ya walimwengu kukusema kwa uzembe wako wa kufumbia macho, bado unashikilia matumaini yasiyo na msingi. Kejeli zinaongezeka, lakini unakataa kukabiliana na ukweli huo mchungu, ukivumilia kwa jina la familia, huku ukijiharibu taratibu ndani kwa ndani."
 
SIMULIZI: NAITWA MUME ZOBA KWA KUMPENDA MKE WANGU.
SEHEMU: 10
MTUNZI: Madodi ✍🏼
INSTAGRAM: @middotz_
.
Nilizidi kumshusha moyo kila mara nilipokumbuka jinsi watu walivyonisema mtaani, lakini moyo wangu ulikuwa na kinga moja kubwa—mapenzi kwa Zuhura. Kila siku mapenzi yangu kwake yalizidi kuongezeka, hata baada ya vituko na masimango yote, sikuweza kumchukia. Wanangu, Issa na Idrisa, pia nilizidi kuwapenda zaidi. Ingawa sura zao zilileta maneno mengi kutoka kwa watu, sikuwahi kuwa na wasiwasi juu ya nafasi yangu kama baba yao.

Mtu yeyote ambaye hakuwa kwenye hali yangu aliendelea kuamini kuwa nimerogwa. Walishindwa kuelewa ni kwa nini ningeweza kuvumilia yote hayo na bado nisiwe na kinyongo wala hasira. Mara nyingi nilisikia minong'ono mitaani: "Iqram anapenda mke wake, lakini lazima atakuwa kashikwa kwa njia zisizoeleweka, vinginevyo asingeweza kuvumilia haya yote. Huyu jamaa lazima kesharogwa."

Mimi sikujali hayo maneno, niliamini kila jambo lilikuwa la kawaida tu. Zuhura alikuwa mzuri sana, na nilijua uzuri wake ulikuwa ukichochea wivu wa watu. Ndiyo maana, niliongeza mapenzi kwake. Nilijua kuwa siku zote, watu waliokuwa wanampenda wangeendelea kumsumbua, lakini mwishoni, mimi ndiye niliyemlaza kitandani usiku kila siku.

***

Zuhura alipoona jinsi nilivyokuwa nimeshaingia kwenye mtego wa mapenzi yake, akaanza kutaka kubadilisha maisha yangu kabisa. Alinijia usiku mmoja, akisema kwa sauti ya utulivu lakini yenye amri. "Iqram, kuna jambo ambalo nataka tukubaliane nalo. Unahitaji kubadilika. Wale marafiki zako wa kijiweni hawakusaidii chochote. Urafiki nao unakupotezea muda na wanakuletea matatizo tu. Hii familia yetu sasa inahitaji umakini wako. Unahitaji kuwa na mimi pekee, siyo watu wengine."

Niliangalia macho yake, nikiwaza kwa kina. Marafiki wangu walikuwa kama ndugu kwangu, lakini Zuhura alikuwa na hoja. Nilihisi kama vile walikuwa wanazidi kunishusha morali kwa maneno yao ya kumkosoa mke wangu. Na kwa kuwa nilimpenda Zuhura, nikaamua kufuata ushauri wake.

"Kwa hiyo unataka niachane kabisa na rafiki zangu?" Nilimuuliza, nikiwa nimeshika mkono wake.

"Ndio, Iqram. Rafiki zako wanaweza kuwa chanzo cha matatizo. Nataka unipe muda wako wote. Mimi na familia yetu ndio muhimu," alisema kwa utulivu, kisha akatabasamu kwa namna iliyozidi kunivuta kwake.

Baada ya mazungumzo hayo, nikafanya kama alivyonitaka. Nilianza kuachana na marafiki zangu mmoja baada ya mwingine. Nilianza kujitenga na kila mtu mtaani, na nilipojaribu kukaa na watu waliokuwa marafiki zangu, Zuhura alikuwa wa kwanza kunikumbusha kuhusu ahadi yangu. "Si nilikwambia? Wale wanaume hawakutakii mema, wanakuchezea akili tu. We niache mimi nikulinde."

***

Mambo yalizidi kwenda mbali zaidi. Nilianza kufuatana na Zuhura kila sehemu. Tulikuwa kama wapenzi walio kwenye kipindi cha mwanzo wa mahaba yao. Alipokuwa akienda sokoni, nilikuwa naye. Alipokuwa akienda dukani, niliandamana naye. Ilifika hatua hata kwenda saluni au gengeni, nilikuwa karibu naye. Wakati mwingine, tulipokuwa njiani, wanaume walimzunguka na kumzonga kwa maneno ya kumtongoza, lakini yeye aliwaambia, "Mpenzi, tangulia nyumbani, nitakufuata." Na mimi nilikuwa natangulia kwa utulivu, nikiwa na furaha kwamba angalau mimi ndiye ninayeingia naye chumbani kila usiku.

Lakini minong'ono mitaani haikukoma. Badala yake, ilizidi. Watu walianza kuniita "Baba Yule Anayeongozwa," huku wakisema mimi ni kichekesho. "We unaona huyu? Anafuatana na mke wake kama mtoto mdogo. Si bure, amekamatwa kabisa!"......ITAENDELEA
 
Mmmh hii story inaboaa, hata kama zoba kias gan uzuri tu hauwez kukufanya uwe bwege kiasi hicho. Hadi nmeshindwa kuimaliza imeboa sana
 
Back
Top Bottom